JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,462
UFAFANUZI WA BODI YA MIKOPO: MKOPO UNATEGEMEA NA UHITAJI WA MUOMBAJI KWA ALIVYOOMBA
Mkuu wa Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania (HESLB), Omega Ngole anafafanua:
“Upangaji wa viwango vya mikopo kwa Wanafunzi wanufaika unatokana na uhitaji wa muombaji kulingana na nyaraka alizowasilisha HESLB wakati wa maombi yake, mfano muombaji akisema ana ulemavu, yatima, historia yake kimasomo n.k inaweza kuchangia kiwango anachotakiwa kukipata.
“Hali hiyo inafanya viwango vitofautiane, kuna makundi yanayopewa kipaumbele mfano yatima, wenye ulemavu au waliofanya vizuri zaidi katika mitihani n.k
"Hao wanaolalamika wanatakiwa kujua kiwango cha mkopo kinatokana na nyaraka zao wenyewe.
"Kiwango cha mkopo hakiwezi kulingana kwa kila Mwanafunzi na ndio maana kila mmoja anaingiziwa fedha kwenye akaunti yake binafsi, hilo ni suala la mtu mmoja mmoja kulingana na mahitaji na ndio maana wapo ambao wamepata mkopo kwa kiwango cha 100%."
Pia soma:
-TAHLISO wanapaswa kusimama na kupigania haki za Wanafunzi kuhusu Mikopo
- Matokeo ya mikopo ya elimu ya juu 2023/2024 na changamoto zake