Bungeni: Maswali ya 'papo kwa papo' kwa Waziri Mkuu

GR, vp mbna kmya, au nawe umehukumia na kanun ya 64.

Hakuna kipya sana muda huu Mkuu ila kazi zinaendele na Luninga ipo ON tunafuatilia kutoka sources zote, anything of interest tutapeana taarifa bila shaka...We are ON
 
kafanye kazi ***** we ujenge taifa lako. unafanya nini asubuhi hii yote kwenye luninga?


Kazi unaitafasirije Mkuu...Big up umesimama kusoma japo inaelekea ukweli huu unakuuma sana na Bado mpaka Bunge liiishe utakuwa umepungua kilo nyingi saana. Inaelekea unatumia JF Mobile na huko ulipo hata TV hakuna. Tembelea Modern Office utapata jibu la kukurupuka kwako
 
Walipo lizungumzia swala la mauji ya arusha hicho kifungu hakikuwepo au walikuwa hawakijui au mambo yamekuwa magumu hasa baada ya kugundua wanachemka waache unafiki....

Umetazama walivyoupotezea muongozo wa Lissu...Halafu hii hoja ya kuufanya muongozo kuwa suala la hiyari wafikie mahala kipingele hiki kitazamwe upya
 
Umetazama walivyoupotezea muongozo wa Lissu...Halafu hii hoja ya kuufanya muongozo kuwa suala la hiyari wafikie mahala kipingele hiki kitazamwe upya
Yaani wanakera sana hawa jamaa iko siku tutawafata huko huko bungeni washenzi wakubwa wamefanya nchi yao....
 
Makinda anawakandamiza sana wapinzani...afu hata PM nae alikuwa anamtegemea Spika amlinde kwenye maswali mengine.Mawazo ya mdau mmoja kuwa hii session ifutwe na yaafiki mana majibu hayana tija kabisa...Waziri mkuu hajui kama waziri wake analala Hotel na familia yake!!?
 
Maswali kwa waziri mkuu ni usanii mtupu. Mfano W/Mkuu anaulizwa kuhusu mawaziri kuishi hotelini, naye anamuuliza mbunge ni mawaziri gani, anapoambiwa ni nahodha, anajibu sawa nimesikia. Hapa tulitegemea W/Mkuu alijue hili kama kweli serikali yake ina nia ya kupunguza gharama, maana hili la nahodha limeandikwa hata na vyombo vya habari.
Pia, spika amepotezea(kwa kisingizio cha kesi zipo mahakamani) maswali kuhusu mauaji yanayofanywa na polisi-maana si Nyamongo au Tarime peke yake, mauaji yamefanyika sehemu nyingi tu kama Mbarali ambako kesi haipo mahakamani. Spika amekosa umakini ktk hili

Naomba ushauri kuhusu kesi za Nyamongo zilizoko mahakamani? Zinahusu Polisi kuua raia au ni kesi za baadhi ya watu kadaiwa kufanya uchochezi? kama ni kesi za uchochezi, Spika ana uhalali gani kudai kuwa maswali hayo yasijibiwe kwa kuwa kuna kesi mahakamani.
 
Kweli hii nchi yetu inazidi kujidhihirisha kuwa inaongozwa na VIHIYO WATUPU! Rais kihiyo,Spika kihiyo,PM kihiyo,IGP kihiyo,Mwanasheria Mkuu kihiyo,Jaji Mkuu kihiyo,Mawaziri vihiyo,Ma-DC/RC vihiyo n.k.

Sikutegemea PM wa Taifa maskini la Tanzania ambalo wananchi wake wanaishi chini ya Dola 1 kwa siku(chini Tshs.1500)!
Sikuamini masikio yangu nilipomsikiliza PM Kayanza Pinda akitetea ulaji wa Posho na Ulaji wa Wabunge wa CCM wa Tshs.150,000/= kwa siku!!!!
Je,hivi ni kweli huyu PM ndiye anayejitambulisha kama MTOTO WA MKULIMA????No,hawezi kuwa mtoto wa mkulima halafu atetea upuuzi huu!

Utetezi wake wa Posho ya 150,000/=kwa siku kwa kila Mbunge umejaa porojo,kebehi na longolongo tupu! Hivi ni nani aliyewaambia Wabunge kuwasaidia Wapiga kura wao au ndugu zao kwa fedha ya posho ya Seating Allowance????Hivi ni wabunge wangapi wanaogawa posho yao kila siku kwa wapiga kura wao wanaokuja pale mjengoni? Maana Pinda kadai kuwa ukitoka kwenye Ukumbi wa Bunge unakutana na mtu anakwambia mzee naomba unisaidie nauli nimeishiwa!!!!!! Huyu mtu(ndugu/mpiga kura anaishiwa nauli alikuwa anatoka wapi???
Ninachojua hawa Wabunge kuna fedha ya Mfuko wa Jimbo wanayolipwa kwa mwezi. Je,kwanini wasitumie hiyo kutatua kero na shida ndogo ndogo za ndugu au wapiga kura wao????

Mimi niseme tu kwamba CCM hawana hoja,Waziri Mkuu Pinda hana hoja! Wanachochotetea hapa ni WIZI,UFISADI NA UFUJAJI WA PESA ZA WALIPA KODI WA TANZANIA!

Mimi naweza kusema kwa ujasiri kabisa kuwa hii pesa ni katika zile wanazoziita TAKRIMA. Kwamba hii pesa CCM wanaing'ang'ania KWA AJILI YA KUENDELEA KUWAHONGA WAPIGA KURA ili uchaguzi unaofuata baada ya miaka 5 waweze tena kupewa ulaji. NAAMIMI KABISA KAMA MBUNGE NI BAHIRI HII PESA YA VIKAO AKIDUNDULIZA KWA VIKAO VYOTE VYA BUNGE KATIKA MIAKA 5 ATAKUWA MILIONEA!

Kwa hiyo pesa hii ya Seating Allowance wanayoing'ang'ania CCM ndiyo pesa ITAKAYONUNUA KURA KWA HONGO ILI KUWARUDISHA HAWA WABUNGE WA CHAMA CHA MAFISADI/MAGAMBA-CCM kwa kila chaguzi zinapofanyika.


Nawasilisha.
 
Tatizo la CCM wazo likitolewa na wapinzani wao wanaona halifai, hoja ya Zitto ni ya msingi na inatakiwa ifanyiwe kazi. Kazi ya mbunge zinajulikana na si kugawa hela kwa wananchi kama wanataka kugawa wagawe hela toka mishahara yao si wanalipwa vizuri
 
Nilishasema huyu Mzee anajaribu kutetea kitu ambacho hakiteteeki! Kwa kusema kwamba Posho ya Wabunge huwa wakitoka tu Mlangoni wanakutana na Wapiga kura wao waliokuja kuwaomba kwa hiyo ndipo inapokwenda! Ina maana huyu Muathirika anataka kutuambia kwamba Omba Omba imekubalika kama ni Sekta rasmi ambayo Serikali ya Magamba imeikubali!

Aache Siasa aongee realities!
 
Pinda hajitambui, ni mtu dhaifu, muoga, mnafiki ambaye CCM wanamtumia wakisema ni mtoto wa mkulima. Ni mtu ambaye hawezi kutoa agizo akalisimamia. Mfano mambo yaliyo mshinda ni suala la ununuzi wa mashangingi amebaki kuwa anasema tu lakini hasimamii, ni waziri mkuu kwa jina ila hana nguvu ya uwaziri mkuu. Anaendeshwa na upepo wa chama na mafisadi akiwemo yeye, si mpendi kabisa huyu Pinda.
 
Pinda hajitambui, ni mtu dhaifu, muoga, mnafiki ambaye CCM wanamtumia wakisema ni mtoto wa mkulima. Ni mtu ambaye hawezi kutoa agizo akalisimamia. Mfano mambo yaliyo mshinda ni suala la ununuzi wa mashangingi amebaki kuwa anasema tu lakini hasimamii, ni waziri mkuu kwa jina ila hana nguvu ya uwaziri mkuu. Anaendeshwa na upepo wa chama na mafisadi akiwemo yeye, si mpendi kabisa huyu Pinda.

nrango,

You're very right. Kweli huyu WM hafai na ni mwoga kiyama! Unanikumbusha pale alipotoa mchozi kuwalilia ma albino wanaouawa!!!!
Yaani badala ya kutoa tamko la kudhibiti hiyo hali Jamaa analia! Shame on him our PM. Bure kabisa!

Natamani Marehemu Edward Moringe Sokoine(RIP) angelikuwepo leo naona Wabunge wengi wa CCM wangelikimbia Bunge!
 
Kwani huyu waziri mkuu wa ccm,...chama cha magamba wote ukiwaliuza watatetea tu,...hao si wamezoea ulafi wa mali na madaraka,....hata ukimuuliza kiranja wao mkuu nae lao moja
 
Nilishasema huyu Mzee anajaribu kutetea kitu ambacho hakiteteeki! Kwa kusema kwamba Posho ya Wabunge huwa wakitoka tu Mlangoni wanakutana na Wapiga kura wao waliokuja kuwaomba kwa hiyo ndipo inapokwenda! Ina maana huyu Muathirika anataka kutuambia kwamba Omba Omba imekubalika kama ni Sekta rasmi ambayo Serikali ya Magamba imeikubali!

Aache Siasa aongee realities!

Hapo kwenye bluu, kumbe ndiyo maana!!!
 
Tunapiga hatua kubwa ya maendeleo kwa kurudi nyuma. Naomba tujipongeze.
Sijui ni mbunge gani wa chama changu ccm mwenye dhamira ya kweli kuona wananchi wanatoka katika umaskini.
 
Mimi naona sasa wakati umefika Chadema lazima ifanye kampeni za mlango kwa mlango kuwaelimisha wa TZ haki zao kuhusu haya manyang'au ya CCM. mie nipo radhi kuchangia hii kampeni lazima wa TZ tuamke huu ni ushenzi mtupu hatuwezi kuwa na viongozi wenye uroho wa kutafuna mali za wananchi halafu wanatetea ulaji BUNGENI
 
PM ni mtoto wa Mkulima aliyegeuka fisadi. Hivi ile mambo yake ya kumiliki Sumry imeishia wapi?
 
Jibu hili ni la kipuuzi kabisa. Huwezi kusema wanalipwa ili wagawe fedha. Fikiri mimi ni maarufu sana kijijini kwangu na nafanya kazi hapa Dodoma. Mara nyingi sana watu kutoka nyumbani wakielekea Dar, Iringa, Mbeya, Morogoro, Singida, Mwanza, Tabora hupita kwangu. Je naweza kwenda ofisini na kusema nataka mnilipe hela ya kujikimu ili niwape watu wanaopita nyumbani kwangu? Mbona huu ni ukosefu wa akili?
Waziri mkuu kutoja jibu na namna hii ni kutudharau wananchi. Sasa kwa nini wasiwape walimu, polisi, wanajeshi na madakatari hela ya kuwapa wananchi wao? Fikiri, ukiwa daktari, unajulikana na kila mtu katika kijiji chako, halafu watu hawaishi nyumbani kwako, sasa je kuwekwe sheria ya kawagawia fedha madaktari ili wawe wanawasaidia wanavijiji wao? Si hapo tu, mtu akiwa polisi, vijijini wanaona ni mtu mwenye mamlaka makubwa sana na mara nyingi wanafikia kwake na wengi wanakuwa hawana hata hela ya kula na kwa kawaida huomba nauli je na mapolisi kwa nini hatuwapi hiyo hela?
Huu ni upumbavu uliokithiri, naomba tuandamane. Mimi nipo tayari kwa lolote haiwezekani? Wakome kabisa kuchezea fedha zetu.
 
Back
Top Bottom