viti viwili 1.2M, Kitanda cha msg 0.6M, Vioo na kufix 0.1M, shaving mashines nzuri mbili 0.3M, Hair bowl mpya ya kisasa 0.7M, consumables and towels weka 0.1M. milioni tatu imeishia hapo ila ukiwa na 5M kwa saluni ya kiume unaanza vizuri sana. cc Cutie M
Hii kazi ni nzuri sana, inalipa vema sana. Cha muhimu ni usimamizi madhubuti. Ni nzuri sana ukifungua mahali karibu nawe, atleast ndani ya wiki uwepo hapo golini hata mara tatu. Vijana wasimamizi na vinyozi hukosa uaminifu pindi boss anapokuwa nao mbali.
Jaman mwenye kujua Hesabu ya saluni kulingana na bei ya kunyolea inakuwaje? Mfano bei ya kunyolea ni 1,500 2,000 au 3,000 hapo makusanyo yanapaswa kuwa shilingi ngapi kwa siku au kwa week??
Nimeupenda sana huu Uzi maana Mimi mwenyewe mjasiriamali na Nina plan ya kufungua Barber shop next year. So wenye uzoefu endeleeni kutoa darasa
Wakuu hapo juu wamechangia vizuri sana tu,ila kuna vitu hawajaviainisha wazi sana.
Karibia frames zote zinazopangishwa unakuta hazikidhi vigezo kwa salon,inabidi uingize gharama zako tena sio kidogo,kama milango,rangi,tiles nk,na wahuni wengine wanakutwanga umeme wa ku-share
Hapo bado kodi ya Frame,ambapo be zake zinafahamika,labda iwe uswahili saana,na si chini ya 100,000 hata huko uswazi,sasa ukijongea centers za eneo ulipo ndio kabisaa.
Na Salon yenye chumba cha massage lazima iwe na frame kubwa au uchukua frames mbili,siku hizi watu wanajenga frame ndogo sana kimaslahi zaidi,sasa hapo lazima ziwe mbili.
Suala jingine ni kuangalia na viti vya kuanza navyo,kwanza lamzima uwe na malengo ya kufikia angalau viti vinne.Ila anza na viwili kwanza,then utaangalia muelekeo wa kazi yako.
Hapo red siku hizi mnapangiana hesabu kwa kiti, kiti kimoja kizae elf 10 na kuendelea inategemea na location.Shukurani mkuu Zanzibar Spices kwa ufafanuzi mzuri sana. Nimefanya utafiti kidogo gharama ya vifaa vya kuanzia haiko mbali sana na mchango wa Husninyo. Pia bei ya fremu inafahamika kutegemeana na site ya ilipo salon. Nikuombe uzoefu wako kwenye hilo la ukarabati wa chumba kimoja kuwa katika average standard kwa kuanzia inaweza cost kiasi gani na pia mfumo bora wa kukusanya na kusimamia mapato kwa mmiliki ambaye hayupo pale full time.