CCM: Tujisahihishe au Tugawane Chama

Moja ya tatizo kubwa linaloikabili CCM kwa sasa ni ukubwa wake, the party is too big kiasi kwamba ikichanganywa na ignorance ya baadhi ya members na viongozi wake suala zima la itikadi na misingi halieleweki na halipewi umuhimu tena. Sasa with such a large organization unahitaji a serious, solution oriented na innovative CEO,mwenye ujuzi wa kudelegate na kufahamu anadelegate nini kwa nani ili apate nini. Something I am sure mwenyekiti wenu siyo! Mwenyekiti na waandamizi wenzake bado wanaongoza kwa mazoea, same way kama ilivyokuwa in the 70's 80's, 90's. Na ndiyo maana hawaishi kutoa mifano ya enzi hizo wakati sometimes haifanani kabisa na wakati tuliopo.

Jingine naloliona ni kwamba ubora wa CCM unakuwa counted kwa populism something which is very wrong for our GOP. Seeking and maintaining populism ndiyo imeifikisha CCM hapo ilipo. Bahati mbaya sana misingi na itikadi hujengwa kwa elimu (ufahamu) wakati populism can just be done with money!!!! Majambazi, wakwepa kodi, wafanya biashara haramu wamekuwa marafiki wakubwa wa CCM ya leo, they maintain the popularity of the party ili wapate ulinzi wa mambo yao. And this has trickled downmpaka kijijini. Ili mambo yako yanyooke hata kama ni mwizi basi associate yourself with CCM.

Hivyo basi CCM kuibadilisha au kubadilika au kujisafisha ni ndoto, na ili ndoto hiyo itimie inabidi CCM ishindwe kwanza ikajipange upya. Unfortunately that is the only way.
 
Ni sahihi, mbali na its massive size, Chama kina run propaganda ya hali ya juu inayokisaidia to stay afloat; lakini hii ni short-lived kwani vijana mijini wameshaanza kuelimika na haitachukua muda elimu hiyo kufika vijijini; elimu ninayoizungumzia ni ile juu ya chama chao kuongoza kwa miaka karibia 20 sasa bila itikadi inayoeleweka; badala yake chama kinaendeshwa kwa ilani za uchaguzi jambo ambalo ni la hatari sana;

Hoja yako kwamba ni muhimu CCM kishindwe kwanza uchaguzi ili kipate nafasi ya kujipanga - hatari yake ni kwamba kikisubiri hilo litokee, ni dhahiri kitawarudia na kuwapigia magoti wenye pesa na kuwapa jukumu la kukirudisha madarakani, unless lengo liwe kujijenga kwenye majimbo badala ya ngazi ya urais; mgawanyiko rasmi kutokana na itikadi ni muhimu sana kabla ya uchaguzi mkuu ujao;
 
Mchambuzi,

Umechambua vizuri sana, nakupongeza.

Tatizo kubwa lililotufikisha hapo ni ubinafsi wa viongozi. Kuna uwezekano mkubwa kwamba viongozi wengi wa chama hawajui hata itikadi ya chama. Hii inathibitishwa na serikali kukumbatia sera za kibepari kinyume na itikadi ya chama.
Mawazo ya kujiendeleza kwa faida ya wote sasa yamegeuzwa kwa faida binafsi, familia, ndugu, jamaa na marafiki.

Vyama vyote vina miongozo, ilani, sera ambazo kwa ujumla zinafanana kwa lengo moja kuu la kuwalendeleza wananchi. Tofauti ni watendaji.

Tusitegemee miujiza ya kujisahihisha tukiwa na watendaji wale wale. Ni muhimu kujua kwamba kupigania uhuru au ukombozi ni jambo endelevu na hivyo ni wakati muafaka kwa wananchi wanyonge walio wengi kuungana kupambana na tabaka la wachache waliotupoteza njia ili kurudi kwenye mstari.
Kuwa na mawazo kwamba watu hao hao waliotupoteza wanaweza kuturudisha kwenye muelekeo sahihi ni utumwa wa fikra.

Hoja nzuri sana; kwahiyo kwa mtazamo wako kama nimekusoma vizuri, hata chama kikimeguka hakuna jipya litakalotokea kwa sababu watendaji wa pande zote mbili watakuwa ni wale wale?
 
Ni muhimu tukawekana sawa juu ya maana ya neno mapinduzi kwenye CCM; nimewahi uliza baadhi ya viongozi wa CCM juu y ahili, wengi hawakuwa na jibu sahihi; Mwongozo unasema hivi:

"Lengo kuu la mapinduzi ya Tanzania ni kujenga nchi ya ujamaa ambamo unyonyaji wa mtu na mtu utakuwa umetokomezwa, ambamo uchumi wa taifa utakuwa unamilikiwa na kudhibitiwa na umma wa wakulima na wafanyakazi washiriki na ambamo uhusiano wa watu katika jamii utakuiwa ni wa udugu na kushirikiana kwa maendeleo ya wote na ambamo kazi imepewa hadhi ya kuwa
wajibu wa kila mtu."
--
Wapo wanaosema kwamba Ujamaa ni Mbaya na umepitwa na wakati; wana hoja lakini sio mia kwa mia; kwa wale wanaosema Ujamaa ni mbaya au umepitwa na wakati, kipi ni kibaya hapo juu? hii itatusaidia kuchukua mazuri na kuacha mabaya ya itikadi ya ujamaa na kujitegemea;
 
Silaha kubwa ya CCM ni muungano, bila muungano CCM haina maana yeyote.
 
Silaha kubwa ya CCM ni muungano, bila muungano CCM haina maana yeyote.

This is a very interesting point ambayo wengi hawaiangalii; binafsi napenda kukiri kwamba sikuangalia sana suala hili; pengine ndio maana suala la muungano ni nyeti sana kwa mustakabali wa CCM kwani kama ukivunjika, CCM itahitaji a major overhaul suala ambalo litakipelekea kupasuka; vinginevyo chama kiamue kubakia na jina lake la CCM hata nje ya muungano, kama vile CRDB ambayo ilikuwa ni benki mahususi ya wakulima imabakia na jina lile lile na kuongezea bank mwishoni i.e. CRDB Bank i.e. 'Cooperative and Rural Development Bank' Bank, wakati hii sio relevant na sio sahihi; CRDB ni mfano wa kijinga lakini nimefurahishwa sana na suala zima la relevance plus survival ya CCM outside the context of muungano;
 
This is a very interesting point ambayo wengi hawaiangalii; binafsi napenda kukiri kwamba sikuangalia sana suala hili; pengine ndio maana suala la muungano ni nyeti sana kwa mustakabali wa CCM kwani kama ukivunjika, CCM itahitaji a major overhaul suala ambalo litakipelekea kupasuka; vinginevyo chama kiamue kubakia na jina lake la CCM hata nje ya muungano, kama vile CRDB ambayo ilikuwa ni benki mahususi ya wakulima imabakia na jina lile lile na kuongezea bank mwishoni i.e. CRDB Bank i.e. 'Cooperative and Rural Development Bank' Bank, wakati hii sio relevant na sio sahihi; CRDB ni mfano wa kijinga lakini nimefurahishwa sana na suala zima la relevance plus survival ya CCM outside the content of muungano;
Pia hii ni sababu mojawapo inayozuia indepedent candidacy, na hata CCM ikivunjika ASP sidhani kama watataka kujiunga na kundi lolote...
Ni sawa na CCM kufa, na kuanzishwa kwa vyama vipya.
It's impractical. But Pan came from Yanga, so something may come from CCM.
 
Mchmbuzi una hoja za msingi sana, ila tatizo kubwa tulilo nalo Tanzania ni policing of law. Sheria zetu hazina usimamizi , wanaoitwa mafisadi just for example wanamakosa ya kijinai ila hakuna wa kuwapelaka mahakamani au kuwashitaki achana na azimio la arusha au zanzibar. Kuna wizi na uhujumu, kuna matumizi mabovu ya madaraka, kuna rushwa, uzembe na uzandiki. Pamoja na katiba mbovu na kuwa na usalama wa taifa, takukuru, cid, dpp hakuna linalotokea. Vionozi badala ya kufanya kazi wanaviziana kwa visa na chuki.

Nakubaliana na wewe ila tatizo letu kubwa ni kusimamia sheria sheria zetu wenyewe kwanza.
 
Sasa inakuwaje Mwalimu katika hotuba zake zilizokuwa zinarushwa kwenye TV mwezi wa kumi kuna moja aliongelea umuhimu wa kuwapa wananchi haki yao ya kugombea kama private candidates au kuchagua private candidates na kwamba kuzuia hili sio sahihi?
 
Upo sahihi; na ndio maana hata huko Libya tumeona jinsi gani wakuu wa usalama waliamua kukata mbuga jangwani kwani tabia yao kuwa upande wa serikali ya kinyonyaji ilipelekea wakubwa wengi wa idara hiyo kuwa na hatia za kujibu kwa Ocampo;wapo kadhaa ambao wamekamatwa; pia tumeona hili huko Misri kwa upande wa idara ya polisi; vyombo hivi vyote vinatakiwa viweke umma mbele kwani neno 'taifa' katika usalama kwa mfano inamaanisha ni 'watu', sio mtu mmoja mmoja kwenye madaraka au uongozi;

Vinginevyo viongozi wetu wamekuwa na tabia ya kujikita zaidi katika kuhimiza kwamba tuna 'utawala wa sheria' kuliko kuangalia suala muhimu zaidi la 'usimamizi wa sheria';
 
Mchambuzi Viongozi ni zao letu. Kinachonisikitisha sana ni kuona vijana wa sasa hawajui nini umuhimu wa kujenga nchi yetu. Kwa mfano, mahitaji ya katiba mpya bora ni wajibu wa kila mtanzania, wajibu huu hauhitaji chama cha siasa au cha kijamii unahitaji utashi na uelewa wa kujua kuwa ubovu wa sheria ndio unatudidimiza, unatuletea mikataba dhalimu, unadhalisha viongozi hovyo, unatufanya wanyone.

Inabidi kuhimizana katika kutambua ushiriki na wajibu wetu. Jiulize wapo vijana wangapi au wananchi wangapi wasio jua tofauti ya azimio la arusha na zanzibar? Je wakati haya mabadiliko yanatokea je katiba ilibadilishwa? Ukisoma katiba ya nchi na jinsi inavyoendeshwa ni vitu viwili toafuti kabisa. hongera kwa kuleta hoja hii.
 
Sahihi kabisa; mbali ya katiba ya jamhuri, huko ni mbali sana, je katiba ya CCM inaruhusu chama kuingia mseto? Jibu ni hapana; angalau Chadema inaweka wazi kwenye katiba yake inaposema:

9.3 Chama Kuingia Mseto na Vyama Vingine
9.3.1 Chama kinaweza kuunda mseto na Chama au vyama vingine vyenye madhumuni na
malengo yanayofanana na Chama ili kuimarisha uwezo wa kushinda uchaguzi mkuu au
wa serikali moja ya mtaa kwa lengo la kuunda utawala wa pamoja.
9.3.2 Chama kinaweza kuunda ubia na vyama vingine katika kuendesha miradi ya kiuchumi
ama huduma.
9.3.3 Chama kinaweza kuungana na Chama ama vyama vingine kuunda Chama kipya.
9.3.4 Uamuzi kuhusu vipengere 9.3.1 na 9.3.3 utafanywa na Mkutano Mkuu wa Taifa na
kuhusu kipengere 9.3.2 na Baraza Kuu.
--
CCM imeenda kinyume na katiba yake kuingia mseto na CUF; Jamani, hata katiba ya chama nayo viongozi wanakosa umakini kwa jambo ambalo pengine linahitaji kikao kimoja tu kusahihisha? Angalau suala la CCM kuacha itikadi ya chama kwenye katiba yake ibaki kusomeka 'ujamaa na kujitegemea' kidogo inaeleweka ingawa ni bado sio sahihi kosa, hata hili la mseto?
 
Sasa inakuwaje Mwalimu katika hotuba zake zilizokuwa zinarushwa kwenye TV mwezi wa kumi kuna moja aliongelea umuhimu wa kuwapa wananchi haki yao ya kugombea kama private candidates au kuchagua private candidates na kwamba kuzuia hili sio sahihi?
Private candidates ni impossible under the current constitution kwa sababu ni marufuku ku advocate kuvunjwa kwa muungano, you can talk about it, ila huwezi kuomba cheo chochote cha kisiasa kama una advocate seccession of let say ZNZ or Tanganyika, it's unconstitutional hence illegal.
Ndiyo maana huwezi kuwa na chama chenye wanachama bara tu, au zanzibar peke yake.
Hii ndiyo iliyomshinda Mtikila kwenye supreme/high court.
The logic behind ni kwamba ukiwa una advocate seccession ni sawa na ku redefine boundaries za Tanzania kitu ambacho ni mwiko kwa Taifa lolote. Huwezi ku redefine boundaries za nchi yeyote, hiyo ni an act of war if not treasonuous.
 
Sahihi kabisa; mbali ya katiba ya jamhuri, huko ni mbali sana, je katiba ya CCM inaruhusu chama kuingia mseto? Jibu ni hapana; angalau Chadema inaweka wazi kwenye katiba yake inaposema:

9.3 Chama Kuingia Mseto na Vyama Vingine
9.3.1 Chama kinaweza kuunda mseto na Chama au vyama vingine vyenye madhumuni na
malengo yanayofanana na Chama ili kuimarisha uwezo wa kushinda uchaguzi mkuu au
wa serikali moja ya mtaa kwa lengo la kuunda utawala wa pamoja.
9.3.2 Chama kinaweza kuunda ubia na vyama vingine katika kuendesha miradi ya kiuchumi
ama huduma.
9.3.3 Chama kinaweza kuungana na Chama ama vyama vingine kuunda Chama kipya.
9.3.4 Uamuzi kuhusu vipengere 9.3.1 na 9.3.3 utafanywa na Mkutano Mkuu wa Taifa na
kuhusu kipengere 9.3.2 na Baraza Kuu.
--
CCM imeenda kinyume na katiba yake kuingia mseto na CUF; Jamani, hata katiba ya chama nayo viongozi wanakosa umakini kwa jambo ambalo pengine linahitaji kikao kimoja tu kusahihisha? Angalau suala la CCM kuacha itikadi ya chama kwenye katiba yake ibaki kusomeka 'ujamaa na kujitegemea' kidogo inaeleweka ingawa ni bado sio sahihi kosa, hata hili la mseto?
CCM haikuingia ubia na CUF mkuu.
 
kwani Mramba na Yona wamepelekwa mbele ya sheria kwa ajili gani, si kuonyesha umma kwamba CCM na serikali yake wanapingana na ufisadi? haijalishi kama walikuwa kwenye uongozi wa CCM au lah;

Okay, lets say that matters - cheo gani kikubwa zaidi kati ya ujumbe wa NEC na Ubunge? Jibu ni Ubunge; sasa kwanini Chama kinachotaka ni kuwatoa watuhumiwa kwenye nafasi zao za NEC na kuwaachia ubunge wao kama ulivyo? haikuingii akilini kwamba kisiasa na ushindani wa 2015 NEC hata kama ni nafasi inferior to ubunge inalipa zaidi kama una nia ya kugombea urais?

Suala hapa sio la spin, ni suala lililo wazi kwamba CCM tangia mwaka 2008 haina lolote la maana inalolifanya zaidi ya makada wake kujipanga kikambi kumpokea Kikwete kijiti 2015; nashangaa kwanini hauoni hilo; vinginevyo naomba nisaidia maelezo kwamba siasa za CCM sasahivi ni zipi; hata katibu mwenezi wa chama Nape Mnauye hafanyi kazi based on his job description, amejikita katika vita dhidi ya wale wanaodhaniwa watatia nia kupitia CCM uchaguzi mkuu 2015;

CDM nakubali bado kwamba wamevuna kura nyingi sana kupitia kelele za ufisadi, lakini unashindwa kujiuliza kwanini? ni kwa sababu sera za CDM haziuziki kwani kama sio kwamba zinafanana na za CCM, basi kuna nyingine CCM ilizifuata na hazikufanikiwa miaka ya nyuma; na given hali mbaya ya kiuchumi ya watanzania wengi ambayo imepelekea jamii kugawanyika kati ya walio nacho na wasio nacho, siasa za ufisadi makujwaani zitavuna kura nyingi sana, whether by perception or reality;

Kuhusu mwenyekiti kuyumba, lazima ayumbe kama machinery yake inalegalega na imegawanyika; kumbuka mwenyekiti ni msimamizi tu, NEC ina nguvu sana katika siasa za CCM
na ndio maana suala la gamba limetolewa huko na kupelekwa kamati maalum; vinginevyo ni desturi yetu watanzania kumsema mwenyekiti vibaya akiamua kutoa maamuzi magumu kama vile alivyofanya mkapa wakati fulani, lakini pia tunalaumu anapo yumba kutokana na udhaifu ulio bayana; nina uhakika kama akijipanga, atautumia uchaguzi mkuu ujao wa chama kurekebisha hilo;

Ndugu Mchambuzi nakushukuru kwa majibu, ingawa yamezaa maswali mapya.
Binafsi naona kama haujawa clear ni nini hasa unachokisimamia hapa. Maana post zako zina jicontradict hata within the same post.
Ningeshauri ukae chini ujue hasa ni nini conscience yako inakiamini halafu kama ikibidi ubadili ID ili ujadili kwa uhuru mpana fanya hivyo,
maana najua bado unapolitical ambitions na si vizuri kuwaparua wakubwa hasa unapokua na picha yako kwenye forum.

Tuanze na suala la akina Mramba, hapo hapo umesema CCM na serikali yake ilitaka kuwaonesha wananchi kuwa wako serious na vita ya ufisadi. Wakati huohuo Mwenyekiti ameonekana Rombo, Igunga, Bariadi na Monduli akiwanyanyua mkono na kuwaombea kura wagombea wa CCM kwenye uchaguzi mkuu wa 2010, Hata Makongoro Nyerere alipigia sana kelele hili kwenye kikao cha NEC, Aprili. Haingii akilini na haiitaji kwenda shule kuona CCM inawachezea watu kwenye suala la Ufisadi.

Halafu naomba nipingane na wewe, kwenye ukubwa wamNEC na mbunge. Kwa kuangalia mishahara na marupurupu na kwa vyama visivyokua na serikali ni kweli mbunge ni cheo cha juu. Lakini kwa chama chenye kuunda serikali kama CCM. NEC ndiyo chombo kinachounda sera ya kutekelezwa na serikali. Hivyo hata mbunge, midhali umepata ubunge kupitia hicho chama, mNEC atakupangia uende bungeni kupigania mambo gani, lakini siyo vice versa kwamba mbunge anaweza kumpangia mNEC aseme nini au kupigania nini kwenye NEC. Hapo naomba ukajipe maarifa zaidi.

