BUNGE LANUKA DHIDI YA GWAJIMA NA SILAA
WAKATI nchi ikisubiri kwa hamu na ghamu hatima ya tozo za mihamala ya simu, Bunge limewahukumu Wabunge Josephat Gwajima wa Kawe na Jerry Silaa wa Ukonga (wote kutoka CCM).
Hii ni kufuatia kauli za kichochezi na uongo uliovuka mawingu. Baada ya kuhojiwa na Kamati mahsusi juu ya kauli zao hatimaye wakatiwa hatiani na hivyo kusukumwa nje ya Bunge na kwamba hawatohudhuria mikutano miwili ya Bunge lakini pia watapokea nusu mishahara yao kwa kipindi chote hadi January 2022.
Akiahirisha kikao cha leo Spika Job Ndugai amesema, "sisi kama Bunge tumemaliza kazi yetu, tumenawa, sasa ni kazi ya vyombo vya usalama kufanya kazi yake". Kwa maneno mengine Ndugai atashangaa kama jua litazama kabla Gwajima na Silaa hawajaingia "behind the bars" kujibu tuhuma.
Sote tunakumbuka niliandika kuhoji kwa nini Serikali ya Rais Samia inamwogopa Askofu Gwajima? Kwamba hata Waziri Gwajima alipoagiza akamatwa IGP Simon Sirro alisubiri "kadi ya mwalimo" ndipo amkamate. Aibu!
Wabunge wameongea kwa uchungu mno kwa nini Askofu Gwajima anamdharau Rais Samia? Wabunge wanahoji ni kwa sababu Samia ni mwanamke? Nimeumia sana lakini nikafarijika kwa mnuko wa Wabunge baada ya Gwajima "kumgusa mama".
Nilisema na ninarudia, kauli ya Gwajima kwamba Serikali imehongwa na viongozi wanachanja hewa ni kashfa nzito sana katika medani ya uongozi. Gwajima alilenga kabisa kwamba Rais Samia amehongwa kuuza Watanzania. Ni wakati muhafaka kuthibitisha pasipo shaka kwamba Rais alihongwa na chanjo aliyochanja na wenzake ni maji au juisi. Asipothibitisha Gwajima atendewe haki anayostahili.
Lakini pia nilipendekeza kanisa la Gwajima lichunguzwe. Je, halitumiki kutakatisha fedha? Sijui Polisi mnanielewa! Narudia, Kanisa la Gwajima halitumiki kutakatisha fedha?
Gwajima na Silaa wamethibitika na Bunge kusema uongo na kuleta taharuki kwa nchi. Hata hivyo dhambi ya Gwajima ni zito kuliko dhambi ya Jerry ya kudai Wabunge hawakatwi Kodi kwenye mishahara yao. Amethibitishiwa kuwa hata yeye anakatwa Kodi. Jerry jitokeze hadharani kuomba radhi Watanzania walioumia kwa kauli yako!
Kwa upande mwingine CCM chini ya Daniel Chongolo hakuna busara zaidi ya kumpokonya kadi ya chama (ambayo hata hivyo najua hana) ili Jimbo la Kawe liwe wazi!
Gwajima alikuwa ni mwanachama wa Magufuli si wa Chama Cha Mapinduzi, CCM. Magufuli (chama chake) hayupo, amekufa kwa chama hicho hakipo! Basi!
#MguseMamaNinuke