CCK yawaonya CHADEMA

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,477
30,130
Kwenye magazeti ya leo, ya Uhuru na Mtanzania, amenukuliwa Katibu mkuu wa chama kipya cha siasa, kilichopata usajili wa kudumu hivi karibuni CCK, Renatus Muabhi, akikionya Chadema, kuwa kinahatarisha maisha ya wafuasi wake, kwa kukaidi maagizo ya serikali, kuhusu uendeshaji wa shughuli zake za kisiasa, ambapo husababisha polisi, kuingilia kati kuzuia shughuli hizo, hadi wakati mwingine kusababisha maafa, kama yalivyotokea hivi karibuni huko Morogoro na Iringa.

Sikushangazwa sana na kauli hiyo, iliyotolewa na kiongozi wa ngazi ya juu kabisa ya chama hicho ya kukilaumu Chadema, badala ya kuilaumu polisi, ambayo ndiyo inafanya makosa makubwa,kwa kuzuia shughuli halali za baadhi ya vyama vya siasa, kwa visingizio vya kipuuzi.

Nasema sikushangaa, kwa kuwa baadhi ya vyama, vinavyojiita vya upinzani,vinaidhinishwa na msajili wa vyama vya siasa, kwa maelekezo maalum na CCM kwa kazi moja tu, ya kuwashambulia Chadema.

Tumemshuhudia Tendwa mwenyewe, akitumika na magamba kwa kutamka kuwa anakusudia kukifuta Chadema. Sasa ili hoja yake iwe na nguvu zaidi, anavitumia hivyo vyama CCM-B, kutoa matamshi ya aina hiyo ili aweze, kutekeleza azma yake ya kuifuta Chadema.

Lakini hata hivyo vyama hivyo CCM-B, na msajili wao wa vyama John Tendwa, nadhani, watakuwa wameipata, meseji aliyotuma, kamanda Mbowe kuwa, Tendwa kama haitakii mema nchi hii, athubutu kuifuta Chadema, aone moto utakaowaka nchini, ambao hakuna chombo chochote cha dola, kitakachokuwa na uwezo wa kuuzima!!
 
cck hawana jipya zaidi ya kudandia basi kwa mbele ambayo ni hatari na matokeo yake ni kifo
 
[h=2][/h]JUMAMOSI, SEPTEMBA 15, 2012 07:23 NA RACHEL MRISHO

CHAMA cha Kijamii (CCK), kimekijia juu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kukitaka kitafakari kiini cha matukio ya mauaji yanayotokea katika mwendelezo wa siasa zake.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa CCK, Renatus Muabhi, alisema ubabe na kauli zinazotolewa na katibu mkuu wa chama hicho, Dk. Willbrod Slaa, zinaweza kuhatarisha usalama wa nchi.

“Kwa kusimamia misingi na maadili, tunapenda kukiasa Chadema kukaa na kutafakari misingi na chanzo cha matatizo yanayokinyemelea, yakiwamo ya wananchi kuuawa katika mikutano yake,” alisema na kuongeza:

“Tunajua na ni ukweli usiopingika kwamba Chadema ni chama ambacho kimejizolea umaarufu mkubwa kiasi cha kuwa tishio kwa chama tawala (CCM). Tabia ya kuwafanya wananchi kuwa kuni za kuchochea siasa chafu iachwe, kwa kuwa wao ndio wanaoteseka na si wanasiasa.

“Chama hiki kimejengwa kwa hali na mali katika mazingira magumu kufikia kilipo hivi sasa, hivyo ni jukumu lao kujitathimini na kutafuta mbinu mpya ya kukwepa siasa hatarishi, ili kufikia azma sahihi,” alisema.

Aliongeza kuwa ubabe na kauli za Dk. Slaa, ikiwamo ya kumtumia ujumbe mfupi wa maneno Mkuu wa Jeshi la Polisi chini, Said Mwema kwamba aandae risasi nyingi ili wakauwe raia haipaswi kufumbiwa macho, kwani inatengeneza kizazi kisicho na utii wa sheria.

Mbali ya kuzungumzia mwenendo wa hali ya kisiasa nchini, Muabhi aliigeukia Serikali na kusema kuwa imeshindwa kusimamia huduma za kijamii na badala yake imejikita katika mbinu chafu za kuzuia hoja za kuikosoa kupitia mijadala na mikutano inayofanywa na vyama vya siasa.

“Hatusemi ni bahati mbaya kwa kuwa mauaji yaliyotokea Septemba 2, mwaka huu ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi, inaonekana kabisa yalifanyika kwa makusudi, jambo ambalo linaonyesha kuwa Serikali imejipanga kufifisha demokrasia kwa njia ya mtutu wa bunduki,” alisema.

 

Inashangaza kweli; Hawaongelei NGUVU ZA POLISI? au CCK ni Wajumbe wa CCM Umoja wa VIJANA... Sababu wametoa kauli hiyo

hiyo
 
Enzi za Mobutu huko Zaire ( sasa DRC) kulikuwa na vyama vya siasa 300 hivi, lakini 295 vilikuwa vyama vyake mwenyewe.
 
Nasema hivi mwaka 2015 magamba yote tutayavua tu hata watumie hao wachumia tumbo kuisakama M4C yetu.
 
Hako ka jamaa ka cck naona kanatafuta umaarufu kupitia jina chadema, maana bila kutaja chadema habari yake isingeandikwa wala kusomwa hivyo isingejulikana kirahisi kama kuna mtu kama huyo na chama kama hicho, kwani ni ukweli usiojificha kwamba katika vichwa vya habari vya magazeti likikosekana neno chadema, hiyo siku biashara ya magazeti itakuwa ngumu sana.
 
Inashangaza kweli; Hawaongelei NGUVU ZA POLISI? au CCK ni Wajumbe wa CCM Umoja wa VIJANA... Sababu wametoa kauli hiyo hiyo
POLICCM Mbona Hamja itaja?au ndo imewatuma?,mnajifanya hamjui kuwa iringa hapakuwa na mkutano bali ufunguzi wa tawi?, Wala hamjui kuwa CCM walikuwa wakiendelea na mikutano ya ndani bila kubugudhiwa?,Fiesta ilikuwa ikiendelea bila bugudha!,Bu bubu CCM wamerudisha fomu kwa maandamano na sensa ilikuwa bado inaendelea,Mkitumwa muwe mnachanganya na yenu vinginevyo ''MNAUMBUKA'' na lugha zenu za vitu vizito vilivyo rushwa toka mbali.Sasa hapa ndo mmetumia akili zenu ZOTE kuandika hii hotuba.USHAURI WA BURE:subirini ndoa ya mkeka
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom