CCM: Kamati Kuu Kukaa Chini Dar

Ina maana Mzee amekabidhiwa tena lile jukumu lake la U-TINGATINGA alilokuwa akilalama wakati akipigwa chini wakati wa uchaguzi wa mgomea wa CCM 2005?

omarilyas

- Maneno yamepitwa na wakati haya mkuu, vipi hakuna mapya? Mbona ndugu yetu Beno mgombea wa mafisadi alipigwa chini uenyekiti wa UV-CCM kwani amekufa?

- Ungeanza kuongelea utinga tinga wa Beno kwanza mkuu, au? Bwa! ha! ha!

FMES
 
Mnasemaga NATIN' PERSONAL kaka....sikujua kuwa mambo kama yale huwa yanaishaga....

Beno bado mchanga hajakomaa kukabidhiwa majukumu muhimu kama hayo

omarilyas
 
Mungu uliye juu tunakuomba utulinde watanzania na hili genge la mafisadi linakutana hatujui, ww ndo unajua wanachopanga......amin

EE bana ee hii ni sawa na kuomba mvua ukiwa jangwani!.Ni dhahiri kuwa katika hao unaosema kuwa ni mafisadi si wote , ingawaje wamo humo wanaonuka ufisadi wa kutisha.
Kuomba peke yake haitoshi lifanyiwe kazi.
FMES tuletee mo dataz
 
Mnasemaga NATIN' PERSONAL kaka....sikujua kuwa mambo kama yale huwa yanaishaga....

Beno bado mchanga hajakomaa kukabidhiwa majukumu muhimu kama hayo

omarilyas

- Yaaani mpaka kuwa mgombea wa mafisadi bado hajakomaa? Hilllarious! Bwa! ha!ha! ha! nothing personal kaka Ha! ha!

Respect.

FMES

Mkulu Lole,

- Bado sijapata data zaidi, later!

FMES
 
- Kikao kimeisha na kufungwa tayari, the dtaz ni pamoja na mengi yalijadiliwa kamati kuu imeshindwa kuafikiana kuhusiana na hoja nzito za makundi ndani ya chama.

- Kikao hicho kimeiamuru kamati ya Sekretariat, kukutana tena tarehe 29, mwezi huu kurudia tena ishus mbali mbali ilizozifikisha kwenye kikao hicho, kabla ya kuzirudisha tena kwao CC.

- Kamati kuu pia imeamua kukutana tena, tarehe 2 Mwezi ujao kwa kikao zaidi cha dharura.

Bado tunajaribu kufuatilia yaliyojiri huko ndani wakati wa hivi vikao.

Respect.

FMES
 
ES,
nini matunda ya hivi vikao (vikao vizito kama ilivyoelezwa hapo awali) kwa mtu wa kawaida kama mimi ? maana kuna kila dalili kwamba hakuna lolote linalozunguzwa humo kumhusu mtanzania wa kawaida, sasa naweza nikawa nimekosea hivyo basi kama lolote linalomgusa mtanzania ambalo huongelewa naomba utupashe la sivyo basi hivyo vikao WIZI MTUPU!
 
- Mkuu mimi sihudhurii hivi vikao, wala kupanga agenda za vikao hivi ila ninaleta dataz tu.

- However, kwa ufahamu wangu politically ni kazi ya bunge letu tukufu la jamhuri kusimamia masilahi ya mwananchi na taifa kwa ujumla, vikao vya vyama vya siasa mara nyingi hujali mienendo yake na namna ya kushinda uchaguzi tu, bunge ndilo linalotakiwa kuwathibiti chama tawala kinapokuwa nje ya sheria, so far hii kwetu ni ndoto!

Respect.

FMES!

Ni vigumu kufikia muafaka kwenye hoja ya makundi kwa kuwa makundi hayo yanamgusa Mwenyekiti wa Chama moja kwa moja na amefika mahali anashindwa aegemee wapi.

Hoja za wapinga ufisadi zina nguvu sana na wananchi sasa wanaelewa kila aina ya ufisadi uliofanywa huko nyuma na evidence zipo. Kwa upande mwingine mafisadi ndiyo waliomsaidia Muungwana kupata hela ya kampeni na hivyo inakuwa ni ngumu kuwakemea ama kuwachukulia hatua.

Kamati Kuu ikikosea ikawakemea watu kama akina Sendeka, Mwakyembe, Mama Kilango, na wengineo ambao wanapiga kelele za ufisadi na kuwatuhumu wenzao kwamba ni mafisadi, CCM itajikuta inapoteza matumaini ya wananchi na uchaguzi ni mwakani na kura za wananchi wanazihitaji, kwa hiyo ni ngumu sana kutoa kauli nzito ya kukemea makundi ndani ya CCM. Njia pekee ya kuyashughulikia hayo makundi ni diplomasia ya kimya kimya, tatizo ni kwamba makundi yote mawili hakuna ambaye yuko tayari ku-back off, maana akifanya hivyo ndiyo anapoteza kila kitu.

Kwa hiyo hata kwenye hicho kikao cha Sekretariati ya CC na kwenye CC yenyewe, sitarajii muafaka zaidi ya kukubaliana kwamba makundi wayashughulikie kimya kimya.

Kikwete anawahitaji wote, japo naweza kusema kwamba kwa sasa anawahitaji zaidi hao wanaopiga kelele za ufisadi. Kwa bahati nzuri hao wanaopiga kelele za ufisadi hawamgusi moja kwa moja JK, wamekuwa wakimjumuisha kwenye hoja zao kwamba Rais anachukia sana ufisadi na anapiga vita ufisadi. Lakini kwa undani ni kwamba JK ni mmoja wa hao mafisadi na ndiyo maana imekuwa ngumu sana kwake kuwashughulikia kwa aina yoyote. Kwa hiyo hilo kundi la akina Mwakyembe na wenzake waendelee kumbeba JK ili asije akawageuka siku akiona na wao wanaanza kusema Rais nae haonyeshi juhudi za kupiga vita ufisadi.

CCM imefikia mahali pagumu na uchaguzi wa mwakani hasa kwa wabunge itakuwa ni vurugu kubwa sana. Tutarajie kura za chuki pamoja na watu kubondana (hapa nina maanisha wafuasi wa CCM watapigana wao kwa wao kutokana na makundi yaliyopo). Mvua za rasha rasha zimeishaanza Kyela na sasa kuna manyunyu pale makao makuu ya jimbo ya Busanda (mjini Katoro).

Nina uhakika mafisadi wanaandaa watu wao na pia hao wapinga ufisadi nao wanajiandaa kupambana na wale watakaokuwa wameandaliwa na mafisadi. Matokeo ya kura za maoni pamoja final list ya wagombea ambayo itapitishwa na vikao vya chama vinaweza kuleta kasheshe ya ugomvi mkubwa.
 
Kikao hicho kimeiamuru kamati ya Sekretariat, kukutana tena tarehe 29, mwezi huu kurudia tena ishus mbali mbali ilizozifikisha kwenye kikao hicho, kabla ya kuzirudisha tena kwao CC.

Naona CC wanapoteza muda wao tu, kwa kifupi ni kwamba CC haijakubaliana na ishuz zilizopelekwa kwao, ama zina information nusu au zinagusa mambo ambayo yanaweza kukiumiza chama, ndiyo maana CC imezirudisha tena.

Je, tutegemee chochote kwenye hicho kikao cha wiki ijayo? Sidhani kama kutakuwa na mapya, maana yote yameishaandikwa kwenye magazeti na Raia Mwema imemaliza kila kitu kuhusu malalamiko ya Makamba.

Sekretariati ya Kamati Kuu inaundwa na hawa watu

Katibu Mkuu wa CCM ambaye atakuwa Mwenyekiti.

Manaibu Katibu Mkuu wa CCM.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Organaizesheni.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi na Uenezi.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Uchumi na Fedha.

Makatibu Wakuu wa Jumuiya za Wananchi zinazoongozwa na CCM.

Ukiwaangalia wote hao kwa ukaribu sana over 75 wana link na mafisadi na kwa hiyo ukisema waandae ishus za makundi ya CCM lazima watakuwa biased kwa kuelemea kwenye kundi la mafisadi kwa kuwa ni mafisadi ndio waliowasaidia kupata hizo nafasi.

JK ana kibarua kizito sana na tayari kimeishamshinda na ndiyo maana ndani ya CCM kila mtu anajisemea lake na pia serikalini kila mtu anakuja na lake.
 
ES,
nini matunda ya hivi vikao (vikao vizito kama ilivyoelezwa hapo awali) kwa mtu wa kawaida kama mimi ? maana kuna kila dalili kwamba hakuna lolote linalozunguzwa humo kumhusu mtanzania wa kawaida, sasa naweza nikawa nimekosea hivyo basi kama lolote linalomgusa mtanzania ambalo huongelewa naomba utupashe la sivyo basi hivyo vikao WIZI MTUPU!

KM, siku hizi unanifurahisha kweli na michango yako hapa jamvini. Unasema kweli tupu fitina kwako mwiko. Nilishasema hapa hii CCM ya sasa ni chama cha mafisadi ambacho kimeweka mbele maslahi ya mafisadi badala ya Watanzania. Hivi vikao ambavyo miaka ya nyuma vilikuwa na umuhimu mkubwa na vilifanya maamuzi mazito yaliyohusu CCM na hata Taifa sasa hivi kumejaa USANII MTUPU kama ilivyomshinda kuiongoza nchi Kikwete pia anakiangamiza chama na kama hawakumshtukia mapema basi ataiacha CCM katika hali mbaya sana na iliyojaa makundi yenye chuki kubwa kati yao. Tusiendelee kupoteza muda kutaka kujua ni kipi kilichojadiliwa huko maana ni USANII NA WIZI MTUPU!!! halafu ukiuliza vikao hivyo vilivyoanza tangu wiki iliyopita vimegharimu kiasi gani basi utasikia mabilioni yameanguka!!!! Maskini nchi yetu ya Tanzania! :(
 
Ama kwa hakika Kada amebadilika.....

Hivi vikao vya ccm licha ya kutuyeyusha vinamwongezea mzigo mlalahoi hasa kwa vile tunafahamu kuwa asilimia kubwa ya mzigo wa gharama za vikao vya chama hucho hubebwa na serikali (i.e. taxpayers)

JK ni mtu dhaifu ambaye hawezi kubadilisha lolote ndani ya CCM.Huyu ni mtu aliwezeshwa kushinda 2005 kutokana na michango ya mafisadi.Hivi tunategemea lolote kutoka kwake muda huu anapoelekea kwenye uchaguzi mwingine hapo 2010?
 
Mkuu Bubu
Awali niliuliza, hivi nani wa kumnyooshea mwenzake kidole kwenye hivyo vikao, nikajibuwa ni vikao muhimu kwa mustakabali wa taifa, kwamba hutoa maamuzi mazito!!

Tusitegemee jipya kutoka kwenye kundi hilo. Nchi hii inahitaji mabadiliko makubwa katika uongozi wake kwani tumefika mahala ambapo CCM haina tofauti na TLP ya mrema, ni USANII MTUPU!!!

Wameanza kutwangana viongozi wenyewe, tukiingia wananchi ni vita kwa kwenda mbele na kuyatuliza mapigano yatayoripuka Tanzania itachukua miaka kuyatuliza kama ilivyo kwa Somalia hivi sasa, kwani chuki inayojengeka miongoni mwa makundi mbali mbali yanayohasimiana ni kubwa.

Tuombe Mungu yasijetokea.
 
- Mkuu mimi sihudhurii hivi vikao, wala kupanga agenda za vikao hivi ila ninaleta dataz tu.

- However, kwa ufahamu wangu politically ni kazi ya bunge letu tukufu la jamhuri kusimamia masilahi ya mwananchi na taifa kwa ujumla, vikao vya vyama vya siasa mara nyingi hujali mienendo yake na namna ya kushinda uchaguzi tu, bunge ndilo linalotakiwa kuwathibiti chama tawala kinapokuwa nje ya sheria, so far hii kwetu ni ndoto!

Respect.

FMES!

Kama ni kazi ya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kuleta maendeleo kwa taifa hili kama ulivyosema, then kuna haja gani ya kuhitaji hivi vyama vya siasa ?Kwa nini BUNGE lisivifute KABISA hivi vyama kwa sababu vinatafuna pesa za ruzuku za walipa kodi iwapo kazi yao ni KUSHINDA TU UCHAGUZI na sio KUPANGA MIKAKATI YA KUWASAIDIA HAO WANAOTOA PESA KUVIENDESHA HIVYO VYAMA ( AMBAO NI SISI WANANCHI ?)?? Kwa hiyo kazi ya vyama vya siasa ni kujali ni jinsi gani watashinda uchaguzi tu ? Thats a typical ccm mind that has spoken na ipo siku nakuhakikishia maneno uliyosema leo yatakuja kuropokwa na kiongozi wa ccm na hapo ndipo watu watakapostuka!

