BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,454
- 8,288
Akio Toyoda ni mjukuu wa muanzilishi wa Toyota - Kiichiro Toyoda. Akio amekuwa President na CEO tangu mwaka 2009 hivyo amekuwa kiongozi mkuu wa kampuni hiyo kwa miaka 14.
Akio alikuwa Man of Year wa mwaka 2012 katika teknolojia ya magari baada ya kuleta mageuzi makubwa katika kampuni ya Toyota; katika usimamizi, uzalishaji wa model za aina nyingi, marketing na usimamizi wa models nyingi ambazo zilitoka. Changamoto yake alikuwa sio mpenzi wa magari ya umeme.
CEO mpya wa Toyota tayari ametangazwa, ni Koji Sato ambaye kabla alikuwa msimamizi wa magari ya Lexus. Koji alikuwa ni mstari wa mbele kwa viongozi na wasimamizi wa Toyota ambao wamepambana katika kukuza teknolojia ya magari ya umeme ya Toyota.
CEO mpya wa Toyota anafahamika kwa kusimamia Lexus kuwa na model za umeme na kuhamasisha Toyota kuwekeza katika teknolojia ya magari ya umeme. Ni msimamizi wa ubunifu wa hydrogen engine za Toyota na Fuel Cell technology za Lexus.
Hatua za Akio Toyoda kuachia nafasi yake kama President wa Toyota; zimeonekana ni hatua mpya ya Toyota kuongeza speed ya kuhamia katika magari ya mfumo wa umeme.