Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
- Thread starter
- #81
CCM imeenda kinyume na katiba yake kuingia mseto na CUF; Jamani, hata katiba ya chama nayo viongozi wanakosa umakini kwa jambo ambalo pengine linahitaji kikao kimoja tu kusahihisha? Angalau suala la CCM kuacha itikadi ya chama kwenye katiba yake ibaki kusomeka 'ujamaa na kujitegemea' kidogo inaeleweka ingawa ni bado sio sahihi kosa, hata hili la mseto?
KAKA MCHAMBUZI NA CCM WENGINE,NAOMBA NIULIZE SWALA MOJA PIA AMBALO HALINA DIRECT CONNECTION NA POST YAKO,SWALI LANGU AMBALO LBD WADAU WAKIJADILI HUMU PIA INAWEZA SAIDI...NI JE NINI MANTIKI YA MAGEUZI AMBAYO TUNAAMBIWA CCM INAFANYA SHV?YAANI KUBADILISHA UTARATIBU WA KUMPATA MGOMBEA URAIS,KUUNDA CHOMBO CHA WASHAURI YAANI MA RAIS WASTAAFU,NA KUUNDA TENA SIJUI KUBORESHA KAMATI YA MAADILI YA CHAMA NA MENGINE NIISHIE HAYO.
KWA MTAZAMO WANGU WAMBALI NAONA MAMBO HAYA HAYANA TIJA KWA CCM,SABABU NINAZO KWANZA KAMATI YA MAADILI IPO KWANINI IUNDWE NYINGINE?ILIYOPO HAUFAI?NA KAMA NDIO KWANINI?PILI MARAIS NA VIONGOZI WAKUU WA NCHI YETU KWAKAWAIDA NI WASHAURI TAYARI ..SO JE KUNA ULAZIMA GANI WAKUWA AUTHORISE KWA KUWAUNDIA CHOMBO?SIO KUONGEZA GHARAMA SIZIZO ZA MSINGI? NA MOVE HII NAONA KAMA CHAMA KINAELEKEA KUPOKONYWA MAMLAKA YA MAAMUZI KWA WANACHAMA NA BADALA YAKE MAAMUZI MENGI YAWE YANAFANYA NA WACHACHE, MIE KWELI NAWAZA HIVYO WKT TUNAONGELEA KATIBA KUPUNGUZA MAMLAKA KWA WATU WACHACHE NAONA KAMA CCM KAMA INAKAZANA THE OTHER WAY AROUND YAANI KUTOA KWA WENGI KUPELEKA KWA WACHACHE..PENGINE LBD MIE SIJAELEWA NA TAFSIRI YANGU SI SAHIHI NAOMBENI WENYE UELEWA PENGINE ZAIDI KTK HILI TUWEKANE SAWA....[/QUOTE]
Sidhani kama nina jibu la moja kwa moja lakini pengine maoni;
- Kuhusu suala la kumpata mgombea urais, utaratibu uliopo ni mbovu sana kwani mianya ya rushwa ni mipana mno; wanaopigia kura jina la mgombea urais ni wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa toka mikoa yote, hawapungui wajumbe 2,000; ni hawa hawa pia ndio uchagua wajumbe wa NEC;
Siku moja jaribu kupanda treni kutoka Mwanza kuja DSM kupitia Dodoma atika nyakati za chaguzi za Urais au NEC; kinachotembea mle ni bahasha, konyagi, chips mayai, whisky na bia; wenye pesa wanatuma mawakala wao mle ambao safari nzima kinachishindaniwa ni dau tu; mpaka treni ifike Dodoma, tayari wajumbe wana msimamo juu ya mgombea fulani kutokana na msimamo wa matumbo yao na mifuko yao; Kwa mgombea mwenye pesa nyingi ni rahisi sana kuwakamata wajumbe wengi kama sio wote kutoka Mwanza, Mara, Shinyanga, na Kagera; na ukijipanga kwa wajumbe wa treni ya Kigoma, Tabora, kuja Dodoma, ndio umemaliza kazi; wajumbe toka mikoa ya kusini, nyanda za juu kusini ukiokota okota kadhaa na huko haukosi ushindi;
Kwa maoni yangu utaratibu huu lazima ubadilishwe ingawa sina uhakika kama mabadiliko ynayozungumzwa yatalenga haya ninayozungumza; Pengine niseme pia kwamba ni sahihi kabisa wajumbe hawa kuchagua wagombea urais, NEC kwani inapanua demokrasia katika michakato hiyo ndani ya Chama; lakini ingekuwa busara zaidi kama wajumbe hawa wangefanyiwa utaratibu wa kupiga kura huko huko mikoani kwao bila ya kuwapa wenye pesa mianya ya kuwakusanya wote kwenye matreni na mabasi; na utaratibu wa kuwapigia kura wagombea huko mikoani lakini sio kabla wagombea wote hawajapitishwa mikoani kujieleza wasifu wao, kuruhusu wajumbe waulize maswali yote yenye shaka juu ya uadilifu wa mgombea n.k.
Kwa mfano, ni suala la ajabu sana katika kura za maoni udiwani, ubunge, hata Urais kwa wajumbe/wanachama kukatazwa kuuliza maswali about the integrity ya wagombea uongozi; in my opinion, it is the basic right of the electorate kutosheka na personal integrity and commitement of a candidate; sidhani kama kuna mtu yoyote wants to vote for a self – seeking, corrupt, power hungry candidate; to question and demand of a candidate to account for his/her past performance in public life (and to an extent private), is legitimate, in my opinion; and this should not remain only at the accusations and allegations levels, but wapiga kura have a right to be fully informed of the background of the candidate; ni matumaini yangu mabadiliko yanayozungumzwa yatalenga huko pia;
- Kuhusu kamati ya washauri, sijui kwa undani sana suala hili lakini ninachoweza kusema ni kwamba KATIBA ya sasa haielezei nafasi ya wazee katika Chama kwa ufasaha; wanatajwa kidogo sana kwenye sehemu ya nne ya katiba chini ya heading WAZEE NA JUMUIYA ZA WANANCHI:
This is too narrow in my view. Wazeee wastaafu ni muhimu wawekwe kwenye chombo chao in my opinion; wapo wanaosema kwamba itawapunguza nguvu, but mimi naona it is the other way round kwani badala ya kusema mfano Mzee karume alisema hili na lile kwenye NEC/CC, sasa itakuwa msimamo wa wazee wa CCM ni this and that, hence kuleta uzito zaidi;
- Kuhusu kamati ya maadili, pia sina uelewa sana wa nini kinaendelea katika hilo lakini jambo lililo wazi ni kwamba kamati hii kwa sasa ni ‘A Toothless Dog;'