Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,003
- Thread starter
- #21
Mwanakijiji,
Inaonekana huyu kijana ana kiburi na ujeuri wa makusudi, kuwalinda wahalifu na marafiki zake, kama anashindwa kukemea chochote bongo basi Zimbabwe itakuwa ni sikio la kufa kwake.
Gm
Kila jambo lina wito wake na kushindwa kufanya jambo moja haina maana ushindwe kufanya jingine. Kama Kikwete hana uwezo wa kusimamia mambo mbalimbali aliutaka Urais wa nini? Kama asingekuwa na uwezo au nia ya kushughulikia matatizo ya Afrika (kwa vile ya kwetu yanamtatiza) kwanini basi alikubali kuwa Mwenyekiti wa AU?
Suala la Zimbabwe ni nyeti na zito kweli na linahitaji ujasiri wa hali ya juu kuanza kulishughulikia.