CCM & TLP zinaendelea kung'ara chadema hoi bin tabani Arumeru East

NAPE WAPIKE VIJANA WAKO HAWA ILI WAKUFAE ZAIDI NA KUTUPUNGUZIA KERO ZA KUANZISHA UTITIRI WA THREADS ZISIZO NA MANTIKI YOYOTE HAPA UKUMBINI KILA WAKATI

Nape, ni kweli tunahitaji changamoto kama hizi kutoka kwa vijana wako hawa hapa jamvini ila matatizo yao makubwa zaidi ni kwamba wengi wao ni:

1. Wepesi wa kuanzisha utitiri wa THREADS humu na kuzikimbia dakika hiyo hiyo,

2. Uwezo wa kujenga hoja au kutetea ni - 98 % hivyo inawawiia vigumu sana kutekeleza wajibu wao kwako ipasavyo,

3. Wanatoa madai mengi bila kufanya utafiti wowote wala kuweka uthibitisho wowote ule,

4. Ni hodari wa aina mipasho inayohitajika kwenye zile kurasa za jokes ...

NB: Mkuu Nape kabla haujaongezea malipo hawa ni vema ukawaandalie workshop ili watu waje kukusaidia kuwapiga msasa ili ukiwamwaga humu hata 20 tu hivi basi hata hiki chama chako ajuza (CCM) huenda kikajihisi umri wa ujana wake tena hapa jukwani.

Seriously do something Nape la sivyo vijana wako wataendelea kama hivi kuchomo THREAD za zamani kama hii hapa na kuirusha upya hewa na wao kukimbia kama kawaida yao.

Hakika hadi hivi sasa tumechoshwa mno na SUBSTANDARD THREADS AND ARGUEMENTS za hivi vijana vituko ulivyovimwaga hapa ukumbini bila wao kujua hata la kufanya zaidi tu ya kutamani kuonekana wako bize kama hivi.
 
Uwezo wa akili yako ni sawa na punje ya Ulezi
Acha uongo wewe, punje ya ulezi ina uhai ikipandwa kwenye ardhi yenye rotuba nzuri na ikapata mvua kwa wakati muafaka inaweza ikatoa mavuno makubwa sana. Huyu Jamaa akili zake ni kama Jiwe
 
Hakyamama ccm wanashinda . Tarehe 1 siyo mbali.

Usimuapize mama yako bure, na kama unamheshimu huwezi kumlinganisha na marehemu ccm. acha kutumia masaburi kufikiri. umenunuliwa kwa sahani ya ubwabwa na pakiti ya chumvi, unaanza kuropoka
 
Nasikitika JF imevamiwa. Kuna viumbe wanalipwa kwa ajili ya kiipigia debe CCM na kuchafua vyama vingine. Ninachokiamini ni kwamba CCM si lolote, si chochote. Hakuna ushindi wa CCM ulio wa uhalali, bali ni uchakachuaji tuu. Hawa akina Bucho, secondID, Mr Emmy na wengineo si wanaharakati wenzetu, bila shaka ni wanachama wa UVCCM. Hii nchi ilikofikia, ni aibu kwa kijana yeyote kuipongeza CCM. labda wafanye hivyo akina Nape, Januari Makamba, Ridhiwan na wenzao maana wale wanajua wanachokipata CCM. Lakini kwa mzalendo wa nchi hii, anayeitakia mema na anayefikiria hatima ya nchi hii kwa miaka 50 hadi mia ijayo, lazima angekuwa wa kwanza kuunga mkono vugu vugu la mabadiliko linaloendelea.
Hakyamama ccm wanashinda . Tarehe 1 siyo mbali.
 
waamuzi ni wana arumeru nyote mtapiga kelele hadi povu za mdomoni ziwatoke lakini wengine tarehe 1.4.2012 tuwaone humu jf, na sababu eti tumeibiwa hatuzitaki.
 
Huyu jamaa ni mwongo sana, mimi nimetoka jana huko kwetu arumeru, kiukweli ccm wana hali mbaya sana, hata kule mbuguni walipokua wakipategemea sana hasa kutokana na misaada toka mirerani kwa akina nyari na ole sendeka napo tumaini linakufa. Kinachoigharimu zaidi ccm mbali na uwepo wa Makumira university na arusha university, ukiunganisha na vyuo kama tengeru na Patandi, wakazi wengi wa arumeru mashariki ni waelewa, kama mjuavyo sehemu kubwa ya wakazi wa mijini hapa tz hawaipendi ccm, na ukiangalia vema utagundua sehemu kubwa ya arumeru mashariki ni urbanized. Usa, kikatiti, mbuguni, tengeru, leganga, na maeneo mengi kama ngarasero. Ama hakika ccm ilizaliwa 2/5/1977 dar es salaam, ilikufa 10/3/2012 na itazikwa rasmi 01/04/2012 pale Usa river, Mungu ailaze roho yake mahali pema ili watu waikumbuke vizuri. Amen
Asante sana kwa update mkuu
 
Unajua kama hauko Arumeru utasema lolote, lakin ukija kwenye ground yenyewe utaon mambo yalivyo magumu kwa CCM, juzi nilikuwa kwenye mkutano wa TLP wakaongea weeeee, mwishoni wakaonyesha alama ya CHADEMA,utasema je TLP wanaonyesha uhai?
ARUMERU wanasema bora UKIMWI kuliko CCM
 
Chama cha mapinduzi (CCM) kimeendelea kung'ara na kuteka hisia za wananchi wa jimbo la Arumeru hali inayokipa wakati mgumu CHADEMA. Baada ya viongozi wakuu wa chama hicho kukumbwa na shutuma za kifisadi hali ndani ya kamati kuu ya uongozi si nzuri na hiyo imesababisha Viongozi wa chama hicho kushindwa kupanga mikakati ya ushindi ya chama hicho na kuelekeza nguvu katika kujibu tuhuma ama kuficha uthibitisho wa tuhuma zinazowakabili.

Upepo wa kisiasa unaovuma jimboni arumeru unaweza kukifanya Chadema kupoteza mtaji wa kura ilizinazo kama CUF ilivyofanya kule Igunga. Aidha Chama cha TLP kinaendelea na kampeni zake vizuri na dalili zote zinaonekana kitashika nafasi ya pili wakati CCM kikishinda uchaguzi huo.
Updates
SAU wazindua kampeni kwa kishindo Arumeru east wazidi kupunguza nguvu ya upinzani
Endelea tu kuota, utakapozinduka tar 02/4/2011 usisahau kutuwekea hii thread.
 
akili yake basi kubwa kama chembe ya ulezi mi nadhan haradani! huyu kama watu basi ni wasira, kama ngombe basi ni tule aliyeasiwa, au kaamka na hangover baada ya kunyweshwa na magamba afu hawamnunulii supu, hahahaha magamba bwana, this time mnalo!mda wenu umeisha wakati
 
waamuzi ni wana arumeru nyote mtapiga kelele hadi povu za mdomoni ziwatoke lakini wengine tarehe 1.4.2012 tuwaone humu jf, na sababu eti tumeibiwa hatuzitaki.

Nyie mko wap kwan? Au ndo mmeamua kuwaunga mkono mume wenu Ccm?
 
Back
Top Bottom