Zitambue taratibu za Kufungua Maabara binafsi ya Afya na Makadirio ya Gharama zake

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,634
26,373
Wakuu,
Kumekuwa na wadau kadhaa wakiulizia ni taratibu zipi za kufuata ili kuanzisha maabara binafsi ya afya(Health laboratory),lakini hayajapatikana majibu ya kina kukidhi haja zao,hivyo nimeona nami nisaidie kidogo katika hilo.

Hapa nitazungumzia Laboratory type C-hizi ni maabara zilizopo mitaani kwetu ambapo unaenda kupima ugonjwa fulani unapewa majibu yako,Huwa kuna type tofauti tofauti kutokana na wizara ilivyoamua.

SEHEMU A;
Zifuatazo ni taratibu za kuanzisha maabara ya Afya binafsi(Private Health lab type C;
  • Moja, ukishapata eneo(location) unalopanga kufungua maabara, utapaswa kuandika barua ya maombi kwenda uongozi wa kijiji husika(Mwenyekiti) kuomba kufungua maabara eneo lake,akikubali kwa maandishi utaenda hatua inayofuata.
  • Pili, barua uliyopata kutoka kwa Mwenyekiti wa Kijiji utaambatanisha na barua nyingine kwa ajili ya kuomba kibali cha kufungua maabara na kuipeleka kwa mratibu wa Maabara wilaya;
JENGO LA MAABARA;
Kabla ya mratibu wa Maabara kuja kukagua jengo lako litapaswa kuwa na vigezo vifuatavyo;
  • Jengo liwe na vyumba vitatu,mapokezi(Reception),Store na working room(lab).
  • Jengo linapaswa liwe na marumaru au sakafu safi na ukuta smooth.
  • Jengo liwe ma madirisha makubwa(5" kwa 6) kwa ajili ya Mwanga.
  • Unapaswa kuwa na Kichomea taka(Incinerator)
  • Jengo linatakiwa liwe na uzio/fence hasa kama linapakana na makazi ya watu
  • Choo cha wanaume na wanawake
  • Jengo Liwe na Mtungi wa kuzimia moto(Fire extinguisher)ya liquid sio powder.
  • Sanduku la Maoni.
  • Masinki mawili ya kunawia-Moja reception na lingine working room(Lab)
  • Mfumo wa maji safi tiririka(bomba)
  • Mfumo wa Maji taka.
  • Eneo la kusubiria wagonjwa(Waiting area).
  • Eneo la kuchukulia vipimo/sample(Phlebotomy)
  • Kibao cha kuonyesha jina la Maabara,huduma,saa/siku na kazi na mawasiliano(Hiki kitakaa mbali kidogo)na Jengo.
VIFAA (MASHINE )MUHIMU ZA KUWA NAZO ;
  • Darubini(Binocular powered microscope)-electric or light
  • Centrifuge machine(electric or manual)
  • HB machine
  • Glucose machine
  • Refrigerator with deep freezer
NB: Hizi ni zile mashine muhimu tu ili uweze kuruhusiwa kuanza kazi lakini unaweza kuongeza kadri ya mahitaji mfano;
BP machine- kwa ajili ya kupima blood Pressure
Waterbath- Kufanyia vipimo vya Tyophoid
Urine analyser-Kufanyia urine Chemistry
Hot oven- kupashia Kemikali zilizoganda, kupashia vifaa
Nakadhalika nk.

SAMANI ZA KUWA NAZO;
  • Meza ya mapokezi
  • Viti vya Mapokezi
  • Kiti cha mhudumu maabara(working room)
  • Meza ya maabara(working room) yenye smooth top(isiyopitisha maji)
  • Benchi kwa ajili ya eneo la kusubiria wateja
  • Dustbins tatu-Moja ya taka za kawaida,moja ya taka hatarishi na nyingine ya Kuwekea sindano zilizotumika.
WATUMISHI WA MAABARA NA VIGEZO VYAO;
  1. Mtaalamu wa Maabara(Laboratory Technician anapaswa kuwa na certificate au zaidi na awe ana Cheti cha Usajili wa baraza la Maabara (FRP)
  2. Msimamizi wa Maabara(anapaswa kuwa na Diploma ya Maabara na Cheti cha kusajiliwa baraza la Maabara (FRP)
Huyu si kwamba anakuwa pale akifanya kazi kila siku hapana,huwa anakuwa ndiye msimamizi wa taratibu za kazi na atakuwa anakuja angalau mara moja kwa mwezi kukagua maabara na hata wakaguzi wakija wakakuta mambo hayapo sawa ndiye ataulizwa.
  • Mhudumu wa usafi/Cashier-hapa sio lazima itategemea na makubaliano yenu. Kama mtaalamu wa Maabara anaweza kufanya usafi na pia kupokea pesa unaweza kumtumia pia.
Note 1: Kama Mtaalamu wa maabara (Lab technician uliyempata ana Diploma na Cheti cha FRP(Usajili) unaweza pia kuongea nae akawa ndiye Msimamizi pia wa Maabara yako.

DOCUMENT MUHIMU ZA KUWA NAZO;
  1. Mikataba ya kazi ya watumishi niliowataja hapo juu
  2. Namba za NIDA za watumishi niliowataja hapo juu
  3. TIN namba ya biashara yako
  4. Ramani ya Jengo lako la Maabara
  5. Vyeti vya watumishi na Leseni zao.
  6. Namba zao za simu.
Maelezo ya Ziada;
Kuhusu namna gani Jengo likae na mambo madogo mengine utaelekezwa na mratibu wa maabara wilaya(Kule ulikopeleka barua ya maombi)ambapo watakuja kukukagua mara kadhaa ili kujiridhisha na maelekezo waliyokupa.

Document zilizozitaja hapo juu zitahitajika kuingizwa kwenye mfumo wa maombi(HFRS)-Health facility Registration System pale utakapopewa maelekezo na Mratibu wa maabara ili ufanye maombi ya Usajili(Application).

Kuna vifaa vidogo vidogo(Supplies),hivi hujumuisha gloves,gauze,pamba,needls, Reagents nk utanunua ukishapewa kibali cha kuanza na utakaa na mhudumu wako uliyempata atakutajia mahitaji yote muhimu.

Hivyo, kwa yeyote anayehitaji kufungua maabara awe Mtaalamu wa Maabara kwa maana ya Kusomea au sio mtaalamu lakini anataka kuwa mmiliki utaratibu ndio huu.

SEHEMU B;
JENGO;
Hapa kuna namna tatu za kupata jengo la maabara;
  • Kujenga mwenyewe jengo jipya-hapa gharama itategemea na eneo unalojengea,ukubwa wa jengo na nakshi zake.
  • Kukarabati jengo ili likidhi vigezo vya maabara-hapa itategemea na makubaliano yenu nani wa kubeba gharama kati ya mwenye jengo na mpangaji.
  • Kupanga jengo ambalo tayari lina Hadhi ya maabara,ambapo utalipia kodi ya pango mwisho wa mwezi.
Kwenye kipengele hiki cha jengo utaona kwamba ni vigumu kupata makadirio halisi kwa sababu gharama itategemea mambo mengi kwahio hapa naweka tu makadirio,nikiamini kwamba umepata jengo ukafanya marekebisho kidogo ya Tshs 4,000,000/=(Milioni nne)

MASHINE MUHIMU

  1. Binocular Microscope.......1,000,000
  2. Centrifuge machine........... 300,000
  3. HB Machine........................ 300,000
  4. Glucose Machine............... 70,000
  5. Refrigerator....................... 300,000
Jumla ya Mashine tunapata 1,970,000/=

VITI NA MEZA
  • Meza kubwa za plastiki 2...... 200,000
  • Viti vya plastiki 4............... 100,000
  • Meza ya maabara 1........... 200,000
  • Kiti cha Maabara 1............. 100,000
  • Mabenchi ya wateja 2............ 100,000
Makadirio ya hapa ni 700,000/=

LESENI NA KODI;

  • Application fee........
  • Ada ya Mwaka ya Maabara.......
  • Leseni ya Maabara(Wilaya)........
  • Kodi ya Mapato.............
Hapa tuweke makadirio ya Tsh 500,000/=

VIFAA(SUPPLIES)
Hivi vipo Vingi sana nitataja vichache tu
Racks
Pippetes
Red tubes
Purple tubes
Glass slides
Cotton
Gauze
Syringes and needles
H.I.V kits
H.Pylori kits
MRDT kits
UPT kits
Urine and stool containers
Kidney dishes
Prickers
Chemicals(Giemsa,Immersion oil etc
Hapa naweka makadirio ya kununua stock ya kutosha Tshs 1,000,000/=

GHARAMA NYINGINEZO;
Hizi ni gharama ambazo zipo ila huwezi kuziona moja kwa moja kwa sababu zinategemea mambo mengi tu
  1. Usafirishaji vifaa
  2. Kupeleka Wakaguzi kufanya ukaguzi
  3. Mishahara ya wafanyakazi
  4. Kuandaa Mikataba ya kazi
  5. Kutangaza maabara yako
  6. Mtaji wa kuanzia
  7. Kuwapeleka Askari wa Zimamoto kukagua Maabara ili wakupe cheti na kukuuzia Mtungi
  8. Kutengeneza sanduku la maoni
  9. Dharura nyinginezo
Hapa nimeweka makadirio ya Tsh 2,000,000/=

JUMLA KUU
Kwahiyo Makadirio ya Jumla ya Kujenga na kuanzisha Maabara ni;
4,000,000
1,970,000
700,000
500,000
1,000,000
2,000,000

Kwa hiyo nikijumlisha,Jumla kuu tunapata Tsh 10,170,000(Milioni kumi laki moja na elfu sabini tu).

Makadirio niliyoweka hapa yanaweza kupanda au kushuka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kupata Jengo, utofauti wa bei za mashine kutokana na ubora na uwezo, mfano HB mashine niliyoweka hapo ni ile ndogo inaitwa Mission plus, lakini kama ukiamua kununua Homecue inafika hadi 800,000 au zaidi, hivyohivyo upande wa Microscope zipo za bei ya chini zaidi ya hio niliyoweka lakini zipo za bei ya juu zaidi zinafika mpaka Milioni 2 mfano Olympus.

MAGONJWA UNAYOWEZA KUPIMA KWA VIFAA NILIVYOVITAJA HAPO JUU;
HB-Uwingi wa damu
Glucose level-Sukari mwilini
Malaria
U.T.I
Mkojo
Choo
H.I.V/PITC
H.Plylori-Vidonda vya tumbo
VDRL(Syphills)
BS
Urinalysis(Biochemistry)

Nimetoa mchango huu kama mdau tu lakini sio mtaalamu wa Maabara,hivyo kwa yeyote mwenye nyongeza katika hiki nilichoandika anakaribishwa.

Ahsante.
 
Barikiwa sana, ila kazi yako kubwa itakua kuomba watu waugue ili ipate wateja, this life is fuvk.

Yaani mtu anaomba uugue ili aje apate hela.
 
Kwa mwenye uhitaji wa centrifuge jamani. Naiuza kwa laki mbili tu, ni mpya full box
Screenshot_20230212-220439_1676228828858.jpg
Screenshot_20230212-220452_1676228801243.jpg
Screenshot_20230212-220505_1676228779155.jpg
Screenshot_20230212-220517_1676228744979.jpg
 
Back
Top Bottom