CCM sasa kwisha! - Kingunge Ngombale-Mwiru

Mchawi wa CCM si CHADEMA wala operesheni sangara.

CCM imekwishapoteza mwelekeo kama chama cha siasa chenye kuwajibika kwa wananchi Na kuleta Maendeleo ya nchi. CCM sasa ni chama cha watu binafsi kinachosimamia maslahi ya watu binafsi wachache pamoja na familia zao.

Kwa bahati mbaya (nzuri kwa wanaotaka mabadiliko) CCM imeshindwa kujisahihisha ki vitendo na hata imeshindwa kutumia nafasi ya wazi kujivua magamba katika uchaguzi huu Mkuu wa chama unaendelea.

Katika muda wote wa uhai wa CCM, ukiondoa kipindi cha uchaguzi mkuu 2010, ni muda huu ambapo Ufisadi unadhihirisha nguvu yake wazi wazi. Hii yote inafanyika si kwa maslahi ya taifa, Nadhani hata si kwa maslahi ya chama cha CCM, bali kwa maslahi ya watu binafsi wachache.

Kwa CCM yenyewe kupoteza mwelekeo, kuwakumbatia mafisadi, kuwatupilia mbali wakulima na wafanyakazi na kushindwa kujisahihisha hata baada ya kugundua makosa basi haya ndiyo yanaipeleka CCM kaburini.
 
Baada ya kuondolewa kwenye korridor za power sasa hatimaye anaona vitu katika 3D ,anaongea kweli tupu mungu mpe umri mrefu ashuhudie mabadiliko 2015

Ashuhudie mabadiliko au ashuhudie machafuko?

Unafikiria CCM hawatang'ang'ania fupa?
 
Mheshimiwa Rais wa JMT alisema "anaesema CCM itakufa atakufa yeye" so Kingunge anakaribia Kuwa R.I.P
 
Anasema chama hicho kimepoteza nguvu kukabili wapinzani, adai Oparesheni Sangara ya Chadema inawatesa.

Asema misingi yote ya TANU, ASP imetoweka. Mwanasiasa mkongwe huyo alitoa kauli hiyo Alhamisi (jana) kwenye mkutano mkuu wa nane wa UVCCM alipopewa nafasi ya kuzungumza na kutoa nasaha zake.

Aliongeza kusema pamoja na CCM kuwa na mtandao na nguvu kubwa, hakijui kutumia nguvu hizo, kama ilivyokuwa katika enzi za TANU na ASP.

Kuhusu wapinzani hasa CHADEMA alisema “chama hicho kinaendesha Operesheni Sangara sisi tupo, UVCCM na CCM inakiachia chama hicho kuzunguka nchi nzima sisi kimya, wanaendelea kuimarika….. sijui hii inatokana na usingizi au sijui ni kutosheka………”

Hata uwe mnazi kiasi gani lakini daima ukweli utabaki kuwa ukweli na hakuna jinsi yoyote mtu ataweza kusimamia uongo ama kuubadilisha uongo kuwa ukweli. Pamoja na kuwa huyo Mzee ni KADA na MNAZI halisi wa CCM lakini ameshindwa kuendelea kukumbatia uongo na hayo aliyosema ndiyo ukweli wenyewe japo ni wazi kuwa wataibuka watu ndani ya CCM akiwapo kijana wa propaganda 'NAPE' kukebehi maneno ya huyo babu.
 
Maskini Kingunge wa watu naamini hawatamuacha hivhivi tu, hivi CCM kabaki nani anaeisapopti kama sio Kaka Alfani na Familia yake???
 
Hivi Dar parking, town centre si bado ana own huyu KIBABU..... Nacho KIGUMU KINGUNGE.... nasikia hajui his age...!!! Anyway i like his standings kuhusu hili...!!!
 
Ni ukweli uliojaa unafiki, hana tofauti na magamba wengine kama Tuluway, Six nk.
 
Anasema chama hicho kimepoteza nguvu kukabili wapinzani, adai Oparesheni Sangara ya Chadema inawatesa.

Asema misingi yote ya TANU, ASP imetoweka. Mwanasiasa mkongwe huyo alitoa kauli hiyo Alhamisi (jana) kwenye mkutano mkuu wa nane wa UVCCM alipopewa nafasi ya kuzungumza na kutoa nasaha zake.

Aliongeza kusema pamoja na CCM kuwa na mtandao na nguvu kubwa, hakijui kutumia nguvu hizo, kama ilivyokuwa katika enzi za TANU na ASP.

Kuhusu wapinzani hasa CHADEMA alisema “chama hicho kinaendesha Operesheni Sangara sisi tupo, UVCCM na CCM inakiachia chama hicho kuzunguka nchi nzima sisi kimya, wanaendelea kuimarika….. sijui hii inatokana na usingizi au sijui ni kutosheka………”

Hii ni habari kuu ukurasa wa mbele wa gazeti la Mtanzania ya leo na habari kamili iko ukurasa wa 3.

My Take hapo kwenye red:
Huenda viongozi wa CCM na UVCCM wanabweteka kwa sababu wanategemea sana vyombo vya dola (eg policcm) kupunguza nguvu ya CDM hasa katika ule mpango uliosukwa wa kila mara kujaribu kukionyesha chama hicho kuwa ni cha vurugu.
..
  • .......................... Mzee Kingunge ni Kingunge kama jina lake lilivyo ........... kuna wakati jina hili lilionekana kama cheo kwa mtu ambaye ni mahiri hasa katika siasa nchini kweu na nchi jirani ya Kenya........ katika haya matamshi yake hakudiriki kuongea wazi wazi kwa kutamka bayana kwamba rushwa ni sumu katika kutafuta uongozi..... hakutumia uzoefu wake kama mzee wa Chama kuelezea jnsi enzi zao walifanya nini kwa watu waliokuwa wanatafuta uongozi kwa kutumia pesa...............
 
Mhn!Anataka wamsikilize tena ili awapangie nani awe rais kama alivyofanya 2005.Nasikia alisema JK ana mvuto na Mwandosya atasababisha chama kishindwe uchaguzi mkuu kwasababu hana mvuto.Mimi huwa siwaamini hawa watu.Kelele zao ni za kujipanga tu ndani ya chama hakuna lolote la kumsaidia mwananchi.
 
Ccm ilishakufa! Imewekewa mipira ya kupumulia! Tusubiri tu siku ya kutangazwa kifo rasmi,yaani 2015. Siku zote chama hakifi kikiwa madarakani,subirini 2015
 
Kifo cha ccm kilianza wakati wakiwa wanafutilia mbali azimio la arusha kule zanzibar na kuruhusu ubepari huria. Ngombale alikuwapo pale na alipaswa kusema palepale kama nyerere alivyolalamika waziwazi. Yeye akakimbilia kuhodhi Ubungo bus terminal na parking lotes za jijini. Alipotimuliwa kote huko njaa imembana hata hawezi kukumbuka juzi alifanya nini. Anachokifanya sasa anataka uchunguzi wa mifupa ya Arafat ufanyike sasa huku akihofia naye kifo chake kitamsuta. Kawawa alikuwa bomba katika hili, sio undumila kuwili.
 
HUO ndio ukweli, ccm hawana pa kutokea! Tuhuma za ufisadi zinazokikabili ni kama kansa iliyokitafuna mwili mzima; uzembe na kutowajibika kwa viongozi toka juu, ukianza na mkuu wa kaya vinawafanya wakose maelezo mbele ya wananchi.
 
Back
Top Bottom