Bunge la bajeti 2011/2012 na yatokanayo

Haya yote ni matokeo ya mdomodomo wa NAPE na kimbelembele cha TRA kuhusu mshahara na posho ya Dr. Slaa.

Ninavyofahamu viongozi wakuu wote wa serikali na wabunge wanalipwa mi-posho mingi ambayo haikatwi kodi kinyume na sheria hadi jana alipohalalisha Mkulo.

Dr. Slaa alikuwa anaandaa kumulipua JK kuhusu POSHO na MARUPURUPU anayolipwa kila mwezi ambayo hayakatiwi kodi. Alikuwa bado akikamilisha kukusanya hizo data. Pia Dr. Slaa alikuwa yuko njiani pia kuwalipuwa wabunge kuhusu POSHO wanazopokea ambazo hazilipiwi kodi e.g. subsistance allowance, Sitting allowance, posho ya mafuta, posho jimbo (kwa wenye majimbo) etc.

Ili kum pre-empty Dr. Slaa, Mkulo ameona ahalalishe huo ukwepaji wa kodi kabla Dr. Slaa haja open a pandora box. Kwa wale tusiokuwa wafanyakazi wa serikali na Taasisi zake TULIE tu. Kwani sasa hivi Serikali imehalalisha watumishi wake na Taasisi zake kukwepa kulipa kodi.

Sheria za nchi hii zina macho, kama suala ni kuwapunguzia wafanyakazi makali ya maisha kwanini basi iwe kwa wafanyakazi wa serikali tu na sio wafanyakazi wote including wa private sector? BE THE JUDGE YOURSELF!
 
hii haikubaliki hata kidogo, kuleta ubaguzi wa kiasi hiki kama lengo nikupunguza makali ya maisha kwa wafayakazi sasa hawa watanzania wanaofanya kazi kwenye taasisi zisizoza serikali watakimbilia wapi?

Serikali ya CCM inajijengea chuki na watazania walio wengi ambao hawafanyi kazi serikalini na watavuna wanachokipanda kwenye uchaguzi ujao.
 
Mapendekezo ya mkulo kufanya marekebisho katika sheria ya ushuru wa bidhaa sura 147 kifungu (iii) vipengele:-

a) Vinywaji baridi kutoka shilingi 63 kwa lita hadi shilingi 69
kwa lita;

b) Bia inayotengenezwa na nafaka ya hapa nchini na ambayo

haijaoteshwa, kutoka shilingi 226 kwa lita hadi shilingi 249
kwa lita;

c) Bia nyingine zote, kutoka shilingi 382 kwa lita hadi shilingi

420 kwa lita;
96​

d) Mvinyo uliotengenezwa kwa zabibu inayozalishwa nje ya

nchi kwa kiwango kinachozidi asilimia 25, kutoka shilingi
1,223 kwa lita hadi shilingi 1,345 kwa lita;

e) Mvinyo uliotengenezwa kwa Zabibu inayozalishwa hapa

nchini kwa kiwango kinachozidi asilimia 75 utatozwa
shilingi 420 kwa lita; na

f) Vinywaji vikali, kutoka shilingi 1,812 kwa lita hadi shilingi

1,993 kwa lita.

Inaigizia serikali mapato mazuri...
 
Tafadhali naomba mwenye bajeti mbadala (ya Upinzani) aiweke humu. Napenda kusoma na kuchambua zote mbili.
 
Kodi isiyoendana na pato la mlipaji na ambaye kwa bahati mbaya hakushilikishwa wakati wa kupanga huwa hailipiki kwa urahisi. Kodi ya aina hii ni furaha kwa mtoza kodi kwani mlipa kodi hutafuta nafuu kwa njia anayoifahamu mwenyewe. Tukubali tukatae walipa kodi wetu si welevu, wao huangalia kuwa wamepata nafuu wao na si kujiuliza anaisaidiaje serikali yake kuleta maendeleo ambayo mwisho wa siku huinua kiwango cha maisha ya wateja wa huduma yake. Kwa maana rahisi kodi yake inaweza kutumika kuimarisha soko la huduma inayotolewa na mfanyabiashara huyo na kwa maana nyingine kwa serikali makini kodi mwananchi ina promote biashara yake na si vinginevyo.

Hivi nani kati yenu wanajamii katika kupambana na trafiki atasema makosa matatu ambayo ni 150,000 atalipa serikalini? kwa haraka na kwa watanzania ninaowafahamu hata watumishi wa umma na hata wateule wa Rais watakubali polisi achukue 50,000 na kama ni kosa moja watakubali polisi achukue 20,000. Nataka niwaambie kama kweli wana JF mnaipenda nchi yenu tujadili kwa kina ili tuone namna bora ya kufanya tozo la adhabu za barabarani linaenda kwenye kapu la serikali.

