Biashara ya Usafirishaji kwa Bajaji: Ueandeshaji, Changamoto, Faida na Ushauri

Wanajamii habarini za muda huu na poleni sana kwa majukumu ya kimaisha. ninataka kuanzisha mradi wa babaji na nilikuwa napenda kufahamu zaidi kuhusu uendeshaji wake hasa hususan running cost zake, returns zake za kila siku na mambo mengine pia.sokwa wale wenye experience na hii biashara naombeni msaada wenu.
 
Hii biashara ni nzuri lakini ina changamoto zake kama zilivyo biashara nyingine. Kwa kifupi nikupa yale machache ambayo ni ya kuzingatia katika hii biashara.

1. Hakikisha chombo kinalala kwako, maana usipofanya hivyo madereva wa bajaj wana kawaida ya kukifanyisha chombo kazi kwa muda wa saa zote 24 za siku kwa utaratibu wa kuwaachia deiwaka. Halafu wewe anakuletea Tsh 15000 tu, wakati unaweza kukuta wametengeneza hadi Tsh 70,000 (Kama siku ikiwa nzuri sana) kwa siku.

2. Hakikisha unasimamia service na uwe na rekodi ya siku unayofanya service maana usipofanya hivyo, kuna uwezekano ukaambiwa kuna service imefanyika ilipe utoe hela wakati hakuna kilichofanyika. Hii inaweza kufanya chombo kikachoka haraka hadi ukashangazwa.

3. Kama huna utaalamu hata kidogo na mambo vyombo vya moto, sikushauri hata kidogo kununua bajaj zilizotumika maana utatumia hela nyingi sana kulipa mafundi na kununua spea. Ni vizuri ununue vyombo vipya na pia usikae navyo sana, fanyia kazi si kwa zaidi ya miaka miwili, uza na ununue vingine.

4. Usiwachekee kabisa hao madereva kwenye masuala ya hesabu maana hawachelewi kukuletea stori za biashara mbaya wakati wakipiga hela hawakuongezi hata sh 100 kwenye hesabu yako. Kama biashara mbaya weka deni, siku zijazo wajazie hiyo hesabu.
 
Duh mkuu ahsante sana. Na hesabu ya siku mpaka leo ni 15000 tu? Haijapanda hata kidogo? Maana gharama za maisha nazo zimepanda.

Sent from my BlackBerry 9930 using JamiiForums
 
Kuna option pia ya kuingia mkataba na dereva ambapo kwa wiki anakuletea 140,000 kwa kipindi maalumu na baada ya hapo unamwachia bajaji inakuwa yake. Ila katika kipindi hicho unakuwa emehakikisha kuwa pesa ya bajaji yako imerudi, pesa ya kununulia bajaji nyingine imepatikana, na pesa kiasi kwa ajili ya maintanance na kulipia gharama za motor vehicle, mapato, JIJi na SUMATRA. Hivyo itategemea na gharama ya bajaji husika.

Kwa TVS wengine wana fanya mwaka mmoja na miezi 11. au wiki 99*140,000=13,860,000. hapa hutoumiza kichwa maana dereva huijali sana bajaji na kuitunza kwa vile ni ya kwake.
 
Duh mkuu ahsante sana. Na hesabu ya siku mpaka leo ni 15000 tu? Haijapanda hata kidogo? Maana gharama za maisha nazo zimepanda.


Sent from my BlackBerry 9930 using JamiiForums

Hesabu ni maelewano tu. Kuna watu hesabu zao ni 20K, Wewe tu.
 
Duh mkuu ahsante sana. Na hesabu ya siku mpaka leo ni 15000 tu? Haijapanda hata kidogo? Maana gharama za maisha nazo zimepanda.


Sent from my BlackBerry 9930 using JamiiForums
Hesabu ni makubaliano na inategemea eneo la biashara.
 
Za wakati huu wana jamvi,

Naomba kushauriwa hukusu biashara ya bajaji. Nina tarajia kununua bajaj ila ningependa kujua bei zake dereva analaza kiasi gani kwa sku na baaadhi ya matengenezo ni jukumu la nani. Vilevile ni baada ya miaka mingapi bajaji iinakua imechoka kabisa.
 
[quote="mzalendo8,
Kuna jamaa nafahamiana nae anaiuza bajaj yake kwa bei poa sana. Utakapokuwa tayari nipm nitawakutanisha!
 
Bei zinatofautiana na mkoa kuna 20000 Kwa siku na 15000 kwa siku na kuna mkataba akimaliza dereva ni yakwake.uliza kuhusu bajaji(tvs king)
 
Back
Top Bottom