CCM sasa kwisha! - Kingunge Ngombale-Mwiru

anasema chama hicho kimepoteza nguvu kukabili wapinzani, adai oparesheni sangara ya chadema inawatesa.

Asema misingi yote ya tanu, asp imetoweka. Mwanasiasa mkongwe huyo alitoa kauli hiyo alhamisi (jana) kwenye mkutano mkuu wa nane wa uvccm alipopewa nafasi ya kuzungumza na kutoa nasaha zake.

Aliongeza kusema pamoja na ccm kuwa na mtandao na nguvu kubwa, hakijui kutumia nguvu hizo, kama ilivyokuwa katika enzi za tanu na asp.

Kuhusu wapinzani hasa chadema alisema “chama hicho kinaendesha operesheni sangara sisi tupo, uvccm na ccm inakiachia chama hicho kuzunguka nchi nzima sisi kimya, wanaendelea kuimarika….. Sijui hii inatokana na usingizi au sijui ni kutosheka………”

hii ni habari kuu ukurasa wa mbele wa gazeti la mtanzania ya leo na habari kamili iko ukurasa wa 3.

my take hapo kwenye red:
huenda viongozi wa ccm na uvccm wanabweteka kwa sababu wanategemea sana vyombo vya dola (eg policcm) kupunguza nguvu ya cdm hasa katika ule mpango uliosukwa wa kila mara kujaribu kukionyesha chama hicho kuwa ni cha vurugu.

hapo ukipopigia red.....mzee anazeeka vibaya, alitegemea ccm nayo izunguke mtaani kufanya operation badala ya kudeliver to the expetation???

Halafuu huyu mzee pia ni kirusi....pamoja na kujifanya si muumini wa dini yeyote ... Jk alimtuma misikitini morogoro kumwombea kura dakika za majeruhi .......mnafiki mkubwa
 
Huyu Kingunge ndiye mchimba kaburi la CCM. Alipotoa ushauri wake pale Chimwaga kuwa bora tuwe na mgombea anayechagulika hata kama hana uwezo wa kuongoza alitegemea nini? Urais sio kuchagulika ni sifa ya kiongozi aliyeko kwenye nafasi. Uongozi ni output sio sura. Wakati Hayati Mwalimu Nyerere anasema urais ni sifa, sio popularity yeye Kingunge anasema urais ni kuchagulika. Bado Kingunge anapaswa afahamishwe kuwa ushindi wa chama sio kampeni pekee yake ni pamoja na utendaji. Hata kama CCM watapiga kampeni mchana kutwa na usiku kucha kama uchumi una dorola, elimu hafifu, matibabu hakuna shida ya leo afadhali ya jana, wananchi wataendelea kuichukia CCM na kuipenda operation Sangara na M4C ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo.
Nitoe mfano wa uchaguzi wa 1995 uliomuweka madarakani Mheshimiwa Mkapa. Hayati Mwalimu Nyerere alisimama kidete kuuelimisha uuma wa watanzania kuwa Mkapa hafahamiki na wengi lakini anazo sifa za uongozi. Baada ya uchaguzi hasa awamu ya ya kwanza ya miaka mitano wananchi walikiri maneno ya mwalimu kuwa Mkapa kweli alikuwa kiongozi bora. NGUVU YA UPINZANI ILI SHUKA kwa kuwa walikosa kuungwa mkono na wananchi walio wengi walioshuhudia mabadiliko ya maendeleo. Kampeni za urais kwa awamu ya pili zilikuwa rahisi sana kwa CCM. Si busara kuendelea kuwalaumu vijana (UVCCM) wakati yeye Kingunge Ngombale Mwiru ni kinara wa siasa za fitina na unafiki, mtu asiyeona mbele hata cm moja. Bahati mbaya hata chama chake bado kinaendelea kumuona kama mtu wa maana ya Hazina ya chama wakati hazina yeyewe ilikwishaliwa na mchwa wa ubinafsi imebakiwa na fitina. CCM ikiendelea kucheka naye haitalia naye itakaposhindwa kwa maana yeye amekwisha kufariki bado kuchimbiwa kaburi tu. Kingunge hatashuhudia kushindwa kwake. Mapenzi ya wananchi kwa chama cha siasa hayaletwi na mabomu ya kuuwa Waandishi wa habari kama vile Mwangosi, kuteka na kutesa madaktari kama vile Dk Ulimboka, propaganda kama vile M4C la hasha, yanaletwa na kuwapenda wananchi na kuwaletea maendeleo ya kweli.
 
je mchango wa kingunge ni upi katika chama na nchi ya tanzania.
Je yeye alitumika kama hirizi ya chama, hivi kwamba anaonwa kutoswa ni kama sasa chama hakina ulinzi na uhakika kimekwisha?
Ufafanuzi tafadhali wadau.
 
Kitu ambacho ni kigumu kwa nyakati hizi ni kwamba NANI KUTOKA CCM ATASIMAMA HADHARANI NA KUKEMEA MAOVU NA WAOVU KWA KUWATAJA NA KUWATAKA WAACHE?
 
Huyu Kingunge ndiye mchimba kaburi la CCM. Alipotoa ushauri wake pale Chimwaga kuwa bora tuwe na mgombea anayechagulika hata kama hana uwezo wa kuongoza alitegemea nini? Urais sio kuchagulika ni sifa ya kiongozi aliyeko kwenye nafasi. Uongozi ni output sio sura. Wakati Hayati Mwalimu Nyerere anasema urais ni sifa, sio popularity yeye Kingunge anasema urais ni kuchagulika. Bado Kingunge anapaswa afahamishwe kuwa ushindi wa chama sio kampeni pekee yake ni pamoja na utendaji. Hata kama CCM watapiga kampeni mchana kutwa na usiku kucha kama uchumi una dorola, elimu hafifu, matibabu hakuna shida ya leo afadhali ya jana, wananchi wataendelea kuichukia CCM na kuipenda operation Sangara na M4C ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo.
Nitoe mfano wa uchaguzi wa 1995 uliomuweka madarakani Mheshimiwa Mkapa. Hayati Mwalimu Nyerere alisimama kidete kuuelimisha uuma wa watanzania kuwa Mkapa hafahamiki na wengi lakini anazo sifa za uongozi. Baada ya uchaguzi hasa awamu ya ya kwanza ya miaka mitano wananchi walikiri maneno ya mwalimu kuwa Mkapa kweli alikuwa kiongozi bora. NGUVU YA UPINZANI ILI SHUKA kwa kuwa walikosa kuungwa mkono na wananchi walio wengi walioshuhudia mabadiliko ya maendeleo. Kampeni za urais kwa awamu ya pili zilikuwa rahisi sana kwa CCM. Si busara kuendelea kuwalaumu vijana (UVCCM) wakati yeye Kingunge Ngombale Mwiru ni kinara wa siasa za fitina na unafiki, mtu asiyeona mbele hata cm moja. Bahati mbaya hata chama chake bado kinaendelea kumuona kama mtu wa maana ya Hazina ya chama wakati hazina yeyewe ilikwishaliwa na mchwa wa ubinafsi imebakiwa na fitina. CCM ikiendelea kucheka naye haitalia naye itakaposhindwa kwa maana yeye amekwisha kufariki bado kuchimbiwa kaburi tu. Kingunge hatashuhudia kushindwa kwake. Mapenzi ya wananchi kwa chama cha siasa hayaletwi na mabomu ya kuuwa Waandishi wa habari kama vile Mwangosi, kuteka na kutesa madaktari kama vile Dk Ulimboka, propaganda kama vile M4C la hasha, yanaletwa na kuwapenda wananchi na kuwaletea maendeleo ya kweli.
Kama ni kuonywa na wapenzi na wanachama wake , CCM imepataushauri mwingi tu na kutoka sehemu mbali mbali.

Walikuwepo kina Kitine, Warioba,Sumaye Kaduma na wengine wengi tu waliotoa mawazo mbadala kurekebisha mambo katika msimamo na mwenendo wa chama , lakini wapi!

Kumomonyoka kwa umaarufu wa CCM hautokani na sera za CHADEMA, la hasha, bali chama chenyewe kuishiwa upeo wa kuona yaliyo mbele, kukumbatia viongozi wasio na maadili la kijamii, kufumbia macho ufisadi, hivi ndio vinavyo kiua chama.

Sasa hata akisema Kingunge hakuna tofauti yoyote itakayotokea.
Kimsingi chama chetu kinakosa mvuto kwa kutokuwa na sera wala dira zinazoeleweka , hasa zile za kuwabeba masikini na vijana.

Bila dira , mvuto na hata sera zinazoeleweka, kuonyesha kule tunakoelekea mwisho wake ni kuchukiwa na wananchi.
CCM inafanya makosa kuelemea katika kutawala badala ya kuongoza.

CCM ilikuwa na think tanks wazuri tu tena wenye kuweza kuleta michanganuo ya kitaifa katika uchumi na hata kijamii ili kuleta mshikamano, wapi kina Prof mbwiliza?
Kulikuwa na wachumi wa kitaifa ambao wangeweza kutengeneza michanganuo inayotekelezeka na kuendeshwa na waTanzania wenyewe, lakini sasa mambo si hivyo.

