Bunge la Katiba: Nani atakuwa Spika?

Nina maana kuwa Spika akitoka Zanzibar, Naibu atoke Bara; Spika akiwa Mwanamke, Naibu awe Mwanamme; na Spika akiwa Mwislamu, Naibu awe Mkristo. Ni mambo ya kubalance kama ambavyo Rais wetu Mhe Kikwete huwa anajitahidi kutosheleza wakati anaunda baraza ya Mawaziri, jee nimesomeka???!!!
umesikika vema mdada.
 
Wadau hebu tujadili nani anafaa kuwa spika wa Bunge maalum la katiba linalotarajia kuanza hivi karibuni. Kwa mujibu wa shughuli hiyo wabunge watakapo kutana kazi ya kwanza itakuwa kuchagua spika jambo ambalo pia wanapaswa kuwa makini ili kupata mtu makini ili kuvusha shughuli hiyo salama. Hebu tujadili nani mwenye uwezo wa kukalia kiti hicho wadau.
 
ila ninacho kijua mimi katiba hii ikipita bila ya Kua na Mahakama ya Kadhi, ambayo katiba ya Kenya

Then, Time will tell.

Toba: Usishangae kwa nini watu wanapata zero darasani au DiV5 kwa Mulugo.

Mbona hii si Mada ya mleta uzi??
 
asalaam aleykum bhandugu,

Nadhan kwa baadhi ya watu nitaonekana wa ajabu na mtu asiyefuatilia mambo, lakin kiukweli sijajua mpaka leo sheria ya katiba inasema nani atakuwa speaker wa bunge la katiba.

naomba mnijuze tafadhali, kama atachaguliwa miongoni mwa wabunge, ataendelea yule wa bunge la tanzania au litajiendesha bila kiongozi!.. (the later sounds funny huh!..)

naomba kuwasilisha.
 
Watajua wenyewe, ila ninacho kijua mimi katiba hii ikipita bila ya Kua na Mahakama ya Kadhi, ambayo katiba ya Kenya nchi ambayo waislamu ni idadi ndogo ukilinganisha na Tanzania, na wana Mahakama ya Kadhi kwa mujibu wa katiba hiyo, basi hakika kwa makusudi Kama Tume ya Jaji Joseph Warioba, Joseph Butiku na John Kabudi ilivyofanya kudharau maoni ya kundi kubwa la nchi hii Waislamu, na Bunge hili nalo, litakua limeongeza Chumvi kwenye kidonda.

Then, Time will tell.

Hivi Mahakama ya Kadhi ipo kwenye Rasimu?

 
Spika wa bunge la katiba atakuwa Zitto Kabwe kama atagombea au kupendekezwa.
 
Hivi Mahakama ya Kadhi ipo kwenye Rasimu?


Kwa makusudi, Jaji Warioba, Joseph Butiku na John Kabudi wamaeamua kudharau maoni ya Waislamu walio wengi katika nchi hii kwa maslahi ambayo hakika sio yatakayo jenga amani katika nchi hii.

Anyway, Wameshaambiwa kua, Rasimu sio katiba. Hoja zinaweza kuongongezwa, kubadilishwa na kufutwa ikibidi.

Alichokifanya Mheshimiwa Rais, ni kile waswahili wanakiita, Mchawi mpe mwana alee, Ili akimuua hawezi kujificha.

Waswahili wanasema, usipo uziba ufa, utajenga ukuta.

Kwa sababu haiingii akilini kudharau maoni ya kundi kubwa kama hilo katika jamii, maoni ambayo viongozi wao wote wa kidini wameyatoa. Hebu jamani jaribuni kua rational kidogo tu hapa.
 
Sita angefaa sana, kuongoza bunge maalum la katiba kwa busara na hekima zake nyingi alizonazo. Huu mzee mie namfagilia. ktk kipindi chake cha uspika alifanya kazi nzuri saana. hana upendeleo.
 
Hii katiba nimeshaona kitakachoendelea ni katiba ya matwakwa ya CCM na wala sio matakwa ya wananchi. Hivyo wala tusipoteze muda kwani hakuna mabadiliko yoyote ya maana tutakayoyaona hata ikiwa Sitta au awe nani ili mradi anatoka CCM basi maamuzi atakayoyasimamia sio ya wananchi bali ya ccm.
 
chenge i guess! magamba lazima wamueke mtu anayejua sheria na uzoefu wa kutosha kupambana na opposition! YANA PALE NI KIBAKA LAZIMA AWE MZOEFU
 
mh sita na mzee wa vijisenti huenda wakachuana kutaka kuchaguliwa uspika habari zinadai mh sitta anaonekana kinara zaidi na anapigiwa chapuo na wengi ,bila huyu atasimamia maslahi ya wengi na kuwaambua ccm ambao hawataki serikali tatu wakti wananchi tunataka serikali tatu.
 
Back
Top Bottom