Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 515
- 2,875
Taarifa kwa wanafunzi 238 wa Samia Scholarship 2022/2023 ambao wamepata chini ya GPA ya 3.8.
Leo tar.2/Novemba /2023 niliandika taarifa ya kwamba wanafunzi 238 kati ya 640 ambao wana ufadhili wa Samia Scholarship ambao wamepata chini ya GPA ya 3.8 na hivyo kuambiwa wameondolewa kwenye ufadhili na kuzuiwa hata kufanya usajili vyuoni.
Taarifa ya awali hii hapa - Wanafunzi 238 wa ufadhili wa Samia Scholarship 2022/2023 hawajui hatma yao
Waziri wa Elimu Prof.Mkenda @professoradolfmkenda aliona taarifa niliyoandika na akafuatilia kujua tatizo lipo wapi ,ameahidi ya kwamba wanafunzi wote ambao wamepata chini ya GPA ya 3.8 wataendelea na masomo na usajili watafanya na fedha wataendelea kulipiwa kama kawaida ila tuu kama mkopo ambao wataulipa na sio kama ufadhili 100% tena sababu wameshindwa kufikisha GPA ya 3.8 kama inavyotakiwa. Na ameahidi taarifa rasmi itatolewa na Wizara ya Elimu muda sio mrefu .
Binafsi nichukue nafasi kumshukuru Mh.Waziri wa Elimu Prof. Mkenda kwa uwajibikaji wake wa kusikia changamoto na kuzitolea majibu,ufafanuzi na utatuzi haraka. Binafsi napongeza hatua hii ni nzuri sababu itaendelea kufanya wanafunzi hao wasome zaidi kufikisha GPA 3.8 ili wapate ufadhili 100% na hata hao ambao hawatafikisha GPA 3.8 wataendelea kupewa fedha hizo kama mkopo . Hivyo ni chaguo la mwanafunzi. Nina shauri wanafunzi chaguo liwe moja tuu kusoma , kusoma,kusoma kwa bidii ili kufikisha hiyo GPA 3.8 kuendelea kupata ufadhili 100% , tofauti na hapo huo ni mkopo na utapaswa kulipwa.
Tutaendelea kufuatilia ufanisi wa Program hii na hatutasita kukosoa ,kushauri na kupendekeza kwa manufaa ya Elimu yetu na nchi yetu , popote tukiona kuna tatizo.
Ahsante sana.
=========== ============
UFAFANUZI WA BODI YA MIKOPO
Mkuu wa Mawasiliano wa HESLB, Omega Ngole amezungumza na JamiiForums na kusema “Ni kweli kuna Kundi la hao Wanafunzi ambao hawajatimiza vigezo, watahamishiwa katika mkopo wa Bodi na wataruhusiwa kufanya maombi ya mkopo kwa kuwa huwezi kupata mkopo kama hujaomba.”
Ikumbukwe kuwa sehemu ya mkataba wa Ufadhili wa Samia ni kuwa Mnufaika hatakiwi kupata chini ya ufaulu wa GPA 3.8, kinyume na hapo ataondolewa katika ufadhili na kuingizwa katika Mkopo wa HESLB.