Bunge lashtuka Madeni ya Wakandarasi na Fidia za Makazi kuzidi Tsh. Trilioni 6.37

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imesema hadi kufikia Desemba mwaka jana, Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) ulikuwa unadaiwa jumla ya Sh6.37 trilioni na watu mbalimbali za fidia na malipo ya makandarasi na wahandisi washauri wa ndani na nje ya nchi.

Kwa mujibu wa kamati hiyo, makandarasi na wahandisi washauri hadi kipindi hicho walikuwa wanadai jumla ya Sh778 bilioni, huku Sh5.59 trilioni zikiwa ni fidia inayohitajika kulipwa kwa wamiliki wa maeneo yote nchini, yanayotakiwa kupitiwa na barabara kuu na za mikoa.

Akiwasilisha bungeni jijini Dodoma leo Jumatatu Februari 5, 2024 taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu shughuli ilizozifanya kwa mwaka 2023, Mwenyekiti wa Kamati, Selemani Kakoso amesema miongoni mwa changamoto zinazoikabili Tanroads ni uchelewashaji wa ulipaji wa madeni ya makandarasi na wahandisi washauri hali iliyosababisha kuongezeka kwa gharama.

Amesema hadi Desemba mwaka 2023, miradi iliyokamilika ilikuwa 94 na makandarasi husika wanaidai Serikali Sh386.36 bilioni huku miradi ya barabara inayoendelea kujengwa ikiwa 69 yenye deni la makandarasi Sh392.6 bilioni na hivyo jumla ya deni lote kuwa Sh778.96 bilioni.

Kakoso ambaye pia ni mbunge wa Mpanda Vijijini ametahadharisha kuwa deni hilo linaweza kuongezeka kwa utaratibu wa riba katika miradi kama hatua hazitachukuliwa haraka.

“Serikali ilipe madeni ya makandarasi na waandisi washauri kwa wakati ili kuondoa ongezeko la gharama zinazosabishwa na riba,” amesema Kakoso na baadaye Bunge likapitisha azimio la kuitaka Serikali ilipe madeni hayo.

Kakoso ametaja changamoto nyingine kuwa ni kuchelewa kwa tathmini za mali na ardhi kwa ajili ya kupisha ujenzi, inayosababishwa na Sheria ya Fidia.

Amesema hadi Desemba 2023, fidia inayohitajika kwenye maeneo yote nchini kulikopita barabara kuu na za mikoa inakadiriwa kufikia Sh5.58 trilioni.

Katika eneo hilo, Bunge limeazimia kwamba “Serikali iwahi kufanya tathmini za mali na ardhi kwa ajili ya kupisha ujenzi, pia maeneo ambayo yanaonekana hayahitajiki kwa sasa yaachwe kwa wananchi ili yaendelezwe.”

Hata hivyo, akizungumzia madai ya makandarasi, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema Serikali imejiwekea utaratibu wa kupunguza madeni hayo na mwezi huu wa pili wameendelea kulipa Sh50 bilioni na kwamba takribani Sh115 bilioni ambazo zimebaki zitakuwa zimelipwa hadi kufikia Aprili mwaka huu.

Novemba 21, 2023, Waziri Bashungwa na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba walikutana na Umoja wa Makandarasi na Watoa Huduma Shirikishi (Tucasa) na kuahidi kuwalipa wale wanaozidai Tanroads na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura).

Akizungumza kwa simu jana, Makamu Mwenyekiti wa Tucasa, Yahya Mnali amesema baada ya kufuatilia madai yao, hatimaye Serikali imeshaanza kuyalipa, japokuwa wapo wachache bado hawajalipwa.

“Novemba 21, 2023 tulikutana makandarasi wote chini ya Waziri wa Ujenzi, alialikwa Waziri wa Fedha na tulizungumza kwa urefu hizo changamoto zinazotukabili na Januari 24 tulikuwa na kikao, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa, akasema kwa kuwa makandarasi wanafanya kazi kwenye miradi ya elimu na afya, madai yao yameshashughulikiwa.

“Ahadi ya mwisho ilikuwa watakamilisha ifikapo mwisho wa Februari mwaka huu,” amesema.

Hata hivyo, akizungumza Desemba 2023, Mnali alisema madai hayo yamechukua muda mrefu.

“Kwa kweli kilio chetu kikubwa ni kucheleweshewa malipo, kiasi kwamba inatudhoofisha. Wapo wanaodai zaidi ya mwaka, miaka miwili na tulielezwa katika mkutano ule kwamba Serikali imedhamiria kulipa hayo madeni hayo,” amesema.

Miongoni mwa makandarasi waliolipwa ni pamoja na Austrid Madunda aliyefanya kazi katika maeneo ya Lupembe na Ludewa mkoani Njombe kupitia (Tarura).

“Sisi tumelipwa hela zote, tulikuwa tunadai Sh206 milioni. Pia wametuambia kama tutapata kazi na tukakosa fedha, twende benki tukakope, watalipa,” amesema.

Kwa upande wake Astery Bitegeko wa kampuni ya Masheshe Investment iliyofanya kazi mkoani Morogoro, alisema alikuwa anadai Sh200 milioni na sasa zimelipwa.

Madeni ya TBA

Akizungumzia madeni ambayo Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) unadai, Kakoso amesema kwa kumtumia dalali wa Mahakama, wakala huo unaendelea na kazi ya ukusanyaji wa madeni.

Amesema taarifa zinaonyesha baada ya maazimio ya Bunge kuhusu ukusanyaji jumla ya Sh7.628 bilioni za pango katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Arusha na Katavi na deni hilo sasa limesalia Sh17.838 bilioni.

Kasi ndogo ujenzi wa minara

Kakoso alisema kamati imebaini kasi ndogo katika ujenzi wa minara nchini katika utekelezaji wa mradi ambapo mkataba uliosainiwa unaonyesha kata 713 zitajengwa minara 758.

Alisema hadi kufikia Desemba 2023, minara 15 tu sawa na asilimia 2 imejengwa, kati yake sita imekamilika na imeanza kutoa huduma za mawasiliano.

Usainishaji wa mikataba hiyo ulifanyika Mei 13 mwaka jana na ulihusisha kampuni za Airtel Tanzania, TTCL, Vodacom Tanzania, Mic Tanzania (Tigo) na Vietel (Halotel).

“Kamati inatoa maoni kuwa, kasi ya utekelezaji wa minara ni ndogo hivyo inasisitiza kuongeza nguvu zaidi ili kuwezesha vijiji vingi kupata minara,”alisema Kakoso.

Kakoso amezungumzia pia changamoto ya utapeli mtandaoni, kuwa hadi kufikia Desemba, 2023 namba za simu 8,117 zilibainika kufanya uhalifu mtandaoni na kufungiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Akichangia mjadala huo, Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Methew Kundo amesema Serikali katika kipindi cha kati ya mwaka 2021 hadi 2023 imejenga minara 1,070 yenye gharama ya Sh170.978 bilioni.

Amesema minara iliyo katika hatua za utekelezaji ni 758, kati yake 320 inatokana na fedha za ndani huku 438 ikitokana na fedha za nje.

Kuhusu changamoto ya minara kuwaka asubuhi na kuzima jioni, Kundo alisema wametoa maelekezo kwa watoa huduma kuwa kila wanapojenga minara ni lazima wawe na huduma ya internet, kuwe na vyanzo vitatu vya umeme ambavyo ni jenereta, betri na nishati ya jua.

TPA ilivyoelemewa

Akizungumzia ufanisi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Kakoso amesema kuna kasi ndogo ya ushushaji wa shehena katika Bandari ya Dar es Salaam inayosababisha msongamano mkubwa wa shehena bandarini ikiwemo meli za mafuta katika boya la SPM ambazo hutumia wastani wa zaidi ya siku 10.

“Mifumo ya Tehama isiyotosheleza, upungufu wa fedha za uendeshaji, watumishi na vitendea kazi, kutokuwepo kwa meli ya abiria katika Bahari ya Hindi itakayotoa huduma Dar es Salaam – Zanzibar – Mtwara – Comoro,” amesema.

Alitaja pia suala la TPA kushindwa kulipa vyeti vya malipo kwa mkandarasi/mshauri (vilivyoiva) kwa ajili ya mpango wa kuendeleza miundombinu ya bandari; na mamlaka hiyo kukosa udhibiti wa mapato yanayotokana na tozo za huduma ya matumizi ya gati zake.

Hata hivyo, amesema bandari za Dar es Salaam, Lindi na Mtwara zimeanza kupokea meli kubwa zaidi kutokana na kukamilika kwa miradi ya maboresho.

Akizungumzia changamoto hizo, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa ya meli na katika kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kujenga gati kubwa yenye urefu wa mita 590 katika Bandari ya Malindi, ambayo itakuwa na uwezo wa kuwekeza meli mbili kwa wakati mmoja.

Amesema pia hatua nyingine ni kujenga bandari ya kisasa wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kwa ajili ya ushushaji wa mafuta pamoja na matanki ya kuhifadhia shehena hiyo.

Amesema mradi huo unaendelea na kwamba mkandarasi amepatikana na watatumia takribani Sh560 bilioni kwa ajii ya kujenga bandari hiyo, hatua ambayo itapunguza msongamano.

Wabunge

Akichangia mjadala huo, Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu amesema eneo la meli za mafuta ni dogo kiasi cha kufanya meli kusubiri kwa muda mrefu na utatuzi wake ni lazima lijengwe eneo jingine la kuhifadhi mafuta (SRH).

Amesema kwa kufanya hivyo kutasaidia katika kuongeza kasi ya ushushaji wa mafuta na kufanya uhifadhi, hatua ambayo itapunguza gharama za nishati hiyo nchini.

Akizungumzia Tanroads, mbunge huyo aliitaka Serikali kuiongezea fedha zitakazosaidia kuboresha barabara.

"Barabara ambazo amepitishwa na Bunge zenye urefu wa kilometa 2,035, mheshimiwa mpaka leo hata moja haijaanza kujengwa na tumebakiza miezi sita bajeti hii 2023/2024 kukamilika.

Kuhusu suala hilo, Kakoso amesema, “bahati mbaya wapo watu wamewekewa alama za kupisha miradi hiyo (ya barabara) kwa zaidi ya miaka 10 wana matumaini ya kupata fidia.

“Kwa maeneo ambayo wanaona hawataweza kulipa fidia na miradi ile haitaweza kwenda kwa wakati, basi wawaruhusu wananchi waendeleze maeneo yao kuliko kuacha iendelee kuwa hivi mpaka sasa,” amesema.

Alitaka pia wizara hiyo kujipanga na kuhakikisha kuwa angalau inafikisha bajeti ya Sh5 trilioni kwa mwaka ujao wa fedha (2024/2025).

Mbunge wa Same Mashariki, Anna Malecela amesema Tanroads ina mzigo mkubwa wa barabara zilizoisha matumizi yake, ambazo zipo 71 zenye urefu wa kilometa 2,840.68 ambazo gharama ya kuzitengeneza ni Sh3.26 trilioni.

Ametoa mfano wa barabara hizo kuwa ni Dodoma-Iringa, Dodoma-Mwanza na Dar es Salaam- Mtwara ambazo zilitakiwa kutengenezwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 na 2023/2024.

MWANANCHI
 
Duu yaani kupisha ujenzi fidia ni Trilioni 6? This is very dangerous

Pia yaani watu wanadai Bil.777 plus Waziri anasema wameanza kulipa yaani bil.50,huu ni mzaha

Mwisho bila Serikali kubadili modality ya project financing Madeni yataendelea kuwa makubwa Kwa yza Riba.

Pesa za kudunduliza zinachelewesha mradi na kuzaa Riba.Kopeni pesa au wekeni bond za mda mrefu mpate pesa za kulipa.

Hapo hatujagusa wazabuni wengine,mbona ni balaa Kwa staili hii?
 
Taarifa ya habari toka bungeni leo ya naibu waziri mkuu kwa kuibiwa transformer 87 mkoa pwani maeneo kibaha taarifa inatupa ukakasi wazawa waelewa Kuna ujuma ndani shirika la tanesco. Aiwezekani kuibiwa transformer yenye umeme bila kuzima umeme na ata mwizi kuikaribia transformer lazima afe ndani one meter. Ukakasi wa taarifa na bado umeme aiwezekani kukata bila tb number watu wa emergency kibari kwajir Patro line immediately na bado umeme ukikatika muda utajukikana eneo husika kwa wananchi na pia kwa watu wa emergency kwa taarifa ya tb number kwa supervisor. Ili linatupa picha waelewa lazima kuwa na badhi ya wajiriwa sio waminifu ushirikiana na wezi. Tunaomba waziri atathimin Ilo ndani shirika la umeme kwa weledi na ujuzi kuondoa tatizo kukomesha . Rakin kuendelea kutangazwa wezi njee shirika wizi sugu utaendelea watu wa emergency wahusika ufanyike upelelezi wa kina na kituma technical information and communication skills kumtambua tanesco wezi sugu wamo wahujumu sugu badhi ya watumishi hasa emergency team ya tanesco wameshirikiana wezi kuhujumu shirika
 
CCM Hao Hao Tena Wanashtuka Nini Wakati Ni Michezo Yao Dailly
 
Kwanini wasiweke camera sehemu zote muhimu? Umeme ni buru kwao.
 
Kufanya biashara na serekali kwa sasa ni kujitakia umasikini wa wazi. Halafu Kuna muenezi anazunguka kutengeneza hadaa kuwa anatatua kero za wananchi kwa watu wa kupangwa, huku wenye matatizo halisi wakipotezewa!
 
Kwenye fidia alaumiwe Nyerere na CCM, walikuwa wapi kupanga miji mapema?
 
Back
Top Bottom