Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
Kwenye magazeti ya leo, ya Uhuru na Mtanzania, amenukuliwa Katibu mkuu wa chama kipya cha siasa, kilichopata usajili wa kudumu hivi karibuni CCK, Renatus Muabhi, akikionya Chadema, kuwa kinahatarisha maisha ya wafuasi wake, kwa kukaidi maagizo ya serikali, kuhusu uendeshaji wa shughuli zake za kisiasa, ambapo husababisha polisi, kuingilia kati kuzuia shughuli hizo, hadi wakati mwingine kusababisha maafa, kama yalivyotokea hivi karibuni huko Morogoro na Iringa.
Sikushangazwa sana na kauli hiyo, iliyotolewa na kiongozi wa ngazi ya juu kabisa ya chama hicho ya kukilaumu Chadema, badala ya kuilaumu polisi, ambayo ndiyo inafanya makosa makubwa,kwa kuzuia shughuli halali za baadhi ya vyama vya siasa, kwa visingizio vya kipuuzi.
Nasema sikushangaa, kwa kuwa baadhi ya vyama, vinavyojiita vya upinzani,vinaidhinishwa na msajili wa vyama vya siasa, kwa maelekezo maalum na CCM kwa kazi moja tu, ya kuwashambulia Chadema.
Tumemshuhudia Tendwa mwenyewe, akitumika na magamba kwa kutamka kuwa anakusudia kukifuta Chadema. Sasa ili hoja yake iwe na nguvu zaidi, anavitumia hivyo vyama CCM-B, kutoa matamshi ya aina hiyo ili aweze, kutekeleza azma yake ya kuifuta Chadema.
Lakini hata hivyo vyama hivyo CCM-B, na msajili wao wa vyama John Tendwa, nadhani, watakuwa wameipata, meseji aliyotuma, kamanda Mbowe kuwa, Tendwa kama haitakii mema nchi hii, athubutu kuifuta Chadema, aone moto utakaowaka nchini, ambao hakuna chombo chochote cha dola, kitakachokuwa na uwezo wa kuuzima!!