Bunge linapaswa kutoa tafsiri ya Mshahara ili kumtendea haki Jerry Slaa. Basic salary ndio mshahara?

Ghafla nimeanza kuona umuhimu wa Katiba mpya.

Kamati ya bunge inashindwa kuelewa tofauti ya basic salary na total salary?

Jerry alisema mshahara wa mbunge haukatwi kodi, je posho ya mafuta, posho ya kutembelea jimbo siyo sehemu ya mshahara wa bunge?

Wataalamu wa Chuo cha kodi na wale wa IFM mkuje hapa mnielimishe.
Jo hivi kwa siku unaanzisha mada ngapi?

Sent from my Infinix X692 using JamiiForums mobile app
 
Nafahamu kuwa kuna baadhi ya taasisi/mashirika ya umma ambako posho zote zimejumlishwa pamoja (consoloditated) na mshahara na hivyo hiyo jumla yote inachukuliwa kama mshahara na hivyo kukatwa kodi. Nafikiri kama wameamua ku-set precedence then taasisi zote ambazo wafanyakazi wake wanakatwa kodi kwenye posho, iwe kwenye consoloditated salary au separate posho(e.g. seating alowances za vikao), wasitishe maramoja na kama walikuwa wanakatwa kimakosa, watunga sheria ya kodi wameisha tupa tafsiri sahihi hivyo makato yote yarejeshwe kwa wote waliokatwa hapo kabla.
Tuache kujipumbaza....posho zote za wabunge zinatakiwa kukatwa kodi. Wafanyakazi kazi wote wanaolipwa posho mbali mbali kwenye mishahara yao uunganishwa na mishahara yao na kukatwa kodi. Mhe. Jerry Silaa ameonewa bure ana hoja ya msingi.
 
Ndiyo.Posho siyo mshahara
Ndio posho sio Mshahara. Lakini Posho na Mshahara ukatwa kodi kwa sababu yote ni mapato kwa mtumishi. Posho ni neno tu, hayo ni mapato kwa mtumishi kama ulivyo mshahara hivyo ni lazima posho ikatwe kodi. Mimi ni mfanyakazi kutoka private sekta...posho na mshahara vyote uunganushwa na kukatwa kodi. Mhe. Jerry Silaa ameonewa ana hoja ya msingi na ni lazima ijadiliwe na kukolewa suruhisho.
 
Hata sisi kazini kwetu tunapata si chini ya laki 3 kila mwezi kama posho ya kujikimu at the same time kukiwa na activity napata posho Kati ya 600,000 hadi 1,200,000 na hakuna kodi.

Wao Wana shughuli za kila mwezi kwenye vikao ,majimboni nk Kwa hiyo ni Halali kupata hivyo unless sheria ibadilishwe vyote viingizwe kwenye salary Ili vikatwe kodi.
Kasome sheria ya kodi na deductions kwenye mishahara ya wafanyakazi. Basi wewe na mwajiri wako mnakwepa kodi ya mapato. Sisi posho na allowances zinakatwa kodi!
 
Wabunge ni walafi ,Allowances zinakatwa kodi mfano House/Transport/Airtime zikiingizwa kwenye salary zinaliwa kodi ,hata kama umefanya Overtime zinakatwa kodi ,kwanini Allowances za wabunge hazikatwi kodi?
Haya ndio maswali alitakiwa aulizwe Tulia kwenye kipindi cha dakika 45, kajifanya kuupiga mwingi huku akijua kuwa anachoongea ni uongo na kibaya zaidi mwandishi ama kwa makusudi ama sijui kw kutojua hakuweza kumuuliza maswali ya msingi, ni kama vile alipangiwa jinsi ya kumuuliza Tulia, kibaya zaidi jamaa anamhoji Tulia kama vile mwanafunzi anaumuuliza mwalimu wake maswali, jamaa alikuwa kama hajiamini.
 
Kasome sheria ya kodi na deductions kwenye mishahara ya wafanyakazi. Basi wewe na mwajiri wako mnakwepa kodi ya mapato. Sisi posho na allowances zinakatwa kodi!
Ndio nakusikia wewe hapo,toka Niko private hadi government sijawahi katwa kodi kwenye posho unless.

Labda ww ndio umeshindwa kutafsiri sheria,ngoja waje watumishi wengine hapa watuambie kama wanakatwa kodi kwenye posho
 
Ndugai au Tulia waweke salary slips zao hadharani ili watuonyeshe mapato yao yote kwa mwezi na makato ya kodi pia kiinua mgongo cha zaidi ya milioni 300 kila miaka mitano watuonyeshe pia makato ya kodi.
Ghafla nimeanza kuona umuhimu wa Katiba mpya.

Kamati ya bunge inashindwa kuelewa tofauti ya basic salary na total salary?

Jerry alisema mshahara wa mbunge haukatwi kodi, je posho ya mafuta, posho ya kutembelea jimbo siyo sehemu ya mshahara wa bunge?

Wataalamu wa Chuo cha kodi na wale wa IFM mkuje hapa mnielimishe.
 
Ghafla nimeanza kuona umuhimu wa Katiba mpya.

Kamati ya bunge inashindwa kuelewa tofauti ya basic salary na total salary?

Jerry alisema mshahara wa mbunge haukatwi kodi, je posho ya mafuta, posho ya kutembelea jimbo siyo sehemu ya mshahara wa bunge?

Wataalamu wa Chuo cha kodi na wale wa IFM mkuje hapa mnielimishe.

Ukiona wewe umuhimu wa katiba mpya anayeita chokochoko atakuwa kaona kabla yako.

Kwa vile sasa hivi angali anadimamisha uchumi wake kwanza hizi zako haiyumkiniki ni hadithi zile zile za sungura na fisi tu.
 
Ndugai au Tulia waweke salary slips zao hadharani ili watuonyeshe mapato yao yote kwa mwezi na makato ya kodi pia kiinua mgongo cha zaidi ya milioni 300 kila miaka mitano watuonyeshe pia makato ya kodi.

Hapo ni rahisi zaidi kumtaka Sirro atuonyeshe suicide note aliyokutwa nayo huyu mwamba:

IMG_20210901_201456_008.jpg


Kuliko kwa yeyote baina ya hao kuonyesha Salary Slip zao.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Basic salary inakatwa kodi na allowances zote anazopata mtumishi zinatakiwa zikatwe kodi mfano house allowance, transport allowance overtime, fuel allowance zote zinatakiwa zilimwe. huku mtaani sisi tunakatwa hivyo why wao wasikatwe

Ni kweli kwamba kwenye sheria za kodi ambazo zinatumika zinaelekeza kutokatwa kodi posho zote zile ambazo analipwa mtumishi wa umma Kama zinalipwa kutokana na fedha za Mfuko mkuu hazina.
Ila kwa watumishi wa umma ambao wanalipwa poshoz kwa fedha ambazo hazitoki Mfuko mkuu hazina mf mashirika ya umma yanayokusanya mapato , taasisi zinazotumia fedha kutoka nje ,Hawa posho zao zote zinatakiwa kukatwa kodi kwa mujibu wa sheria ya kodi.
Basic salary kwa mujibu wa sheria inakatwa kodi, isipokuwa wale wa kima cha chini , inakatwa pia Bima ya afya, Mfuko wa hifadhi ya jamii,na mambo mengine Kama mtu akikopa kupitia mshahara.
Kwa hiyo ni hivyo sheria ya kodi inaelekeza hivyo siyo kwa wabunge tu Bali kwa watumishi wengine wote wa umma wanaolipwa posho hizo kutokana na fedha za Mfuko mkuu hazina ,kuanzia, Marais wastaafu,Rais , makamu wake, waziri mkuu, mawaziri ,manaibu waziri makatibu wakuu , ma RC na DC, watendaji mawizarani,mikoani hadI wilayani wanalipwa posho za aina mbalimbali Kama posho za kujikimu, vikao,kukaimu vyeo,usafiri, mawasiliano, nyumba, kukirimu wageni, zote hizo kwa mujibu wa sheria ya kodi hazikatwi kodi.
Hapa swali la kujiuliza ni kwa nini hao waliotunga na kupitisha vifungu hivyo walikuwa na nia gani.
Aidha nimesikia kwenye posho za wabunge kuna posho wanaolipwa hao wabunge ili wakawalipe mshahara madereva na makatibu wao,
Mishahara kwa mujibu wa sheria inatakiwa ikatwe kodi Kama imevuka threshold ya kima cha chini. Hivyo ni vyema wabunge wakaguliwe Kama kweli wana makatibu na madereva wanaowalipa mishahara kwa mujibu wa sheria zetu za kazi
Manake nawafahamu baadhi ya wabunge hawana madereva Mara nyingi tunawaona wanajiendesha wenyewe tu na Magari yao.
Jerry slaa a me trigger hoja kwa nini hao wasamehewe kodi kwenye posho na wengine wasisamehewe posho hizo hizo?
Manake nakumbuka nilialikwa Kwenye kikao flani na taasisi flani ukafika wakati wa kusaini posho , unasaini laki 3 unapewa laki mbili na nusu , ukiulizwa unaambiwa wamekata kodi, tulijuilizauliza pale tukaona isiwe shida tukawashukuru tu wale wahasibu walikuja kutulipa hizo posho, posho zenyewe tulilipwa bila kutegemea tulikuwa hatujui kama kile kikao kilikuwa na posho.
Jerry slaa kwa mtazamo wangu alikosea kwa kauli yake kwani aliiweka Kama vile kuonyesha wabunge wanakwepa kodi. Wakati exemption ipo kisheria.
ila slaa kwa mtazamo wangu pia hakustahili adhabu aliyopewa bunge linatakiwa lifanye review ya posho zote wanazolipwa watumishi wa umma na wabunge na kutoa muongozo mzuri usio na mkanganyiko
 
Hapo kilindoni si kuna lami mkuu?

Kwani zile posho na marupurupu lukuki ya wabunge, ma DC, RC, wakurugenzi, Mawaziri, Maspika na vigogo wengine nani analipa?

Vipi zile tunazopigwa bado nani analipa?

Vipi tunapokumbwa na covid 19, mahospilalini nani analipa?

Vipi hasara za kila la leo za mashirika ka ATCL?

IMG_20210824_125202_848.jpg


Kwamba mabarabara? Huo si ni upigaji mwingine tu mkuu?
 
Jerry alichemka na ni kujitaftia umaarufu, mshahara kwa sheria ya usimamizi wa bunge unakatwa kodi na upo kwenye salary slip, posho nyingine ambazo ni huduma kwa ofisi ya mbunge haikatwi direct tax mfano,mafuta, misharara ya dereva/katibu, posho ya mfuko wa jimbo etc, hizi hupita tu kwa mbunge husika ili kurahisisha usimamizi wa fedha husika, kwa mfano posho ya jimbo siku hizi mpaka baraza la madiwani linahusishwa kuhusu matumizi yake so huwezi sema ni income kwa mbunge kwani siyo salary na hana full control nayo.
Vipi kuhusu kanuni ya kutafuta kiinua mgongo cha mbunge
 
Back
Top Bottom