Rais Samia na Makamu wa Rais wa Marekani wametajwa tena na Forbes kuwa miongoni mwa wanawake 100 wenye nguvu na ushawishi mkubwa Duniani

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,305
9,734
Ndugu zangu Watanzania,

Rais samia Anaendelea kuchanja mbuga ulimwenguni kote ambako Dunia inaendelea kutambua mchango wake katika maendeleo na mchango wake katika kile Secta Katika kuleta matokeo chanya kwenye maisha ya watu.

Kwa mara nyingine tena ametajwa na Forbes Kama miongoni mwa wanawake mia moja wenye nguvu na ushawishi mkubwa sana Duniani ambako kwa sasa ameshika nafsi ya 93.ambapo katika list hiyo ya wanawake 100 yupo pia makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris pamoja na wanawake wengine.

Jina la Rais samia limeendelea kuitikisa na kuiteka Dunia kutokana na mchango wake chanya katika uchumi na hatua za kisera na kisheria ambazo amezichukua na ambazo zimeleta matokeo chanya kwa watanzania tangia alipochukua madaraka ya urais katika mazingira magumu kwa kila kitu.

Tumeona namna Rais wetu alivyoifungua nchi yetu kiuchumi na kidiplomasia na sasa jina la Tanzania linatajwa na kutangazwa mpaka na shirika la ujasusi la Marekani CIA. hiyo yote ni kazi ya Rais samia na mikono ya Rais samia katika kuifinyanga Tanzania na kuiweka katika Ramani ya ulimwengu .

Dunia imetambua kazi mbalimbali zilizofanywa na Rais samia.kazi ya kumrejeshea mtoto wa kike ndoto na matumaini ya kutimiza ndoto ya kupata elimu mpaka chuo kikuu,kazi ya kuwafanya hata watoto wa masikini wawe na uhakika wa kupata elimu bila kikwazo baada ya Rais samia kufuta ada hadi kidato cha sita,kazi ya kujenga zahanati,vituo vya afya, hospitali za wilaya, mikoa kanda na hadi rufaa.

kazi ya kutoa ajira na fursa za ajira kwa maelfu ya vijana,kazi ya kuimarisha demokrasia na uhuru wa watu kuzungumza na kujieleza na kutoa maoni yao,kazi ya kuimarisha haki katika utendaji wa serikali,kazi ya kuboresha maslahi ya watumishi wa umma,kazi ya kuwafanya watanzania wajivunie kuzaliwa Tanzania nakuwa Watanzania,kazi ya kuwafanya watu wawe huru kwenda watakako ndani ya nchi yao ,kazi ya kuifungua nchi yetu, kuchochea Secta Binafsi na biashara kwa kuweka mazingira mazuri na wezeshi kwa atakaye kufanya biashara au kuwekeza nchini,kazi ya kujenga uchumi jumuishi unaogusa maisha ya watu na kukua katika mifuko ya watu.

kazi ya kuleta Tabasamu na kuinua viwango vya furaha kwa watanzania,kazi ya kuiweka serikali mikononi mwa Watanzania , kazi ya kuliheshimisha Taifa letu kimataifa,kazi ya kurejesha imani ya wawekezaji na wafanyabishara wakubwa.

Hayo yote yamefanikiwa kutokana na ushupavu na umadhubuti wa Rais samia.ni uhodari na akili kubwa na maono makubwa na ujasiri mkubwa na wa kipekee wa Rais Samia ndio umefanikisha hayo yote ambapo sasa Dunia imetambua mchango wake na ushawishi wake hapa Duniani miongoni mwa mamilioni ya wanawake.

Rais samia ni kama maji usipoyanywa utayaoga tu

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu

0742-676627.
 
Aaaah c'mon.
Anko pumzisha Fuvu Hilo.
Hivi Mkeo hachukii Mana Kila mida Samia Samia huchokii ?
Mimi kazi yangu ni kululetea habari kwa kadri zinavyojili hapa ulimwenguni ili usipotoshwe maana najuwa uwezo wa kusoma kwa mbumbumbu aina yako ni ngumu sana zaidi ya kulishwa Matango pori na kuimbishwa kama kasuku.
 
Huu ni ujinga hizo nguvu na ushawishi wake zinamsaidia Nini mtanzania? Mafisadi yamemshinda mvua mpaka mafuriko yanaua watu lakini mabwawa ya umeme hakuna maji na nchi Iko gizani, maisha magumu vitu vinapanda bei eti ushawishi,
 
Ingia Forbes Ndugu yangu kila kitu peupe naujionee namna Rais wetu anavyoendelea kuiteka Dunia.
Ingependeza zaidi unaleta uzi wako na chini unaweka link kuliko kuleta habari nusunusu alafu unaniambia niingie tena forbs kama ulijua taarifa zipo Forbes basi usinge leta uzi huku tungeenda wenyewe kuangalia Forbes
 
Ingependeza zaidi unaleta uzi wako na chini unaweka link kuliko kuleta habari nusunusu alafu unaniambia niingie tena forbs kama ulijua taarifa zipo Forbes basi usinge leta uzi huku tungeenda wenyewe kuangalia Forbes
Nimekurahisishia sana ndugu yangu maana pengine usingehahamu kwa uharaka nini kinaendelea huko Duniani.
 
Huu ni ujinga hizo nguvu na ushawishi wake zinamsaidia Nini mtanzania? Mafisadi yamemshinda mvua mpaka mafuriko yanaua watu lakini mabwawa ya umeme hakuna maji na nchi Iko gizani, maisha magumu vitu vinapanda bei eti ushawishi,
Acha uongo wako hapa .giza lipo kwako lakini siyo Tanzania. Nani kakwambia serikali imeleta mafuriko??
 
Jikite kwenye hoja
Jana niliulizwa jambo na mtu limenitafakarisha sana na nikakosa jibu labda nisaidiwe kujibu.
Aliniuliza, kwa nini Rais Samia katika kumpigia chapua na sifa kemkem wanatumika watu wenye upeo mdogo (mfano huyu Lucas mwashambwa ) badala ya watu wenye uelewa mkubwa?
Inaweza kuwa sifa ni za kweli au ni za uongo, lakini mbona kundi linalitumika ni hili la watu wa ajabu?
Nisaidieni ni jibu nini mie!

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Mimi kazi yangu ni kululetea habari kwa kadri zinavyojili hapa ulimwenguni ili usipotoshwe maana najuwa uwezo wa kusoma kwa mbumbumbu aina yako ni ngumu sana zaidi ya kulishwa Matango pori na kuimbishwa kama kasuku.
Kwahiyo katika dunia hii huna habari nyingine zilizojiri unazo za samia tu wewe chura wa kihansi
 
Back
Top Bottom