Bunge kusitisha kurusha 'LIVE' vikao vyake!

This is silly!! Kama kanuni zipo na zinavunjwa, kwa nini wahusika wasichukuliwe hatua kwa mujibu wa taratibu za uendeshaji wa bunge badala ya kuwaadhibu wananchi kwa kuwanyima haki ya kujua nini kinaendelea bungeni kwa wakati huo (live dialogue) kwa maendeleo ya wananchi wenyewe. Ama ukubwa wa pua si wingi wa makamasi. Magamba walidhani kuwa wengi bungeni watakuwa na hoja za maana kumbe wengi wao ni Low Thinkers!!, Chezea CDM!!

ccm wanatakiwa waelewe tatizo haliwezi kutatuliwa kwa kuunda tatizo lingine,watafute namna nyingine ya kukabiliana wao kwa wao lakini haki ya sisi wananchi wa kawaida kujua kinachoendelea ktk bunge letu lililokosa utukufu ibaki pale pale na sio kutuchagulia hichi tukifahamu hichi tusikifahamu hilo halikubaliki kwasababu huko ni kuvunja uhuru wa vyombo nchini.
 
Kama hayo ni Kweli nitahamasisha wa Tz kususia kulipa kodi mpaka bunge live itakaporudishwa ...hatuwezi kulipa kodi halafu tukose haki yetu ya Kuona live wabi he wetu wakituwakilisha
 
unaongelea uhuni gani,? Wa makinda kuminya kanuni za bunge, au wa Ndugai kunywa viroba kabla ya kuingia bungeni au wa Kigwangala kuleta hoja ya kutongozea kura 2015.?

na wewe ni great thinker? Bila shaka yoyote wewe ni great sinker.
 
Hi CHADEMA, ama mdau yeyote mwenye namba za simu (Airtel, Tigo, Voda, Zantel, TTcl) za katibu wa Bunge Ndg Thomas Kashilila atumwagie hapa kwenye jamvi tumpatie ujumbe kuwa ajenda yake hiyo haifai. Mwenye namba zake tafadhali atuwekee hapa, ndo dawa yao.

namba yake Katibu wa Bunge hii hapa 0754 997 645 Dr. Kashillilah TD.
 
Ni uamuzi mgumu lakini pia ni tabia mbaya na ya kitoto kufanya fujo bungeni
Kemea spika anaeshindwa kufuata kanuni za bunge...haki haiombwi inadaiwa, na anaedai haki siku zote anaonekana anasababisha fujo...chadema kazi yake ni pamoja na kuokoa mburura kama wewe.!
 
kweli kwa hali kama hii kuna haja gani ya kuwa mwanaccm? halafu mfute vpndi live kwa faida ya nani? kamwe haitawezekana na mkitaka msiishi kwa amani majumbani kwenu na maofisini kwenu pitisheni hii hoja halafu tusione live bunge mtaipata fresh.... serikali isyowajali wananchi..pumbavu zenu.
 
Sasa tatizo ni kuvunja kanuni au hayo matangazo ya TV? Je, kwa kusitisha matangazo kanuni zitaacha kuvunjwa? hivi kama mbwa wakao ana tabia ya kuwabwekea wageni wako utawaambia wageni wakome kukutembelea au utamfungia mbwa? Hivi nchi inaendeshwa na mtu mmoja au na matakwa ya watu. je watu walishatoa maoni kuwa hawtaki kukiona kipindi hicho? acha tuone laivu tupime mbivu na mbichi hatutaki ucahaakachuaji.
 
Ccm ni kama kamati ya TFF tu,wanakuwa na maamuzi ya kipumbavu,awaangalii mbele ni kukurupuka tu!.
 
Wapitishe tu hilo azimio halafu na wananchi tutapitisha maazimio yetu tuone nani mwenye serikali sasa. hawa jamaa nchi imehamia digital broadcasting wao wanang'ang'ania analog tu, sijui wamelogwa au ndo wenge la chadema linawasumbua. yaani safari hii wataumbuka maana hapo ndo watashuhudia maandamano mwanzo mwisho ya kudai haki ya kuona bunge na kuwakataa viongozi wa bunge. Let them try us and they will hear us
 
Hapo ndipo ccm wanapojimaliza kabisa.tutawaomba wana Jf ambao wapo dod oma kufatilia vikao wawe wanatujuza kila kinachoendea bungeni.ianzishwe ukurasa wa JF BUNGENI LIVE.
 
Uamuzi huu ukitekelezwa utazaa mambo magumu sana katika fani ya uandishi wa habari. Maana hata magazeti yataanza kuambiwa yasiandike yanayotokea bungeni. Mengi yatafungwa nk. Huenda Bungeni waandishi wasiruhusiwe kuhudhuria. Hiyo itakuwa hatua ya kurudi tulikotoka?

Huo umaarufu ni wao wenyewe wanawapa. Na hata wakizuia kutangazwa habari zitawafikia wananchi tena watafanya wabunge hao hao sasa waanze kuuza michango yao wanayotoa bungeni. Ni kiasi cha kuichapisha na kuwauzia wananchi wajisomee. Huu utakuwa upuuzi tani moja. Nausubiri upitishwe.
Nadhani walishindwa kukubali kuwa wameona wanadhalilika wakasingizia umaarufu.
 
Katika kile kinachodaiwa ni hali ya kushangaza katibu wa bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania ametangaza rasmi kusitishwa kwa matangazo live kutoka bungeni mjini Dodoma kwa madai kuwa kuna baadhi ya wabunge wanatafuta umaarufu kupitita bunge? Sasa wanafanya hivo ili kuwakomesha, huoni hapo haki ya msingi inapokonywa bila kujua ?
 
Pumba zitapungua.

unajua kama una akili timamu huwezi shabikia eti bunge lisionyeshwe live. sasa hv tu bunge linaonyesha live lkn kwenye taarifa ya habari vitu vinahaririwa sana na tena kuwapiga mkwara baadhi ya taarifa zisirushwe je itakapopita hii hoja si ndio itazidi. kuna vitu vingine tusitie siasa sana. amkeni usingizini jaman nyie magamba.
 
Sasa wakirusha kwa njia ya redio wananchi hawasikilizi? Watu wazima lakini wanafikiri kwa kutumia Ma ka li-o. Ni bora waache kabisa kurusha matangazo kwa redio au Bunge lisiwepo kabisa.
 
Back
Top Bottom