Bodi ya mikopo imepata wapi mamlaka haya?

malimwengu

Member
Aug 29, 2011
21
12
Hivi karibuni Bodi ya Mikopo ya wanafunzi (HESLB) imetoa majina ya wadaiwa sugu ambao hawajaanza kukatwa kile kinachoitwa 'mikopo yao' kwa mujibu wa sheria ya bodi ya mikopo kifungu cha 9 ya mwaka 2004. Wanaodaiwa wengi ni wale waliomaliza chuo kati ya mwaka 1994 mpaka 2005.

Katika majina bodi ambayo imeyatoa kuna majina ya watu ambao wao walipata ufadhili wa serikali, wapo waliopata ufadhili wa mashirika tofauti mfano ule wa mpango maalum wa wanawake ambao hawajafikia kiwango kwa wakati ule ambao waliitwa pre entry.

Kipindi hicho waliofaulu tu nfio walipewa scholarship na serikali na waliitwa Government sponsored students an wengi walipata division one na two tu.

Sasa leo iweje watu ambao hawakukopeshwa na bodi majina yao yatoke kama wadaiwa? Huu ni udhalilishaji ambao kama kuna baadhi ya watu wataamua kwenda mahakamani kudai fidia, serikali itaingia hasara kubwa kuliko ile ya richmond. Hatua za haraka zichukuliwe kabla hili halijawa janga la kitaifa. wanasheria tunaomba msaada wenu katika hili tuweze kuepuka hasara hii
 
Mie itakuwa ngumu kulipa..........kila mwezi nakatwa kodi ya Tsh 105,000/= inalipwa na serikali inachukua fedha hii...manaidai tena nini?
 
Mie itakuwa ngumu kulipa..........kila mwezi nakatwa kodi ya Tsh 105,000/= inalipwa na serikali inachukua fedha hii...manaidai tena nini?

Nimekatwa kodi zaidi ya miaka 5(direct kutoka mshaara),je haijatosha hiyo fedha nilizokopeshwa? Mbona matonya alipi kodi au kisa ni ombaomba? Je hawauoni mie nimetoa mchango mkubwa sana hapa tz? Laki 2 na 20 kwa mwezi kwa miaka mi3 na laki 3 na 30 kwa miaka miwili,haijatosha hyo fedha? Piga jumla yake zen wakate hela yao hiyo 1.2m kwa miaka mi4,chenji wanidumbukizie akount yangu ya mlimani 010408........
 
Hivi karibuni Bodi ya Mikopo ya wanafunzi (HESLB) imetoa majina ya wadaiwa sugu ambao hawajaanza kukatwa kile kinachoitwa 'mikopo yao' kwa mujibu wa sheria ya bodi ya mikopo kifungu cha 9 ya mwaka 2004. Wanaodaiwa wengi ni wale waliomaliza chuo kati ya mwaka 1994 mpaka 2005.

Katika majina bodi ambayo imeyatoa kuna majina ya watu ambao wao walipata ufadhili wa serikali, wapo waliopata ufadhili wa mashirika tofauti mfano ule wa mpango maalum wa wanawake ambao hawajafikia kiwango kwa wakati ule ambao waliitwa pre entry.

Kipindi hicho waliofaulu tu nfio walipewa scholarship na serikali na waliitwa Government sponsored students an wengi walipata division one na two tu.

Sasa leo iweje watu ambao hawakukopeshwa na bodi majina yao yatoke kama wadaiwa? Huu ni udhalilishaji ambao kama kuna baadhi ya watu wataamua kwenda mahakamani kudai fidia, serikali itaingia hasara kubwa kuliko ile ya richmond. Hatua za haraka zichukuliwe kabla hili halijawa janga la kitaifa. wanasheria tunaomba msaada wenu katika hili tuweze kuepuka hasara hii

Siyo hivyo tu wengine tumeishamaliza mikopo na wengine waliishafariki dunia miaka mingi na wengine walifeli mwaka wa kwanza ,wa pili na pia wa tatu sasa hawa watalipaje mkopo huo?
 
Mimi niligraduate 1995. Lakini sikujua kama nadaiwa mpaka jina langu lilipokuwa published mwaka juzi!!! Sdhani kama kuna mtu aliyemaliza miaka ile ambaye alikuwa anajua kuwa anakopeshwa. Tulichokijua then it was cost sharing!!
 
Sheria yao ilianisha kabisa kuwa itawakata hata wale ambao walipata sponsorshi (sio mkopo) ambao ni kwenye miaka ya 1994 hadi 1997 hivi... Ndio maana kipindi kile tuliigomea sana hii kitu lakini tulionekana "mabwege" sasa ndio inakula kwetu!!
 
kama mbwai mbwai sasa kodi yangu wanayonikata inanisaidia wapi? Barabara nakatwa TLB na kwenye mafuta nalambwa % flan,hospital dawa nanunua,umeme maji nalipia,sasa serikali inanisaidia wapi? Kama vp na mie nakusanya salary slip zangu zote tangia 2007 nawapelekea TRA wanilipe fedha walizokata kama PAYE,nikalipie bodi chenji ninunue hekari mbili lugwadu niendeleze kilimo kwanza,waache upumbavu wao hao bodi,kama wanataka hela waanze za epa,madini,wanyama kwenye vitalu,wizi kwenye wizara,warudishe nyumba zote!
 
Mwenyewe nimemaliza 2008, nimejifungulia duka langu dogo sasa sijui watanipata wapi. Walipitisha sheria kwamba, wanafunzi wote waliodhaminiwa na serikali kuanzia nadhani mwaka 1984 warudishe pesa walizopewa. Tangu lini sheria ikatungwa leo ikatumika kudhibiti mambo ya nyuma?. Hakuna mtu atakayehukumiwa kwa sheria ambayo haikuwepo.
 
Ndugu wana JF.
Mimi ni mhitimu wa UDSM mwaka 2006, na kwa bahati nzuri nimeajiriwa katika chuo kikuu kimojawapo cha serikali hapa nchini. Kuanzia mwaka 2008 tulianza kukatwa madeni ya HESLB na mpaka sasa ninavyozungumza nimebakiza kama 500,000 tuu nimalize deni langu. Hivi majuzi rafiki yangu mmoja aliniambia kuwa ameshangaa kukuta kwenye website ya loan board kukuta jina lake kama mdaiwa sugu ambaye hajaanza kulipa wakati amebakiza hela kidogoo sana kumalizia deni lake (kama laki 3 hivi), na anakatwa kila mwezi kwenye mshahara wake.

Leo na mimi nikajawa na curiosity kutaka kujua kama na jina langu limo, na kweli nikalikuta nimo kwenye list ya wadaiwa sugu wa HESLB. Je, hii naashiria nini jamani? Nahisi harufu ya ufisadi!!!! Au ni uzembe wa loanboard kutokuupdate information zake kwenye website? Au mwajiri wangu ananikata hela lakini hapeleki loanboard? Sielewi bandugu. Ngoja niendelee kutunza salary slip zangu.
 
hv hawa jamaa wamekupa ajira mpaka wadai hela yao................ me kusoma nimesoma ila ajira sina mpaka sasa so me ntawalipa nn.........?
 
Back
Top Bottom