Tumeona uchaguzi mkuu katika nafasi mbali mbali za CCM nchini, hata hivyo sioni unafuu wowote katika kupata matumaini mapya, na hata Mwenyekiti wa CCM ameona sana sana kutapakaa kwa rushwa, kitu ambacho ni mmomonyoko mkubwa wa uhai wa CCM.

Bahati mbaya sana ni kwamba kila kiongozi anapenda kuwa mwanaiasa, lakini bado sijaona mwanasiasa anayeunganisha nyanja zote za siasa,uchumi na maendeleo , kitu ambacho ndio matumainio ya wananchi masikini na walio wengi.
 
ccm si rahisi hivyo kufa, na hata ikibidi ife mpaka ilazimishwe.
Ccm ni zaidi ya chama ni genge/kampuni yenye hamu ya kutajilika, kujilimbikizia mali na ufahari wa uwezo na nguvu za kuogopya.
Hapa si mahali pa watu tegemezi na wanyonge, ni kwa wababe na wenye nguvu za pesa na majina makubwa, au vinginevyo uwe na sifa za ziada za kibinadamu kama uzuri/urembo na umahiri wa 'propaganda'
Kuwatoa kwenye dola inahitaji dhamira ya kweli ya wanyonge
 
Kolimba alionaga mbali saaaana ambako CCM kipindi kile hawakuona kama wasingemkolimba na kufuata ushauri wake labda hili anguko lisingekuwepo lkn Mungu yu mwema wao walimkolimba badala yakuchukua maoni kwake na nini kifanyike
 
Sielewi kwanini tamko la Mzee Kingunge linapewa uzito mkubwa namna hii; Hivi mpaka leo wapo wanachama wa CCM wanaosubiri mtazamo wa Mzee Kingunge ndio wafanya uamuzi wa aidha kuendelea kuwa wanachama au kuhama chama? Viongozi wa maana watakuwa ni wale tu wataanzia pale alipoishia Marehemu Kolimba kwamba: "CCM Haina Dira", kwani ni kutokana na ukosefu wa Dira ndio maana CCM kwa miaka 20 sasa inatanga tanga pamoja na kina Mzee Kingunge;
 
Anasema chama hicho kimepoteza nguvu kukabili wapinzani, adai Oparesheni Sangara ya Chadema inawatesa.

Asema misingi yote ya TANU, ASP imetoweka. Mwanasiasa mkongwe huyo alitoa kauli hiyo Alhamisi (jana) kwenye mkutano mkuu wa nane wa UVCCM alipopewa nafasi ya kuzungumza na kutoa nasaha zake.

Aliongeza kusema pamoja na CCM kuwa na mtandao na nguvu kubwa, hakijui kutumia nguvu hizo, kama ilivyokuwa katika enzi za TANU na ASP.

Kuhusu wapinzani hasa CHADEMA alisema “chama hicho kinaendesha Operesheni Sangara sisi tupo, UVCCM na CCM inakiachia chama hicho kuzunguka nchi nzima sisi kimya, wanaendelea kuimarika….. sijui hii inatokana na usingizi au sijui ni kutosheka………”

Hii ni habari kuu ukurasa wa mbele wa gazeti la Mtanzania ya leo na habari kamili iko ukurasa wa 3.

My Take hapo kwenye red:
Huenda viongozi wa CCM na UVCCM wanabweteka kwa sababu wanategemea sana vyombo vya dola (eg policcm) kupunguza nguvu ya CDM hasa katika ule mpango uliosukwa wa kila mara kujaribu kukionyesha chama hicho kuwa ni cha vurugu.

Sio tu policcm bali sasa wameanza kutumia JWTZccm, potelea mbali watatumie tu watatuua wabaki wao wenyewe na mwisho wa siku watauana wenyewe kwa wenyewe.
 
Mzee kashindwa tu kusema kuwa "Tuliipenda sana ccm ila bwana kaipenda zaidi RIP ccm.,.."
 
Kweli anazeeka vibaya bana, alikuwa wapi siku zote hadi anawastua vijana kushakucha? wafanye kitu gani sasa kugeuza mambo?
yaani akae kimya kwakuwa hakusema mapema?. hata kama amechelewa lakini angalau amesema. tukianza kuulizana siku zote tulikuwa wapi basi kwa kila jambo tutaona tumechelewa na kamwe hatutabadilika- si kwa siasa tu ni kwa kila jambo ktk maisha. aidha huu ndo wakati wa watu kumpa vidonge vyake huyu mzee, si kwa kusema amechelewa , aeleze basi nini kifanyeke,
 
Back
Top Bottom