Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,814
- 11,991
Hayo yameelezwa Mkoani Mwanza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso (Mb) wakati Kamati hiyo ilipokagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa vivuko vinavyojengwa na Mkandarasi Mzawa Songoro Marine na kuridhishishwa na utekelezaji wa miradi hiyo.
Kuhusu utekelezaji wa vivuko, Kamati imesema bado kuna umuhimu wa kuongeza huduma za vivuko katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mikoa ya Mara, Geita, Mwanza na Kagera hivyo Serikali ione namna ya kusimamia utekelezaji wa miradi kwa haraka ili iweze kuhudumia wananchi wa maeneo hayo.
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiahidi Kamati kufuatilia malipo la Mkandarasi Mzawa Songoro Marine ili akamilishe ujenzi wa vivuko vipya vitano pamoja na ukarabati wa vivuko viwili.
Naye, Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Lazaro Kilahala ameeleza kuwa Wakala huo
unaendelea kusimamia ujenzi na ukarabati wa vivuko hapa nchini ili kuongeza utoaji wa huduma za usafiri kwa wananchi.
Akitoa taaarifa ya ujenzi wa vivuko, Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine, Khalid Songoro ameeleza kuwa katika Karakana ya Mwanza wanaendelea na ujenzi wa vivuko vipya vya Kisorya – Rugezi, Ijinga – Kahangala, Bwiro – Bukondo na Nyakaliro – Kome pamoja na ukarabati wa vivuko vya Mv. Nyerere na Mv. Kilombero II.