Biashara ya Usafirishaji kwa Bajaji: Ueandeshaji, Changamoto, Faida na Ushauri

Nina hela yangu 10m.ninataka kuiwekeza. naomba mnishauri kama nikinunua bajaji 2 zitalipa wadau.
 
yeah inalipa,.. Ay nunua hizi pickups mpya za kisasa iwe inabeba mizigo.. Kama upo dar trip fupi ni sh15000 ... Kwa hiyo una uhakika wa kukusanya zaidi ya 70elf per day out of mafuta... Chenji itakayobaki nnua SANLG uifanye bodaboda.. Itakuletea 40,000 week...
Ni mtazamo tu,...
 
inalipa sana ukipata dereva mzuri. kwa dar hesabu ya siku ni 15,000. ila mikoani kama mbeya ndio bonge la dili mana kwa siku ni 30,000. dereva akiwa kimeo utajutia.
 
Ni kweli kwa mbeya inalipa sana. Kwani kwa siku inalaza 30,000/=. kwa hapa dar ukiwa na dereva mzuri ni 15000 kwa siku.
 
HATA MIMI NINGEKUSHAURI SANA UWE MWANGALIFU HIYO BIASHRA UOMBE MUNGU akupatie Driver MUAMINIFU na mwenye hofu ya Mungunbila hivyo kaka utaambiwa kila leo sijapata kitu.

Tafakari sana kabla hujaamua, Vinginevyo kama aliyesema mikoani ni pazuri zaidi. Mungu akuongoze maana mtaji wako huo inabidi upate biashara itakayokurudishia kitu.
 
Salaam kwenu nyote!

Kwa mwana JF yoyote anaefanya biashara ya Bajaji nina shida kidogo..kuna kautafiti kadogo nataka kufanya.
Nimekuwa nafanya biashara za bajaji kwa takribani miaka mitatu sasa.

Kwa sasa naona kama gharama za uendeshaji wa Biashara hii zinapanda kila kukicha, awali ulitakiwa kulipia road licence, kodi ya mapato na bima ili uweze kufanya biashara hii. But hivi sasa SUMATRA wamekuja kwa kasi ya ajabu wanatoa na wao leseni na wana taratibu ambazo ziko a bit complicated.

Nilitamani kujua wamiliki wengine wa Bajaji wanatoza hesabu ya Tsh ngapi kwa siku, (binafsi toka nimeanza natoza 15,000). Pia ni namna gani ya kukabiliana na changamooto hizi, ukiachia mbali fikra zangu zakuongeza hesabu ya siku.
 
Mimi nilishaifanya ila kwa sasa nimeachana nayo. so nina experience nayo. uliza lolote.
 
Mkuu Ndibalema asante kwa kuitikia wito. Naomba nikucheki kwa Pm

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Unataka kufanya utafiti kwa mtu mmoja halafu utoe conclusion? Nafikiri ungeweka maswali yako hadhari ungepata majibu kukoka kwa watu mbalimbali ambao wanaijua hiyo biashara.
 
Unataka kufanya utafiti kwa mtu mmoja halafu utoe conclusion? Nafikiri ungeweka maswali yako hadhari ungepata majibu kukoka kwa watu mbalimbali ambao wanaijua hiyo biashara.
Umeona eeh! neggirl Mimi nakushauri weka maswali yako hapa, unaweza pata majibu mengi mazuri yatakayokusaidia kwa huo utafiti wako. ni vizuri kupata maoni ya watu tofauti, achana na pm.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom