BIL 1.8 zapelekwa kujenga Hospitali ya Wilaya ya Moshi

Jun 20, 2023
54
51
Serikalai yamwaga Bilioni 1.8 ujenzi Hospital ya wilaya Moshi

SERIKALI imetoa shlingi Biliioni 1.8 kwa ajili ya ujenzi wa Hospital ya wilaya ya Moshi inayojengwa Kata ya Mabogini ukanda wa tambarare itakayohudumia wananchi Zaidi ya 535803 kutoka majimbo ya Moshi Vijijini na jimbo la Vunjo.

Hayo yamo kwenye Taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Shadrack Mhagama aliyoitoa kwakamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali za mitaa iliyotembelea na kujioneamaendeleo ya ujenzi wa Hospital hiyo mapema alhamis wiki hii.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo,hadi sasa ujenzi huo unatekelezwa kwenye majengo manne likiwamo jingo la utawala,jengo la mionzi,jengo la kufulia pamoja na jengo la kutolea dawa ambako kiasi cha sh,Miioni 800 kitatumika kumailisha ujenzi huo.

Alisema jengo la utawala limetengewa milioni 407,jengo la mionzi limetengewa milioni 168 wakati jengo la kufulia likitengewa milioni 135 na jengo la kutolea dawa likitengewa sh,milioni 173 huku akiainisha changamoto za kuchelewa kuanza kwa ujenzi huo kuwa ni mfumo pamoja na mvua .

Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Hai,Saasisha Elinikyo Mafuwe,alitolea ufafanuzi wasintofahamu ya kujengwa kwa Hospital hiyo eneo la Mabogini ni kwamba ilitokana na ushauri wa kitaalamu na si kwamba kuna upendeleo.

Kata ya Mabogini ipo kwenye JImbo la Moshi Vijijini ambako mbunge wake ni Profesa Patrick Ndakidemi na Saasisha aliwaeleza wananchi wa jimbo hilo kuwa hakuna ubaguzi wowote uliofanyika kupeleka mradi huo ukanda huo.

“Ndakidemi ni mbunge wa kata zote,ni mbunge wa vijiji vyote na eneo hili ndiyo lilikuwa eneo rafiki kujengwa hapa na siyo kwa sababu anawapenda wale na anawachukia wale hapana,sababu za kitaalamu zinaonyesha ni hapa na serikali imeamua ni hapa na watu wa mabogini ni watu lazima kituo kipate sehemu ya kujengwa na kuanzia maendeleo ni hapa”.alisema.

Aliwataka wanachi wa Jimbo la Moshi vijijini kuendelea kumwamini Profesa Ndakidemi akimwelezea kama moja ya maprofesa bora afrika na kuacha harakati za kuhujumu maendeleo anayoyafanya kwa misingi ya kisiasa.

“Sisi ndiyo waathirika wa siasa za upinzani kulikoma mengine,leo unataka kumtoa profesa Ndakidemi umlete mwingine aanze kujifunza kwa miaka mitano,hapo haiwezekani ,hatuwezi kuwa wabunge wote lazima wengine wakubali kua huu ni wakati wa Profesa Ndakidemi,”alisema.

Akizungumzia ujenzi huo,Profesa Ndakidemi amesema baada ya ujenzi wa hospitali ya wilaya inayojengwa Mabogini kukamilika na kufunguliwa, wananchi wataweza kupata huduma bora kwa uharaka na kwa unafuu na kuwasaidia kuwapunguzia gharama za matibabu ambazo walikuwa wanazitumia kusafiri zaidi ya kilomita 20 kwenda kupata huduma hizo katika hospitali za Mawenzi na Kibosho.

Pia Profesa Ndakidemi amsema baadhi ya wananchi walikuwa wanapata matibabu kwa gharama kubwa kwenye hospitali binafsi zilizoko mjini Moshi nak uongeza kuwa Mpaka sasa serikali imeshatoa shilingi bilion 1.8 kwenye ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya.

MWISHO
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom