CCM taabani Bukombe

Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,286
4,492
Hali ya kisiasa kwa CCM jimboni Bukombe ni ngumu sana. Prof Kahigi Mgombea wa CHADEMA anakubalika kuliko maelezo, bendera na vipeperushi vya CCM vimetolewa na kuchomwa moto! Wananchi wamekataa kabisa ujinga wa CCM na ahadi zao za alinacha. Emmanuel Vuhahula mgombea wa CCM anategemea kura za kuchakachua tu ila CHADEMA wataleta mawakala na wasimamizi wao kutoka Tarime maana hao wanajulikana kwa umakini wa kuzuia wizi wa kura. Nimetembelea Masumbwe na Lunzewe, Katoke, Nyamakunkwa, Ushirombo na Iyogelo hizo ni kata kubwa kwenye jimbo hili. Wananchi wamekuwa wakizomea na kutawanyika kwenye mikutano yote ya CCM na Vuhahula hajui la kufanya jimbo linaondoka kwake.

Prof Kahigi endelea kumwaga sera!
 
hongera chadema kwa kupita bila kupingwa...tayari mna jimbo moja mkononi kabla ya uchaguzi....CCM INA VITI 21 VYA UBUNGE NA 500 VYA UDIWANI....15% YA VITI VYOTE....! je nchi huchukuliwa kwa kuachia viti vyote hivyo?
 
Mzee wa upupu hivi CUF wna viti vingapi so far?
 
Jamani, yasije kuwa kama ya Busanda mwaka jana, CCM walizomewa weee baadae upinzani tukaanguka.

Tuendelee kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha hawa wakereketwa wanatoka kwenda kupiga kura, kuhakikisha hatuibiwi kura, na ku focus kwenye kuvutia wengine zaidi na zaidi kununua sera za CHADEMA.

Vinginevyo yatakuwa ya "chenga twawala."
 
Kosa la Busanda halirudiwi huku!
 
Safi sana Chadema.
Mageuzi huanza na wewe.
Umejiandaa je kuleta mageuzi jimboni mwako?
 
hongera chadema kwa kupita bila kupingwa...tayari mna jimbo moja mkononi kabla ya uchaguzi....CCM INA VITI 21 VYA UBUNGE NA 500 VYA UDIWANI....15% YA VITI VYOTE....! je nchi huchukuliwa kwa kuachia viti vyote hivyo?

Mataputapu ya leo hayana adabu, yanakuongoza vyema sana Mzee wa Masematiksi, sijui Ma Muuza kaweka nini
 
Wewe vipi jibu la Masa umelifuta halafu unauliza tena unafikiri sisi hatuoni, jibu ni hilo hilo ulilolifuta.
Ndugu, hapa huwezi kufuta andiko la mtu, kuna rekodi. Nilichofanya ni kunukuu kipande ambacho niliona kinahusiana na Busanda. Hayo ya Bihalamuro niliona siyo niliyouliza.

Sasa kama alikusudia kile alichosema kuhusu Bihalamuro pia kieleze kilichofanyika Busanda basi angetumia umakini kwenye kuunda sentensi yake. Hakuweka koma baada ya neno Bihalamuro.

Ukisema "Nadhani CHADEMA walifanya makosa Busanda na Bihalamuro CCM waliiba kura na kununua mawakala wa wapinzani!" maana yake, kwa nilivyofundishwa darasa la kwanza mpaka la tatu, ni kwamba Bihalamuro ndio kuliibiwa kura na kununuliwa wapinzani. Angaweka koma kabla ya neno CCM basi yote baada ya koma yangehusisha Buhilamuro na Busanda. Soma tena hiyo sentensi yake unaweza kunielewa.

Tutawezaje kuchukua uongozi wa nchi, wapinzani wenzangu, kama hatuko makini kwenye ufasihi wa mawasiliano na pia wakati mwingi kujawa na jazba?
 
Kumbe ulielewa unajifanya kulizunguka jibu.
 
Hapana, ni baada ya wewe kuonyesha kilichonuiwa kuandikwa mara ya kwanza.

Mwanzoni ilivyoandikwa ndivyo ilivyoeleweka, kumbe alimaanisha kitu kingine. Hakuwa makini, na wewe ukarukia kunishambulia mimi kwa kitu ambacho kumbe kilikosewa na mwandishi kwa kutozingatia au kutojua misingi ya uandishi ya tangu darasa la kwanza mpaka la tatu. Cha ajabu yeye huyo huyo ndio akanifananisha mimi na mlevi kwa kukichukulia kile alichoandika kwa maana yake halisi.

Hapa nimejifunza kwamba kumbe walevi huwa wanawaona ambao hawajalewa ndio walevi.

Nilikuwepo.
 
Ndugu, hapa huwezi kufuta andiko la mtu, kuna rekodi. Nilichofanya ni kunukuu kipande ambacho niliona kinahusiana na Busanda. Hayo ya Bihalamuro niliona siyo niliyouliza.

Sasa kama alikusudia kile alichosema kuhusu Bihalamuro pia kieleze kilichofanyika Busanda basi angetumia umakini kwenye kuunda sentensi yake. Hakuweka koma baada ya neno Bihalamuro.

Ukisema "Nadhani CHADEMA walifanya makosa Busanda na Bihalamuro CCM waliiba kura na kununua mawakala wa wapinzani!" maana yake, kwa nilivyofundishwa darasa la kwanza mpaka la tatu, ni kwamba Bihalamuro ndio kuliibiwa kura na kununuliwa wapinzani. Angaweka koma kabla ya neno CCM basi yote baada ya koma yangehusisha Buhilamuro na Busanda. Soma tena hiyo sentensi yake unaweza kunielewa.

Tutawezaje kuchukua uongozi wa nchi, wapinzani wenzangu, kama hatuko makini kwenye ufasihi wa mawasiliano na pia wakati mwingi kujawa na jazba?

Shida yako ni ufahamu kitu ambacho siwezi kukusaidia!
 
Namfahamu Prof Kahigi
Ni makini na adili
Naamin CCM wamechemsha mpaka sasa bado kubwagwa kwenye sanduku very soon.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom