CCM sasa kwisha! - Kingunge Ngombale-Mwiru

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Anasema chama hicho kimepoteza nguvu kukabili wapinzani, adai Oparesheni Sangara ya Chadema inawatesa.

Asema misingi yote ya TANU, ASP imetoweka. Mwanasiasa mkongwe huyo alitoa kauli hiyo Alhamisi (jana) kwenye mkutano mkuu wa nane wa UVCCM alipopewa nafasi ya kuzungumza na kutoa nasaha zake.

Aliongeza kusema pamoja na CCM kuwa na mtandao na nguvu kubwa, hakijui kutumia nguvu hizo, kama ilivyokuwa katika enzi za TANU na ASP.

Kuhusu wapinzani hasa CHADEMA alisema "chama hicho kinaendesha Operesheni Sangara sisi tupo, UVCCM na CCM inakiachia chama hicho kuzunguka nchi nzima sisi kimya, wanaendelea kuimarika….. sijui hii inatokana na usingizi au sijui ni kutosheka………"


Hii ni habari kuu ukurasa wa mbele wa gazeti la Mtanzania ya leo na habari kamili iko ukurasa wa 3.

My Take hapo kwenye red:
Huenda viongozi wa CCM na UVCCM wanabweteka kwa sababu wanategemea sana vyombo vya dola (eg policcm) kupunguza nguvu ya CDM hasa katika ule mpango uliosukwa wa kila mara kujaribu kukionyesha chama hicho kuwa ni cha vurugu.
 
ameona mbali na inavyoelekea si rahisi kufanya kama waliokuwa vijana wa tanuna asp. kwa sasa kila mmoja anaangalia maslahi yake mbele zaidi. Pia inaelekea amesahau kuwa mazingira yale ya mwanzo ni tofauti na sasa
 
Akina Mukama na Sophia Simba et al wataanza kumsakama mkongwe huyo -- "alikuwa wapi siku zote, kwa kuwa kang'olewa katika kamati za juu za chama, etc etc -- ingawa ukweli wa aliyoyazunguma utabakia pale pale -- ukweli!
 
Huyu mzee tangu wamnyang'anye Ubungo Bus Terminal anazeeka vibaya! Muda wote alikuwa haoni kuwa CCM inaelekea kaburini??
 
Tatizo wana hela sana, wanahongwa na wakubwa wa CCM, sasa nani anahaja ya kuzuguka kijenga chama na wao wameshiba, wanajua maisha yatakwenda hivyo for life
 
Wala haijachukua hata dakika 5!
hahahaaa hao ndio ccm
tatizo kubwa mfumo wao kwa sasa unaongozwa kwa rushwa na kutumia vibaya vyombo vya dola
kiukweli kama hawawezi kukubali makosa na kujirekebisha watapotea na kusahaulika
 
Baada ya kuondolewa kwenye korridor za power sasa hatimaye anaona vitu katika 3D ,anaongea kweli tupu mungu mpe umri mrefu ashuhudie mabadiliko 2015
 
Kingunge anashauri wafanye nini maana record ya miaka 50 iko wazi!
 
Ebanaeeee Mubyaz kwani ndio wao hawa?
Unajua, wanasiasa wetu wanatakiwa kujifunza uvumilivu na kukubali pale wanapokosolewa (hasa na watu wa ndani ya vyama husika).

Najua, wengine wanaenda extreme lakini vema kutambua kuwa wale wanaowakosoa wanafanya vile kwa wema.

Kama Mzee Kingunge kayasema haya, ni ishara kuwa mambo si shwari hata kama wataendelea kumpotezea.

Hapa ndo naikumbuka hii topic - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/238496-wazee-waitabiria-kifo-ccm-anguko-la-ccm-laja.html
 
Hivi lengo la kuwatoa wastaafu woote CC lilikuwa nini vile?naombeni kujua!
 
Wakati Nyerere alipoanzisha azimio la Arusha na kuingiza siasa yake ya ujamaa na kujitegemea,alipata wafuasi na wasaidizi kwenye serikali yake akiwemo Mzee Kingunge.Kama sikosei Kingunge yeye aliamua kuwa mjamaa kuliko nyerere,nakumbuka hakuwa au si muumini wa dini yeyote,maana bungeni haapi kwa biblia wala quran.
Nyerere ujamaa wake ulipomshinda at least alikubali na kuacha mabadiliko ila alibaki na imani yake thabiti kuhusu analoliamini,Madarakani aliwaacha wenzake waliokuwa wana imani na ujamaa wakati wa ruksa.
Ideology ikabadilika ikawa si ujamaa tena,wao akina Kingunge wamo tu,akaja mkapa aliyegawa kila kitu hakuna ujamaa Kingunge yupo,maadili yote yaliyowekwa na nyerere na akina kingunge kudai kuamini hakuwahi hata mara moja kukemea.
kwa mjamaa kama yeye kuja kumiliki kampuni iliyokuwa inajihususha na ubadhirifu pale Ubungo noa aubi tu hata kuhusishwa na familia yake.
OBSERVATION NI KUWA kINGUNGE SI MKWELI,si muumini wa kweli wa ideology aliyojidai kuiamini yeye kwake ilikuwa ni kuwepo na kubaki madarakani ameisaliti hata nafsi yake mwenyewe,angekaa pembeni wakati wajizi yalipokuwa yanajiuzia nyumba serikali,ufisadi,epa,richmond na dowans.na sikuwahi kumsikia akikemea kwa dhati.
Nyerere alisema ccm si mama yake,Kingunge yu tayari kufa nayo ili mradi iendelee kuwa madarakani na yeye afaidike pamoja na familia yake.kinachomuudhi ni kuwa makosa yao yatawafanya wakose ulaji si kuwahudumia watanzania,HANA UZALENDO.
je hadi sasa haingii kanisani wala msikitini?afadhali arudi fasta asimfanyie unafiki Mungu anazeeka safari i karibu,katufanyia unafiki watanzania na ujamaa wake wauongo amalizane na sisi tu lakini si Mungu.Hatoi angalizo wala ushauri hayo ni machozi ya mamba anafikiri kama cdm wakiingia madarakani familia yake ya kifisadi itapona?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom