Capella keyboard

castongo

Member
Mar 16, 2008
57
67
Kuna wanaochora Muziki "Nota" kwa kutumia program inayoitwa capella.
Kuna ujanja wa kubadili keyboard kurahisisha uchoraji


Yacapella.exe
NB:
(KUIANZISHA - doubleclick Icon)(KUISITISHA - bonyeza escape "Esc" key)(KUIPOZI -pause "F9").

NI NINI?
Script ndogo (1.mb) ya kubadili mpangilio wa computer keyboard kwa muda.

KWANINI
kwaajili ya kurahisisisha matumizi ya program ya kuchora nota za muziki - Capella.

KWA NANI:-
Wale wanaotumia program ya Capella kuchora nota.Wale wenye kutumia computer za windows.Wale wanaotumia computer keyboard kuchora nota, tofauti na wale wanaotumia mouse, au midi keyboard.Wale wenye "touch typing",- kuchapa bila kuangalia keyboard.Wale wenye kufikiria kwa kiswahili...-- (......Vigezo vyote na masharti kuzingatiwa).


UCHORAJI WA KAWAIDA
Kwa computer keyboard kwenye capella, "setting zikiwa kawaida" utatumia yafuatayo:-
"1" kwa Nota ya mapigo manne."2" kwa Nota ya mapigo mawili."4" kwa Nota ya Pigo moja."8" Kwa Nota ya Nusu pigo."6" Kwa Nota ya robo pigo."a, b, c, d, e, f g" kwa toni za nota."+" kwa accidental nusu toni juu."-" kwa accidental nusu toni chini."F2" kwa kushuka Octave chini."F3" kwa octave ya kawaida."F4" kwa kupanda octave juu."." kwa nota yenye doti."Space bar" kwa mapumziko.[NB: Unaweza pia kutumia "Shift" au "Caps lock" kupanda au kushuka octave moja.]


KWA YACAPELLA.EXE
Nimeweka mambo katika namna inayofikirika kirahisi zaidi kwa kiswahili,
Kupunguza mzigo wa processing kwenye akili,
Kusogeza mambo ndani ya mwendo wa kawaida wa typing.

-- Yacapella.exe, inapanga keyboard namna nyingine "kwa muda tu.." ili kurahisisha na kuharakisha mambo.


KWA VIPI
Kwa kuweka:-
"1" kwenye "z"."2" kweye "l"."4" kwenye "m"."8" kwenye "n"."6" kwenye "r"."+" kwenye "j"."-" kwenye "t"."F2" kwenye "s"."F3" kwenye "k"."F4" kwenye "p".

ILI:-
Nikitaka kuweka nota "NZIMA" (mapigo manne) nibonyeze "z" badala ya "1".Nikitaka kuweka nota ya mapigo "MAWILI" nibonyeze "l" badala "2"Nikitaka kuweka nota ya pigo "MOJA" nibonyeze "m" badala "4".Nikitaka kuweka nota ya "NUSU" pigo nibonyeze "n" badala "8".Nikitaka kuweka nota ya "ROBO" pigo nibonyeze "r" badala "6".Nikitaka ku-"JUMLISHA" nusu toni ya accidental juu, nibonyeze "j" badala ya "+".Nikitaka ku-"TOA" nusu toni accidental chini, nibonyeze "t" badala ya "-".Nikitaka ku-"SHUSHA" octave nibonyeze "s" badala ya "F2".Nikitaka kurudisha kwenye octave ya "KAWAIDA" nibonyeze "k" badala ya "F3".Nikitaka ku-"PANDISHA" octave nibonyeze "p" badala ya "F4".

NADHANI UNAONA UHUSIANO KATI YA:-
"NZIMA" na "z" (Kwaajili ya kuchora nota nzima - yaani mapigo manne)."MAWILI" au "MBILI" na "l" (Kwajili ya kuchora nota ya mapigo mawili)."MOJA" na "m" (Kwaajili ya kuchora nota ya pigo moja)."NUSU" na "n" (Kwaajili ya kuchora nota ya nusu pigo)."ROBO" na "r" (Kwaajili ya kuchora nota ya robo pigo)."JUMLISHA" na "j" (Kwaajili ya kuchora nota accidental nusu toni juu)."TOA" na "t" (Kwaajili ya kuchora nota accidental nusu toni chini)."SHUSHA" na "s" (kwaajili ya kuchora nota octave chini)."KAWAIDA" na "k" (Kwaajili ya kuchora nota kwenye octave ya kawaida)."PANDISHA" na "p" (Kwaajili ya kuchora nota octave juu).--[NB: Unapochora nota kwenye F Clef, weka "Caps Lock" ili octave ya kawaida ianzie "C" ndani ya staff.]


Ni kiasi cha kukariri uhusiano huo, na baada ya hapo mambo yanakua rahisi.

Kawaida kabisa naiwasha script hii wakati ninapoanza kuchora nota, nai- pause wakati wa kuandika lyrics au kusave file, kwa kubonyeza "F9" na kuizima ninapomaliza. Kuizima bonyeza "ESC" key juu kushoto. Au rightclick alama "H" kwenye windows task bar chini kulia. [kuizima kwa Esc lazima uwe umeiondoa kwenye pause]

Kwa kutumia script hii, nimejikuta naweza kuangalia karatasi ninayocopy peke yake bila kuhamisha hamisha macho na hivyo kuchora kwa kasi zaidi. Kwaajili ya ufanisi zaidi, wakati mwingine nachora nikiwa natamka.

Kama una mapendekezo ya mpangilio unaokufaa wewe zaidi, unaweza kuniandikia castongo@gmail.com, au pale pale kwenye dropbox, ila katika mapendekezo yako zingatia kwamba hautumii herufi zile unazotumia kuandika toni, yaani "a-g" au kama unatumia "drmfslt", kwakuwa hakuna herufi inayotakiwa kujirudia.

Enjoy

Idownload hapa https://www.dropbox.com/s/8p9z6z86382rlnt/Yacapella.exe?dl=0
au tembelea https://castongo.carrd.co/
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom