CCM kuiba kura Igunga?

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
watanzania tumeshuhudia malumbano na matatizo kibao tangu uchaguzi wa mwaka jana,huu uchaguzi wa igunga ndio wa kwanza tangu uchaguzi mkuu mwaka jana,watanzania wote tuna hamu tujue uwezo wa ccm,je bado wanakubalika kwa watanzania
uchaguzi huu utakuwa kipimo tosha kwa kikwete na serikali yake,je wataiba tena kura kama walivyozoea??macho yetu yote IGUNGA
 
Hawana mbinu nyengine wanayoitegemea (hiyo ndiyo siraha yao ya mwisho).
 
kwani hamkuona wale jamaa walivyokua wakimlilia Rostam?.....jamaa kawaambia amejivua gamba, watu wanaimba "hatutakiii, hatutakii"....we unafikiri CCM wanahitaji kuiba kura hapo?.....mbona its obvious.....mnazijua akili za watanzania au mnazisikia tu?
 
kwani hamkuona wale jamaa walivyokua wakimlilia rostam?.....jamaa kawaambia amejivua gamba, watu wanaimba "hatutakiii, hatutakii"....we unafikiri ccm wanahitaji kuiba kura hapo?.....mbona its obvious.....mnazijua akili za watanzania au mnazisikia tu?

mkuu hapo tunapima serikali nzima,je bado wanatakiwa?
 
kwani hamkuona wale jamaa walivyokua wakimlilia Rostam?.....jamaa kawaambia amejivua gamba, watu wanaimba "hatutakiii, hatutakii"....we unafikiri CCM wanahitaji kuiba kura hapo?.....mbona its obvious.....mnazijua akili za watanzania au mnazisikia tu?

Wale waliandaliwa mkuu,
 
Anayedhani kuna kura ziliibiwa ni mwendawazimu tu na hana kumbukumbu, tazama CCM ilikuwa na sababu gani ya kuiba wakati hata sehemu ilikopoteza waliopiga kura ni wana CCM. Acheni utetezi kabla hata mchezo kuanza. Tafuteni kingine IGUNGA ni ya CCM.
 
tunasikia walilipwa hela kibao,kuna mama mmoja alikuwepo al;ilipwa 50,000 kazi aliyopewa ni kulia
Halafu katoka hapo na kicheko kuwa kapata wakati fedha hizo ni sehemu ya fedha zake zilizoibiwa na huyohuyo aliyempa. weli mtaji wa CCM ni ujinga wa watu.
 
watanzania tumeshuhudia malumbano na matatizo kibao tangu uchaguzi wa mwaka jana,huu uchaguzi wa igunga ndio wa kwanza tangu uchaguzi mkuu mwaka jana,watanzania wote tuna hamu tujue uwezo wa ccm,je bado wanakubalika kwa watanzania
uchaguzi huu utakuwa kipimo tosha kwa kikwete na serikali yake,je wataiba tena kura kama walivyozoea??macho yetu yote IGUNGA[/QUOTE).
Mdau ina maana ushindi wa mbunge aliyejiuzulu(Mh.Rostam) ulikuwa wa wizi wa kura? Lakini pia nakumbuka hotuba ya Rostam kuhusu aliyoyasimamia Jimbo la Igunga-Mfano, kila kaya katika Jimbo hilo ina bima ya afya. Je, hiyo haiwezi kuwa nguvu na hoja ya C.C.M. kushinda tena? Tusielekeze macho tu,bali pia fikra zetu pia,kwani unaweza kuangalia ukashindwa kutafsiri unachoangalia!
 
Watu wa Igunga ni vigumu kubashili kwani wana uelewa mdogo sana, kumbuka ni miongoni mwa wilaya zenye wasomi wachache sana, so tutegemee miujiza. Ila nashauri Dr. wa ukweli aandae mpango kabambe kulingana na eneo husika ili jimbo la huyo Mui***n lirudi Tanzania.
 
Mimi sipo upande wowote, ila kampeni nzuri zisizo na ulaghai wala rushwa, siasa safi na zenye maslahi kwa taifa na matumaini kwa watanzania hasa wana igunga, chama chochote chenye sera bora kitashinda uchaguzi igunga.. Wananchi tuamke tuwakatae mafisadi watakaoleta matisheti, kofia, na khanga kwa ajili ya kupata kura...haijalishi chama tawala au upinzani...tukatae rushwa kwenye uchaguzi jamani
 
Back
Top Bottom