Gharama za tiba serikalini kuwa kubwa sana inatokana na serikali kufanyia biashara miundombinu ya afya

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,954
4,326
Ni bahati mbaya sana utekelezaji wa ile dhana ya cost sharing, serikali imejikuta inafanyia biashara miundo mbinu yake ya afya sawa na wawekezaji binafsi wa huduma za afya.

Muwekezaji binafsi akijenga hospitali yake anatarajia hela aliyotumia kujenga hiyo hospitali iwe imerejeshwa na wagonjwa ndani ya muda fulani na baada ya hapo aanze kupata faida. Vivyo hivyo akinunua CT scan, MRI machine, radiotherapy machine, X ray machine na vifaa tiba vingine hususani mashine za kupima damu, ultra sound machines, echo machines, ECG machines, neonatal incubators, operating tables, delivery tables, operation lamps, surgical instruments, heart- lung machines na kadhalika. Hii ni miundombinu ya huduma za afya. Ni tofauti na vitu kama dawa, vitendanishi (reagents), gloves, syringes, iv fluids, gauze na kadhalika ambavyo ni consumerbles.

Muwekezaji binafsi anawajibika apate faida kutokana na miundombinu hiyo pamoja na inayotokana na consumerbles itakayomwezesha kulipa mishahara ya watoa huduma, umeme, maji, kodi za serikali nk na yeye abakize ya kumtosha.

Dhana ya mgonjwa kuchangia huduma ya afya (cost sharing) kwenye vituo vya huduma za afya vya serikali ilikuwa ni kwa gharama za consumerbles na siyo kwa miundombinu za afya, mishahara na posho za watoa huduma, maji, umeme na matumizi mengineyo (OC) ya vituo hivyo. Lengo lilikuwa ni mgonjwa kuchangia kiasi fulani cha gharama ya dawa, vitendanishi na consumerbles zingine alizotumia kama gloves, nyuzi na syringes ili viweze kununuliwa vingine kwenye kituo hiko.

Mashine kama ile ya CT scan na MRI scan unaweza kuilinganyisha na Video Camera. Inachukua video images za slices (tomo) za mwili wa binadamu kwa kasi kubwa ikiongozwa digitally na mpiga picha anayeitwa radiographer. Mashine hiyo ikisha setiwa na radiographer ina uwezo wa kuchukuwa (scan) hizo video images kutoka kichwani hadi miguuni ndani ya dakika zisizozidi tatu na kutoa CD yake. Mpiga picha huamua sehemu ya mwili anayotaka ikomee hiyo scan kufuatana na daktari wa mgonjwa alipotaka kuona. Baada ya hapo hiyo CD ya hizo picha (image slices scans) husomwa na kuwa interpreted na daktari bingwa wa radiology.

Cha ajabu ni hizo gharama zinazotozwa kwenye hizo picha (scans). Kichwa laki 3, shingo laki 2, kifua laki 3, tumbo laki 3, pelvis laki 2 na kadhalika. Halafu daktari bingwa wa radiology analipwa mshahara ( net pay) wa shillingi zisizozidi kwa mwezi million 2 tu ili hali mbunge analamba zaidi ya 10m kwa mwezi. Serikali inaamua kumwongezea daktari huyu na mpiga picha wake (radiographer) kiasi fulani kidogo kilichotokana na fedha walizolipia wagonjwa kwenye hizo scans.

Kwa mwekezaji binafsi bei hizo za scans ziko sawa kwani yeye anahitaji kurudisha mabillioni ya pesa aliyotumia kununua hiyo CT scan au MRI scan. Serikali haipaswi kutoza kiasi chote hicho cha pesa kwa wagonjwa hospitalini kwake. Bei ya hizi scans hazipaswi kuzidi shilingi elfu thelathini kwenye vituo vya tiba vya serikali. Vivyo hivyo kwa vipimo vingine na gharama za upasuaji, mionzi (radiotherapy) na kadhalika. Serikali iongeze mishahara ya hawa mabingwa angalao nao ifikie 10m kwa mwezi kutoka vyanzo vingine na siyo kwenye hizi tozo za miundombinu ya afya. Miundombinu hii imetokana na kodi za wananchi wote ili wapate nafuu ya maisha.

Hizi gharama kubwa sana za matibabu kwenye vituo vya tiba vya serikali ndivyo vinafanya ndoto ya Universal Health for all na ile Bima ya Afya kwa wote kuwa gumu kutekelezeka.
 
Back
Top Bottom