CCM: Tujisahihishe au Tugawane Chama

Nashuhudia mkiweweseka.Leo ndio mnamkumbuka Mwl, tena kwa njia ya kuweweseka kiasi hicho!! Poleni maana kumekucha nanyi bado mko kwenye lepe la usingizi.Watanzania, wamewaacha kama mwanamke mzinzi, mmejaa soni. Mmebaki kuwashikia na kuwaelekezea mitutu ya bunduki na mabomu ya machozi.Hata wakati tunaelewa nchi yetu ni muflisi, jambo mnalolijuwa ni kuongeza magari ya deraya ya polisi ili kuwafunga midomo wananchi, na kununua mitambo ya kijasusi kuwadhibiti wananchi wenu!!
Leo adui wa ccm si ujinga, maradhi na umaskini ila adui mkubwa wa ccm ni wananchi waliowachoka kwa vile mmeshindwa kuongoza na sasa mnataka kutawala. Hatutaki kwa maneno, hatutaki kwa silaha. Sisi ni watu huru.Down with ukoloni mweusi wa ccm.
Kumekucha!!
Unakiri kwamba CDM inaweza kushika uongozi wa nchi.Wananchi wanajuwa hilo hata bila ya nyinyi kukubali.Lakini, acheni kuwapangia CDM sera, siyo kazi yenu.Ondokeni salama. Tanzania itasimama tena.
Wakati anafariki London, Mwl alisema "Najuwa nitakufa,Watanzania mtanililia sana, lakini naenda kuwaombea" Haijawahi kutokea mtu akayasema haya akaribiapo kufa.
Kwa vile hamkujuwa Mwl mmefika hapo mlipo,kurarurana hadharani kama mbwa mwitu. La ajabu mnakwenda kaburini kwake sijui kutambika? Mwl alikuwa mcha Mungu.Hakuna kujikosoa, maana mmechafuka mno.Magamba you are cursed!!! Mlipowapokea waliolaaniwa na Mwl leo yamewafika. Yule aliyelaaniwa na MWL ndiye chanzo cha kuanguka ccm.Mlifikiri mna hekima na busara kuliko Mwl haya sasa jiokoeni tuwaone. Kwishnei!
Kwa heri ya kuonana mwaka 2015.
 
Mkuu mchambuzi umenena maneno mazito na mwenye macho asome aelewe. Nchi yetu inahitaji mabadiliko makubwa ya kiitikadi na kisera. Vyama vyetu vya siasa vyote vimejaa wasaka tonge sijaona Chama makini chenye nia ya dhati ya kuleta ukombozi wa pili katika nchi yetu. CCM inahangaika na ufisadi eti inawamulika watu watatu tu!! Sijui kama hao wakiondoka maisha ya watanzania yataboreka. Tutafute kiini cha tatizo. Nadhani Mwenyekiti wa CCM aliposema kujivua gamba hakuwa na maana finyu kama ambavyo wanataka kutuaminisha. Nadhani alikuwa na maana pana ya kufanya mabadiliko makubwa ndani ya CCM kama dhana kamili ya nyoka kujivua gamba.

Jamani CCM isipoangalia itakuwa kama KANU, UPC, MPC, UNIP, nk.

Nakubaliana na wewe; Mwenyekiti taifa - Kikwete alipokuja na wazo la kujivua gamba, ni jambo lisilo na ubishi kwamba alilenga suala la party’s rebirth kwa ujumla, na kama mafisadi kwa njia ya ushahidi wapo, vikao vingefanyia kazi suala hilo kwa utaratibu uliopo; lakini kwa sababu mwenyekiti ni msimamizi tu wa shughuli zote za chama na sio mtendaji, suala la gamba likawa spinned na makundi mawili ambayo ni wazi yamemwelemea Kikwete kwani wao ndio ndio party machinery - kwani hawa ndio watendaji na watekelezaji wa maamuzi ya vikao; sina maana kwamba suala la ufisadi lisipewe uzito, ila suala nalozungumza hapa ni kwamba inakuwaje miaka ya nyuma masuala yote ya ufisadi na yale ambayo yalionekana ni ya kuasi chama yalikuwa yanashughulikia kimya kimya na vikao maalum bila kuharibu hali ya hewa ya nchi na kuwapotezea wananchi muda? Mfano, tuliona jinsi gani Mzee Jumbe na Seif Sherrif walishughulikiwa kwa kuonekana waasiwa CCM; na ndani ya mfumo wa vyama vingi, tumeona jinsi gani kina Kiula, Mramba, Yona wameshughulikiwa na CCM na serikali yake; Tujiulize, kwanini mapambano dhidi ya Yona na Mramba hayakuwa majukwaani na badala yake yalikuwa kwenye vikao na matokeo yake tumeyaona – watuhumiwa kupelekwa mbele ya vyombo vya sheria kujibu hoja huku Chama kikiendelea na shughuli zake nyingine bila bugudha? Watuhumiwa ufisadi wa sasahivi wana tofauti gani mpaka vita dhidi yao ziende majukwaani na sio vikao maalum? Kuna nini hapa?? Kwa hili Nape amekosea na kama atapewa adhabu au kuteuliwa ubunge, au ubalozi ili aachie nafasi yake ya sasa, anastahili; kwani kama kweli wanaotajwa kwa ufisadi wana tuhuma za kujibu, njia iliyotumiwa Nape na wenzake ya kupeleka vita hivi majukwaani badala ya kwenye vikao, kama kweli walikuwa na tuhuma za kujibu, basi ndio wamepona kwani tafsiri ya wengi hivi sasa juu ya Nape na wenzake kukiuka taratibu inawapa hisia wengi kuangalia hili suala kama ni la visasi, fitina, chuki, na ubinafsi zaidi ya kitu kingine chochote; inawezekana Nape na wenzake walikuwa na nia safi, lakini kukiuka taratibu za chama juu ya hili ndio kimewaokoa watuhumiwa - 'kama walikuwa na kesi ya kujibu'

Vinginevyo Nape angerudia his job description:

  1. Kusimamia, kueneza na kufafanua masuala yote ya itikadi, siasa na sera kitaifa;
  2. Kupanga na kusimamia mafunzo na maandalizi ya makada na wanachama kitaifa;
  3. Kufuatilia utekelezaji wa sera za chama za kijamii na ilani za uchaguzi wa CCM;
  4. Kudumisha uhusiano mzuri na vyombo vya habari na kuwa na mipango ya mawasiliano na uhamasishaji wa umma kwa jumla;
  5. Kufuatilia hali ya siasa;
  6. Kufuatilia mwenendo wa jumuiya za kijamii;
Mengine nje ya haya angeshiriki kwa nafasi yake kwenye vikao au kamati; ila asisahau kwamba ufisadi mama yake ni Azimio la Zanzibar ambalo liliruhusu viongozi kuwa na mshahara zaidi ya mmoja, nyumba ya (za) kupanga, na kuwa na hisa katika makampuni binafsi, bila ya mipaka maalum; ndio maana nasisitiza tugawane chama ili wa azimio la Zanzibar wachague upande wao na sisi wengine wa azimio la Arusha tuchue upande wetu, tulifanyie marekebisho kidogo na pia tuchukue mwongozo wetu wa chama wa 1981 tusonge mbele; hakika huu utakuwa ni ushujaa; nipo tayari kuthubutu na kuwa mwanachama wa kwanza wa kambi hii;
 
Nashuhudia mkiweweseka.Leo ndio mnamkumbuka Mwl, tena kwa njia ya kuweweseka kiasi hicho!! Poleni maana kumekucha nanyi bado mko kwenye lepe la usingizi.Watanzania, wamewaacha kama mwanamke mzinzi, mmejaa soni. Mmebaki kuwashikia na kuwaelekezea mitutu ya bunduki na mabomu ya machozi.Hata wakati tunaelewa nchi yetu ni muflisi, jambo mnalolijuwa ni kuongeza magari ya deraya ya polisi ili kuwafunga midomo wananchi, na kununua mitambo ya kijasusi kuwadhibiti wananchi wenu!!
Leo adui wa ccm si ujinga, maradhi na umaskini ila adui mkubwa wa ccm ni wananchi waliowachoka kwa vile mmeshindwa kuongoza na sasa mnataka kutawala. Hatutaki kwa maneno, hatutaki kwa silaha. Sisi ni watu huru.Down with ukoloni mweusi wa ccm.
Kumekucha!!
Unakiri kwamba CDM inaweza kushika uongozi wa nchi.Wananchi wanajuwa hilo hata bila ya nyinyi kukubali.Lakini, acheni kuwapangia CDM sera, siyo kazi yenu.Ondokeni salama. Tanzania itasimama tena.
Wakati anafariki London, Mwl alisema "Najuwa nitakufa,Watanzania mtanililia sana, lakini naenda kuwaombea" Haijawahi kutokea mtu akayasema haya akaribiapo kufa.
Kwa vile hamkujuwa Mwl mmefika hapo mlipo,kurarurana hadharani kama mbwa mwitu. La ajabu mnakwenda kaburini kwake sijui kutambika? Mwl alikuwa mcha Mungu.Hakuna kujikosoa, maana mmechafuka mno.Magamba you are cursed!!! Mlipowapokea waliolaaniwa na Mwl leo yamewafika. Yule aliyelaaniwa na MWL ndiye chanzo cha kuanguka ccm.Mlifikiri mna hekima na busara kuliko Mwl haya sasa jiokoeni tuwaone. Kwishnei!
Kwa heri ya kuonana mwaka 2015.

Una hoja nzuri, ila ningependa kujua je, unaongea na mimi kama mwanachama wa CCM au mmoja wa Viongozi wanaosimamia dira, sera na itikadi?

Kuhusu kupangia CDM sera, kikubwa ni wewe kuelewa mantiki ya ujumbe wangu juu ya kwanini CCM na CDM bado hawana itikadi practical , implementable and sustainable kumwokoa mtanzania na nimeeleza kwanini nasema hivyo;
 
Wana CCM siyo watu wa kuamini,siku MCHAMBUZI akipewa madaraka utayaamini maneno yangu! Wakiwa nje ya madaraka ni wana mawazo mazuri,subiri wapate kautawala...!

Tatizo la CCM linaanziia kwenye itikadi ya chama kushika hatamu; chama kikishika hatamu matokeo yake ni kila jambo kuamuliwa kisiasa bila kunagalia madhara ya muda mrefu. Ukitaka kujua siasa/chama ndicho kilichoshika hatamu angalia nguvu ya uchumi inashikiliwa na nani? Wakiamua kupandisha posho hakuna wakuwaambia huwezi kula usichokipanda. Utaongezaje posho wakati 30%? ya mapato yanapotea bila maelezo? Kwamaana nyingine nikuwa kwakuwa bunge halifanyi kazi yake vizuri ya kuisimamia serikali ndiyo maana haya yanatokea ambayo hasa ndicho out put ya bunge kwenye uchumi wa nchi. Sasa wnapoongeza wanatoa wapi hiyo pesa? Wataalamu wao kila siku hadith ndiyo inatawala na wale wanaopiga soga na kuhesabu kilichopatikana (Social/humanities) ndiyo wenye dau kubwa huku wazalishaji (wakulima na wana science) wakiambulia ahadi hewa kwakuwa hawajui kupiga kelele zaidi ya kunyanyua majembe na vyuma kuleta goods and services kwenye market.

Ondoa siasa kwenye mambo yakitendaji ibakie kwenye maamuzi tu alafu futa mambo ya kupewa mishahara kwenye siasa zaidi ya posho wakati wa vikao (maana ndiyo kazi yao) kuamua kipi kifanyike kati ya menu waliyoandaliwa na wazalishaji uone kama siasa safi haitapatikana. Ondoa wanasiasa wote kwenye ngazi ya utendaji na mtu kuweka sheria kwa wale wote wanao husika na haki pamoja na ulinzi kutojihusisha na siasa hata baadaya ya kuacha kazi zao mpaka muhula mmoja wa uongozi upite uone hapo mambo kama hayajawa fiti.

Hii model ya uongozi ni yakikoloni nayo iliwekwa ilikudhibiti raia na siyo raia kujiendeshea mambo yao kwa maelewano.
 
Kama mchambuzi utasimamia hapa na kuwaeleza wazi ndani ya CCM, nakupa hongera

Nashukuru; ila sidhani kama ni lazima kufanikisha hilo ndani ya vikao; isitoshe mimi ni mwanachama wa kawaida, sio kiongozi, na hii inanipa mwanya mzuri zaidi kukaa na vijana wenzangu vijiweni, humu JF kama wapo wenye mapenzi na CCM na sehemu nyingine nyingi kupeana mawazo na pia kuhamasishana juu ya mustakabali wa nchi yetu kupitia chama chetu hiki hiki ila kwa mtazamo wa kukigawa chama; vinginevyo kufanya haya ndani ya vikao ni kuendeleza yale yale ya fitina, chuki, ubinafsi; na mtu utaishia kulishwa sumu kama alivyowahi onya Mwenyekiti wa CCM Kikwete kwamba hali imefikia huko; alternative to that kama moyo wako si wa kizalendo bali moyo unaotumwa na tumbo, hakuna shaka kwamba utaishia kununuliwa na kambi zinazosaka Urais 2015;
 
Timbilimu,
ulinena jambo la maana sana kwamba:
"Wana CCM siyo watu wa kuamini,siku MCHAMBUZI akipewa madaraka utayaamini maneno yangu! Wakiwa nje ya madaraka ni wana mawazo mazuri,subiri wapate kautawala...!"

Nazielewa hisia zako kwani historia inatoa ushahidi juu ya yote haya unayozungumza; ila Timbilu, naomba uweke reservation kidogo ndani yako kwamba kuna watu ambao hawawezi kuvumilia upuuzi huu wa kushabikia Chama kisicho na itikadi, bora kiwe na itikadi inayoeleweka na tatizo libakie utekelezaji; inasikitisha mtu kama Nape akienda kwenye vikao vya UVCCM wanampokea kwa kauli zao mbiu 'Kauli yetu ni kuilinda siasa ya ujamaa na kujitegemea' na nape kutoa tabasamu linaloambatana na makofi; ni upuuzi kama huu ambao nikipata hata nafasi ya kuongoza tawi nitatoa elimu kwa vijana wenzangu kwamba tubadilike; inasikitisha kuona wazee wetu huko kwenye matawi ambapo ndiko roho ya chama ilipo kwani wanachama wapo matawini, sio kata, wilaya au mikoa; inasikitisha unawaona wenyeviti na makatibu wamebeba katika za chama chao, katiba ambayo imepitwa na wakati; wamebeba azimio la arusha, azimio ambalo halipo tena; wanabeba mwongozo wa 1981, mwongozo ambao sehemu zake nyingi zilmeshatupwa; unabaki kujiuliza, hivi inahitaji nini kufikia kiwango cha sisi kuitwa wendawazimu? Wazee wa watu huko matawini wakiwa kama wenyeviti, makatibu, hata hawajui kwamba kuna azimio la zanzibar, wao wanajua azimio la Arusha, Iringa (juu ya elimu) na Musoma (Kilimo); this is a disgrace and it is what i am ready to fight for - kuwapa wanachama wa ccm elimu ya kweli ili wachague upande;
 
Mkuu naona ulistahili kupata fursa kwenye mkutano wa NEC-CCM ili uwasilishe hii makala yako kwa wajumbe kabla ya mkutano wao labda wangekuelewa.

Mapinduzi ya kweli ya Chama Chetu Cha Mapinduzi Ndani ya NEC - CCM HAYAWEZEKANI.
 
Ulikuwa wapi MCHAMBUZI siku zote hizo mpaka chama kimebaki makapi?
Tunataka watu wa aina yako kwa kipindi hiki kigumu.

Miaka minne iliyopita, msimamo wangu ulikuwa kwamba Mwalimu Nyerere alitujengea nchi yetu kwa usatadi sana kisiasa na kijamii lakini aliboronga kwenye suala la uchumi; leo hii nakiri kwamba nilikosea sana kuwa na mtazamo huo, nilidhani naelewa kila kitu lakini haikuwa kweli. na ni maneno ya huyo huyo baba wa taifa mwalimu nyerere yaliyoniamsha - katika kitabu chake cha tujisahihishe anasema: “mwanzo wa elimu ni kutambua kuwa haujui kitu.”

Pia nimekuwa nafuatilia maendeleo ya nchi yetu kiuchumi tangia Mzee Mtei ajiuzulu kwa kutokubaliana na sera za Mwalimu na baadae kwenda jiunga na IMF kikazi Washington ambako alikuwa anasimamia package za sera za mageuzi ya kiuchumi Tanzania; nini imekuwa matokeo yake miaka 25 baadae? alirudi, akatuletea Chadema, chama muhimu sana katika siasa za nchi hii kwani CCM imeanza kuwa na discipline, lakini nje ya hapo, hali ya uchumi wa wanavijiji tanzania tokea 1967 - 1985 na uchumi wa Mzee Mtei na IMF wa 1985 - 2011 tofauti kubwa ni nini? Tazama IMF/WorldBank wanavyokazana kurudisha mambo ya Mwalimu - serikali kujikita katika kutoa huduma za kijamii n.k kwani hata suala la shule za kata halikubuniwa na wanasiasa wetu, huo ulikuwa mpango uliokuwa endorsed na IMF/WorldBank; isitoshe, elimu bure tokea msingi hadi chuo kikuu mwalimu alifanya hivyo kwa miaka mingi sana lakini ikashindikana na ni moja ya sababu za mzee mtei kukimbia serikali ya mwalimu kwa hoja kwamba sera zake ni mbovu na hazimsaidii mtanzania; je, katika ilani ya uchaguzi ya mwaka jana ya Chadema juu ya elimu bure msingi hadi chuo kikuu, mzee mtei alishiriki katika mpango huo? i remain to wonder.

Technician mimi ni mwanachama wa kawaida, na pia my assumption ni kwamba wewe pia ni hivyo hivyo; tuna nafasi nzuri zaidi ya kutatua mgogoro wa chama chetu tukiwa nje ya chama kwani hauitaji uongozi kufanya hayo, kikubwa ni kuwapa wanachama na viongozi wa chini elimu ya nini kinatokea, huko huko tunapokunywa nao kahawa na kashata na kucheza bao;
 
Nafikiri kuna a clear ideological divide katika CCM haswa baada ya wanamtandao kusweep into power.....Kuna wale wanaotaka mazuri ya mwalimu yarejeshwe haswa katima maadili ya uongozi (siasa na biashara nk) hawa naweza kuwaita NEO-CONSERVATIVES na kuna wale walionufaika sana sana na kujilmbikizia mali au wenye uroho wa mali na madaraka na hawataki kitu kubadilika ikiwemo mfumo huu wa kifisadi ulioanza muda wa mwinyi na kuimarika muda wa MKapa hawa naweza kuwaita ni STATUS-QUO...kitu kibaya wote wana fikiri wakijitoa ndani ya chama nguvu zao zitapungua au kuzimwa (mfano wa Mrema) na hii inakipa shida chama sasa...nakubaliana na wewe CDM siyo mbadili wa CCM, wapizani wa kweli watatoka humo humo CCM, (kumbuka Maalima seif na Dr SLaa)

NEO - CONSERVATIVES, i like that; swali langu kwako, je njia sahihi ya kutoa chama cha upinzani toka ndani ya CCM ni top - down kwa maana ya kusubiri wanasiasa kadhaa wajiengue halafu wanachama waanze kujiunga taratibu au njia sahihi ni bottom - up kwa maana wanachama waanze kudai chama chao mbadala then viongozi waanze kufurika huko; nini mtazamo wako katika hili;
 
Mchambuzi hayo unayonena ni kweli lkn yamenenwa sana na watu wengi tuu,nakubaliana na wewe kuwa hata CDM waliowengi wakubwa kwa vijana waliopo madarakanai hawana utashi wa kweli kuleta maendeleo katika nchi hii (I mean non political statistical development). Nashnagaa hata wazee wa CCM wanashindwa kutukemea viongozi waliopo madarakani, yupo wapi Mkapa,Mwinyi,Salim,Warioba,Malecela, na hata Mh. Kikwete...Utasikia wanaogopa kutoa maelekezo makali kwa viongozi wetu wanaoabudu matumbo yao shv eti kwasababu nao wamefanya madhabi...that is not true na hata kama wanaogopa hilo basi nashindwa kuelewa..kwani baba yako akifanya makosa ndio hatakiwi kukuelekeza we mwanaye njia sahihi ya kupita??kufanya makoso ndio experience hiyo wanayotakiwa ku share na kurekebisha mwenendo wa viongozi wetu. Baba wa taifa mbona alisema kuna makosa aliyatenda kwenye uongozi wake lkn bado alikemea sana maovu ndani ya chama na nchi wakati wa uhai wake...iwe vp wazee wetu waliobaki kutofanya hivyo? Anyway hata Nyerere akiwa kijana alipambana na mkoloni Mzungu na na hata watawala machifu waafrica...so my take...tuache kulalalama na kuongea sana desturi ya Tanzania ni hiyo na CDM nao ndio vivyo hivyo maneno mengii tu ndo maana bado naamini CCM yenye mabadiliko ndio nuru ya taifa letu...tudiscuss nini cha kufanya sio kulalama na kuandika kasoro sasa wewe kama kijana wa CCM mwenye mawazo mbadala what should be our way forward??????/

Nipo tayari kuwa mwanachama wa kwanza wa chama mbadala cha CCM kitakachotokana na CCM ya sasa; our way forward ni sisi kuanza kuji organize kwa hilo popote tulipo na kuanza kuwapatia wanachama wenzetu (maana sisi sio viongozi, which gives us more leverage) kuwapatia elimu juu ya haya tunayoyazungumza; suala la kuangalia hapa ni kwamba CCM splitting is not only inevitable but also desirable at this juncture; tatizo lililopo ni woga ambao unatawaliwa na siasa za "anza wewe" - kwa maoni yako, ikiwa tunakubaliana na hoja kwamba CCM splitting kiitikadi na baadae kuwa vyama viwili is inevitable, je tufuate a top - down approach - yani kusubiria vigogo kadhaa waanze kuchomoka na kuhamia upande wa pili then tujiunge nao au tufuate a bottom - up approach ambapo elimu kwa wanachama itawapelekea wao ku demand chama kimeguke kiitikadi and then uchaguzi wa viongozi ndio ufuate?

Njia zote zina faida:
kama tutaamua kusubiri a top - bottom approach, kiongozi yoyote wa CCM ya sasa, sanasana Mwenyekiti Kikwete akifanya uamuzi mgumu wa kuachia chama kigawanyike, daima atakumbukwa na vizazi vya nchi hii kwa kuokoa taifa letu;

kama tukiamua kufuata a bottom - up approach, chama kipya kitakuwa ni chama cha watu kwani chama chochote cha kweli ni kile kinachotokana na watu, sio mtu mmoja mmoja;

Lakini ni matumaini yangu swali lako juu ya way forward halitokani na wewe kuwa kazini humu JF kupima joto na kupeleka taarifa huko kunakohusika; niwie radhi kama sipo sahihi;
 
Nimekupata Mchambuzi...!na way fprward yako umeichangnua vizuri,kwanza nikupe chanzo cha kuuliza swali hilo...ni kuwa Tanzania tumekuwa watu wa kuongea muno na kuchambua sana kuanzia wananchi hadi viongozi kwa kutafuta ujiko,tena siku hizi wamekuwa magwijiwa kijitangaza kuwa wanauwezo,akili na kipaji cha kuongoza...wawe wa chama tawala na wa upinzani wote tu.Wapi bana fanya kazi watu waone unauwezo na akili sio kujitangaza tuu mwalimu hakujitangaza lkn leo tunamuita baba wa Taifa. Nikupe mfano wakitu kimoja siku hizi kiongozi akikosea na akisemwa tena vijana Utasikia "ni wivu tu" Sasa yaani we uvurunde alafu uwambie watu ni wivu na wakae kimya???kwahiyo usiwajibike kuleta maendeleo kwakua unajua wakisema ni wivu?this cant be tolerated for reasonable men surely. Nije kwenye hoja yako ya kuelimisha..ndio kuelimisha ni sawa lkn kaka shv watu wameshaelimika naweza sema vya kutosha au basically hey know what is going on...!sasa lazima elimu iwe sambamba na plan za kurekebisha yanayoelimishwa...Kama unavyoshauri kuwa na vipande au kujisafisha CCM kwa top-bottom approach ulivyoainisha lkn bila kuanza kwa vijana wenye muono kama wako ku act sio kunena tu bali ku act itakua kazi bure.Anyway mie nafikiri tusubiri 2012 kwenye kikao chetu cha NEC mwenendo na mambo yatakayoenda ndio iwe mwanzo wa what next...kama kutakuwa na dhamira ya dhati kuwapa wenywe uwezo kuongoza bali hali itakuwa swali lkn kama ni kupangana kwa ajili ya future fruits basi..nadhani utakubaliana na mie kuwa that can be your right time kuwa na CCM asili na kampuni kama mgogoro wa yanga na simba miaka ya nyuma. LKN naamina asili wakiwa very strategic then watafanikiwa regardless of how poor they are because umma shv unaelewa what is happening.
 
CDM ni chama makini na kinaweza kutuongoza tukaondokana na ufisadi huu ambo CCM imeujenga kuanzia kwenye uongozi wa Mwinyi, Mkapa, na Kikwete sasa ambapo UFISADI ndo umezidi sana.
Mpaka imefikia wananchi wanaomba rais ajiudhuru tu.

Tunatakiwa tupate Nyerere wa pili ambaye kwa sasa katika nchi yetu Dr. Slaa ndiye anaweza kuwa Nyerere wetu wa pili.
Alijitolea kupinga UFISADI kwa nguvu zake zote na pale alipoanzisha hoja ya MAFISADI WA EPA pale Bungeni wabunge karibia wote wa ccm walimzomea. Na aliposhauri EPA iundiwe kamati ya bunge Spika alikataa.

Pia alishawahi kuwataja MAFISADI WAKUBWA wanaoitafuna nchi pale Mwembeyanga bila kuogopa na Mkuu wa kaya naye alikuwemo kwenye hiyo listi (List of shame). Hawa mafisadi waluotajwa tunaona kwa sasa ndio wanaitafuna nchi na wametusababishia umaskini mkubwa sana wakati nchi yetu ni kati ya nchi tano tajiri barani Afrika.
 
Mchambuzi,

..nadhani hujamtendea haki Mzee Mtei kuhusu mchango wake ktk kushulikia matatizo ya uchumi tuliyokuwa tukikabiliana nayo miaka ya themanini.

..kumbuka kwamba ni Mtei huyohuyo alikuwa waziri wa fedha wa Mwalimu Nyerere during the "old good days", era ambayo unasema wakulima walikuwa na hali nzuri.

..nchi ilikuwa kwenye some serious economic problems. haya siyo mambo ya kuyasoma kwenye mabuku na maripoti. ungekuwa na umri mkubwa wa ku-experience jinsi uchumi wetu ulivyo-shrink wakati ule usingekuwa hapa ukimlaumu Mtei kwa kutoa ushauri alioutoa.

..matatizo yale yangeendelea kuna uwezekano kabisa yangetokea machafuko nchini. Hali ilishaanza kujionyesha kidogo kidogo ambapo wananchi walishaanza kuchoshwa na hali ile na kuna uwezekano kabisa wangechukua hatua. nakumbusha jaribio la kina Hatty McGhee[Hatibu Gandhi], Mohamed Tamimu, Eugene Maganga, etc la kutaka kupindua serikali ya Mwalimu.

..kila alichojaribu Mwalimu Nyerere kilishindikana na ilichobakia ilikuwa ni kukubaliana na IMF/WB ili kunusuru kidogo tulichokuwa tumebakia nacho.

..sasa hivi uchumi wetu una matatizo lakini huwezi kuyalinganisha na yale ya mwaka 1982--1986. matatizo tuliyonayo sasa tunaweza kuya-manage sisi wenyewe ikiwa tutajipanga vizuri, yale ya wakati ule yalihitaji MISAADA toka nje. ukinishikia bunduki kichwani ukaniambia nichague kuishi ktk matatizo ya miaka 80 au haya ya sasa hivi i would choose haya ya sasa hivi.

NB:

..nakushauri usome kitabu cha maisha ya Mzee Mtei. Yapo mambo mengi sana ameyaeleza mle ndani. kuna crisis zaidi ya moja ambazo alipambana nazo akiwa waziri wa fedha chini ya Mwalimu Nyerere.

..Mzee Mtei alikwenda kufanya kazi IMF kwa mapendekezo na baraka za serikali ya Tanzania wakati huo ikiongozwa na Mwalimu Nyerere. Ilikuwa zamu ya Tanzania kuongoza idara ya Afrika IMF na Mwalimu akampendekeza Edwin Mtei. majuzi nafasi hiyo ilijitokeza tena na Raisi Mkapa akampendekeza Mzee Peter Ngumbulu.

..akiwa IMF Mtei alikuwa akifanya kazi kwa karibu na viongozi wa Tanzania kama Mwalimu Nyerere, Edward Sokoine, Mzee Alhaj Ali Mwinyi, Mzee Joseph Warioba, Mzee Cleopa Msuya etc etc.

..alipomaliza mkataba wake na IMF, Mzee Mtei aliongoza Tume ya serikali ya kurekebisha mfumo wa ukusanyaji kodi nchi. Ripoti ya Tume hiyo na mapendekezo yake ndiyo iliyopelekea kuanzishwa kwa TRA.
 
@mtambuzi

Ukiondoa fikra za mwalimu nyerere utakuwa na akili lakini zaidi ya hapo ni wimbo tu..

Fikra za mwalimu hazina nafasi kwenye chama chetu kwa sasa...

Tuondoe mafisadi..na kuwepo na uwajibikaji kwenye chama na serikali (mwanachama aliyeko serikali akikosea apigwe chini)

Kuvua gamba litaondoka na wengi wewe subiri utaona..
 
CDM ni chama makini na kinaweza kutuongoza tukaondokana na ufisadi huu ambo CCM imeujenga kuanzia kwenye uongozi wa Mwinyi, Mkapa, na Kikwete sasa ambapo UFISADI ndo umezidi sana.
Mpaka imefikia wananchi wanaomba rais ajiudhuru tu.

Tunatakiwa tupate Nyerere wa pili ambaye kwa sasa katika nchi yetu Dr. Slaa ndiye anaweza kuwa Nyerere wetu wa pili.
Alijitolea kupinga UFISADI kwa nguvu zake zote na pale alipoanzisha hoja ya MAFISADI WA EPA pale Bungeni wabunge karibia wote wa ccm walimzomea. Na aliposhauri EPA iundiwe kamati ya bunge Spika alikataa.

Pia alishawahi kuwataja MAFISADI WAKUBWA wanaoitafuna nchi pale Mwembeyanga bila kuogopa na Mkuu wa kaya naye alikuwemo kwenye hiyo listi (List of shame). Hawa mafisadi waluotajwa tunaona kwa sasa ndio wanaitafuna nchi na wametusababishia umaskini mkubwa sana wakati nchi yetu ni kati ya nchi tano tajiri barani Afrika.
Kilichojenga ufisadi sio uongozi wa Mkapa, mwinyi, Kikwete; mzazi wa ufisadi ni IMF/Worldbank ambao waziwazi waliona Ujamaa sio njia sahihi kwa nchi yetu; nah ii ikapelekea azimio la Zanzibar kuzaliwa mwaka 1992; IMF/WorldBank walikuja kuwa maadui wakubwa wa Ujamaa, na hii ikapelekea vibaraka wengi wa ubeberu na ubepari humu nchini kupata mianya ya kuzidi kunyonya wachache, tena kwa Baraka zote IMF/WorldBank; Mzee Mtei, aidha kwa kujua au kutojua, ana mkono katika hili;
Kuhusu Dr. Slaa – hata kama atafanikiwa kuwa Rais wa tano wa Tanzania, mdudu anaeliangamiza taifa letu atazidi kuwa yule yule – sera holela za worldbank/IMF, sera ambazo wote, CCM na CDM wanapigana vikumbo kuingia ikulu ili wazitekeleze kwa ufanisi; sera zinazo endorse ufisadi; tumeelezwa mengi katika kitabu cha confessions of an economic hitman; pia mengi tumeelezwa na watu wa ndani na wazito waliokuwa WorldBank – Joseph Stiglitz katika kitabu chake cha globalization and its discontents; tafuta ukweli pia juu ya kwanini Mradi wa Mchumua kwa miaka mingi umebaki kwenye makabati; tabia ya CDM kukimbilia kwa wafadhili wanapoona wanaonewa katika harakati za siasa za nchi ina support hoja yangu kwamba aidha kwa kutoelewa au kwa kuelewa, wakishika madaraka wataendeleza yaleyale; CDM ina viongozi makini sana, vijana wenye upeo na usomi wa hali ya juu kuliko vijana waliopo kwenye uongozi CCM (hili halina ubishi) lakini inashangza kuona CDM katika kutafuta legitimacy inakimbilia donors kulalamika wanaonewa badala ya kukimbilia UMMA;kidogo naona wameanza kujirekebisha kawa hili; ieleweke wazi kwamba kwa kiasi kikubwa, (with exception of few countries kama Sweden, Norway na Denmark) donors na mafisadi lao ni moja – kuinyonya nchi hii mpaka ikauke kabisa; wanachotaka donors ni chama au rais ambae ataufagilia ukoloni mamboleo; atokee CCM, CDM, CUF, kwao haijalishi;
Chama cha kuleta mageuzi na mapinduzi ya kweli ni kile kitachoanza kwa kutambua hilo;
 
Nimekupata Mchambuzi...!na way fprward yako umeichangnua vizuri,kwanza nikupe chanzo cha kuuliza swali hilo...ni kuwa Tanzania tumekuwa watu wa kuongea muno na kuchambua sana kuanzia wananchi hadi viongozi kwa kutafuta ujiko,tena siku hizi wamekuwa magwijiwa kijitangaza kuwa wanauwezo,akili na kipaji cha kuongoza...wawe wa chama tawala na wa upinzani wote tu.Wapi bana fanya kazi watu waone unauwezo na akili sio kujitangaza tuu mwalimu hakujitangaza lkn leo tunamuita baba wa Taifa. Nikupe mfano wakitu kimoja siku hizi kiongozi akikosea na akisemwa tena vijana Utasikia "ni wivu tu" Sasa yaani we uvurunde alafu uwambie watu ni wivu na wakae kimya???kwahiyo usiwajibike kuleta maendeleo kwakua unajua wakisema ni wivu?this cant be tolerated for reasonable men surely. Nije kwenye hoja yako ya kuelimisha..ndio kuelimisha ni sawa lkn kaka shv watu wameshaelimika naweza sema vya kutosha au basically hey know what is going on...!sasa lazima elimu iwe sambamba na plan za kurekebisha yanayoelimishwa...Kama unavyoshauri kuwa na vipande au kujisafisha CCM kwa top-bottom approach ulivyoainisha lkn bila kuanza kwa vijana wenye muono kama wako ku act sio kunena tu bali ku act itakua kazi bure.Anyway mie nafikiri tusubiri 2012 kwenye kikao chetu cha NEC mwenendo na mambo yatakayoenda ndio iwe mwanzo wa what next...kama kutakuwa na dhamira ya dhati kuwapa wenywe uwezo kuongoza bali hali itakuwa swali lkn kama ni kupangana kwa ajili ya future fruits basi..nadhani utakubaliana na mie kuwa that can be your right time kuwa na CCM asili na kampuni kama mgogoro wa yanga na simba miaka ya nyuma. LKN naamina asili wakiwa very strategic then watafanikiwa regardless of how poor they are because umma shv unaelewa what is happening.

Upo sahihi; vijana wengini (SIO WOTE) wanaingia kwenye siasa kutafuta uongozi ili wajitengenezee mazingira ya kuvuna pesa aidha kwa kununuliwa na viongozi au kutumia nafasi zao kuhujumu nchi; hawana dhamira ya kuweka nchi kwanza, tumbo baadae bali tumbo kwanza, nchi baadae; inabidi vijana tufikie hatua ya kusema sasa basi, sasa nataka kulinda heshima yangu na pia maslahi ya vizazi vya baadae; kama kijana una nia ya kutafuta pesa, kwanini usitafute huko kwenye soko huria, kwa kuuza mbao, kufuga kuku, mbuzi, kulima ufuta n.k? na kama una elimu nzuri, una nafasi ya kufanya makubwa zaidi kwani ujasiriamali pia unajenga nchi yako – utaajiri vijana wenzako, utalipa kodi, na utaweza changia chama chako kifedha hata bila kujikita kwenye siasa; binafsi sioni kosa kwa kijana kuwa na biashara zako halali na kuzitumia kujenga chama chako kwa njia ya uongozi au kwa njia nje ya uongozi; ili mradi fedha ziwe safi; lakini sio sahihi kuingia kwenye chama na kutafuta uongozi kwa matarajio ya kujijenga ki-uchumi; watu wa namna hii ndio wanaokiharibu chama;
Inasikitisha vjjana wa umri wa miaka 30-35 kukubali kushabikia upande fulani wa kisiasa na kutumika na wazee wanaotafuta uongozi, wazee ambao vita vyao ni fitina tupu, sio ufisadi; wazee/wanasiasa ambao miaka 15 ijayo watakuwa wastaafu wakati wewe kijana ndio kwanza utakuwa na umri wa miaka 45-50, mchanga kabisa kisiasa; litakuwa jambo la fedheha sana iwapo by mwaka 2025 utajikuta njia panda na kujuta kwanini ulichagua the wrong side of history, especially kama utakuwa bado na interest za siasa; hili litawakuta wale wanaoshabikia upande mmoja wa siasa bila kuelewa kiini cha vita hivyo ni nini; ushabiki unao base on personalities za viongozi hao badala ya sera na dira fulani kwa taifa; ushabiki huu ni short lived; by the time wazee hao wanaachia ngazi kisiasa kutokana na umri, vijana hawa ambao watakuwa umri wa miaka 45-50 wakati huo most likely wataishia aidha kwa Ocampo kujibu tuhuma za mauaji ya alaiki kwani itakuwa dhahiri kwamba walishiriki iwapo siasa zao zitatupeleka kwenye machafuko; kama sio kwa ocampo, basi vijana hawa wataishia kutuletea tu vurugu nchini aidha kwa harakati zao za kujinasua na kashfa (kwani tayari watakuwa wananuka) au kutafuta kukubalika kisiasa kwa nguvu; wakati huo, wazee wa sasa wanaopigana vijembe vya fitina wote watakuwa wanastarehe miguu juu kama wastaafu na familia zao; Sina maana kwamba wazee katika chama hawana nafasi au hawana maana; hoja yangu hapa ni kwamba kuna wazee wa maana sana wana CCM ambao tunawahitaji kimawazo lakini wengi ya hawa wapo kimya katika nyakati hizi kuwashauri vijana ipasavyo; wazee walio active ni wale ambao wanatumia siasa kwa manufaa yao binafsi na kuwateka vijana wasiokuwa na dira; ni dhahiri kwamba wakimalizana na siasa, watawatupa vijana wanaobebana nao sasa na badala yake kuepuka siasa za migongano na kujikita na shughuli za familia zao; This applies to kambi zote zinazohasimiana sasa ndani ya CCM; we should start learning how to think ahead;
 
Kilichojenga ufisadi sio uongozi wa Mkapa, mwinyi, Kikwete; mzazi wa ufisadi ni IMF/Worldbank ambao waziwazi waliona Ujamaa sio njia sahihi kwa nchi yetu; nah ii ikapelekea azimio la Zanzibar kuzaliwa mwaka 1992; IMF/WorldBank walikuja kuwa maadui wakubwa wa Ujamaa, na hii ikapelekea vibaraka wengi wa ubeberu na ubepari humu nchini kupata mianya ya kuzidi kunyonya wachache, tena kwa Baraka zote IMF/WorldBank; Mzee Mtei, aidha kwa kujua au kutojua, ana mkono katika hili;
Kuhusu Dr. Slaa – hata kama atafanikiwa kuwa Rais wa tano wa Tanzania, mdudu anaeliangamiza taifa letu atazidi kuwa yule yule – sera holela za worldbank/IMF, sera ambazo wote, CCM na CDM wanapigana vikumbo kuingia ikulu ili wazitekeleze kwa ufanisi; sera zinazo endorse ufisadi; tumeelezwa mengi katika kitabu cha confessions of an economic hitman; pia mengi tumeelezwa na watu wa ndani na wazito waliokuwa WorldBank – Joseph Stiglitz katika kitabu chake cha globalization and its discontents; tafuta ukweli pia juu ya kwanini Mradi wa Mchumua kwa miaka mingi umebaki kwenye makabati; tabia ya CDM kukimbilia kwa wafadhili wanapoona wanaonewa katika harakati za siasa za nchi ina support hoja yangu kwamba aidha kwa kutoelewa au kwa kuelewa, wakishika madaraka wataendeleza yaleyale; CDM ina viongozi makini sana, vijana wenye upeo na usomi wa hali ya juu kuliko vijana waliopo kwenye uongozi CCM (hili halina ubishi) lakini inashangza kuona CDM katika kutafuta legitimacy inakimbilia donors kulalamika wanaonewa badala ya kukimbilia UMMA;kidogo naona wameanza kujirekebisha kawa hili; ieleweke wazi kwamba kwa kiasi kikubwa, (with exception of few countries kama Sweden, Norway na Denmark) donors na mafisadi lao ni moja – kuinyonya nchi hii mpaka ikauke kabisa; wanachotaka donors ni chama au rais ambae ataufagilia ukoloni mamboleo; atokee CCM, CDM, CUF, kwao haijalishi;
Chama cha kuleta mageuzi na mapinduzi ya kweli ni kile kitachoanza kwa kutambua hilo;

Kwenye hizo ifm/wb conditionalities unaweza kutoka kama nchi ikiwa kuna ufanisi..

Kinachotokea ni kuwa ujamaa siyo mzuri kihivyo kama ambavyo wewe unataka tuamini nay!

Ujamaa una mapungufu makubwa..sana kwenye mfumo wa kuendesha maisha ya watu huru na kufanya kazi kwa bidii..

Tatizo letu kubwa ni kwamba hizo fursa za ubepari hatuzitumii kama ambavyo hatukutumia fursa za ujamaa..

Tatizo ni uwajibikaji na utendaji mbocu wa watu zaidi kuliko mfumo..
 
Well said.

Mchambuzi nikwambie na kukutoa hofu kuwa achana na hao vijana wanaotafuta makundi kujitajirisha kisiasa maana hawajui watendalo...!Kwa kijana na hata mzee wa CCM shv kufikiria nani anatakiwa kuwa rais ajae mie naona nikujichosha uwezo wake wa kufikiri.....mtu anayefikiri critically juu ya changamoto zinazolikabili taifa letu na CCM shv hawezi waza urais kabla ya Chama na nchi ilivyosasa. Ila kaka kusema chadema wanawasomi zaidi ya CCM napingana na wewe hapo...hhe hehe na ndio democracy....unajua CCM vijana wasomi wapo wengi tu tena hata wenye uwezo kushinda wa CDM..tatizoo.....narudia tatizooo...wenzetu CDM wanawatumia pamoja na uchache wao..lkn kwetu...hao ni threat....hivyo hawatumiwi na hawapewi mwanya si umetoka kusema kwenye post zako ubaguzi wa kujuana umesahau mara hii??? heh eehhehhe
 
@Machmbuzi
Hali iliyofikia CCM haiwezi kujisahihisha na kurudi kuwa chama cha wananchi bila kugawanyika. Hilo sahau. Ndio mana sometime sijui kama nimfisu kikwete au nimlaumu .

Kwa maoni yangu CCM ikigawanyika chini ya kikwete hiyo itakuwaa ni moja ya positive achivement chini ya uongozi wake. Its the only foward ili watu waimbe wimbo mmoja. zaidi ya hapo yatabaki maigizo tu.
 
Back
Top Bottom