Bw. vijisenti kuachia ngazi wiki ijayo?

jimbo la chenge limekaa vizuri likiwa wazi. Kama Dr. Slaa akipiga mikutano ya nguvu cdm wanalichukua. Sasa hivi kuna upinzani dhaifu wa UDP ambao hata hawajui watawafikisha wapi wananchi wao.

Ila wananchi wa kule wanapenda sana utani. Kam cdm wakipata kijana anayejua kurusha vijembe vya kuwafurahisha watu basi anaweza kushinda . Wale watu hawapendi sana mtu ambaye yuko serious ndo maana cheyo huwa anashinda kwa sababu tu ya vijembe vyake vile.

Ila kiukweli vijisenti huwa anashinda kwa kununua tu hawezi hata kuongea. Mke wake ndo huwa anapiga kampeni maana kanajua kupiga vijembe na ndo kanagwa pochi.
 
Aachie ngazi apitie gerezani asubirie hukumu yake, watamlinda ila tukichulua nchi buku mbili na kumi na tano tutatenga magereza ya wanasiasa mafisadi na zulmati.
 
tetesi nilizonazo ni kuwa Bwana vijisenti ameaafiki maamuzi ya CC CCM na kuwa ataachia ngazi zote ndani ya ccm na serikalini wiki ijayo......hususani Ubunge.....hili llitamwacha lowassa katika njia panda kwa sababu ataonekana ni pekee yake aliyekiuka maagizo ya cc kuhusiana na dhana nzima ya kujivua gamba...................................nionavyo Bwana vijisenti kaamua kutii ili kulindwa asishitakiwe...........
Kama ni kweli itakuwa ushindi mkubwa kwa Nape!
 
RACHEL kuachia ngazi peke yao haitoshi.NEC yote imeingia madarakani kwa kutumia rushwa.Kwa hiyo ili tuone kwamba CCM iko kweli serious na kujivua magamba,lazima NEC yote iondoke.Vinginevyo yote wanayofanya ni usanii mtupu.
tetesi nilizonazo ni kuwa Bwana vijisenti ameaafiki maamuzi ya CC CCM na kuwa ataachia ngazi zote ndani ya ccm na serikalini wiki ijayo......hususani Ubunge.....hili llitamwacha lowassa katika njia panda kwa sababu ataonekana ni pekee yake aliyekiuka maagizo ya cc kuhusiana na dhana nzima ya kujivua gamba...................................

nionavyo Bwana vijisenti kaamua kutii ili kulindwa asishitakiwe...........
 
Chenge anaweza kujivua GAMBA lakini huyu alikuwa messenger, waliomtuma bado wapo na watawatuma akina Chenge wengine. Politically, Chenge is a nobody, labda kama ataamua kumwaga mboga hadharani ili kila aliyehusika abebe msalaba wake.
 
tetesi nilizonazo ni kuwa Bwana vijisenti ameaafiki maamuzi ya CC CCM na kuwa ataachia ngazi zote ndani ya ccm na serikalini wiki ijayo......hususani Ubunge.....hili llitamwacha lowassa katika njia panda kwa sababu ataonekana ni pekee yake aliyekiuka maagizo ya cc kuhusiana na dhana nzima ya kujivua gamba...................................

nionavyo Bwana vijisenti kaamua kutii ili kulindwa asishitakiwe...........[/QUOTE]

Mkuu Ruta kama kapewa deal ya kuachia ngazi ili asishtakiwe kwa ufisadi mkubwa alioufanya yeye na mafisadi webzie akina Mkapa, Mramba, Idrissa naona hiyo deal imejaa ufisadi mkubwa. Kama ni kweli, kwa mara nyingine tena maslahi ya mtu binafsi na chama cha magamba yamepewa kipaumbele badala ya yale ya nchi ambapo pesa za walipa kodi zaidi ya $12 millioni zimegawanywa miongoni mwa mafisadi.
 
jimbo la chenge limekaa vizuri likiwa wazi. Kama Dr. Slaa akipiga mikutano ya nguvu cdm wanalichukua. Sasa hivi kuna upinzani dhaifu wa UDP ambao hata hawajui watawafikisha wapi wananchi wao. Ila wananchi wa kule wanapenda sana utani. Kam cdm wakipata kijana anayejua kurusha vijembe vya kuwafurahisha watu basi anaweza kushinda . Wale watu hawapendi sana mtu ambaye yuko serious ndo maana cheyo huwa anashinda kwa sababu tu ya vijembe vyake vile. Ila kiukweli vijisenti huwa anashinda kwa kununua tu hawezi hata kuongea. Mke wake ndo huwa anapiga kampeni maana kanajua kupiga vijembe na ndo kanagwa pochi.
Ni kweli nakubaliana na wewe mke wa chenge ndio kila kitu kuanzia kuongea ,kugawa pesa hata kuwanunulia vijana pombe na bange ni yeye na kama sio huyo bibie kushinda ubunge ingekuwa ni ngumu. Kuna watu wameongelea kuhusu majivuno, kiburi, jeuri na dharau za Chenge, niwakumbushe tu Chenge ni Mnyantunzu na tena ni msomi wa Havard lazimaAwe hivyo hizo ni tabia zao lakini nafkiri kama kapewa altenative ya kujivua gamba au ya kupelekwa kwa pilato atachagua kujivua gamba we unafkiri hizo nyodo atampelekea nani gerezani!!!?? lazima awe mdogo na Unyantunzu wake
 
Hii ni nzuri ila ningefurahi zaidi kama viongozi walioko madarakani sasa ndo waachie ngazi. Kina JK, Pinda, Werema, Ngeleja, Anne Makinda, Mkulo nk. Hawa ndo ambao si rahisi kwa wananchi kuwaondoa kwasasa na wakiondoka mambo yatabadilika. Hao kina Chenge, Lowassa, Karamagi hata wakiondoka sasa sidhani kama ugumu wa maisha utapungua zaidi ya nafsi zetu kusuuzika huku tukiendelea kutaabika.
 
Chenge anaweza kujivua GAMBA lakini huyu alikuwa messenger, waliomtuma bado wapo na watawatuma akina Chenge wengine. Politically, Chenge is a nobody, labda kama ataamua kumwaga mboga hadharani ili kila aliyehusika abebe msalaba wake.

Mkuu inawezekana ana Godfather katika unyangau ndio maanake akasema hizo pesa wanazomtuhumu labda ni ndogo kuliko hao Ma masterminder wa syndicate.Kama hakuna watu wa kumkingia kifua agekuwa amevuliwa ubunge na kushtakiwa licha ya Kusoma Havard.
 
mkuu uko sawa kabisa na kapanga anaelekea nayeye kwenye jimbo lake siku ya jumatano alhamisi ataisha waandishi wa habari
sasa atakachosema sijajua tumwachie Mungu hope na yeye atakodisha watu wa kulia maana wa jimbo lake wanavyolia hata wakati wa ile shughuli yetu ya ndoa sasa sembuse kungatuka si wanautoa uchozi kama wendawazimu

hili la kujiuzulu wanadhani ndiyo mwisho wa kila kitu lakini uwajibikaji utaanza pale tutakapoona wanapelekwa mahakamani kujibu hizi tuhuma za kutupora mali zetu isivyo halali na kinyume cha sheria......................
 
Kama ni kweli itakuwa ushindi mkubwa kwa Nape!
nape hajasababisha rostam kurudisha nyadhifa za uongo, ALIYEMTAJA ROSTAM PALE MWEMBE YANGA NDIYE, nape amtafute ambaye hajatajwa aibue ufisadi wake kisha amtimue, hapa nape hahusiki kabisaaaa, akijaribu kujisifu mzomeeni, anadandia gari kwa mbele.
 
Hii ni nzuri ila ningefurahi zaidi kama viongozi walioko madarakani sasa ndo waachie ngazi. Kina JK, Pinda, Werema, Ngeleja, Anne Makinda, Mkulo nk. Hawa ndo ambao si rahisi kwa wananchi kuwaondoa kwasasa na wakiondoka mambo yatabadilika. Hao kina Chenge, Lowassa, Karamagi hata wakiondoka sasa sidhani kama ugumu wa maisha utapungua zaidi ya nafsi zetu kusuuzika huku tukiendelea kutaabika.

hao kwenye nyekundu wanajiona wao ni miungu na ndiyo maana wanawatoa wenzao makafara..........lakini mwisho wa siku itabidi nao watueleze mchango wao kwenye ufisadi tajwa........................hawawezi kujitetea ya kuwa hawakuwa wanajua kitu.......................kwenye rada JK akiwa ni waziri wa mambo ya nje aliwahi kudai ya kuwa ile rada ni muhimu................sijui alikuwa anaongea kama mwanasheji au kama mwasiasa...............wakati nchi hata jeshi la anga hatuna na rada tajwa haina uwezo wa kuifunika nchi nzima na ina gharma kubwa ya kuiendesha....................na tuongeapo ni mbovu haifanya hata kazi lakini pesa zimekwenda..................
 
Mkuu Ruta kama kapewa deal ya kuachia ngazi ili asishtakiwe kwa ufisadi mkubwa alioufanya yeye na mafisadi webzie akina Mkapa, Mramba, Idrissa naona hiyo deal imejaa ufisadi mkubwa. Kama ni kweli, kwa mara nyingine tena maslahi ya mtu binafsi na chama cha magamba yamepewa kipaumbele badala ya yale ya nchi ambapo pesa za walipa kodi zaidi ya $12 millioni zimegawanywa miongoni mwa mafisadi.

I concur with this view....................
 
Kwa wale mnaofikiri ya kuwa Chenge a.k.a. Mzee wa Vijisenti na EL a.k.a. Richmonduli kwamba watajiuzulu nyadhifa zao zote kama alivyofanya RA kule Igunga ni ndoto za mchana. Hawa jamaa wawili ni 'hardcore magambaS' wa CCM.

Lowassa alishasema kuwa HAWEZI KUJIUZULU MARA 2.Never on earth. Kama wakti ule alikubali kupoteza u-PM kwa skandali ya Richmond kwa sasa hayuko tayari kujiuzulu Ubunge na nyadhifa zake zote ndani ya CCM. Kama mnafuatilia vizuri matamshi yake aliyotoa juzi pale DOM baada ya kuulizwa maoni yake kuhusu kujiuzulu kwa rafiki yake kipenzi RA. EL alisema hakutegemea kuwa RA amgelichukua UAMUZI KAMA HUO. Hii ina maana kwamba EL hataweza kuchukua maamuzi ya RA hata kidogo! Amesema muda ukifika na yeye atatoa maamuzi yake,lakini si ya kujiuzulu.Subirini muone.

Kwa mzee wa Vijisenti hana mpango huo yeye lao moja na EL.Labda utokee muujiza wa aina yake kwa hawa wawili kufikia uamuzi wa RA.
Kwanza kuna jambo la kuangalia hapa kuwa KUJIUZULU KWA RA KUMESHTUA VIGOGO WENGI WA CCM akiwemo Nnape mwenyewe. Viongozi wengi wa CCM wamepigwa butwaa na kuduwaa kwa kitendo cha RA. Most of them have remeined speechless to date! Hata domokaya Nape aliyekuwa mwamba wa kuwadonyoa na kuwadodosa mapacha 3 naye amepigwa sindano ya ganzi tangu juzi hajapiga makelele yake ya jukwaani baada ya RA KUMSHUTUMU BINAFISI kuwa wao Nape na Chiligati ndiyo wamekuwa sehemu ya GUTTER POLITICS kama alivyoziita RA.

Yawezekana kabisa keshatonywa na wazee wa Chama Cha Magamba kuwa Nnape chama unakiuuwaaaaaaaaaa!
 
Hii ni wazi kabisa rostam na chenge wamepewa 'immunity' na kikwete. Kikwete ana vita na Lowassa ingawa naamini wote ni majambazi sioni sababu za lowassa kutengwa na kufanyiwa huu unyama hadharani. Ushahuri kwa lowassa ni ahakikishe anaondoa na uraisi wa kikwete. Lazima lowassa asikubali kufanyiwa huu udikteta na ajue kwamba demokrasia ikikua lazima na ukweli ujulikane. Kwanini peke yake atengwe na kuonekana yeye ndio chanzo cha wizi kwenye serikali za ccm? Kama lowassa ni gamba inaonekana wazi kikwete ndie nyoka mwenyewe na watanzania hatutaki magamba wala majoka yenyewe.

Chadema tummalize kikwete na ccm for good. Tuhakikishe hakuna mtanzania kama kikwete wala mkapa anapata uraisi Tanzania tena.
 
Kama ni kweli itakuwa ushindi mkubwa kwa Nape!
nape hajasababisha rostam kurudisha nyadhifa za uongo, ALIYEMTAJA ROSTAM PALE MWEMBE YANGA NDIYE, nape amtafute ambaye hajatajwa aibue ufisadi wake kisha amtimue, hapa nape hahusiki kabisaaaa, akijaribu kujisifu mzomeeni, anadandia gari kwa mbele.
 
Mkuu naomba wana JF ututoe wasiwasi, hizi tetesi chanzo chake ni kipi? Huyu AC ni Lawyer aliyebobea pia ni Mnyantuzu mchozi (mtafutaji) hivyo anaamini hana hatia hadi ithibitike kotini. Kama atajivua gamba huyu AC na EL lazima afuate nyayo.
 
Kuachia ngazi ni mazingaombwe tu, bila mtu kushitakiwa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Hi dhana ya mtu kuachia nagazi halafu hakuna hatua za kisheria zinachukuliwa inajenga utamaduni wa watu kupora mali za umma wakijua kuwa ukiachia ngazi unapongezwa na kuonekana shuja.
Point, hiyo kitu ya kuachia ngazi baada ya wizi inanichefua sana jamani kwa nini wasipigwe risasi hadharani kama china?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom