Bunge kusitisha kurusha 'LIVE' vikao vyake!

huwezi kuwaadhibu wananchi kutokuona kinachoendelea bungeni kwa kizingizio cha wabunge kutokufuata utaratibu na kanuni za bunge na kutoa mada ambazo hazina misingi ni sawa na kusema daladala zote Dar es salaama hamna kutembea maana zinafunja sheria za barabara.Hii inaonyesha dharihi kuwa viongozi wa bunge wameshindwa kazi yake maana kuna sheria za kuwaadhibu wabunge ambao wanaenda kinyume na taratibu za bunge
 
BUNGE KUSITISHA KURUSHA VIKAO VYAKE.

Amesema kuwa ili kuleta maadili kwa baadhi ya wabunge ambao wamekuwa wanashindwa kufuata kanuni za bunge na kutumia nafasi hiyo kwa kutafuta umaarufu kwa sasa wameomba kufutwa utaratibu wa kurusha matangazo ya bunge ya moja kwa moja badala yake watarekodi ili kuondoa hoja zisizokuwa za msingi.

Ameongeza kuwa kuna idadi kubwa ya wabunge wamekuwa wakikiuka kanuni za bunge makusudi na kusababisha kuleta vurugu bungeni wakati jamii ikiendelea kutazama mabishano yasiyokuwa na hoja za msingi.

Hapo ndio mwisho wa akili za mtu mwenye PHD Kashilila mjinga na mpumbavu wa mwisho kabisa
Anaona kutokuonyesha bunge live ndio kutafanya wabunge wawe na nidhamu na kufwata kanuni???
hakuna dhabu kwa wanaovunja kanuni na kufanya makosa bungeni??

Nina mashakama Elimu na upeo wake... akapimwe kwanza akili.
 
Hiyo tasnifu ambayo dk kashilila alipatia shahada ya uzamivu iko maktaba gani hapa duniani - pengine inaweza kutupa vidokezo ni mtu wa aina gani (akili ndogo au kubwa). Hii title inaweza kuwa inatupa matarijio makubwa wakati yeye ni matope.
 
Hivi mbona enzi zile za Samuel Sitta akiwa speaker hakukuwa na madudu kama yaliyopo sasahivi huko Bungeni?? Ukijiuliza utagundua tu kuwa ni kwa vile bunge la sasa linaendeshwa kichama zaidi na kanuni zinapindishwa ili kuilinda serikali.Sidhani kama kuna mbunge yeyote anayetafuta umaarufu ila upindishwaji wa kanuni za bunge na uendeshwaji mbovu ndo umepelekea vurugu zilizojitokeza hivi karibuni.Tatizo hapa sio kuonekana live ktk media ila ni namna ya kuliendesha kiusawa pasipo kuelemea upande wowote ule.Heshima ya bunge itarudi tu endapo litaendeshwa ktk misingi ya vyama vyingi na kudemokrasia sio kwa kuzuia media kurusha live matangazo ya session za bunge.Tusiwe wavivu wa kufukiria na wepesi wa kufanya maamuzi mabavo kama haya,uhuru wa vyombo vya habari hapa nadhani utakuwa umeingiliwa na nasubiri kusikia wanahabari watachukua hatua gani juu ya hili.
 
na Janet Josiah na Josephat Isango

amka2.gif
SIKU chache baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai, kulalamikiwa kwa kuendesha Bunge kinyume cha kanuni, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, amewatetea huku akiwatwisha lawama hizo baadhi ya wabunge.
Kutokana na kadhia hiyo ya kukosolewa, Dk. Kashililah alisema kuwa Bunge linaandaa utaratibu wa kusitisha vikao vya Bunge kurushwa moja kwa moja (live) ili kuzuia purukushani za wabunge kuonekana kwa wananchi.
Akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari katika Ofisi za Bunge jana kuhusu shughuli zilizotekelezwa katika Mkutano wa Kumi wa Bunge na mapendekezo ya kuundwa kwa kamati mpya, Dk. Kashililah alisema vurugu zilizojitokeza zilitokana na kutofuatwa kwa kanuni ambazo zipo wazi.
Alisema vurugu zinazotokea ni kutokana na baadhi ya wabunge kutozifahamu vema kanuni au kufanya makusudi, hasa kanuni ya 60 na 68, ambazo kama zingefuatwa hayo yote yasingetokea.
Dk. Kashililah alisema baadhi ya wabunge walikuwa wakishindwa kufuata kanuni kwa makusudi kwa kutumia kifungu kimoja tu cha 68 cha kuomba taarifa, utaratibu au mwongozo bila ya kufuata taratibu zinavyotakiwa badala ya kuombea kanuni iliyovunjwa kwanza ndipo aseme yake.
"Mfano, mbunge anajua kuwa anatakiwa kutumia kanuni ya 68 kuomba taarifa, utaratibu au mwongozo, atasimama, baada ya kusimama ataambiwa na Spika aseme, naye atasema amesimama kwa kanuni ipi na anachoombea taarifa ni nini. Lakini baadhi yao wakiomba tu utaona kabla ya kuruhusiwa hapohapo wanaanza kuzungumza," alisema.
Aliongeza kuwa hali hiyo ya kuzijua kanuni na kutozifuata ndiyo inasababisha kuwapo kwa vurugu hizo ambazo wakati mwingine kwa kutumia kanuni hizo hizo zinamtaka Spika ama aliyekalia kiti chake kuahirisha Bunge.
Dk. Kashililah alisema wanaamua kutoonesha vikao vya Bunge moja kwa moja kutokana na baadhi ya wabunge kukiuka kanuni, kwa kuzungumza mambo yasiyofaa ili waonwe na wapiga kura wao.
"Bunge ni sehemu ya siasa, na mule ndani zimo pande mbili zinazovutana na kwa wale wabunge waopenda kamera ya televisheni utawaona wanazungumza mambo yasiyofaa hadi mishipa inawasisima ili waonwe na wapiga kura wao, mkitoka na kuwauliza watakwambia ni siasa ile.
"Kina mama ambao wanajua kuwa siku hiyo watauliza maswali utawaona siku hiyo wanavalia kikweli kweli ili waonekane…kwa kweli sisi tunaokaa tunaona mambo mengi na mengine yanasikitisha," alisema.
Alisema walipoomba kuzima, baadhi yao walitoa onyo kwamba waache, ila Bunge linajipanga kufanya utaratibu wa kukaa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kuliwezesha Shirika la Utangazaji la Taifa na televisheni nyingine namna ya kurusha shughuli za Bunge.
"Tunataka kukaa na TCRA, TBC na televisheni nyingine pamoja na waandishi wa magazeti kuangalia namna ya kuweka maadili ya kazi, kwa sababu hata TBC wakati mwingine hawafuati maadili, wanampiga picha Spika Makinda akiwa ameinama huku ikionekana amelala," alisema.
LHRC yanena
Nacho Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesema kuwa utendaji wa Spika wa Bunge kwa ujumla umekuwa na mivutano yenye upendeleo wa vyama katika kujadili na kuchangia hoja.
Kwamba Spika na naibu wake na wenyeviti wamekuwa wakitumia vibaya kanuni za Bunge kuwadhibiti wabunge kulingana na vyama vyao. Ni ukiukwaji wa kanuni na matumizi mabaya ya muda ambayo yanaendelea kuliathiri Bunge.
"Baadhi ya wabunge wamekuwa na matumizi ya lugha zisizostahili hata kushambuliana wao binafsi, huku wengine wakitumia nafasi zao kupingana na wananchi na kulidhalilisha Bunge mbele ya jamii," ilisema tathmini hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wake, Dk. Hellen Kijo-Bisimba.
Alisema kuwa wamebaini upungufu kwenye uongozi na utendaji wa Bunge, yaani Spika, naibu wake na wenyeviti, huku kanuni za Bunge na usimamizi wa mijadala wa kiti ukitumika vibaya.
Wanaharakati hao walisema kuwa Naibu Spika alitumia vibaya kanuni ya 58 iliyosababisha hoja ya John Mnyika kuondolewa kinyume cha kanuni husika, hali iliyosababisha kutoheshimiana, matumizi ya lugha zisizo za staha wala rasmi na kejeli za hapa na pale.

source: tanzaniadaima
 
BUNGE KUSITISHA KURUSHA VIKAO VYAKE.

