INSPECTOR JOE
Member
- Apr 14, 2014
- 26
- 12
Habari wanajamii naomba msaada wenu, miaka takribani mitano nyuma nilikuwa kwenye mahusiano ambayo yalipelekea kuwa mzazi wa mtoto mmoja wa kiume.
Kiuhalisia maisha hayakuwa mazuri sana ila tulikuwa na furaha na tuliishi kwa kupendana sana. Safari yetu ilikuwa nzuri kiujumla, lakini ikatiwa doa na mama mzazi wa mzazi mwenzangu kwa kumchukua mwanae kinguvu huku akinisema kwa ubaya jambo ambalo lilinikereketa vibaya kila kukicha.
Ni mwaka sasa umetamatika baada ya mimi na mzazi mwenzangu kutengana lakini imefika mahali upendo umepungua sana. Nilikuwa nimezoea kumpigia simu kujua hali ya mtoto na yeye lakini mama yake amekuwa mtu wa kuvuruga hadi mawasiliano yetu.
Imefika mahali natamani kuanza safari mpya maana nimechoka kiuhalisia maana nimejikuta namchukia sana mama mzazi wa mke wangu kutokana na tabia alizozionyesha za kumchukua mwanae kwa nguvu akiambatanisha na vitisho huku pia akidai namtesa mwanae wakati toka nimenza kuishi nae sijawahi kufanya, kuelezea kila kitu siwezi kwa haraka haraka.
Maana niliyofanyiwa mpaka naomba ushauri wenu ni mengi na yanumiza. Nimwache abaki na mama yake au nirudiane naye?