Bunge linapaswa kutoa tafsiri ya Mshahara ili kumtendea haki Jerry Slaa. Basic salary ndio mshahara?

Ni kweli kwamba kwenye sheria za kodi ambazo zinatumika zinaelekeza kutokatwa kodi posho zote zile ambazo analipwa mtumishi wa umma Kama zinalipwa kutokana na fedha za Mfuko mkuu hazina.
Ila kwa watumishi wa umma ambao wanalipwa poshoz kwa fedha ambazo hazitoki Mfuko mkuu hazina mf mashirika ya umma yanayokusanya mapato , taasisi zinazotumia fedha kutoka nje ,Hawa posho zao zote zinatakiwa kukatwa kodi kwa mujibu wa sheria ya kodi.
Basic salary kwa mujibu wa sheria inakatwa kodi, isipokuwa wale wa kima cha chini , inakatwa pia Bima ya afya, Mfuko wa hifadhi ya jamii,na mambo mengine Kama mtu akikopa kupitia mshahara.
Kwa hiyo ni hivyo sheria ya kodi inaelekeza hivyo siyo kwa wabunge tu Bali kwa watumishi wengine wote wa umma wanaolipwa posho hizo kutokana na fedha za Mfuko mkuu hazina ,kuanzia, Marais wastaafu,Rais , makamu wake, waziri mkuu, mawaziri ,manaibu waziri makatibu wakuu , ma RC na DC, watendaji mawizarani,mikoani hadI wilayani wanalipwa posho za aina mbalimbali Kama posho za kujikimu, vikao,kukaimu vyeo,usafiri, mawasiliano, nyumba, kukirimu wageni, zote hizo kwa mujibu wa sheria ya kodi hazikatwi kodi.
Hapa swali la kujiuliza ni kwa nini hao waliotunga na kupitisha vifungu hivyo walikuwa na nia gani.
Aidha nimesikia kwenye posho za wabunge kuna posho wanaolipwa hao wabunge ili wakawalipe mshahara madereva na makatibu wao,
Mishahara kwa mujibu wa sheria inatakiwa ikatwe kodi Kama imevuka threshold ya kima cha chini. Hivyo ni vyema wabunge wakaguliwe Kama kweli wana makatibu na madereva wanaowalipa mishahara kwa mujibu wa sheria zetu za kazi
Manake nawafahamu baadhi ya wabunge hawana madereva Mara nyingi tunawaona wanajiendesha wenyewe tu na Magari yao.
Jerry slaa a me trigger hoja kwa nini hao wasamehewe kodi kwenye posho na wengine wasisamehewe posho hizo hizo?
Manake nakumbuka nilialikwa Kwenye kikao flani na taasisi flani ukafika wakati wa kusaini posho , unasaini laki 3 unapewa laki mbili na nusu , ukiulizwa unaambiwa wamekata kodi, tulijuilizauliza pale tukaona isiwe shida tukawashukuru tu wale wahasibu walikuja kutulipa hizo posho, posho zenyewe tulilipwa bila kutegemea tulikuwa hatujui kama kile kikao kilikuwa na posho.
Jerry slaa kwa mtazamo wangu alikosea kwa kauli yake kwani aliiweka Kama vile kuonyesha wabunge wanakwepa kodi. Wakati exemption ipo kisheria.
ila slaa kwa mtazamo wangu pia hakustahili adhabu aliyopewa bunge linatakiwa lifanye review ya posho zote wanazolipwa watumishi wa umma na wabunge na kutoa muongozo mzuri usio na mkanganyiko


Je wewe unaona hiyo sheria inatenda haki?

Je kunahaja ya mapitio au ibaki kama ilivyo? Elezea.
 
Wabunge ni walafi ,Allowances zinakatwa kodi mfano House/Transport/Airtime zikiingizwa kwenye salary zinaliwa kodi ,hata kama umefanya Overtime zinakatwa kodi ,kwanini Allowances za wabunge hazikatwi kodi?
Mkuu mi hapo kwenye kukatwa overtime pay ndo nachoka...yan nimejibania kufanya mambo yangu ili nipate hiko kidogo niongezee kwenye salary bado nacho kodi inakipitia dooh
 
Ghafla nimeanza kuona umuhimu wa Katiba mpya.

Kamati ya bunge inashindwa kuelewa tofauti ya basic salary na total salary?

Jerry alisema mshahara wa mbunge haukatwi kodi, je posho ya mafuta, posho ya kutembelea jimbo siyo sehemu ya mshahara wa bunge?

Wataalamu wa Chuo cha kodi na wale wa IFM mkuje hapa mnielimishe.
Hata TRA wanajua mshahara wako ni ile Gloss Salary...yaani unachokipata chote bila makato.

Jerry yupo sahihi.
 
Back
Top Bottom