Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
Kwa hali tuliyofikia sasahivi, CCM imebakiza option mbili kubwa: Kujisahihisha na tena upesi; au kukivunja Chama katika mapande mawili makubwa ili kutoa vyama viwili tofauti. Nitafafanua baadae kidogo.
Ni muhimu pia niseme kwamba katika haya, ninalindwa na kipengele kifuatacho cha Mwongozo wa Chama Changu Cha Mapinduzi (CCM) 1981: Kipengele Cha 57(5), Ukurasa wa 22 Kujikosoa na kukosoana ni silaha ya Mapinduzi.
Miaka karibia 50 iliyopita, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alitoa kitabu chake cha TUJISAHIHISHE (May 1962). Miaka 50 baadae, CCM haina mwarubaini mwingine zaidi ya kumrudia Mwalimu Nyerere ili kujirudisha katika mstari. Badala ya kupoteza muda an kauli butu za tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele, ni muhimu viongozi wa CCM watumie kilele cha sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika kuanza kuthubutu ili chama chetu cha mapinduzi (CCM) kweli kiweze kusonga mbele.
Katika kitabu chake cha TUJISAHIHISHE. Mwalimu anasema:
[Ukiondoa matatizo wayapatayo binadamu kwa sababu kama mafuriko, nzige, kiangazi, n.k, matatizo yao mengi hutokana na unafsi. Unafsi ni wa aina nyingi. Swali ambalo twalisikia mara kwa mara, Hali yetu ya baadae itakuwaje?, ni swali ambalo sina shaka kuna wanaouliza kwa nia safi kabisa. Lakini mara nyingi linatokana na unafsi. Mtu anayeuliza anafikiri TANU iliundwa kwa faida yake binafsi. Ni kama kwamba TANU ilipoundwa ilimwahidi kwamba ikiwa atakubali kuwa mwanachama, au kiongozi, basi TANU itamfanyia yeye jambo fulani kama tunzo! Anasahau kabisa kuwa TANU inajishughulisha na haja za Jumuiya kwa ujumla. Lakini kwa mtu wa aina hiyo, hata kama TANU inatimiza madhumuni yake kwa jumuiya, ataona kuwa ni umoja ambao hauna maana kwa sababu haumtimizii haja zote za nafsi yake. Huu ni unafsi. Kama wanachama wa TANU, na hasa viongozi, hawatakihukumu chama chetu kwa mahitaji na nafsi zao wenyewe, chana hakitadumu. Wanachama wa aina hiyo ni ugonjwa katika chama.
Dalili nyingine ya unafsi, na ambayo ni ugonjwa mbaya sana ni fitina. Kanuni moja ya TANU inasema hivi: Nitasema Ukweli Daima. Fitina Kwangu ni Mwiko. Lakini bado tunao wanachama ambao ni wafitini wakubwa bila kujitambua. Ni wa aina mbali mbali. Wengine humwona mwenzao anafanya kosa. Badala ya kumwambia pale pale kijamaa kwamba atendalo ni kosa, watanyamaza kimya. Lakini hawanyamazi kabisa. Watakwenda kumteta katika vikundi vya siri. Mateto haya si ya kumsaidia mwenzao, ni ya kumdhuru. Hii ni aina moja ya fitina. Wengine hugawa watu katika mafungu. Fulani japo kafanya kosa kubwa sana hasemwi. Lakini Fulani wa pili akifanya kosa japo dogo, kosa lile hukuzwa likawa kama mlima Kilimanjaro. Hawa hutafuta sababu ya kumtetea Fulani wa kwanza, au za kumaulumu Fulani wa pili, ambazo hazifanani kabisa na ukweli. Kwa watu wa aina hii, ukweli ni jambo ambalo hutegemea mtu, si kitu kinachojitegemea chenyewe bila kujali mtu. Fulani wa kwanza akisema katika majadiliano kuwa mbili na mbili ni tano, wao watakubali. Lakini Fulani wa pili akisema sivyo, mbili na mbili ni nne, watamwona ni mtu mbaya kabisa ambaye hastahili hata kusikilizwa. Hawa hawajali ukweli, hujali nafsi tu. Kwao, ukweli ni maoni yao na matakwa yao. Hatuna budi, hasa katika majadiliano na mazungumzo yanayohusu jumuiya, tujifunze kusikiliza hoja zenyewe zinazotolewa na wenzetu, na kuzijibu zile hoja kwa kuzikubali au kuzikataa, bila kujali kama anaezitoa ni rafiki au si rafiki. Pia wanaopingwa hawana budi wakubali kuwa kinachopingwa ni zile hoja zao, sio wao wenyewe. Bila mazoea haya, mazungumzo hayana maana; yanakuwa ni kupoteza wakati, maana huwa tumekwisha kuzihukumu hoja za mtu hata kabla hajazitamka; kadhalika, hoja zetu zikijibiwa kwa kupingwa halafu tunawakasirikia waliozipinga tunafanya mazungumzo yasiwe na maana, kwa sababu tunapenda hoja zetu zikubaliwe tu hata kama si hoja safi.
Ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo; haujali adui wala rafiki. Kwake, watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa. Ukiniona nataka kulipiga teke jiwe kwa kuwa unafikiri kuwa ni dongo au mpira, natumaini utanionya. Lakini nikilipuuza onyo lako kwa sababu eti wewe ni mdogo au kwa sababu sikupendi, nikalipiga teke, basi litanivunja dole japo ningekuwa nani. Ukweli haupendi kupuuzwa.
Wakati mwingine, mtu tunayempinga huwa ana makosa kweli lakini hoja tunazozitoa ni za kinafsi na hazihusiani kabisa na hoja zake. Nikisema mbili na tatu ni sita, nakosa. Lakini ni bora kunionyesha kwamba pengine nafikiri tunazidisha kumbe tunajumlisha. Ni kweli mbili mara tatu ni sita; lakini mbili na tatu ni tano, siyo sit.a Lakini ukijaribu kuwashawishi wenzetu wakatae mawazo yangu na kukubali yako kwa kusema kuwa meno yangu ni machafu, au natoa kamasi daima, utakuwa unatumia hoja ambazo hazina maana. Huu ni mfano wa upuuzi; lakini mara nyingi hoja tunazotumia kuwashawishi watu wakatae mawazo ya wale tusiowapenda, au kukubali mawazo yetu, huwa hazihusiani kabisa na mambo tunayoyajadili.
Makosa yetu mengine hutokana na woga; woga unaotuzuia kumlaumu mkubwa japo tunajua kuwa kakosa, au unaotuzuia kumtetea mdogo anayelaumiwa na wakubwa japo tunajua hana makosa. Na msingi wa woga ni unafsi. Pengine huwa tunaogopa sisi wenyewe kulaumiwa au kupata hasara fulani. Pengine twaweza kuwa hatuna cheo chochote ambacho tunaogopa kupoteza; pengine huwa hatuna tamaa yoyote ya kupata cheo fulani. Lakini woga unaweza kutokana na tamaa ya kila binadamu kupendwa na binadamu wenzake. Sisi sote tunayo tama hii, au sivyo tusingekuwa binadamu. Woga huu huweza kumfanya mtu kuvumilia maovu, hasa kama maovu yale yanatendwa na walio wengi kwa walio wachache, au yanatendwa na wakubwa kwa wadogo. Kwa kuogopa kuwaudhi wengi tunawaacha watende makosa bila kuwasahihisha, wasije wakatuchukia. Huu ni unafsi mbaya sana Ni kweli kwamba demokrasi haiwezi kudumu ikiwa wachache watakubali matakwa ya wengi. Lakini matakwa ya wengi hujulikana katika majadiliano au mazungumzo wa wazi.
Kadhalika, matakwa ya wachache hujulikana katika majadiliano na mazungumzo. Bila wachache kusema wazi wazi matakwa yao, majadiliano hayana maana. Wakati mwingine, hata baada ya majadiliano, wachache japo wamekubali kutii uamuzi wa wengi wanaweza kuendelea kuamini kwamba mawazo yao ni sawa, na ya walio wengi yamepotoka. Demokrasi inawapa haki, na ukweli unawapa wajibu wa kuendeleza mawazo yao mpaka wengi waone kuwa ni ya kweli. Bila hivyo Maendeleo katika mawazo hayawezekani, kwani mara nyingi wazo zuri hutokana na mtu mmoja tu. Mwanzo laweza likapingwa, pengine kwa nguvu kabisa, na walio wengi, lakini hatimaye wengi hulikubali. Huu ndio msingi wa Maendeleo katika mawazo ya binadamu.
Makosa ni makosa na dhuluma ni dhuluma, japo watendao makosa hayo au dhuluma ile ni wakubwa au ni wengi. Chama kinachopenda ukweli na haki hakina budi kiwape wanachama wake uhuru na nafasi ya kusahihisha makosa na kuondoa dhuluma. Wanachama hawana budi waone kuwa ni wajibu wao kuutumia uhuru huo, na nafasi hiyo. Wanachama wasiotumia uhuru huo na nafasi hiyo, kwa sababu ya kuogopa kuchukiwa au kupoteza nafasi zao, wanafanya kosa kubwa la unafsi, ambalo ni adui wa haki na ukweli.
Kosa jingine linalotokana na unafsi tunalifanya wakati wa kuchagua viongozi. Wakati mwingine hufanywa na wanachama; wakati mwingine hufanywa na viongozi wenyewe, au wale wanaotaka uongozi. Nimesema mahali pengine kwamba viongozi wetu hawana budi watokane na WATU. Viongozi wa TANU hawana budi watokane na wanachama wa TANU wenyewe, bila hila, vitisho, rushwa, au ujanja wa aina yoyote. Lakini mara nyingi wanachama huchagua viongozi bila kufikiri kwa makini kama viongozi hao wanaiweza, au hawaiwezi, kazi wanayochaguliwa kufanya. Wanachama wetu watafanya makosa makuwa sana ikiwa watachagua viongozi wa ovyo tu. Hii ni jambo la hatari kwa demokrasi na chama chetu, na maadui wa TANU wanaweza kusema kwamba demokrasi haina maana kwa sababu haizai viongozi wanaoweza kazi zao. Hii ni kweli, maana wote twajua kwamba demokrasi inaweza kuchagua viongozi wazuri. Lakini ni wajibu wetu katika kuhifadhi demokrasi kuona inachagua viongozi ambao wanaziweza kazi zao. Kazi za kuchagua viongozi ni kazi ya wanachama wetu; lakini viongozi wetu wanaweza kusaidia kwa kuelezea wanachama wetu kwamba jambo la kuchagua viongozi ni kubwa sana. Haifai kuchagua kiongozi kwa sababu ni mjomba, au binamu au ana sauti au sura nzuri. Wala haifai kuacha kumchagua mtu kuwa kiongozi kwa sababu kama hizo. Jambo kubwa ni kuchagua kiongozi mwenye tabia nzuri na anayeiweza kazi. Hatuna budi tutii kanuni hii katika kuajiri wafanya kazi katika TANU au Serikalini. Hawa pia hawana budi wachaguliwe kwa sababu wanaiweza kazi wanayoajiriwa kufanya, na ni watu wenye tabia nzuri.
Kosa jingine ni kutojielimisha. Kanuni yetu moja inasema: Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu wote na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote. Wengi wetu hufikiri kuwa kujielimisha ni kwenda Kivukoni, au kupata nafasi kwenda kusoma katika nchi za nje. Wengine hufikiri kuwa kujielimisha ni kujua kusoma na kuandika. Hilo ni kosa, lakini sio kubwa kama la pili. Wengi wetu, hasa baadhi ya viongozi, hufikiri kuwa tunajua kila kitu na hatuna haja ya kujifunza jambo lolote zaidi. Mtaalamu mmoja wa zamani alisema kuwa mwanzo wa elimu ni kutambua kuwa haujui kitu.]
Mwalimu Nyerere, Tujisahihishe, kurasa 1- 4, May 1962.
-----
Maneno haya ya Mwalimu kwa kiasi kikubwa (sio chote) ni mwarubaini wa matatizo yanayokiyumbisha CCM na serikali yake. Ni tiba kwa matatizo kama vile:
Kama alivyoasa Baba wa taifa miaka ya nyuma, Viongozi wenye nia nzuri na Tanzania wasione CCM kama ni mama yao; Ni dhahiri kuna viongozi ndani ya CCM wenye nia ya dhati kuwakomboa maskini kimapinduzi kama inavyoainishwa ndani ya katiba ya Chama; lakini wengine wengi zaizi uongozi wao unasukumwa na fitina, unafiki, chuki, woga, na ubinafsi; Lakini iwapo viongozi wenye nia nzuri na taifa hili wanahisi wamefikia kikomo katika juhudi zao kukirudisha chama kuwa cha wakulima na wafanyakazi, ni muhimu kwa viongozi hao kuthubutu sasahivi kwa kuigawa CCM katika vipande viwili vinavyopishana kiitikadi. Hii sio dhambi, wanaoona ni dhambi lazima watakuwa na mapungufu katika fikra zao. Watakaothubutu watakumbukwa kwa ushujaa wao hata kama mwanzoni watabezwa na wachumia tumbo waliopo ndani ya CCM.
Kama kila mtu anakubaliana na hoja kwamba chama cha siasa kinaendeshwa na kuongozwa na itikadi, suala la CCM kugawanyika haliepukiki, sana sana ni suala la muda tu na la nani aanze zezi hilo maneno kama yale ya Spika Makinda kuwajibu wabunge kwamba anza wewe wanapotishia kwenda kinyume na msimamo wa serikali ya CCM bungeni ni ishara ya woga anaouzumgumzia Mwalimu. Vinginevyo kwa viongozi kubakia kwenye uongozi wa CCM isiyo na dira kwa miaka 20 (tangia azimio la Zanzibar 1992 la kuvunja azimio la arusha) ni ishara kwamba viongozi hao hawajali mustakabali wa chama na wanaowaongoza; wanajali zaidi matumbo yao kuliko wananchi kwani katika mazingira ya Azimio la Arusha Sambamba na Azimio la Zanzibar (1992) hakuna cha zaidi ya fitina, chuki na ubinafsi kwani chama hakina dira. Marehemu Kolimba alibezwa bila sababu. Na matokeo yake ni kwamba hata viongozi wa sasa mfano Nape huwa anaishia kubabaisha na majibu kila mara anapoulizwa CCM inafuata itikadi ipi. Mbaya zaidi, majibu kwamba ni Ujamaa na kujitegemea ni ya kupotosha umma. Hili ni tatizo kubwa sana kwa Chama kuliko ufisadi kwani ufisadi ni uzao wa Azimio la Zanzbar. Na ni bora ufisadi ukapewa jina lingine vinginevyo kwa ruksa ya Azimio La Zanzibar, wapo wengi watakaoitwa mafisadi kwa makosa kwa sababu tu wametumia fursa rasmi ya azimio la Zanzibar kujitafutia riziki wakati wengine wamekosa nafasi kutumia fursa hiyo; sina maana kwamba nahalalisha azimio la Zanzibar au suala la kujilimbikizia mali ovyo kwa kutumia madaraka vibaya, bali naelezea ujinga wetu wa CCM ambao unapelekea chama kuongozwa kwa fitina, wivu, woga na unafiki. Azimio la Arusha lilikataza viongozi kuwa na mishahara miwili, nyumba ya (za) kupanga na kuwa na hisa katika makampuni binafsi; azimio la Zanzibar liliruhusu hayo yote rasmi bila ya mipaka; Ni kiongozi gani wa CCM hivi sasa ambae hana angalau moja ya hayo juu yaliyoruhusiwa na Azimio la Zanzibar? Mgombea urais yupi wa CCM ambae mwaka 2015 hatokuwa na angalau moja wapo ya hayo hapo juu? Lowassa? Membe? Magufuli? Pinda? Migiro? Mwakyembe? Mwandosya? Sitta? Ngeleja? Nimeishiwa majina, tafadhali nisaidieni.
Muda umetupa mkono, CCM Tujisahihishe au Tuvunje chama ili upande mmoja urudie mambo mazuri ya azimio la Arusha na upande mwingine uendelee na Azimio la Zanzibar kama lilivyo. Kwanini mbadala ni kujisahihisha au kuvunja chama? Ni kwa sababu sera za Chadema hazina tofauti na za CCM juu ya nini kila chama kinataka kuwafanyia watanzania, ilani zao zote za uchaguzi mkuu uliopita mengi yalikuwa ni yale yale, tofauti kubwa ni kwamba ya Chadema ilitawaliwa na mambo matatu Ufisadi, Ufisadi, na Ufisadi, - jambo ambalo katika mwongozo wetu CCM 1981, tunalizungumzia vizuri sana; mfano mwingine ni kwamba suala la elimu bure tokea msingi hadi Chuo Kikuu ambalo lilikipa CDM mvuto sana ni suala ambalo CCM ililifanya kwa miaka mingi sana chini ya Nyerere na kutofanikiwa hali ambayo ilipelekea hata muasisi wa Chadema Mzee Mtei kuona Sera za Mwalimu zilikuwa mbovu na hivyo kujiuzulu na kupewa kazi na IMF kama pongezi.
Labda kama Chadema watabadilika au kama vyama vingine vya upinzani vitakuja na mpango wa kweli wa kuwakomboa watanzania; vinginevyo ule unaotegemea kupakatana na IMF na WorldBank ambao hata mwalimu Nyereer aliukataa kwa hoja zilizo wazi kabisa kuelewa, hautafanya Chadema kuwa tofauti wakichukua uongozi; Ndio maana kwa waelewa wengi, hadi hivi sasa, hakuna mbadala wa kweli kwa CCM kisera, mbadala uliopo ni ule wa kuweza kupata ubunge na udiwani kwa urahisi zaidi mfano ukihamia Chadema; Vinginevyo ndio maana nje ya hoja ya ufisadi na katiba mpya, pamoja na umakini wao na mafanikio yao katika maeneo kadhaa ya hoja ambayo kwa kweli yanayostahili pongezi, Chadema haina hoja za msingi mbele ya umma kwanini Tanzania maskini kwani hata Mzee Mtei akiamua kuwa mkweli juu ya hili, lazima atakubali kwamba kushiriki kwake kuwaruhusu IMF na WorldBank kiholela ilikuwa ni grave mistake na ndio msingi wa matatizo yetu leo; sio siasa ya ujamaa pekee;
CCM, Tujisahihishe au tuvunje chama ili kuwapa fursa wale walio na mapenzi bado na CCM kuyachukua mazuri ya chama chetu na kuyapa meno ili kuyatumia kikamilifu katika siasa hizi za ushindani. Changamoto iliyopo iwapo CCM itavunjika, ni who will choose the right side of history and who will choose the wrong side of history; vinginevyo mpaka tutakapofikia huko, tutazidi kuwindwa na maneno kama ya Spika Makinda ya Anza Wewe.

- Matatizo katika mchakato wa katiba mpya;
- Sakata la Kujivua Gamba;
- Uteuzi wa kidugu katika nafasi za chama na serikali;
- Mbio za urais 2015 (CCM);
- Utumishi mbovu wa umma na utendaji mbovu unaopelekea matatizo kama ya sakata la Luhanjo na Jairo;
- Uwepo wa baadhi ya wabunge wa CCM bungeni wenye tabia ya kuunga hoja hata kama hazina maslahi ya taifa, pengine kutokana aidha na upeo wao mdogo, udhaifu/uvivu wao wa kufikiri au unafiki na ubinafsi wao;
- Unafiki na ubinafsi wa baadhi ya wajumbe wa NEC & CC ya CCM na hivyo kukisindikiza chama kaburini.