Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,363
- 58,386
hawako serious hawa jamaa hakuna kitu kingine. wangekuwa serious wasingefanya ujinga kama huu.
Jamaa anachukia kuona all the time uko online. yeye kimodem chake kikiishiwa haonekani mwezi
teeteheteeteeteheteheeee mzee wa liver bwana kama kweli vile ni sawa na wale weekday wanapost hatari mida ya asubuhi mpaka jioni halafu kuanzia 12 haonekani na siku za weekend..
vipi yule afisa wa bodi imeishia wapi?..
Hao ujue wanakuwa wanatumia muda wa ofisini............wakitoka tu internet access kushney......Mie silipi hadi tule aliyepachika majina hewa alipe zote
malimwengu kauliza swali la msingi tu lakini tunavoruka...lol!!!
kuna hatari ya kuanza kuwa defensive bila hata kujua kama mkopo unakuhusu au lah!!
mkopo ulianza lini? na je udhamini wa serikali na mkopo vyote vinahitaji kulipwa?
sasa kama hukujaza hiyo karatasi imetoka wapi?Jamani nimedakwa sasa hivi na mtu wa Msolopa............auction mart.........nimempa maelezo nasubiria kupelekwa mahakamani. Ajira hawajanipa alafu wakuja kudai tu. Mie Sikuomba mkopo nilipsomeshwa na govt sababu nilipata div one......sikujaza chochote. Wanileteee karatasi niliyojaza kudadeki.
Ndugu wana JF.
Mimi ni mhitimu wa UDSM mwaka 2006, na kwa bahati nzuri nimeajiriwa katika chuo kikuu kimojawapo cha serikali hapa nchini. Kuanzia mwaka 2008 tulianza kukatwa madeni ya HESLB na mpaka sasa ninavyozungumza nimebakiza kama 500,000 tuu nimalize deni langu. Hivi majuzi rafiki yangu mmoja aliniambia kuwa ameshangaa kukuta kwenye website ya loan board kukuta jina lake kama mdaiwa sugu ambaye hajaanza kulipa wakati amebakiza hela kidogoo sana kumalizia deni lake (kama laki 3 hivi), na anakatwa kila mwezi kwenye mshahara wake.
Leo na mimi nikajawa na curiosity kutaka kujua kama na jina langu limo, na kweli nikalikuta nimo kwenye list ya wadaiwa sugu wa HESLB. Je, hii naashiria nini jamani? Nahisi harufu ya ufisadi!!!! Au ni uzembe wa loanboard kutokuupdate information zake kwenye website? Au mwajiri wangu ananikata hela lakini hapeleki loanboard? Sielewi bandugu. Ngoja niendelee kutunza salary slip zangu.
Ndicho hasa na mi nataka kufahamu hiyo mikopo ilianzia wapi na udhamini uliishia wapi?Nadhani tunaoandika humu ni baadhi ya wadaiwa according to Board ya Mikopo. Kama nilivyosema hapo nyuma, wakati tunamaliza hiyo miaka ya 90, bodi haikuwepo na hatukuwa tunakopeshwa bali tulikuwa sponsored na serikali. Kilichokuwepo pale ni cost sharing!!
By the way, hivi wale wenzetu waliokwenda kusoma Rusia, India n.k. kwa gharama za serikali nao wapo kwenye hiyo list ya wadaiwa?? Maana kuna watoto wa vigogo wengi kwenye hiyo list............. including Nape!!
Mie itakuwa ngumu kulipa..........kila mwezi nakatwa kodi ya Tsh 105,000/= inalipwa na serikali inachukua fedha hii...manaidai tena nini?