Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu yafungua dirisha la maombi kwa siku 40, yatoa muongozo

SirSalumu

Member
Jul 1, 2019
19
8
Tuusome kwa makini ili tupate mikopo inshallah

======

Tunapenda kuwafahamisha wanafunzi wahitaji wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu ya juu inayotolewa na Serikali kupitia HESLB kuwa mfumo wa uombaji wa mkopo kwa njia ya mtandao utakuwa wazi kwa siku 40 kuanzia Jumanne, Julai 21, 2020 hadi Jumatatu, Agosti 31, 2020.

Tunawashauri wanafunzi wahitaji kutumia muda wa sasa hadi mfumo utakapofunguliwa (Julai 16, 2020 hadi Julai 21, 2020) kusoma ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Mwaka 2020/2021’ unaopatikana kuanzia sasa katika tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) katika lugha za Kiswahili na Kiingereza.

Mwongozo huu unatoa maelekezo ya kina kuhusu sifa, utaratibu na vigezo vitakavyotumika katika uchambuzi wa upangaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2020/2021.

Aidha, baada ya kuusoma, tunasihi waombaji mikopo kuhakikisha wanaandaa nyaraka zote muhimu kama zinavyoelekezwa katika Mwongozo huo.

Imetolewa na:

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu

DAR ES SALAAM

Alhamisi, Julai 16, 2020
 
Attachments

  • GUIDELINES_AND_CRITERIA_2020_2021.pdf
    670.3 KB · Views: 71
  • MWONGOZO_WA_UTOAJI_MIKOPO_2020_2021.pdf
    708 KB · Views: 149
Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu wametoa Muongozo wa utoaji Mikopo kwa wanafunzi tafadhali soma kabla kuangalia vigezo na masharti yote kwa mwaka 2020/21
 
Attachments

  • MWONGOZO_WA_UTOAJI_MIKOPO_2020_2021.pdf
    708 KB · Views: 41
Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu wametoa Muongozo wa utoaji Mikopo kwa wanafunzi tafadhali soma kabla kuangalia vigezo na masharti yote kwa mwaka 2020/21
Kipengele cha waliofadhiliwa wanasema wa download form kweny tovut yao ijazwe na mzamin cyo barua kam zaman sas mbn kwenye website hy form aipo
 
Hivi wale , ambao tuli hahirisha mwaka , kwa sababu ya kukosa pesa , je sisi tunachukua utaratibu gani ?
 
Hivi ni kweli kwamba mtu aliyesoma private kwa level fulani kama O Level hapewi mkopo?
 
Sorry mkuu na vipi kwa upande wa wale ambao walipata chuo na mkopo mwakajana lakin hawakwenda kabisa kuripoti wanaweza kuapply pia mkopo tena na wakapata chuo!?
Kama ulipata chuo na hukwenda kupostpond nenda TCU na Chuo ulichochaguliwa kwa sababu ukijarilbu kuomba mwaka huu bila kufanya hivyo kulingana na mifumo ilyowekwa na TCUinaonyesha tayari no mwachuo. .kuhusu Mkopo unaomba tu hakuna shida
 
Hivi wale , ambao tuli hahirisha mwaka , kwa sababu ya kukosa pesa , je sisi tunachukua utaratibu gani ?
Nenda TCU mzee wakutoe kwanza kama haukupostpond chuo kwa maana kutoa taarifa kuwa utaendelea mwaka ujao. Kama ulipiga kimya lazima ufike TCU kwanza lkn Mkopo unaweza kuapply bika shida
 
Hivi ni kweli kwamba mtu aliyesoma private kwa level fulani kama O Level hapewi mkopo?
sio kweli inategemea hiyo shule ada yake ilikuwa Shilingi ngapi mfano huwezi kusoma international school of Tanganyika then uombe Mkopo upewe... Shule mfano Airwing ni Private tena kuna wanafunzi wamesoma toka form one had I six na wameomba Mkopo wakapata
 
[SUP]kama unasoma muongozo huo kwa wale MNA hofu mmesoma private schools. Kwenye sehemu ya king'amua uwezo utaelewa vizuri[/SUP]
 
[SUP]kama unasoma muongozo huo kwa wale MNA hofu mmesoma private schools. Kwenye sehemu ya king'amua uwezo utaelewa vizuri[/SUP]
Mkuu, kwenye kuomba mkopo kunahitajika copy ya cheti cha form4 na kama kinahitajika ni sehemu gani..?
Naomba msaada kidgo hapa nataka nijipange full nije ofisini kwenu
 
Jamani Mimi nili cancel admission kwenye chuo husika ili kuomba chuo kingine kwhyo na Mimi Nina haja ya kwenda TCU na hungali kule nilisha cancelled na chuo husika
 
Nenda TCU mzee wakutoe kwanza kama haukupostpond chuo kwa maana kutoa taarifa kuwa utaendelea mwaka ujao. Kama ulipiga kimya lazima ufike TCU kwanza lkn Mkopo unaweza kuapply bika shida
Wakuu...Mimi nili cancel admission kwenye chuo husika kbx ili kuomba chuo kingine maana kulingana na mifumo yetu ukisha chaguliwa chuo kimoja inatakiwa u-comfirm au Kama ukitaki u-cancel admission nakuomba chuo kingine lkn nilichaguliwa kwahiyo na mm apa natakiwa kwenda TC kabla ya kuomba mwaka mpya wa masomo
 
Kama ulipata chuo na hukwenda kupostpond nenda TCU na Chuo ulichochaguliwa kwa sababu ukijarilbu kuomba mwaka huu bila kufanya hivyo kulingana na mifumo ilyowekwa na TCUinaonyesha tayari no mwachuo. .kuhusu Mkopo unaomba tu hakuna shida
Kwaiyo mkuu hata kama ukwenda kufanya usajili pale chuoni kuna aja ya kwenda TCU kujitoa coz chuo wakishafanya usajili cwanapeleka majina ya wanafunzi wao walio lipoti chuo na ww kama ukufanya usajili inamana siyo mwanafunzi tena wa kile chuo xaxa hapo kunaaja ya kujitoa TCU?
 
Back
Top Bottom