BUNGE linatarajia kufuta utaratibu wa kurusha matangazo ya moja kwamoja kupitia televisheni kwa madai ya kukomesha vitendo vya baadhi ya wabunge kukiuka kanuni za bunge na kuleta vurugu kwa kutafuta umaarufu bila kujua kwamba tabia hiyo inaleta picha mbaya katika jamii.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Bunge Dk.Thomas Kashilila jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya mapendekezo ya kuanzisha kamati ya bajeti na kuvunjwa kwa baadhi ya kamati za bunge.

Amesema kuwa ili kuleta maadili kwa baadhi ya wabunge ambao wamekuwa wanashindwa kufuata kanuni za bunge na kutumia nafasi hiyo kwa kutafuta umaarufu kwa sasa wameomba kufutwa utaratibu wa kurusha matangazo ya bunge ya moja kwa moja badala yake watarekodi ili kuondoa hoja zisizokuwa za msingi.

Ameongeza kuwa kuna idadi kubwa ya wabunge wamekuwa wakikiuka kanuni za bunge makusudi na kusababisha kuleta vurugu bungeni wakati jamii ikiendelea kutazama mabishano yasiyokuwa na hoja za msingi.

Dk Kashilila amesema kuwa kwa sasa kuna baadhi ya kamati za bunge ambazo zimevunjwa kutokana na baadhi ya kamati hizo kuingilia katika utendaji jambo ambalo limekuwa likipoteza maana ya kamati hizo.

Hivi karibuni baadhi ya kamati ikiwemo ile ya Mashirika ya umma POAC zimefutwa na kuacha maswali mengi kwa baadhi ya wananchi juu ya hatua hiyo.


Ina maana hakuna sheria za kudeal na hao wabunge? Hilo linaonyesha udhaifu tu wa bunge!
 
Nadhani nidhamu ya wabunge itashuka zaidi kwa kuwa hawatakuwa na woga wakijua hawatazamwi moja kwa moja na wananchi. Ni mtazamo wa akili ndogo kudhani kuwa kutoonekana live kutawafanya wabunge kutovunja kanuni kwani kufanya hivyo kutawafanya hata wale walokuwa waoga kutoa lugha chafu wafanye hivyo. Ni sawa na usiku na mchana. Utamuona mtu mstaarabu sana mchana lakini awapo gizani utajiuliza mara kadhaa iwapo ni yule yule au mwingine
 
Kutokana namtizamo waofisi yabunge kutotaka kutangaza tena kipindi chabunge mojakwamoja toka bungeni dodoma nabadala yake kiwe kikirekodiwa nakueditiwa ndio kirushwe..naonahamna kipindi kingine kilichobaki TBC chenye mvuto wenye ukweli hivyo kufanya kupunguza idadi yawatazamaji nikiwemo namimi.Naomba kuwasilisha.........
 
This is silly!! Kama kanuni zipo na zinavunjwa, kwa nini wahusika wasichukuliwe hatua kwa mujibu wa taratibu za uendeshaji wa bunge badala ya kuwaadhibu wananchi kwa kuwanyima haki ya kujua nini kinaendelea bungeni kwa wakati huo (live dialogue) kwa maendeleo ya wananchi wenyewe. Ama ukubwa wa pua si wingi wa makamasi. Magamba walidhani kuwa wengi bungeni watakuwa na hoja za maana kumbe wengi wao ni Low Thinkers!!, Chezea CDM!!

Sababu eti wabunge wanafanya sifa ili waonekane kwa wapiga kura, hiyo ndo sababu ya kufuta utaratibu wa kuonesha bunge live!
 
Kutokana namtizamo waofisi yabunge kutotaka kutangaza tena kipindi chabunge mojakwamoja toka bungeni dodoma nabadala yake kiwe kikirekodiwa nakueditiwa ndio kirushwe..naonahamna kipindi kingine kilichobaki TBC chenye mvuto wenye ukweli hivyo kufanya kupunguza idadi yawatazamaji nikiwemo namimi.Naomba kuwasilisha.........

Magezeti yatapanda bei maana ndo yatakuwa yanasema ukweli, hasa Gazeti la Tanzania Daima!
 
Only in tanzania,
kwa hio bora tupate uchambuzi biased wa hawa waandishi wetu? Tufanye judgement kwa kutumia judgements za watu?
Mie nilidhani ni rahisi zaidi kuwaadhibu waandishi wanaokiuka maadili ya kazi kwa kupiga picha zisizotakiwa?
Anyway tutaona, manake theres nothing zaidi ya kusema hatupendi tunachoweza kufanya. Offcouse wataamua wanachotaka.
 
Ina maana hakuna sheria za kudeal na hao wabunge? Hilo linaonyesha udhaifu tu wa bunge!

Hapa ni kuwakomoa wananchi ambao ni wapenzi wa hoja mujarabu za CHADEMA, kutokuonesha live bunge kunazuiaje wabunge kuvunja kanuni? kwanza ni kuwadhalilisha wabunge kuwaambia wanaongea kwenye bunge ili waonekana kwenye tv na wapiga kura wao!
 
Hii kiboko!!!! Hansard siri na sasa wanarudi katika ujima aw Bunge kijifungia na kukaa kama kamati!!!!! This must be resisted....
 
Kumbe wabunge sio wawakilishi wa wananchi kwamba wanayojadili ama vitendo vyao hatupaswi kuviona ama kuvisikia live...

Only in Tanzania!
 
weee kuku kweli, weka namba yako nikutukane kama unanipata.... mfano line imeshajiliwa shinyanga, ameishi mbeya na sasa yupo dar es salaam. kinondoni, kijitonyama, kwa arimaua kisiwani utampata mtu huyu.....

Weka hapa no ya kashilila uone adabu, kwa spika na naibu nimetupia tano tano.
Number yake hiyo hapo 911,haya tukana sasa?
 
Namnukuu naibu spika.

Alisema hivi wala sitohairosha bunge ili watu waone uoza huu wa chama cha upinzani unaofanywa ndani ya bunge, maneno haya aliyaongea ilipozuka zomeazomea upande wa upinzani. Je naibu spika kama nyinyi mnataka kutunyima kuuona uoza huu wa kambi ya upinzani itakuaje? Au zomezomea ile unataka kutumbia imeliumbua bunge, spika na naibu wake na sio wapinzani?

Na Je kutolionyesha bunge ndio utawafanya wapinzani wasiongee tena chochote bungeni?
 
Kumekuwa na taarifa za lengo la kusudio la kutoonyesha bunge live,yaani litarekodiwa kisha kuhaririwa na kisha kurushwa.SABABU kudhibit vurugu na wabunge wanaotaka cheap popularity.HIV NI NAN MWENYE JUKUMU HILO NI WANCHI WALIOMUTUMA AU WABUNGE WENZIE,KAZI YA MWANASIASA YEYOTE NI KUTAFUTA CHEAP POPURALITY,TUTAJUAJE MBUNGE WETU ANAPELEKA TULIYOMTUMA AU ANALALA ?SISI WANANCH NDIO MAJAJI WA WABUNGE WETU SI WAO NA TBC.HILI NI BUNGE DHAIFU LINALOONGOZWA NA VIONGOZ DHAIFU.
 
kutoönyeshwa bunge ni kwa faida ya ccm, maana kila kukicha wanazidi kudhoofu, hadi kufiki hatua Juliana mwanasiasa wa mitandaoni kupokelewa na raisi ujue hali ni mbaya sana.!
 
Umetaja sana CCM kama hili ni tatizo linalohusu jando la CCM pekee.

Kwa faid ya taifa.

Wewe CAHDEMA?

Asante sana kwa maneno yako yakinifu.

Mkuu Kiranga ningetaja vipi NCCR-Mageuzi, ama CUF ama CHADEMA ilhali naijadili CCM?
 
Back
Top Bottom