Bw. vijisenti kuachia ngazi wiki ijayo?

Huu utatu usio mtakatifu lazima utupiliwe mbali kabisa. Ni suala la muda tu.
 
Bwana Vijisenti, hawezi kabisa. Kwanza ndo mwenye siri nyingi za maovu yote yaliyofanyika kisheria uchwara kwa miaka zaidi ya 18, ubinafsishaji mbaya, ukwapuaji BoT, yeye ndo anayejua Balali yuko wapi na kwanini alitangazwa kafa, anayajua makampuni yote hewa, ananguvu kuliko hata mwenyekiti wa chama chao.
 
logically hatutakiwi kushabikia watu kujivua magamba....hii yote ni danganya toto na ni sera madhubuti ya kulindana...great thinkers naomba tuwe makini katika hili suala...
 
Ahaaa!wapi!mpaka wamfukuze yule ana wapima ccm kwani ameshajua kuwa akuna wakumgusa au kufukuza au kumpa barua ya kumtimua jamaa ana roho ya chuma.maana anazijua vizuri zile siasa zaz bora wote tukose.kama alivyofanya kwa sita ktk kinyang`anyiro cha kiti cha uspika.
 
Hvi mnajuu kwamba Chenge aliwakodisha RITES mabehewa yake ya abiria pale TRC na kwamba kati ya hayo mabilioni ambayo RITES wanaidai serikali ya jamhuri ya watanzania waliolala na CHENGE yumo? Chapeni usingizi wabongo huku mkiimbiwa nyimbo nzuri za maisha bora n.k,n.k,n.k za kuwabembeleza
 
tetesi nilizonazo ni kuwa Bwana vijisenti ameaafiki maamuzi ya CC CCM na kuwa ataachia ngazi zote ndani ya ccm na serikalini wiki ijayo......hususani Ubunge.....hili llitamwacha lowassa katika njia panda kwa sababu ataonekana ni pekee yake aliyekiuka maagizo ya cc kuhusiana na dhana nzima ya kujivua gamba...................................

nionavyo Bwana vijisenti kaamua kutii ili kulindwa asishitakiwe...........

Du imesimama hiyo.Habari njema kwa Wana wa Tanzania.Manake ni nafasi njema kwa wapenda maendeleo na demokrasia Tanzania kupata nafasi nyingine kusonga mbele na kuimarisha taifa kwenye ustawi na kutupatia furaha Watanzania na pia ni nafasi nyingine ya CCM kutumia nafasi hii kujenga na kuimarisha chama hicho kuwa moja ya vyama vyenye vuguvugu la kuleta maisha bora kwa raia wake kwa faida ya wote.Lakini pia kwa vyama vya upinzani kujiimarisha na kuwajenga wananchi waamini kuwa kama wakipewa dhamana ya kuchukua madaraka ya Serikali watalijenga Taifa na si kuliboa Taifa,na kwa kipindi hiki ni nafasi njema kwa CHADEMA na kwa kiasi fulani CHAMA CHA CUF.
 
Wizi katika nchi hii haujasababishwa na Chenge, wizi umesababishwa na unaendelezwa na CCM.
CCM ndo inatakiwa iondoke.
 
Yote tisa hapo cha msingi na sekondary ni watuachie jimbo tukawashe moto....sio kujiuzulu tuu mimi nataka hawa magamba hata wafe wote maana wabishi kukubali sana

logically hatutakiwi kushabikia watu kujivua magamba....hii yote ni danganya toto na ni sera madhubuti ya kulindana...great thinkers naomba tuwe makini katika hili suala...
 
Huyu bwana mbona kangamala hivi ni nani amemhakikishia usalama wake hadi hiyo 2012 kwenye uchaguzi wa ccm Dodoma......................ni vyema akajitokeza hadharani tumfahamu........
 
Mi nahisi hizi ni hisia za mwandishi wa hii thread maana hakuna uwiano wowote wa chanzo cha habari na mwandishi, tumaweza kujikuta tunapoteza nguvu nyingi kujadili hoja zisizokuwa na msingi wala mantiki eti tu kwa sababu hoja inavutia.

A friend of my enemy is my enemy too
Na uhalisia ndiyo huo watu wanajadili hisia za mtu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom