kilolambwani
JF-Expert Member
- Dec 3, 2010
- 395
- 75
Acheni wagongane vichwa, Januari Makamba si amesema huo ni mpango wao wa taifa wa kuondoa posho, leo waziri mkuu anajikanyaga.
Kweli hii nchi yetu inazidi kujidhihirisha kuwa inaongozwa na VIHIYO WATUPU! Rais kihiyo,Spika kihiyo,PM kihiyo,IGP kihiyo,Mwanasheria Mkuu kihiyo,Jaji Mkuu kihiyo,Mawaziri vihiyo,Ma-DC/RC vihiyo n.k.
Sikutegemea PM wa Taifa maskini la Tanzania ambalo wananchi wake wanaishi chini ya Dola 1 kwa siku(chini Tshs.1500)!
Sikuamini masikio yangu nilipomsikiliza PM Kayanza Pinda akitetea ulaji wa Posho na Ulaji wa Wabunge wa CCM wa Tshs.150,000/= kwa siku!!!!
Je,hivi ni kweli huyu PM ndiye anayejitambulisha kama MTOTO WA MKULIMA????No,hawezi kuwa mtoto wa mkulima halafu atetea upuuzi huu!
Utetezi wake wa Posho ya 150,000/=kwa siku kwa kila Mbunge umejaa porojo,kebehi na longolongo tupu! Hivi ni nani aliyewaambia Wabunge kuwasaidia Wapiga kura wao au ndugu zao kwa fedha ya posho ya Seating Allowance????Hivi ni wabunge wangapi wanaogawa posho yao kila siku kwa wapiga kura wao wanaokuja pale mjengoni? Maana Pinda kadai kuwa ukitoka kwenye Ukumbi wa Bunge unakutana na mtu anakwambia mzee naomba unisaidie nauli nimeishiwa!!!!!! Huyu mtu(ndugu/mpiga kura anaishiwa nauli alikuwa anatoka wapi???
Ninachojua hawa Wabunge kuna fedha ya Mfuko wa Jimbo wanayolipwa kwa mwezi. Je,kwanini wasitumie hiyo kutatua kero na shida ndogo ndogo za ndugu au wapiga kura wao????
Mimi niseme tu kwamba CCM hawana hoja,Waziri Mkuu Pinda hana hoja! Wanachochotetea hapa ni WIZI,UFISADI NA UFUJAJI WA PESA ZA WALIPA KODI WA TANZANIA!
Mimi naweza kusema kwa ujasiri kabisa kuwa hii pesa ni katika zile wanazoziita TAKRIMA. Kwamba hii pesa CCM wanaing'ang'ania KWA AJILI YA KUENDELEA KUWAHONGA WAPIGA KURA ili uchaguzi unaofuata baada ya miaka 5 waweze tena kupewa ulaji. NAAMIMI KABISA KAMA MBUNGE NI BAHIRI HII PESA YA VIKAO AKIDUNDULIZA KWA VIKAO VYOTE VYA BUNGE KATIKA MIAKA 5 ATAKUWA MILIONEA!
Kwa hiyo pesa hii ya Seating Allowance wanayoing'ang'ania CCM ndiyo pesa ITAKAYONUNUA KURA KWA HONGO ILI KUWARUDISHA HAWA WABUNGE WA CHAMA CHA MAFISADI/MAGAMBA-CCM kwa kila chaguzi zinapofanyika.
Nawasilisha.
Nashanga kabisa. Chief whip wao anasema serikali imeliona hilo, likawekwa kwenye mpango wa miaka mitani ili posho hizo zifutwe. Akakubaliana na Mbowe kuwa posho hizi kwa watumishi ni tatizo, kuwa watumishi hawafanyi kazi bali kufukuzia posho. semina, warsha. makongamano nk. Akadai aliyeliona hilo kwanza siyo Zitto bali serikali. Sasa namshangaa huyu Pinda. Kweli amepinda. hajui hata yaliyomo kwenye mipango ya serikali yake.
Nani yupo sahihi, Pinda au Lukuvi? NAMLILIA EDWARD MORINGE SOKOINE.