Uchaguzi 2020 CCM sio kila hoja ni ya kupinga, namna nyingine ya kupinga hoja ni kuiboresha zaidi

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,604
Alichokifanya Polepole leo, ni kitendo cha aibu na kudhalilisha watanzania wenye maono ya kuona nchi yao inavuka kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine.

Dunia isingeweza kufanya mapinduzi makubwa ya maendeleo kama kila jambo lingekuwa linapingwa tu, eti kwasababu limetolewa na mtu usiyempenda ama ambaye mnatofautiana kiitikadi.

Tundu Lissu jana kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, aliongea hoja nzuri sana kuhusu suala la kuwa na sera ya lugha ambayo inaweza kuisadia hii nchi kutoka ilipo na kwenda level nyingine. Ni ukweli usiopingika, kwa nchi masikini kama Tanzania, huwezi kuwa na watu ambao ukiwatoa nje ya dunia wanaweza kufa kiu kwa kushindwa kuomba maji. Kuna wapuuzi wanajaribu sana, kusema eti, mbona China wanaongea kichina na wana maendeleo? Upuuzi mtupu.

Lissu ameadress hoja nzito, nilitegemea kuwaona CCM ama Polepole, wakija kuliboresha zaidi wazo la Lissu na ikibidi kuwe na mjadala wa kitaifa wa hili suala, ili tuweze kuona ni namna gani hili suala linaweza kufanikiwa, na kuwafanya watanzania wawe ni watu ambao wanaweza kujidai ndani na nje ya Tanzania.

Ni upumbavu kupinga kila hoja.
 
Unasema "Dunia isingeweza kufanya mapinduzi makubwa ya maendeleo kama kila jambo lingekuwa linapingwa tu, eti kwasababu limetolewa na mtu usiyempenda ama ambaye mnatofautiana kiitikadi."

Kwani huyo Lissu aliyetoa unachodai "hoja nzito" aliwahi wapi kukubaliana na chochote ambacho CCM inafanya?

There's a saying that says "Don't give everything to a person that isn't giving you anything".
 
😀😀😀
Unawasema wapinzani.. ila mudomo kukuwasha lazima ukumbuke chama bombaaaa.. Rais Jembe.. ukuongelee CCM

Magufuli 2020💯
 
😀😀😀
Unawasema wapinzani.. ila mudomo kukuwasha lazima ukumbuke chama bombaaaa.. Rais Jembe.. ukuongelee CCM

Magufuli 2020💯
Kwahiyo Polepole aliyekuwa anapingana na hoja Murua za Lissu naye ni mpinzani? maana ndo nimemsema leo
 
CCM ya Magufuli hakuna utulivu, ni mwendo kasi kwa kila jambo.
Kwanza huo Uwelewa wa kutulia na kufanyia kazi mawazo mazuri ya WAPINZANI hawana. Wao wanawaza kuua upinzani na wapinzani wenyewe basi.
 
Sifa mojawapo ya kuwa ccm ni lazima uwe na upoyoyo fulani...China ya sasa Inafahamu umuhimu wa lugha hasa kiingereza ndio maana imefanikiwa kukaa kwenye ramani ya dunia kiuchumi
Nilienda Poland nikashangaa jinsi Wa'polish' wanavyochangamkia fursa za ajira Jumuiya ya Ulaya: wale niliokutana nao kati yao walikuwa wanajua lugha tano Polish, Russian, English, French na German. Walinifanya na mimi nianze kupenda kujifunza lugha zaidi ya zile ninazozifahamu.
 
Wewe mwenyewe hukumuelewa Lissu alichomaanisha unahamisha goli na kwenda kumsigina mtu mwingine?

Kama Lissu hukumuelewa utaelewaje alichosema HarakaHaraka?
 
Nilienda Poland nikashangaa jinsi Wa'polish' wanavyochangamkia fursa za ajira Jumuiya ya Ulaya: wale niliokutana nao kati yao walikuwa wanajua lugha tano Polish, Russian, English, French na German. Walinifanya na mimi nianze kupenda kujifunza lugha zaidi ya zile ninazozifahamu.
Kama mtu hajapata nafasi ya kusafiri na kuiona dunia ilivyo hawezi kuelewa dhana ya kujua lugha zaidi ya moja
 
Kwa hiyo unataka kusema Tanzania haina sera ya lugha? Unataka kusema majaji na watanzania hawajui kiingereza kiasi kwamba wakiongea Lissu inabidi ajifiche uvunguni?
Chagu. Nyerere wakati anastaafu aliainisha mambo waliofanya vizuri na yale yaliowaendea kombo. Alisema kweli Kiswahili kimefanikiwa kuwaunganisha wananchi kama taifa. Lakini alitoa Rai kuwa watu wakazanie English kwa sababu ni KISWAHILI cha dunia .

Leo hii mtz , nje ya mipaka yetu ni bubu.
 
Jaduong usikariri maneno ya wanasiasa waongo. Nenda Botswana wamejaa watanzania wanafanya kazi za maana. Nenda Usa kuna maelfu ya watanzania wanafundisha huko. Kwa hiyo tusipotoshe watu Tanzania inatumia Swahili na English lakini kuwatukana watanzania hawajui English ni makosa. Kwani English ni mother language yetu? Mbona wajeruman wanaishi bila hiyo English?
 
Back
Top Bottom