Najue wengi watasema adui muombee njaa lakini njaa ya serikali ni njaa yako na ni njaa yangu na ni njaa ya wote.

Si wapendi watu wa serikali hii lakini naipenda Tanzania na napenda ianze kujengwa leo hata kama ipo kwenye mikono ya wale niwachukiao bado nataka kuiona tanzania ya watanzania wenye faraja.
 
Kabisa ndugu yangu
Naona hapa walilenga kuwafurahisha polisi kwa kazi ya mauaji wanayoifanya

Mara 20000 kisa umetanua barabara na sasa sijui itakuwa 50000 na vibarabara vyetu hivi sijui itakuwaje
 
NINI mantiki ya kipato kutokutozwa kodi kwa misingi ya umelipwa na nani? Hapa ndipo ninapoona ubaguzi wa wazi sisi tukatwe kodi katika vipato vyetu ila wao walipwe bila lukatwa kodi?

je, Usemi wa "Lipa kodi kwa maendeleo yako" unatuhusu kina nani?
 
Ubaya wake nini?

ubaya ni kwamba wanaofanya kwenye mashirika binafsi tutaendelea kunyongeka kwani ndio tunaokatwa kodi kubwa. Hapa mkulo hajawa msikivu kwa wananchi wote. kama kodi inatolewa itolewe kwa raia wote wa tanzania na ibakizwe kwa wageni tu. sisi sote ni wapiga kura sasa kwa nini wasamehewe wa serikalini tu? huu ni ubaguzi ambao katiba hairuhusu.
 
93.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa matumizi, katika mwaka 2011/12 Serikali imepanga kutumia jumla ya shilingi bilioni 13,525.9 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo.

Kati ya fedha hizo, kiasi cha shilingi bilioni 8,600.3 kimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, ikijumuisha shilingi bilioni 3,270.3 kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Serikali, taasisi na wakala za Serikali na shilingi bilioni 1,910.4 kwa ajili ya Mfuko Mkuu wa Serikali. Aidha, jumla ya shilingi bilioni 4,925.6 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ambapo shilingi bilioni 1,871.5 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 3,054.1 ni fedha za nje.

 
katika thread ya "wasomi waichambua bajeti" nimeandika yafuatayo juu ya kifungu hiki:

"Kusamehe kodi ya mapato kwenye posho wanazolipwa wafanyakazi wa Serikali na wanaofanya kazi kwenye Taasisi zinazopata ruzuku kutoka kwenye bajeti ya Serikali.."

Huu ni ubaguzi wa wazi katika bajeti. Fikiria wewe ni mtumishi wa sekta isiyopata ruzuku ya serikali, unakwenda katika semina au warsha au mkutano ambao pia unahudhuriwa na watumishi wa serikali na mashirika yanayopata ruzuku ya serikali. Nyote mnalipwa posho ya Tshs 50,000 kwa siku. Wewe posho yako ihesabiwe kama sehemu ya mapato yako wakati wa kukokotoa kodi ya mapato lakini kwa hao wengine isihesabiwe hivyo! Nyote ni watanzania, mnakula chakula kile kile, mnalala sehemu ile ile. Huu si ubaguzi wa hatari?

Sina la kuongezea; ni vyema kumbe mawazo yetu yamefanana.
Ninachoomba, kila mwanaJF atafute anwani ya baruapepe ya mbunge wake ampeperushie nijadara hii. Kumbuka kla mbunge ana anwanipepe kwenye website ya bunge. Wasiposoma mijadala hii, kama wakija kwa wapiga kura tuwawajibishe kwa maswali.
 
Hapo ni kodi ya kuwatoa vitambi polisi!!! maana kimsingi hata polisi anajua huwezi kumlipisha mtu hata elfu hamsini kwa kosa la barabarani... kwahiyo kila mtu atatafuta njia nzuri ya kumalizana kimyakimya na polisi eg., kumpa elfu ishirini or else... Bajeti ya mwaka huu ni neema kwa polisi nadhani sasa wanasheherekea kwa kwenda mbele.
 
Nisichokielewa ni what value do they add katika kuongeza pato la taifa na pato la mtu mmoja mmoja mpaka wasamehewe kodi hao viongozi, no doubt kwamba hiyo pesa wanayolipwa ni kodi basi ikienda kwa mtu inakuwa kipato na inatakiwa kukatwa kodi.

Kipato chochote cha ziada kiendane na value addition sio mlundikano wa vyeo kwa watu wasio na Tija ya Taifa.

Hala hala notification isitumike kama chanzo cha mapato manake miundombinu tuliyonayo haitoshi kwa madereva kufuata sheria zote za barabarani na idara zinazohusika na miundomibinu pia zitozwe fine, kwa mfano jiji wakishindwa kuweka taa za kuongeza magari au Tanroads wasipoweka alama stahili za barabarani. Trafiki wazembe pia watozwe fine kwa kushindwa kutimiza wajibu wao. Isije kuwa tunamtwisha kila mzigo mlipa kodi na kutajirisha watumishi wazembe.
 
[FONT=BookmanOldStyle,Bold][FONT=BookmanOldStyle,Bold]
Mapato TSh milioni
A:
[/FONT]​
[/FONT]Mapato ya Ndani 6,775,952
(i) Mapato ya Kodi (TRA) 6,228,836
(ii) Mapato Yasiyo ya Kodi 547,116

[FONT=BookmanOldStyle,Bold][FONT=BookmanOldStyle,Bold]
B:
[/FONT][/FONT]Mapato ya Halmashauri 350,496

[FONT=BookmanOldStyle,Bold][FONT=BookmanOldStyle,Bold]
C:
[/FONT][/FONT]Mikopo na Misaada ya Nje 3,923,551

[FONT=BookmanOldStyle,Bold][FONT=BookmanOldStyle,Bold]
D:
[/FONT][/FONT]Mikopo ya Ndani 1,204,262

[FONT=BookmanOldStyle,Bold][FONT=BookmanOldStyle,Bold]
E:
[/FONT][/FONT]Mikopo ya Masharti ya Kibiashara 1,271,634

[FONT=BookmanOldStyle,Bold][FONT=BookmanOldStyle,Bold]
JUMLA YA MAPATO YOTE 13,525,895

F:
[/FONT][/FONT]Matumizi ya Kawaida 8,600,287
(i) Mfuko Mkuu wa Serikali 1,910,376
(ii) Mishahara 3,270,292
(iii)Matumizi Mengineyo 3,419,619
Wizara 2,727,472
Mikoa 49,981
Halmashauri 642,166

[FONT=BookmanOldStyle,Bold][FONT=BookmanOldStyle,Bold]
G:
[/FONT][/FONT]Matumizi ya Maendeleo 4,924,608
(i) Fedha za Ndani 1,871,471
(ii)Fedha za Nje 3,054,137

[FONT=BookmanOldStyle,Bold][FONT=BookmanOldStyle,Bold]
JUMLA YA MATUMIZI YOTE 13,525,895
Naomba kutoa Hoja.
[/FONT][/FONT]
 
katika thread ya "wasomi waichambua bajeti" nimeandika yafuatayo juu ya kifungu hiki:

"Kusamehe kodi ya mapato kwenye posho wanazolipwa wafanyakazi wa Serikali na wanaofanya kazi kwenye Taasisi zinazopata ruzuku kutoka kwenye bajeti ya Serikali.."

Huu ni ubaguzi wa wazi katika bajeti. Fikiria wewe ni mtumishi wa sekta isiyopata ruzuku ya serikali, unakwenda katika semina au warsha au mkutano ambao pia unahudhuriwa na watumishi wa serikali na mashirika yanayopata ruzuku ya serikali. Nyote mnalipwa posho ya Tshs 50,000 kwa siku. Wewe posho yako ihesabiwe kama sehemu ya mapato yako wakati wa kukokotoa kodi ya mapato lakini kwa hao wengine isihesabiwe hivyo! Nyote ni watanzania, mnakula chakula kile kile, mnalala sehemu ile ile. Huu si ubaguzi wa hatari?

Sina la kuongezea; ni vyema kumbe mawazo yetu yamefanana.
Ninachoomba, kila mwanaJF atafute anwani ya baruapepe ya mbunge wake ampeperushie nijadara hii. Kumbuka kla mbunge ana anwanipepe kwenye website ya bunge. Wasiposoma mijadala hii, kama wakija kwa wapiga kura tuwawajibishe kwa maswali.

Mfano wako siyo relevant kwani gharama za kusafiri kikazi hazikatwi kodi. Chukua mfano mwingine mfano wa cash transport allowance kwa ajili ya kwenda kazini na kurudi nyumbani. Aliye serikalini hatakatwa kodi lakini yule wa sekta binafsi atailipia kodi ya mapato pamoja na NSSF. Ni ubaguzi wa hali ya juu kuliko hata ule wa South Africa miaka ile
 
Mkuu umenena vizuri sana. Hili suala la kuongeza notification fine nadhani ni kutaka kuwafurahisha traffic. Hivi serikali haina watu wa kufikiri kiasi hicho? Kila siku PCCB na watu wengine wanatuambia kuwa Traffic Police ndio wanaongoza kwa rushwa hapa nchini, leo unasema unaongeza fine ya papo kwa papo hao hao ndio wakusanye hiyo fine. Nadhani sasa trafic imekuwa deal. Huko CCP Moshi itabidi watu wafanye michakato ili wakimaliza tu wapangiwe traffic na wengine ambao wako general duty kwa sasa itabidi waende bagamoyo ili wapangiwe traffic manake kuna neema huko.
 
Somo hiki kifungu cha bajeti na ufikirie kwa makini wewe mwenyewe. Ila zingatia angalau maswali ya je hiki kifungu kina maana gani? na je chanzo chake ni nini haswa?



B. Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332
77. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho ya sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332 kama ifuatavyo: -
i)Kusamehe kodi ya mapato kwenye posho wanazolipwa wafanyakazi wa Serikali na wanaofanya kazi kwenye Taasisi zinazopata ruzuku kutoka kwenye bajeti ya Serikali.

Kodi hii inypendekezwa kusamehewa ni katika posho ambazo hulipwa kwa watumishi wa kadi za juu tu, hivyo mananchi wa kawaida hatanufaika na chochote. Ni heri wanekubali mapendekezo ya TUCTA kupunguza inacome tax ambayo inamgusu kail mtumishi.
 
Ujinga mtupu wa serikali hii. kwa ujinga waliojaza vichwani wanaoshabikia kupandishwa kwa faini wanadhani hiyo ndiyo dawa ya kumaliza ajali.
How stupid watanzania are? Tumeshuhudia mara nyingi ajali zikisababishwa na madreva wazembe wakishirikiana na Polisi.
Mwema anajua jambo hili wazi na viongozi wetu wanajua jambo hili wazi. Kumshika dreva na kumuadhibu wakati wao polisi waliwapa leseni kwa magendo hawaoni ndio tatizo.
Muhimu ni kutoa onyo kwa madreva wanaotumia barabara vibaya na kama hawawezi kusikia wanyang'anywe leseni basi na mtu asiruhusiwe kupewa leseni tena. Hiyo ndiyo dawa. Sasa hapa kinachokwenda kufanyika ni kama mradi wa kuwakomoa madreva na kuwaongezea vipato matrafiki na mabosi wao. RTO atakachokuwa akifanya ni kuwatuma vijana wake nakusema leo kila mmoja atengeneze shilingi laki 5 kama faini kwa kuwa serikali haina pesa, na kwa hiyo wakikukuta tairi imepungua upepo unaambiwa nenda ukalipe 50,000 au niachie 30,000 uende. Makosa mengi yanayotozwa faini yalitakiwa watu kuonywa lakini sivyo wanavyofanya. Na mtu akipiga hesabu kwa nini akalipe 50 analipa 30 na maisha yanakwenda mbele na makosa yanaendelea kama kawaida. Kwani faini zilipopandishwa kutoka 5,000 mpaka 20,000 nia si ilikuwa hiyo hiyo? mbona ajali zaendelea kutesa? Nasema ni ujinga tu!
Ajali zitaendelea kutesa kama kawaida. We Tanzanians are stupid kwa sababu hatujifunzi kwa yaliyopita. Tunatumia akili gani sijui!
 
Tatizo kubwa lipo kwenye utekelezaji, mambo mengi ni mazuri kwa kuyasoma ila kimbembe kitajitokeza wakati wa kutekeleza kwasababu Rushwa, Kutowajibika, uzembe, ubinafsi na kutokuwa wazi kwa viongozi (wasimamizi)

Baadae nitarudi kueleza kwa undani, ndugu zangu
 
Uzoefu unaonyesha kuwa posho hizo ni pamoja na sitting allowance, house allowance, utilities allwances ambazo zimekuwa zikilipwa kwa watumishi wachache wa ngazi za juuu na kati (decision makers). hata hivyo wakati wote ambapo posho hizo idara, na taasisi za serikali zimekuwa haziwakati kodi watumishi hao kama inavyoelekezwa katika sheria ya kodi ya mwaka 2004. kimsingi uamizi utakuwa ni wa kuharalisha ukwepaji wa kodi ambao umekuwa ukifanywa kwa muda mrefu. na aina nyingine ya ufisadi

Nawapo pole sana wafanyankazi wa kazi wa ngazi ya chini kwan inaelekea watendelea kulala hoi na kuachwa mbali sana na mabosi wao
 
Back
Top Bottom