Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,608
Alichokifanya Polepole leo, ni kitendo cha aibu na kudhalilisha watanzania wenye maono ya kuona nchi yao inavuka kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine.
Dunia isingeweza kufanya mapinduzi makubwa ya maendeleo kama kila jambo lingekuwa linapingwa tu, eti kwasababu limetolewa na mtu usiyempenda ama ambaye mnatofautiana kiitikadi.
Tundu Lissu jana kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, aliongea hoja nzuri sana kuhusu suala la kuwa na sera ya lugha ambayo inaweza kuisadia hii nchi kutoka ilipo na kwenda level nyingine. Ni ukweli usiopingika, kwa nchi masikini kama Tanzania, huwezi kuwa na watu ambao ukiwatoa nje ya dunia wanaweza kufa kiu kwa kushindwa kuomba maji. Kuna wapuuzi wanajaribu sana, kusema eti, mbona China wanaongea kichina na wana maendeleo? Upuuzi mtupu.
Lissu ameadress hoja nzito, nilitegemea kuwaona CCM ama Polepole, wakija kuliboresha zaidi wazo la Lissu na ikibidi kuwe na mjadala wa kitaifa wa hili suala, ili tuweze kuona ni namna gani hili suala linaweza kufanikiwa, na kuwafanya watanzania wawe ni watu ambao wanaweza kujidai ndani na nje ya Tanzania.
Ni upumbavu kupinga kila hoja.