Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,504
- 9,283
Kulingana na Ripoti iliyotolewa na NBS, kwa sensa ya 2022 Tanzania imefikia kiwango cha 83% cha kujua kusoma na kuandika miongoni mwa watu wazima yaani miaka 15 na kuendelea ikiwa ni ongezeko la 6.3% toka 78.1% cha sensa ya 2012.
Katika kuhakikisha Watanzania wote wanajua kusoma na kuandika, Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali imeendelea kutekeleza afua mbalimbali ikiwemo kuondoa vikwazo vya kupata elimu kama vile kutolewa kwa elimu ya msingi bila ada, elimu ya lazima sasa kuwa ya miaka 10, kutekeleza programu zenye lengo la kuwafikia Watanzania waliokosa fursa za elimu kwa mfano: Elimu ya Watu Wazima na ujifunzaji endelevu, utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa kisomo pamoja na kutoa fursa kwa wanafunzi walioacha masomo kwa sababu mbalimbali kurudi shuleni na kuendelea na masomo (re-entry program) kupitia Waraka Na. 2 wa mwaka 2021.
Pamoja jitihada hizo, Serikali imeendelea kuboresha huduma za maktaba nchini katika ngazi za Mikoa, Wilaya na shule ikiwa ni pamoja na maktaba mtandao ili kuwawezesha Watanzania wengi zaidi katika maeneo mbalimbali kupata huduma ya kujisomea huko waliko.
Aidha, Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kwa lengo la kuongeza fursa kwa Watanzania wengi zaidi kujiunga na Elimu ya Watu Wazima.