Bungeni: Mwigulu Nchemba achafua hali ya hewa!

Lissu kawatega CCM lakini kwa sababu it is a SILLY party hawakujua na hivyo wakajiingiza kwenye mtego! Amefunua 'veil' ya unafiki, na sasa CCM watatakiwa wachague ama ku-defend Silly bugdet au kuiunga mkono hiyo silly budget. You need more than a first class economics kung'amua huu mtego wa Lissu, na tayari Mwigulu na Komba wameshanasa. CCM you are in trouble.
 
CCM wanatapatapa kweli yaani wanatetea bajeti ambayo haimsaidii mwananchi wa hali ya chini.
 
Nawapongeza wabunge vijana wa Chadema,mimi siyo mwanachama wa chama chochote japo napenda sana siasa.David Mbunge wa Mbozi Magharibu ameongea vizuri sana hongera.Kwa Tundu Lissu aliamsha mori ya wakandamizaji wa watanganyika,nilitegemea Mwigulu awapongeze wenzie lakini duh wasomi wetu itabidi tuwaulize hizo degree zenu za first class mmezitoa wapi.Mzee wetu Komba apunguze jazba huu ni wakati wa vijana na maendeleo kama hamuwezi kwenda kwa pace yao chomoka tu bungeni unafanya nini kama huwezi ku-deliver?Ushauri tu kwa Mh.Tundu Lissu ,anamawazo mazuri lakini apunguze hasira.
Kwa kweli kwa wabunge waCCM kweli shame on them,wanalalamika halafu wanakubaliana na hoja kweli haingii akilini nadhani wao ndio tuwapeleke Mirembe maana hawatusaidii kwenda tunakotaka.
Mwigulu Nchemba naomba utangulie mwenyewe Mirembe umeudhi sana watanzania shame on you!!!!!!!!!!
 
nchemba aendelee kutapatapa tu ukombozi wa Iramba Mashariki unakaribia 2015. nawahamasisha vijana wa Iramba waendelee na juhudi za ukombozi kupitia cdm.
 
Sasa mkosa hoja kama huyo sijui kafata nini bungeni! Maana hata kama ni kutukana.......basi atleast he could have a link and meaning consistent to what had been argued by then!! Sio mtu anaonyesha makelele tuuuu...........bora kaongea!!
 
Yaani sielewi kabisa, maisha ya watz bado ni ya kufikirika zaidi kuliko uhalisia. Kila siku washabiki wa UJINGA na UPUMBAVU bado wanaongezeka na hali haieleweki. Sifikiri kama kuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuunga mkono bajeti ya trilioni 15 huku fedha kwa ajili ya maendeleo zikiwa ni kiasi cha trilioni tano tu, zingine trilioni 10 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida (mishahara, posho na allowances). Halafu kibaya zaidi, bado watz na WABUNGE tuliowachagua kutuwakilisha, wanaushabiki wa vyama bila ya kuzingatia UHALISIA wa mambo.

Hivi unaweza kubeza maneno aliyosema TUNDU LISSU kwa sababu tu wewe ni mshabiki au mwanachama cha ccm? Unaweza ukabeza maneno aliyoongea mbunge wa MBALALI kwa sababu tu wewe ni chama pinzani? Haiingii akilini hata kidogo.

Kweli, bajeti ni mbovu, na LISSU ameongea ukweli halisi kuwa "SHAME ON THE GOVERNMENT, SHAME ON CCM AS A RULING PARTY AND SHAME ON THE PARLIAMENT, including him". Kuna lipi baya katika maneno hayo? Japo siyo wabunge wote wanaopitisha upuuzi huu bungeni, lakini kwa sababu wengi wao wanapitisha, ni kweli,"SHAME ON THEM ALL"

Mtu kama Mwigulu na Komba, wanaongea nini? mimi hata sijaelewa. Hivi kweli, hata chadema wakichukua nchi hii sikumoja watakuwa wanaongea UJINGA na UPUUZI kama huu wa Mwigulu na Komba kwa sababu tu wao ndio wenye serikali? Mbona Bulaya ameongea vizuri sana? Au na yeye anajiandaa kwenda CDM? Mi hata sijui kama yupo mtu katika uelewa wake wa kawaida anajivunia kuwa Mtz, mimi NAVUMILIA TU, nitafanyaje ilihali nimezaliwa Mtz? Lakini in real sense, hakuna cha kujivunia hapa Bongo. Hata baada ya miaka hamsini ya kutawala, chama cha mapinduzi bado kinatoa ahadi kwa wananchi kama vyama vya upinzani. Nashangaa kweli. Badala ya kusema ni kipi wametekeleza, bado wanatoa ahadi. AIBU SANA.

Hata baada ya miaka hamsini ya kutawala, bado, serikali imeshindwa kupunguza matumizi yake, na badala yake, matumizi ya serikali yanazidi gharama ya miradi ya maendeleo. Najiuliza, ahadi za rais kikwete za meli ktk ziwa victoria, Nyasa na Tanganyika zipo kweli bajeti gani?

Kuna kitu kimenishtua, bajeti ya wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi ya mwaka wa fedha 2011/2012 ilikuwa bilioni ishirini na kidogo hivi, lakini fedha ambazo wizara ilipokea kutoka hazina kwa ajili ya miradi ya maendeleo ni bilioni nne. Sijui kuna miradi gani ilitekelezwa kwa fedha kiduchu kiasi hicho.

Seriously speaking, THERE IS NO FUTURE AND PROSPEROUS LIFE UNDER CCM GOVERNMENT!!!! Kama tumeshindwa kwenye sanduku la kura, haimaanishi watu wanaipenda ccm, tutafute njia mbadala, napendekeza MAPINDUZI YA SERIKALI, kwani hili litasiadia hata kuondoa mikataba yote ya kinyonyaji ambayo ccm imeingia na wazungu wanaoliibia taifa hili maliasili kwa ushuru kiduchu.

STK ONE,
 
Shida ya bunge letu, ni uvyama na wala si maslahu ya wananchi. Hii inakera sana.
 
Kwa kweli Nchemba amenikasirisha sana..kwanza najiuliza kile kiburi amekitoa wapi..anaongea kwa kiburi as if yeye sijui ni nani kwenye Tanganyika yetu..alikosa busara zaidi pale aliporusha budget kivuli na kusema ni takataka..what a shame kwa mbunge kufanya vile tena anayetoka chama tawala..imeniudhi sana.
 
Kuthibitisha ni jinsi gani hiki chama cha mafisadi kinazidi kufa, Wabunge wake wanadhani Watz na wale wale wa zama hizo!!!!
 
hiyo ndo 1st class yake na mwisho wa kufikiri kwakwe, ayo yote anayoyasema mbona wanafunzi bodi inasumbua, ifke mahali kama mchumi atoe mapendekezo, kwa kauli zake ha2tegemei m2 kama yy achangie vile na kudharau mawazo ya wenzake, alijua anawaponda wapinzani, kumbe anazidi kukishusha chama chake kwa wananchi. Bye bye CCM, mmefikia mwisho wa kufikiri kwa hao wanaojiita wachumi.
 
Time will tell,nimesikitishwa na mchema kwa kutochangia bajeti na kutumia muda aliopewa kuzungumzia bajeti ya upinzani na kutukana na kushambulia upinzani na kuchana bajeti ya upinzani.Hii inaonyesha kuwa ccm imeishiwa watu wenye busara na haina jipya.Watanzania tunataka hali bora ya maisha sio matusi ya mchemba namshauri abadilike au aendelee kuimaliza ccm yake
 
Aisee kumbe Mwigulu Nchemba hana akili kabisa. Anahitaji kupelekwa Mirembe CCM inakufa anaamua kutupa matope Bungeni kutukana upinzani waigizaji na vichaa na eti wana pepo mtaka vyeo.

Hasira zake nafikiri ni failure kule arumeru. Anataka kurudia yale ya Lusinde arumeru ama kweli CCM imekwisha. Ametupa bajeti ya Upinzani na kuiita rubbish
Neno waigizaji na pepo mtaka vyeo linaashiria kuikubali bajeti ya upinzani. Only that he can't take it lying down. Chances are he is defending his budjet, he is the architect
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Inatia mashaka na elimu ya mwigulu.Ndo maana wenye kumjua wanasema alitumia jina la mtu aliyefaulu lakini hakuwa na pesa ya kusoma.Hakuna jina la kisukuma kwa wanyiramba.Tundu kasema mpango mkakati wa serikali ni kutenga 8.6 trilioni kwa maendeleo kwa miaka mitano mfululizo.Mwaka jana badget wakatenga 4.6 trilioni,mwaka huu 4.2 trilioni.Kama Mwigulu ni mchumi alitakiwa achangie budget ya mwaka na si kujibu hoja za wapinzani ukizingatia wapinzani budget yao ni mbadala wala haitatumika.Akataka misifa ya ajabu,hata kwao Iramba akasahau kutolea mapungufu ya budget husika.Ni aibu kuwa na watu wa namna hii bungeni.Lissu kasema ukweli juu ya mapungufu aliyoyaona kwa mwaka huu ukilinganisha na mwaka jana.Mwigulu hovyo! anatetea ujinga na uchumi wa CCM hana lolote Shame to Him!
 
nchemba aendelee kutapatapa tu ukombozi wa Iramba Mashariki unakaribia 2015. nawahamasisha vijana wa Iramba waendelee na juhudi za ukombozi kupitia cdm.

2015 Kitila atasimama, Mungu atawakomboa wananchi wa Iramba.
 
Back
Top Bottom