Bunge la bajeti 2011/2012 na yatokanayo

mwankuga

JF-Expert Member
Aug 30, 2010
334
120
Wakati Watanzania wengi wanasubiri kwa hamu bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 20111/2012,hali ya maisha inazidi kupanda.Hapa Dodoma wananchi wa kawaida wanaendelea kutafuta riziki zao,huku wengi wao wakiwa hawategemei jipya katika bajeti hiyo.Wananchi wengi wanasema bajeti haiwasadii kwa lolote zaidi ya kuwaumiza kwani wakubwa wamekuwa wakijijali wenyewe.Wakati hayo wakiendelea,kwa upande wa pili,serikali inategemea kusoma bajeti yake (mapato na matumizi) hapo tarehe 08/06/2011.
Pengine kinachosubiriwa ni takwimu za mapato na matumizi kwa upande wa miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida katika ofisi za umma.Bajeti hiyo imeandaliwa kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025,Mpango wa Maendeleo kwa miaka 5 ambao unaanza kwa mwaka wa fedha 2011/2012,MKUKUTA 11,Ilani ya CCM ya uchaguzi ya 2010-2015 na itazingatia vipaumbele alivyovitaja rais katika hotuba ya kufungua bunge aliyoitoa tarehe 18/11/2011.
Aidha vipaumbele vya taifa kwa miaka 5 (2010-2015) ni kama ifuatavyo;
1) ELIMU.
" Kuboresha kiwango cha elimu kwa kuhakikisha vitabu vya kufundishia vinapatikana shuleni,kujenga maabara,upatikanaji wa madawati na kuweka mazingira bora ya kujifunzia kwa walemavu.
2) Kilimo,Mifugo na Uvuvi.
" Kujenga na kukarabati miundombinu ya umwagiliaji,kuwezesha kuwepo kwa pembejeo za kilimo,mifugo na uvuvi,kuendeleza tafiti,kuwezesha sekta binafsi ili kuwekeza katika kilimo,mifugo na uvuvi na kuhakikisha masoko kwa wakulima yanakuwepo
3) Nishati.
" Kuzalisha umeme kwa uwingi kwa kutumia vyanzo mbalimbali,kuimarisha miundombinu ya kuzalisha na kusambaza umeme,kuimarisha miundombinu ya kuzalisha na kusafirishia gesi asilia.
4) Miundombinu na Usafirishaji.
Kujenga na kukarabati barabara,madaraja na vivuko,kujenga na kuimarisha majengo ya serikali,kuimarisha miundombinu ya reli,viwanja vya ndege na bandari.
5) Maendeleo ya Viwanda.
6) Afya
7) Maji
8) Ardhi,Nyumba na Makazi
9) Huduma za Afya
10) Masuala Mtambuka
Lakini suala kubwa ni kuona serikali inaweka mikakati ya kupunguza matumizi yake na kukusanya mapato hasa kwa makampuni makubwa yakiwemo ya uchimbaji wa madini ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakisamehewa kodi,na mzigo wa kodi ukimwegemea zaidi mwananchi wa kawaida.Kawa kawaida kodi kwa vinywaji kama vile bia,sigara n.k vinategemewa kupanda,kwani serikali imekuwa ikifanya hivyo kwa miaka yote.Watumishi wa umma wasitegemme jipya katika mishahara .Tusubiri tuone
 
ningefurahi kama kipaumbele cha kwanza cha serikali kingekuwa kuandaa katiba mpya na kupunguza matumizi makubwa yasiyo ya lazima ya serikali ili hako kanakoitwa ka national cake kagawiwe kwa watu wengi zaidi.
 
Tukitaka kuwa wakweli bajeti kwa mtu wa kawaida haileti hafueni yeyote, bali ni njia ya kuhalalisha ulaji wa wabunge, mawaziri na watendaji wa serikali wa ngazi ya juu; chukua mfano wa hizi posho za vikao, ukijumlisha posho za vikao wanazolipwa wabunge wakati wa vikao vya bunge na kamati zake, pamoja na zile wanazolipwa watendaji wakuu wa serikali kwa kuhudhuria vikao mbali mbali, utakuta ni karibu robo ya bajeti nzima ya matumizi ya kawaida, hata hivyo ukweli ulivyo posho hiyo ni wizi mtupu kwani vikao husika ni sehemu ya kazi zao zinazosababisha walipwe mshahara na vinafanyika wakati wa saa za kazi. Mbali na hayo, posho hiyo ni mbali na posho ya kujikimu ambayo pia uwa wanalipwa siku zote wanapokuwa kwenye vikao.
 
Awali ya yote sijaweza kuiona ratiba ya vikao vya bunge linaloanza kesho hata ITV haikuonyeshwa,lakini bajeti ambayo 2/3 ama (70%) yake=8.8tr ni kwa ajiri ya matumizi ya kawaida ina maana gani?

Hapo awali tulishaambiwa zaidi ya 45% ni mikopo ya nje,na 40-45% ya bajeti inaliwa na viongozi kuna maana gani? na kama kiasi tunachokopeshwa ndo kinaliwa na viongozi wetu na bado 70%=(2/3)ya bajeti yote ni kwa ajiri ya kula,kunywa,kutanua na kulala ni lini tutaweza kuwa na shule zenye maabara,ni lini kila zahanati itakuwa na ambulance,je,ni lini tutaweza kujenga na kununua mitambo ya kuzalisha umeme wa kutosha Tz?ni lini? ...Naikumbuka sana theory ya poverty vicious circle
 
Taarifa ya Afisa Habari wa Bunge,ni kwamba ratiba ya vikao vya bunge itatolewa leo baada ya kipindi cha maswali na majibu.Lakini umeuliza maswala ya msingi sana.Tumefika sehemu tumekuwa kama jiwe hatuwezi kubadilika.Bajeti haina msaada kabisa kwa raia wa kawaida zaidi ni manufaa kwa wakubwa.Tunahitaji msukumo mpya sasa
 
Bajeti ni upuuzi, wenye vitengo na idara zao wanafurahia sasa!

Hapa ndipo tulipofikia.Maisha bora kwa kila mtanzania ni ndoto ya mchana.Maisha bora kwa kila kigogo kwani ndio inamlenga zaidi bajeti
 
Hapa ndipo tulipofikia.Maisha bora kwa kila mtanzania ni ndoto ya mchana.Maisha bora kwa kila kigogo kwani ndio inamlenga zaidi bajeti
<br />
<br /
Wengine hela wamekula tunashindwa kwenda field kisa chuo HAKINA HELA YA MAFUTA,WALIOENDA FIELD WANAKATAZWA KUINGIA MGODINI WANAISHIA GETINI MANA KAMPUNI HAINA TAARIFA ZA FIELD ZAO,THEN HAWANA MKOPO,TUTAISHI VIP KWA UPUUZI HUU?
 
kurasa maalumu kwa ajili ya bajeti ya serikali ya tanzania 2011/2012 .yeyote mwenye mchango na yote yanayoendelea kwenye bunge hili la bajeti anakaribishwa kutujuza .tanzania itajengwa na wenyewe moyo asanteni

budget-summary.jpg

" pamoja na majibu ya kisiasa ya waziri" Mbunge wa CCM kwa naibu waziri. Ktk swali la nyongeza.
 
haya ambao mko free na mnaangalia TV tuandikieni kila wanachozungumza ili tuwe live na nyinyi kama post yenu ilivyo
 
Kuna sauti inajichanganya na vipaza sauti vya bunge kama redio hivi. imejirudia km mara 3.
 
Zungu anatoa rai kuongeza masaa ya ukaguz wa nyaraka kwa tra bandarin. hvyo wazir ana ahid kuboresha tech na masaa ya kufanya kaz wameshaonge na wakorea.
 
Mhe. Mdee, mtindo kandamizi wa makadirio mzgo wa magar badala kuangalia thaman halis ya mzigo. Je serikal inaongelea vip swala hili..
Spika anamwambia wazir km anaweza ajibu km hawez atajibu siku nyengine, wazir kakataa kulijibu, anasema ni jipya. Lilikuwa ni swala nyongeza.
 
mhe. Mdee, mtindo kandamizi wa makadirio mzgo wa magar badala kuangalia thaman halis ya mzigo. Je serikal inaongelea vip swala hili..
Spika anamwambia wazir km anaweza ajibu km hawez atajibu siku nyengine, wazir kakataa kulijibu, anasema ni jipya. Lilikuwa ni swala nyongeza.
thanks mkuu kwa update ubarikiwe
 
Eshacky
Nini maana ya swali la longeza ina maana muuliza swali hajaridhika na majibu ya waziri anataka ufafanuzi na swali la nyongeza always linakuwa jipya
Kwani si waziri angejibu tuu kuwa mchakato unaendelea kushughulikia hilo kama walivyozoea badala ya kusema swali ni jipya
 
mkuu swali la nyongeza, huulizwa baada ya swali la msingi, na swal la nyongeza linapaswa liwe na mada moja ya lile swal la msingi, na kumbuka mawazir huwa wanajiandaa na haya maswal, sasa km mbunge akauliza swal ambalo si mada moja ya swal la msing, hvyo inakuwa ngumu kwa wazir husika kutoa majibu sahih kwa kuwa hajajianda. Ni hivyo kwa uelewa wangu.
 
Mhe. Mdee, mtindo kandamizi wa makadirio mzgo wa magar badala kuangalia thaman halis ya mzigo. Je serikal inaongelea vip swala hili..
Spika anamwambia wazir km anaweza ajibu km hawez atajibu siku nyengine, wazir kakataa kulijibu, anasema ni jipya. Lilikuwa ni swala nyongeza.

Hivi huu mtindo wa Spika kumsemea Waziri utaisha lini?? ''Waziri kama unaweza jibu au kama uwezi utajibu siki nyingine'' ni hatari hasipokemewa ktk hili kwakweli.
 
Back
Top Bottom