LETS WAIT!!

Neways, tuendeleeni na mada!
 
[SIZE="4 kwa ufahamu wangu politically ni kazi ya bunge letu tukufu la jamhuri kusimamia masilahi ya mwananchi na taifa kwa ujumla, vikao vya vyama vya siasa mara nyingi hujali mienendo yake na namna ya kushinda uchaguzi tu, bunge ndilo linalotakiwa kuwathibiti chama tawala kinapokuwa nje ya sheria, so far hii kwetu ni ndoto!

Respect.

FMES!

[/SIZE]

Kwanza nakupongeza kwa kuwa muwazi kiasi hiki. Kwa wale wanaoshindwa kukubali ukweli huo ndio ukweli kuhusu dhana ya CCM kama chama. Ni kweli kabisa kuwa tangia wazee wetu kuamua kuanzisha kitu kinachoitwa CCM hata enzi zile za chama kushika hatamu huo ndio umekuwa mtizamo wa wana-CCM. Mwanzoni ilikuwa ni dhana ya wengi waliokuwa hawana nguvu kisiasa kukabiliana na Mwalimu aliyekuwa akiendelea na dhana ya TANU ndani ya chama kipya CCM. Lakini sasa huu ni mtazamo rasmi unaukubalika na wengi na ambao ulibarikiwa mbele ya hadhara ya watanzania na Mwenyekiti wake katika mkutano wake mkuu wa mwisho alipotamka bayana kuwa " Chama Cha Mapinduzi ni electoral machine".

Inashangaza kuwa bado kuna watu wanaendelea kukinasabisha chama cha CCM na TANU ambacho kumuondoa mkoloni ilikuwa ni njia ya kufanikisha ujenzi wa taifa na maendeleo ya mtanzania kwa kuhakikisha kuwa chama kinakuwa sauti ya asiye na sauti katika kuishauri, kuelekeza na kuisimamia/kuidhibiti serikali.

Ni wazi kuwa hatua ya kukimbilia ama kulazimika kuanzisha mfumo wa siasa za ushindani wa vyama(ilipaswa kuwa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi) imeathiri sana chama cha mapinduzi kiasi ya kwamba kimeshindwa kabisa kujitambua kuwa kipo kwa ajili ya kushauri, kuelekeza na kudhibiti serikali katika kuhakikisha kuwa kinalinda maslahi ya mtazania badala ya kulinda maslahi yao/yake pekee kwanza.

Si ajabu hivi sasa tunashuhudia enzi za UFISADI KUSHIKA HATAMU baada ya kuondokana na enzi za CHAMA KUSHIKA HATAMU...

omarilyas
 
Kama ni kazi ya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kuleta maendeleo kwa taifa hili kama ulivyosema, then kuna haja gani ya kuhitaji hivi vyama vya siasa ?Kwa nini BUNGE lisivifute KABISA hivi vyama kwa sababu vinatafuna pesa za ruzuku za walipa kodi iwapo kazi yao ni KUSHINDA TU UCHAGUZI na sio KUPANGA MIKAKATI YA KUWASAIDIA HAO WANAOTOA PESA KUVIENDESHA HIVYO VYAMA ( AMBAO NI SISI WANANCHI ?)?? Kwa hiyo kazi ya vyama vya siasa ni kujali ni jinsi gani watashinda uchaguzi tu ? Thats a typical ccm mind that has spoken na ipo siku nakuhakikishia maneno uliyosema leo yatakuja kuropokwa na kiongozi wa ccm na hapo ndipo watu watakapostuka!

LETS WAIT!!

Neways, tuendeleeni na mada!

- Mkuu Kada, hii ni bongo sio majuu na this is all we have yaani hivi vyama, na kumbuka kuwa uchaguzi ujao CCM hana mpinzani.

- Hili sio kosa langu ni la taifa zima mimi na wewe tukiwa icluded, hebu soma darasa la Mkuu Omarilyas hapo juu.

Respect

Yalishasemwa siku nyingi. Tukaishia kupiga makofi na vigelegele....

omarilyas
 
Kwanza nakupongeza kwa kuwa muwazi kiasi hiki. Kwa wale wanaoshindwa kukubali ukweli huo ndio ukweli kuhusu dhana ya CCM kama chama. Ni kweli kabisa kuwa tangia wazee wetu kuamua kuanzisha kitu kinachoitwa CCM hata enzi zile za chama kushika hatamu huo ndio umekuwa mtizamo wa wana-CCM. Mwanzoni ilikuwa ni dhana ya wengi waliokuwa hawana nguvu kisiasa kukabiliana na Mwalimu aliyekuwa akiendelea na dhana ya TANU ndani ya chama kipya CCM. Lakini sasa huu ni mtazamo rasmi unaukubalika na wengi na ambao ulibarikiwa mbele ya hadhara ya watanzania na Mwenyekiti wake katika mkutano wake mkuu wa mwisho alipotamka bayana kuwa " Chama Cha Mapinduzi ni electoral machine".

Inashangaza kuwa bado kuna watu wanaendelea kukinasabisha chama cha CCM na TANU ambacho kumuondoa mkoloni ilikuwa ni njia ya kufanikisha ujenzi wa taifa na maendeleo ya mtanzania kwa kuhakikisha kuwa chama kinakuwa sauti ya asiye na sauti katika kuishauri, kuelekeza na kuisimamia/kuidhibiti serikali.

Ni wazi kuwa hatua ya kukimbilia ama kulazimika kuanzisha mfumo wa siasa za ushindani wa vyama(ilipaswa kuwa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi) imeathiri sana chama cha mapinduzi kiasi ya kwamba kimeshindwa kabisa kujitambua kuwa kipo kwa ajili ya kushauri, kuelekeza na kudhibiti serikali katika kuhakikisha kuwa kinalinda maslahi ya mtazania badala ya kulinda maslahi yao/yake pekee kwanza.

Si ajabu hivi sasa tunashuhudia enzi za UFISADI KUSHIKA HATAMU baada ya kuondokana na enzi za CHAMA KUSHIKA HATAMU...
omarilyas

Ahsante sana Omarilyas kwa kutupatia Watanzania msemo mpya. Sasa hivi si chama tena kimeshika hatamu bali ni FISADIS WAMESHIKA HATAMU
 
- Mkuu Kada, hii ni bongo sio majuu na this is all we have yaani hivi vyama, na kumbuka kuwa uchaguzi ujao CCM hana mpinzani.

- Hili sio kosa langu ni la taifa zima mimi na wewe tukiwa icluded, hebu soma darasa la Mkuu Omarilyas hapo juu.

Respect

FMES

sasa kama ni majuu ndio vyama vilete maendeleo ? umepata wapi hilo wazo kwamba ni vyama vya ughaibuni tu ndio vinapaswa kuleta maendeleo ? hiyo napinga KABISA mzee. Hatuwezi kuendesha mambo kibongobongo tu na tukategemea maendeleo, NEVER! So usitumie kigezo cha kusema bongo sio majuu ili ionekane ni sawa vyama vya siasa kutowaletea maendeleo wananchi!
 
Ahsante sana Omarilyas kwa kutupatia Watanzania msemo mpya. Sasa hivi si chama tena kimeshika hatamu bali ni FISADIS WAMESHIKA HATAMU

Kaka kama ulinipata vizuri niliongelea kuwa UFISADI UMESHIKA HATAMU na sio mafisadi. Kwangu mimi hili suala ni pana zaidi ya hawa tunaoambiwa tena sasa kwa kulazimisha kabisa kuwa mafisadi huku wengine wakijinadi kuwa ni wapambanaji dhidi ya mafisadi kitu ambacho sikubaliani nacho. Suala la UFISADI ni la kimfumo zaidi ya watu ama kundi mojawapo la kisiasa. CCM inaweza kuwa ni ngome kuu ya mafisadi na ndio maana hata dhana yake kama chama cha kisiasa imekuwa kama alivyoelezea FMES lakini UFISADI kama mfumo ni zaidi ya CCM ama hao tunaombiwa kuwa ni MAFISADI PAPA...

omarilyas
 
Back
Top Bottom