Unamuongelea Nape the whole thread. Nashangaa unamuona Nape anachafua hali ya hewa wakati hata Mwenyekiti wenu kwenye tamasha la Injili alitamka waziwazi kwamba anayoyasema NAPE ndiyo msimamo wa NEC, na hakuna aliyejitokeza kumpinga JK kwa kauli yake hiyo, sasa mkuu mbona unarudia kulekule kwa wapambe wa mafisadi?...unajua Mzee Mwanakijiji aliwahi kusema, Where there is Right or Wrong, Good or Bad, a position of NEUTRALITY is a sign of WEAKNESS. Wewe unataka kuhave your cake and eat it too. CCM ikipasuka sasa haitakua kama unavyofantasize, kwamba ya Azimio la Arusha na Azimio la Zanzibar, ikipasuka itakua ni CCM pro Mafisadi na CCM against Mafisadi, which side will you take sir?

Unasema Mwenyekiti ni nafasi ya usimamizi tu!!... Please mkuu. Mwenyekiti anaset agenda ya term yake, anaset priority za policy, na ni wajibu wa mwenyekiti kuset ITIKADI ya chama, kwa kutambua dunia inabadilika. Baada ya kujua haya mambo makuu matatu zaidi ya kuongoza vikao, anatakiwa atumie USHAWISHI wake kama mwenyekiti ili yapite kwenye vikao vya maamuzi. Watu wanaposema Mwenyekiti anayumba ni kwa sababu hajatumia ushawishi wake unaoendana na kofia aliyoikalia kupitisha direction ya anapotaka chama kiende.

By the way NEC imeanza kuwa na nguvu kipindi hiki cha Awamu ya nne tu au hata huko nyuma? Na Wenyeviti waliotangulia walikua wanawaandaaje wajumbe kukiwa na very sensitive issue?

Hiyo ya 2012 inawezekana akafanya makubwa, ila kwa kweli its a toss!
 
CCM imeenda kinyume na katiba yake kuingia mseto na CUF; Jamani, hata katiba ya chama nayo viongozi wanakosa umakini kwa jambo ambalo pengine linahitaji kikao kimoja tu kusahihisha? Angalau suala la CCM kuacha itikadi ya chama kwenye katiba yake ibaki kusomeka 'ujamaa na kujitegemea' kidogo inaeleweka ingawa ni bado sio sahihi kosa, hata hili la mseto?[/QUOTE]

KAKA MCHAMBUZI NA CCM WENGINE,NAOMBA NIULIZE SWALA MOJA PIA AMBALO HALINA DIRECT CONNECTION NA POST YAKO,SWALI LANGU AMBALO LBD WADAU WAKIJADILI HUMU PIA INAWEZA SAIDI...NI JE NINI MANTIKI YA MAGEUZI AMBAYO TUNAAMBIWA CCM INAFANYA SHV?YAANI KUBADILISHA UTARATIBU WA KUMPATA MGOMBEA URAIS,KUUNDA CHOMBO CHA WASHAURI YAANI MA RAIS WASTAAFU,NA KUUNDA TENA SIJUI KUBORESHA KAMATI YA MAADILI YA CHAMA NA MENGINE NIISHIE HAYO.

KWA MTAZAMO WANGU WAMBALI NAONA MAMBO HAYA HAYANA TIJA KWA CCM,SABABU NINAZO KWANZA KAMATI YA MAADILI IPO KWANINI IUNDWE NYINGINE?ILIYOPO HAUFAI?NA KAMA NDIO KWANINI?PILI MARAIS NA VIONGOZI WAKUU WA NCHI YETU KWAKAWAIDA NI WASHAURI TAYARI ..SO JE KUNA ULAZIMA GANI WAKUWA AUTHORISE KWA KUWAUNDIA CHOMBO?SIO KUONGEZA GHARAMA SIZIZO ZA MSINGI? NA MOVE HII NAONA KAMA CHAMA KINAELEKEA KUPOKONYWA MAMLAKA YA MAAMUZI KWA WANACHAMA NA BADALA YAKE MAAMUZI MENGI YAWE YANAFANYA NA WACHACHE, MIE KWELI NAWAZA HIVYO WKT TUNAONGELEA KATIBA KUPUNGUZA MAMLAKA KWA WATU WACHACHE NAONA KAMA CCM KAMA INAKAZANA THE OTHER WAY AROUND YAANI KUTOA KWA WENGI KUPELEKA KWA WACHACHE..PENGINE LBD MIE SIJAELEWA NA TAFSIRI YANGU SI SAHIHI NAOMBENI WENYE UELEWA PENGINE ZAIDI KTK HILI TUWEKANE SAWA....
 
CCM imeenda kinyume na katiba yake kuingia mseto na CUF; Jamani, hata katiba ya chama nayo viongozi wanakosa umakini kwa jambo ambalo pengine linahitaji kikao kimoja tu kusahihisha? Angalau suala la CCM kuacha itikadi ya chama kwenye katiba yake ibaki kusomeka 'ujamaa na kujitegemea' kidogo inaeleweka ingawa ni bado sio sahihi kosa, hata hili la mseto?

KAKA MCHAMBUZI NA CCM WENGINE,NAOMBA NIULIZE SWALA MOJA PIA AMBALO HALINA DIRECT CONNECTION NA POST YAKO,SWALI LANGU AMBALO LBD WADAU WAKIJADILI HUMU PIA INAWEZA SAIDI...NI JE NINI MANTIKI YA MAGEUZI AMBAYO TUNAAMBIWA CCM INAFANYA SHV?YAANI KUBADILISHA UTARATIBU WA KUMPATA MGOMBEA URAIS,KUUNDA CHOMBO CHA WASHAURI YAANI MA RAIS WASTAAFU,NA KUUNDA TENA SIJUI KUBORESHA KAMATI YA MAADILI YA CHAMA NA MENGINE NIISHIE HAYO.

KWA MTAZAMO WANGU WAMBALI NAONA MAMBO HAYA HAYANA TIJA KWA CCM,SABABU NINAZO KWANZA KAMATI YA MAADILI IPO KWANINI IUNDWE NYINGINE?ILIYOPO HAUFAI?NA KAMA NDIO KWANINI?PILI MARAIS NA VIONGOZI WAKUU WA NCHI YETU KWAKAWAIDA NI WASHAURI TAYARI ..SO JE KUNA ULAZIMA GANI WAKUWA AUTHORISE KWA KUWAUNDIA CHOMBO?SIO KUONGEZA GHARAMA SIZIZO ZA MSINGI? NA MOVE HII NAONA KAMA CHAMA KINAELEKEA KUPOKONYWA MAMLAKA YA MAAMUZI KWA WANACHAMA NA BADALA YAKE MAAMUZI MENGI YAWE YANAFANYA NA WACHACHE, MIE KWELI NAWAZA HIVYO WKT TUNAONGELEA KATIBA KUPUNGUZA MAMLAKA KWA WATU WACHACHE NAONA KAMA CCM KAMA INAKAZANA THE OTHER WAY AROUND YAANI KUTOA KWA WENGI KUPELEKA KWA WACHACHE..PENGINE LBD MIE SIJAELEWA NA TAFSIRI YANGU SI SAHIHI NAOMBENI WENYE UELEWA PENGINE ZAIDI KTK HILI TUWEKANE SAWA....[/QUOTE]

Naona maoni yako yana mantiki ila "pengine" the main driving force ya restructuring hii, ni kupunguza gharama za uendeshaji chama.

Kumbuka ni miaka mingi sana imepita toka mindset ya wana CCM ibadilike kutoka "What will i contribute to strengthen my Party na Kuwa what will the Party do for me". Hilo wazo lako litawezekama iwapo tu wanaCCM watakua tayari kuhudhuria mikutano na kujigharamia Fully malazi na matumizi yao.

Hebu imagine wakati wa mkutanao mkuu ikitokea ukawa Dodoma, unaamabiwa guest House Zote zimeshachukuliwa na CCM pamoja na kulipiwa kwa siku tatu. Vyumba zaidi ya 1500 kwa siku tatu, achilia mbali pocket posho ambayo sijui ni kiasi gani kwa kila mjumbe.

Tunaambiwa kuna sababu za kupunguza rushwa kwenye chaguzi, n.k
 
Tunaambiwa kuna sababu za kupunguza rushwa kwenye chaguzi, n.k[/QUOTE]

Brother,nimekuelewa na pengine ndio hivyo kupunguza gharama kama ulivyochambua jinsi matumizi yanavyokuwa makubwa wkt wa mkutano wa wajumbe..lkn kaka sio kila kitu kinaogopwa gharama. Utawala ni gharama?so?na pia ni market..!na hakuna market ambayo in run costless...tujue hayo tusije tumbukia kwenye mfumo wa ki bunge ambao wanachaguliwa kuwakilisha then baadae wanajiwakirisha wao hadi kipindi cha uchaguzi.I stll think mchakato hu wa mabadiliko hayo uangaliwe kwa mapana zaidi usikurupukwe hata kidogo.
 
Ndugu Mchambuzi nakushukuru kwa majibu, ingawa yamezaa maswali mapya.
Binafsi naona kama haujawa clear ni nini hasa unachokisimamia hapa. Maana post zako zina jicontradict hata within the same post.
Ningeshauri ukae chini ujue hasa ni nini conscience yako inakiamini halafu kama ikibidi ubadili ID ili ujadili kwa uhuru mpana fanya hivyo,
maana najua bado unapolitical ambitions na si vizuri kuwaparua wakubwa hasa unapokua na picha yako kwenye forum.

Tuanze na suala la akina Mramba, hapo hapo umesema CCM na serikali yake ilitaka kuwaonesha wananchi kuwa wako serious na vita ya ufisadi. Wakati huohuo Mwenyekiti ameonekana Rombo, Igunga, Bariadi na Monduli akiwanyanyua mkono na kuwaombea kura wagombea wa CCM kwenye uchaguzi mkuu wa 2010, Hata Makongoro Nyerere alipigia sana kelele hili kwenye kikao cha NEC, Aprili. Haingii akilini na haiitaji kwenda shule kuona CCM inawachezea watu kwenye suala la Ufisadi.

Halafu naomba nipingane na wewe, kwenye ukubwa wamNEC na mbunge. Kwa kuangalia mishahara na marupurupu na kwa vyama visivyokua na serikali ni kweli mbunge ni cheo cha juu. Lakini kwa chama chenye kuunda serikali kama CCM. NEC ndiyo chombo kinachounda sera ya kutekelezwa na serikali. Hivyo hata mbunge, midhali umepata ubunge kupitia hicho chama, mNEC atakupangia uende bungeni kupigania mambo gani, lakini siyo vice versa kwamba mbunge anaweza kumpangia mNEC aseme nini au kupigania nini kwenye NEC. Hapo naomba ukajipe maarifa zaidi.

Unamuongelea Nape the whole thread. Nashangaa unamuona Nape anachafua hali ya hewa wakati hata Mwenyekiti wenu kwenye tamasha la Injili alitamka waziwazi kwamba anayoyasema NAPE ndiyo msimamo wa NEC, na hakuna aliyejitokeza kumpinga JK kwa kauli yake hiyo, sasa mkuu mbona unarudia kulekule kwa wapambe wa mafisadi?...unajua Mzee Mwanakijiji aliwahi kusema, Where there is Right or Wrong, Good or Bad, a position of NEUTRALITY is a sign of WEAKNESS. Wewe unataka kuhave your cake and eat it too. CCM ikipasuka sasa haitakua kama unavyofantasize, kwamba ya Azimio la Arusha na Azimio la Zanzibar, ikipasuka itakua ni CCM pro Mafisadi na CCM against Mafisadi, which side will you take sir?

Unasema Mwenyekiti ni nafasi ya usimamizi tu!!... Please mkuu. Mwenyekiti anaset agenda ya term yake, anaset priority za policy, na ni wajibu wa mwenyekiti kuset ITIKADI ya chama, kwa kutambua dunia inabadilika. Baada ya kujua haya mambo makuu matatu zaidi ya kuongoza vikao, anatakiwa atumie USHAWISHI wake kama mwenyekiti ili yapite kwenye vikao vya maamuzi. Watu wanaposema Mwenyekiti anayumba ni kwa sababu hajatumia ushawishi wake unaoendana na kofia aliyoikalia kupitisha direction ya anapotaka chama kiende.

By the way NEC imeanza kuwa na nguvu kipindi hiki cha Awamu ya nne tu au hata huko nyuma? Na Wenyeviti waliotangulia walikua wanawaandaaje wajumbe kukiwa na very sensitive issue?

Hiyo ya 2012 inawezekana akafanya makubwa, ila kwa kweli its a toss!

Alwatan,
Nashukuru sana kwa mchangi wako mzuri; Kwanza na awali ya yote, sipo humu kutafuta cheo au uongozi; nipo humu kuzungumzia hoja zinazotokana na kukerwa kwangu na chama changu cha CCM kuyumba na msimamo wangu ni kwamba jambo la msingi linayokifanya kuyumba ni yaleyale aliyoyanena Marehemu Kolimba - hakuna dira; hatuna itikadi inayoeleweka, wapo wanaokiongoza kwa kupitia azimio la arusha, na wapo wanaokiongoza kwa kupitia azimio la zanzibar - kisera;

Suala la mimi kubadili ID yangu ili niweze kuzngumza kwa mapana sidhani kana ni jambo la maana kwangu kwani sina woga au unafiki katika nayoyazungumza, na hayo ni matatizo makubwa sana katika uongozi wa chama chetu, ukiongezea na fitina na ubinafsi;

Kuhusu Mwenyekiti kuwanadi watuhumiwa wa ufisadi katika kampeni, ni hoja yenye mashiko kwani imeshazungumziwa sehemu nyingi vilevile; lakini sote tunaelewa kwanini ilitokea hivyo; vinginevyo suala la msingi hapa ni kwamba utaratibu wa kuwashughulikia hao watuhumiwa ulitakiwa usiwe wa majukwaani, na wangewahi wakati ule kabla ya kampeni kufanyia haya mambo kupitia vikao ambavyo sasa ndio wameamua kufanya hivyo, pengine wangepatikana na hatia na tusingekuwa nao katika uongozi, who knows; vinginevyo as it stood as of October 2010, kwasababu utaratibu huo haukufuatwa, sikuona tatizo la mwenyekiti kwenda kuwainua mikono majimboni; kisiasa inawezekana lilionekana ni usanii, lakini kwa taratibu za chama, ilikuwa ni sahihi kama nilivyokwisha eleza;

Kuhusu Nape, sio kweli ninamuongelea the whole thread lakini kila inapotokea namna hiyo ni sahihi given title ya hii thread kwani
Nafasi ya katibu Itikadi, Siasa na Uenezi na Siasa katika chama cha Siasa ni nyeti na ni kiungo muhimu katika kujenga BRAND ya chama katika siasa za ushindani. Kwahiyo Nape ni Marketing Manager wa CCM; suala la brand equity lipo mikononi mwake, sasa kwanini nisimzungumzie? Nafasi ya katibu mwenezi ni sura ya Chama mbele ya umma, kwahivyo ni muhimu kwa kiongozi wake kuwa mbunifu na kuwa mwepesi wa kusoma mabadiliko ya mazingira ya siasa za nchi ili kuhakikisha kwamba chama kinaenda na wakati na kinakuwa kwenye mstari wakati wote. Ni kosa mimi kusema ni hatari kama anakuwa hana majibu ya uhakika juu ya itikadi ya chama chetu?Ni kosa mimi kuumizwa pale vijana wa UVCCM wanapoimba mbele yake kwamba 'KAULI YETU NI KULINDA SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA' na yeye kutabasamu na kupiga makofi? Suala hili ni timing bomb, na Nape ana nafasi ya ku influence ili haya yabadilike kabla vijana wa UVCCM hawajagundua kwamba kumbe wanadanganywa kwani wanaokaa meza kuu ni mabwanyenye na mabepari yanayofurahia nyimbo za vijana wa UVCCM wakiimba kwa furaha na shangwe kazi yao ni kulinda siasa ya ujamaa na kujitegemea; Kama hulioni tatizo hili, basi ni sahihi kuona kana kwamba ninamuandama Nape;

Vinginevyo, kama umekuwa unanisoma tangu mwanzo, ninachosema kuhusu Nape kimsingi ni kwamba aachane na siasa za mafisadi kwani ni uzao wa azimio la Zanzibar, suala la gamba haliwezi tatuliwa kwa mwendo wa sasa, lazima itikadi zigawanywe; na Nape ana mengi ya kufanya to rebrand the party in public while mengine yanafanyika kwenye vikao; vinginevyo bila kutenganisha itikadi za vyama, gamba hili sio la kobe au nyoka, ni la kitunguu, uta peal mpaka kitunguu kiishe;

Kuhusu nafasi ya ubunge na MNEC, maelezo yako yamegusa palepale ninapozungumza kwani umeonyesha jinsi gani nafasi ya NEC ina nguvu katika maamuzi ingawa haina maana kwamba ni nafasi ya juu kuliko ubunge; kwahiyo vikumbo vya sasa ni kupigana ili kubaki katika nafasi za maamuzi ya huko tuendako, otherwise wasingekuwa wanahimiza watu kujitoa MNEC bila kujali mtuhumiwa kubakia kwenye ubunge;

Kuhusu Mwenyekiti kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi magumu, upo sahihi lakini mkitoka kwenye vikao, kama watendaji wanaenda tekeleza kinyume inakuwaje? tumesoma kwenye magazeti juzi jinsi gani kiongozi mmoja mzito wa kamati kuu alivyokuwa anapingana na katibu mkuu wake - CCM - Mukama na kufikia hatua ya kutishia kujiuzulu, only to calm down later alipogundua kwamba hata mwenyekiti ana msimamo ule ule; huu ni ushahidi tosha kwamba pamoja na kwamba mwenyekiti kuwa ndiye kiongozi mkuu wa chama, huko chini madudu mengi sana kiutendaji na kiutekelezaji hutokea; solution ya yote haya mimi nadhani ni uchaguzi mkuu wa chama 2012, ingawa nakubaliana nawe kwamba its a toss.
 
CCM haikuingia ubia na CUF mkuu.

Serikali ya umoja kati ya CCM na CUF Zanzibar si ni serikali ya mseto au? Pengine nina uelewa mdogo katika hili; Na katika mazingira ya kawaida, si katiba ya Chama inatakiwa iwe ina anticipate hayo and therefore have that provision? Swali langu la msingi hapa ni je, ni katika mwongozo upi au katiba ipi suala la CCM kuunda serikali ya mseto na chama cha upinzani linafafanuliwa kama vile Chadema wanavyofanya katika katiba yao? Au kwa CCM suala hili lilitokana tu na azimio la kikao. Hoja yangu ya msingi ni kwamba, suala la mseto linahitaji mwongozo na ni lazima uwepo kikatiba;unless CCM zanzibar na CCM bara wana katiba tofauti;
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom