Mimi shabiki namba moja wa Masoud ila sijui ana maana gani hapa. Ni Chadema. Kitaeleweka tu masoud. lakini kama anafikiri wananchi wamekosa chama cha kweli nasema Tanzania inakosa tume ya uchaguzi
Kwa mimi nilivyomuelewa ni kuwa hii machine inatumika KUTENGENEZA KARATASI ZA KUPIGA KURA LAKINI KWA SABABU KUNA MAGUMASHI DETECTOR HIZI KARATASI ZITACHAKACHULIWA NDO MANA MATOKEO YA 2005 YALIKUWA TOFAUTI
SOMA MWANAHALISI LEO 06/10/2010 UTAWEZA KUJUA KIVIPI HAWA WATU WANACHAKACHUA
Kwa akili ya kupambanua mambo haraka haraka naona Masoud hapa anataka kutuambia hivi: Hii MAGUMASHI DETECTER ni x-ray au microscope yaCCM (Rangi ya kijani). Kila mtu anajua kuwa kila mwana CCM husema kuwa ukimkata ngozi na wembe inatoka ''green blood''. Sasa fikiria mtu mwenye damu ya kijani anafananaje!!!Kwa hiyo rangi ya MAGUMASHI DETECTOR inajieleza yenyewe kuwa ni mtambo wa CCM!
Kwa hiyo MAGUMASHI DETECTOR ni chombo cha CCM ambacho kazi yake ITAKUWA KUCHAKACHUA MATOKEO YOTE YA KURA ZITAKAZOPIGWA HIYO SIKU YA TRH 31/10/2010. Hii MAGUMASHI imeandaliwa maalumu kwa ajili ya kupotosha,kubadili na kufuta karatasi zote za wale watakaopiga kura za kuwanyima CCM kura.
Lipumba aliwahi kuambulia kura sifuri (0) kwenye kituo alichopigia kura kwa maana kuwa hata yeye mwenyewe hakujipigia kura!!!!
Maana yake ni kwamba MAGUMASHI inabadilisha na kufuta kura zozote zilizo kinyume na CCM bila kujali hata kama umejipigia mwenyewe.
Hi MAGUMASHI ni hatari sana.
Namshukru Kipanya kwa kututahadharisha kuwa UWIZI WA KURA LAZIMA UTAKUWEPO NA UTAFANYWA NA WANA CCM(Rangi ya kijani).
Kinachotakiwa ni ulinzi wa uhakika ili kuzuia kura zetu wasije wakapata nafasi za kuziingiza kwenye mashine hili.
Safari hakuna kulala mpaka kieleweke.
Mnakumbuka kile kipindi chake kupitia TBC cha Maisha Plus??? TBC ni CCM na Kipanya ni wa CCM.
Nilikuwa najaribu kutafuta maana hasa ya neno MAGUMASHI. Kama sitakosea itakuwa ni ufupisho wa MATOKEO,ya KUGUSHI MAZURI kwa uSHINDI !!!!!!!
CCM wameshajipanga kugushi matokeo ya Uchaguzi ili washinde kwa kishindo. Tuweni macho sana siku ya Uchaguzi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.