Barua ya Wazi kwa Rais Kikwete Kuhusu Zimbabwe

Mwanakijiji,

Inaonekana huyu kijana ana kiburi na ujeuri wa makusudi, kuwalinda wahalifu na marafiki zake, kama anashindwa kukemea chochote bongo basi Zimbabwe itakuwa ni sikio la kufa kwake.

Gm

Kila jambo lina wito wake na kushindwa kufanya jambo moja haina maana ushindwe kufanya jingine. Kama Kikwete hana uwezo wa kusimamia mambo mbalimbali aliutaka Urais wa nini? Kama asingekuwa na uwezo au nia ya kushughulikia matatizo ya Afrika (kwa vile ya kwetu yanamtatiza) kwanini basi alikubali kuwa Mwenyekiti wa AU?

Suala la Zimbabwe ni nyeti na zito kweli na linahitaji ujasiri wa hali ya juu kuanza kulishughulikia.
 
Bravo MKJJ.

Hii forum inazidi kuweka msisitizo. Please JK seaze this moment to show leadership..tafadhali onyesha njia kwa vitendo tumzuie huyu mzee Mugabe asiendelee kuangamiza watu na taifa la zimbabwe.

Kama Tanzania, wakati huo ikiwa taifa changa kabisa na masikini iliweza kuvunja uhusiano wa kibalozi na Uingereza pale Ian Smith na ma settler wenzie walipotangaza UDI (NOV 1965). Nini kinainyamanzisha Tanzania ya leo miaka arobaini baadaye?

JK if this was another country, 'the leader' would have recognized this historical moment to establish his credentials as a stateman of substance and JK history will record you as such, the person who put an end to the suffering of zimbabweans. By doing that you will have jumped the que of african leaders in waiting to inherit the mantle of statemanship from the great man himself Nelson Mandela. JK kama washauri wako hawajakuambia hili, basi wakati wao wa kujiuzuru umewadia as they say since yesterday!

If Tanzania as the chair of AU took this opportunity to sever diplomatic ties with Harare, other African countries will follow suit ( sure you can mobilize this). Mugabe has already extingushed whatever little international standing he has hence he is not in a position to launch any significant diplomatic offensive.

JK huyu mzee kwanini viongozi wa Africa mnamlinda? JK utajivunia mafanikio yapi ya uenyekiti wako wa AU? Tafadhali tuondolee aibu hii ya Mugabe. Is it because of the 'jinamizi la uchaguzi wa zanzibar? well you may be pleased to know that 'two wrongs dont make a right'. Halfu Mugabe ana jeuri ya kusema akishindwa uchaguzi, maveterani wako tiyari kumpigania. Busara gani hizi za mzee wa zaidi ya miaka themanini? After rwanda we said 'Never Again' (Darfur proved us wrong, and zimbabwe if we are not careful is sliding towards exactly that! JK kama chair wa AU, unaangalia tu! Ama tunasubiri hadi Marekani watume majeshi yao, and then do what we do best kulalamikia mataifa makubwa kuingilia mambo yasiyo yao?

Time is of essence. mnasubiri mpaka watu wangapi wafe? mpaka watu wangapi wakatwe mapanga? hii siyo bahati nasibu kusema kwamba 'mtu wa 1000 kukatwa panga tunavunja uhusiano wa kibalozi'

Kumuenzi baba wa Taifa ni pamoja na kufuata maadili yake (principles) katika nyanja ya siasa za kimataifa. Next time Mugabe shows up in Dar moja kwa moja Keko! Thats what the Americans did with Gen Antonio Manuel Noriega of Panama yet makosa yake hayakuwa mazito kama haya ya 'comrade' Mugabe.
Adios.
 
Four MDC youth activists found dead near Harare
Times Online
June 19, 2008

Jenny Booth said:

The bodies of four opposition activists are reported to have been found near the Zimbabwean capital Harare this morning, as violence escalates ahead of next week's election.

The Movement for Democratic Change, Zimbabwe's main opposition party, said that four of its youth members were abducted on Tuesday. Their bodies were found discarded in different places around Chitungwiza, southeast of Harare.

The deaths come hours after Thabo Mbeki, the South African President, flew to Zimbabwe to urge Mr Mugabe to cancel next week's vote and negotiate a deal with the opposition in a bid to control the violence.

The MDC said that latest bodies brought to around 70 the total number of its
activists, their spouses and children who have been murdered by Zimbabwe's
security forces and government supporters since the first round of the
presidential election on March 29 failed to yield a conclusive result.

Nelson Chamisa, an MDC spokesman, said that the party suspected that the
latest victims had been beaten to death after being attacked at a local
councillor's residence by youth supporters of President Mugabe's Zanu-PF
party, armed with clubs and whips. "Now it's about 70 we've lost," said Mr Chamisa. "The situation in the country is getting worse. A free and fair election is impossible." The MDC says the ruling party unleashed an army-led campaign of intimidation against opposition voters after the first vote, in which its party leader Morgan Tsvangirai defeated Mr Mugabe but fell short of an outright majority.

Mr Tsvangirai has said that Zimbabwe is now run by what is essentially a "military junta".

Until the last week the violence has mainly been confined to rural areas, but the most recent attacks have taken mob action from poor townships into
prosperous suburbia. In the past week, the wives of at least three MDC officials has been murdered. Abigail Chitoro, 27, the wife of Harare's recently elected MDC mayor, was so badly beaten by the mob that dragged her and her four-year-old son from their home that even her brother-in-law struggled to identify the body. The clothes she was wearing, her distinctive haircut and the blindfold that Zanu (PF) supporters forced her to wear as they firebombed her home gave the only clue to her identity. The child was dumped alive at a police station.

The UN has blamed Mr Mugabe's supporters for most of the attacks.

Mr Mugabe, however, has blamed the MDC for the mounting violence ahead of the June 27 run-off, and has threatened to arrest opposition leaders over
it. Mr Mbeki met Mr Mugabe and Mr Tsvangirai separately in Zimbabwe yesterday to try to mediate an end to the increasingly violent crisis.

South Africa's Business Day newspaper, a respected financial daily, quoted
unnamed sources as saying that Mr Mbeki tried to set up a meeting between
the pair - their first ever - but did not receive a firm commitment from
Zimbabwe's president.

Robert Mugabe na genge lake la wahuni lazima washitakiwe.
 
It is about time to the West should start declaring certain individuals in Zimbabwe armed forces as war criminals. Na kama alivyofanyiwa Slobodan Milosevic saa ya Mugabe nayo inafuatia. Huwezi kuwatenda watu wako hivyo na ukaendelea kutawala.
 
Wakuu
Matatizo yanayoikumba Zimba si kosa la Mugabe.

Mutakumbuka matatizo yameanza baada ya wazungu kufukuzwa,hivyo basi inaodhihirisha ni jinsi gani wazungu walivyo wanoko na washenzi hadi wakacreate dudu la uhakika lililozaa matatizo yooote haya muyaonayo zimbabwe.

Neno moja nalolitaka kwenu watanzania ni kutafutia njia ya kumsadia mugabe na watu wake waondokane na hali mbaya ya kiuchumi then maissue ya siasa yafute.
Hata huyo Tsava akichukua nchi bado ni kibaraka tuu wa wazungu,hakuna jipya,zaidi ya ukoloni mpya.

Na ni Mwalimu huyo huyo ambaye alizungumzia suala la "uraia" baada ya Idi Amin kuanza kuhoji uraia wa waasia wa Uganda na kuanza sera zake za kibaguzi kule. Mwalimu alizungumza siku ile August 21, 1972 pale Chuo cha Ualimu Chang'ombe, Mwalimu alisema hivi "Afrika lazima ikatae kudhalilishwa, kunyonywa, na kusukumwa sukumwa. Na kwa moyo huo huo ni lazima tukatae kuwadhalilisha, kuwanyonya, na kuwasukuma sukuma wengine. Ni lazima tutende siyo maneno tu".

Matatizo ya Zimbabwe yamesababishwa na Mugabe, period. Alianza kufanya unyama dhidi ya Matabele kwa vile walikuwa wako upande wa Joshua Nkomo. Aliwakumbatia veterans alipoona wameanza kumhoji kwa nini anawapendelea watu ambao hawakuhusika na mapambano, hususan, mke wake Grace. Si tu aliwanyang'anya mashamba bali aliwaondoa wazimbabwe weusi waliokuwa wakifanya kazi na kuishi kwenye mashamba hayo na kuwapa cronies wake ambao hawana utaalam wa kilimo. Wakati wa visingizio umekwisha. Matatizo haya ameyaleta mtu mweusi mwenzetu. Tusimuonee haya.

Nyerere alisimama kidede kumpinga Idi Amin hata pale wenzake walipompa uenyekiti wa O.A.U! laiti Idi Amin angechukua nchi wakati huu, bila shaka angeendelea kupeta!

Ni hawa viongozi wetu wakati wenzetu wanauawa huko Darfur walikuwa karibu wampe uenyekiti wa A.U. rais wa Sudan. Mpaka hapo tutakapoweza kusimama na kuwekana sawa wenyewe dunia itaendelea kutuona ni vikaragosi!

Mungu alinusuru bara letu. Mungu awanusuru wazimbabwe. Kama alivyosema Robert Nesta Marley " Afrika liberate Zimbabwe....."
 
Mwanakijiji thanks for your letter. I believe it will make a difference. I know, critics might say its nothing, but this shows how most of us are just concerned with humanity. What is happening in Zim is deplorable. It is what makes Africa what it is today, a cursed and hopeless continent. Perhaps you could explore sending it to him to the State House and print it through magazeti.

Kwa kweli Mugabe sijui tumfanye nini. I just dont get it, killing and torturing your own people simple because they dont agree with you!
 
Matatizo ya Zimbabwe yamesababishwa na Mugabe, period. Alianza kufanya unyama dhidi ya Matabele kwa vile walikuwa wako upande wa Joshua Nkomo. Aliwakumbatia veterans alipoona wameanza kumhoji kwa nini anawapendelea watu ambao hawakuhusika na mapambano, hususan, mke wake Grace. Si tu aliwanyang'anya mashamba bali aliwaondoa wazimbabwe weusi waliokuwa wakifanya kazi na kuishi kwenye mashamba hayo na kuwapa cronies wake ambao hawana utaalam wa kilimo. Wakati wa visingizio umekwisha. Matatizo haya ameyaleta mtu mweusi mwenzetu. Tusimuonee haya.

Nyerere alisimama kidede kumpinga Idi Amin hata pale wenzake walipompa uenyekiti wa O.A.U! laiti Idi Amin angechukua nchi wakati huu, bila shaka angeendelea kupeta!

Ni hawa viongozi wetu wakati wenzetu wanauawa huko Darfur walikuwa karibu wampe uenyekiti wa A.U. rais wa Sudan. Mpaka hapo tutakapoweza kusimama na kuwekana sawa wenyewe dunia itaendelea kutuona ni vikaragosi!

Mungu alinusuru bara letu. Mungu awanusuru wazimbabwe. Kama alivyosema Robert Nesta Marley " Afrika liberate Zimbabwe....."


Fundi, we have wrote countless of times here..the worst enemy of Africa are Africans. Huna haja ya kuanza kurevisit history. Facts are out there for everybody to see..anayekubali au anayekataa..mwache. Ila Mugabe anapigana na Ukuta! No society can suffer permanently!
 
Fundi, we have wrote countless of times here..the worst enemy of Africa are Africans. Huna haja ya kuanza kurevisit history. Facts are out there for everybody to see..anayekubali au anayekataa..mwache. Ila Mugabe anapigana na Ukuta! No society can suffer permanently!

People have short memories. Some were not even around when all these were happening. Hence the need to keep reminding them of our history. As we used to say......Aluta Continua!
 
Mwanakijiji,

Utajibiwa Na Salva,Ndiyo kazi yake kwa sasa na Muungwana amebakia kusoma hotuba za sherehe na kusafiri,Mie nadhani uitume kwa E-mail ya Salva.Na ni mmoja wa watu wanaopita sana hapa JF na kusoma
 
It is about time to the West should start declaring certain individuals in Zimbabwe armed forces as war criminals. Na kama alivyofanyiwa Slobodan Milosevic saa ya Mugabe nayo inafuatia. Huwezi kuwatenda watu wako hivyo na ukaendelea kutawala.
MWanakiji Milosevic na Mugabe ni mambo mawili tofauti,Mie Mugane kwa upande mmoja simuungi mkono,hasa katika mambo yanayohusu kuendeleza Uchumi wa Nchi ya wazimbabwe.

Ila suala la Kuachia Vibaraka wa mataifa ya nje waje waongoze nchi,Mie naungana na Mugabe,Kina Morgan wanatumiwa na kupewa pesa na Wazungu walionyang'anywa mashamba ili wamuondoe Mugabe,thus why Mugabe is Not ready to leave the country to people who are being used by white people.

For my opinion i think Mugabe is Ready to step down,but not to leave the country for the people who doesnt know the reason for fighting for Zim Independence.
 
Mwanakijiji hayo yote uliyoyandika ni ya kweli lakini anuani ulikoituma siko.Kwani huyo Mh.Rais kwa mambo yanavyokwenda kwa CCM na serikali kupoteza dira na kuendelea kuvulunda kila siku kwa kashifa za WIZI NA UFISADI .Matokeo yake kupoteza imani kwa wananchi tusije tukashangaa katika uchaguzi ujao baada ya Mh.Rais kushindwa akageuka Mugabe au Mwai Kibaki hii ndio sababu kubwa inayomfanya kua kimya katika matukio ya Kenya na Zimbabwe.Kunawakati nilichukizwa na baadhi viongozi na magazeti ya nchi za magharibi yalipouita umoja wa nchi huru za Afrika"klabu ya madikteta"Kwa sasa nakubaliana na kauli zao viongozi wengi wa hizi nchi zetu hawatafautiani na Mugabe hivyo wakati wote ulindana lengo lao kubwa ni kua madarakani milele au kuiba fedha za walalahoi katika kipindi kifupi na kuondoka madarakani na kupumzika na kula pesa yako kama ilivyokua kwa Rais wa awamu ya tatu Mkapa Mwanakijiji huu ndio ukweli.MUNGU IBARIKI AFRIKA.
 
Mimi nadhani kuna haja ya barua nyingine ya kumtaka Rais wetu asifanye mambo kwa shinikizo la watu wa nje ....in this case Non-africans! ....we want to keep our sovereignty, including our foreign policy sovereignty. Mambo ya kupata viamri kutoka kwa visketi pale State D au Waziri Mkuu bila kura yoyote pale ulaya, hatutaki....hatutaki kabisa. Kama ana madeni nao kwa namna yoyote yatakayomfanya ashindwe kutete maslahi yetu, aachie ngazi kistaarabu, asituingize wote kwenye matatizo.

Kujenga ni kazi lakini kubomoa ni rahisi.
 
Chemical warfare waged on civilians
http://www.thezimbabwetimes.com
June 18, 2008

assaultvictim.gif


Example of severe injury on buttocks of recent violence victim.
 
Dua! Na bado watu wanamtetea huyu dikteta! Ati wasituingilie kwenye uhuru wetu kama waafrika! Uhuru wa kuwafanyia wenzetu haya?
 
Huyu ni sawa na wakina Bizmungu tuu kwani anawaumiza watu wake kwa ajili ya kuhakikisha kuwa anaendelea kubakia madarakani huu ni udhalimu wa hali ya juu na wafaa kupingwa na kila mtanzania mwenye mapenzi mema na waafrika wenzake.

Haiwezekani huyu kuumiza watu ili yeye aendelee kuwepo madarakani.

Nimeongea na mwenyekiti wa vijana wa MDC bwana Washington Katema kaniambia kuwa hali ni mbaya sana na haswa vijijini kwani watu wanateswa na kuteseka sana sana .

Tushikamame na kuwasaidia dhidi ya mkoloni mweusi kama tulivyofanya kwa mkoloni mweupe.
 
Milosevic na Mugabe wako sawasawa.. wote wawili waliongozwa na twisted sense of nationalism. Wote wawili waliamini kuwa wao ni baraka ya Mungu kwa watu wao kiasi kwamba walitaka kufanya lolote lile kama wapendavyo. Milosevic alikuwa ni chinjachinja wa Balkani, na sasa Mugabe amegeuka kuwa china china mpya wa Afrika!
 
MDC the main culprit in Zimbabwe violence: police

[-] Text [+] HARARE (Reuters) - Zimbabwe's police have arrested 390 opposition supporters and 156 members of the ruling party over violence since elections in March, the police chief said on Friday, blaming the opposition for most of the trouble.

The opposition Movement for Democratic Change (MDC), Western countries and human rights groups accuse President Robert Mugabe's ruling ZANU-PF of a campaign of violence ahead of a June 27 presidential election run-off.

"It is without doubt that between the two political parties ... the MDC is the main culprit in the political violence that we are currently witnessing in the country," police chief Augustine Chihuri told reporters

source:http://africa.reuters.com/wire/news/usnL20723866.html
 
Bunge Backs Tough Stand On Zimbabwe




21 June 2008
Posted to the web 21 June 2008

A parliamentary committee yesterday endorsed the Government's tough stance on Zimbabwe, saying it fully supports the official sentiments of the members of the Southern African Development Community (Sadc). The chairman of the Parliamentary Committee for Foreign Affairs, Security
and Defence, Mr Wilson Masilingi, said they agreed with the official denunciation of the state-sponsored violence just a week before the election
run-off pitting President Robert Mugabe against MDC candidate Morgan Tsvangirai. The statement issued by the MP for Muleba at the National Assembly in Dodoma was in response to Foreign Affairs and International Co-operation minister Bernard Membe's warning in Dar es Salaam on Thursday that Tanzania was appalled by President Mugabe's style, which threatened to plunge the country into chaos.

Nominated MP Anna Abdullah said that while the Government's statement was positive, it had, however, taken too long for it to denounce the breakdown of law and order and condemn the rampant human rights abuses in Zimbabwe. Speaking to The Citizen, Mr Masilingi and Ms Abdullah said that "even though Zimbabwe is a sovereign state, Tanzania has a historical stake and can, therefore, not keep quiet as that country spirals into anarchy".

Earlier, in her contribution to the Budget debate, Ms Abdullah said: "It's good that the Government has issued a condemnation of Zimbabwe even though
this should have come earlier. Tanzania, as the current chair of the African Union, must be in the forefront in condemning what is going on in Zimbabwe."
Later, she told The Citizen that President Mugabe deserved to be condemned by his fellow African leaders for trying to cling to power by force. "Our country supported Zimbabwe's struggle for independence but it was not so that he could become the President for life," she said. Zimbabwe, she added, was neither a chieftainship nor a kingdom. "Democracy and the rule of law must be respected," she said, denouncing recent reports that quoted Mr Mugabe and his wife, Grace, threatening not to hand over power should he be defeated in run-off poll.

Mr Masilingi said he had been shocked by a report of the Sadc political committee, which confirmed gross human rights abuses and mounting insecurity against the people of Zimbabwe and election monitors. "We share the Government's concern and urge the relevant organs of the Sadc member countries follow closely all that is happening in Zimbabwe." The MP said President Mugabe must cooperate with fellow regional leaders to make sure the re-run election was free and fair. "It is in the interest of the people of Zimbabwe as well as the region to have peaceful and democratic elections," Mr Masilingi said. In an indication that gone are the days when Zimbabwe took Tanzania's support for granted, Foreign minister Membe on Thursday cast doubt on the possibility of a free and fair election on June 27.

He told journalists in Dar es Salaam: "I want to tell you what I told fellow Southern African Development Community (Sadc) members. We have got evidence that the elections will not be free and fair." He added: "Zimbabwe has been our great friend. We have stood by them since the Lancaster agreement on land issues in 1980, but on governance issues, we have started to differ with the incumbent president." Last week, President Mugabe vowed to "go to war" to prevent the Movement for Democratic Change from taking power - as the race for the presidency entered its final phase. "We are prepared to fight for our country and to go to war for it," he told a rally of cheering supporters.



zimbabwe-torture-vi_681062c.jpg

A torture victim is given treatment for his burns in a hospital in Harare, Zimbabwe. He was set on fire by suspected Zanu PF militia



Assassins Aim at Zimbabwe Opposition

http://graphics8.nytimes.com/images/2008/06/22/world/22zimbabwe-span-600.jpg[/img[/CENTER]]

[quote="Tsvangirayi Mukwazhi, post: Associated Press"][size=3]

The killing of scores of opposition party workers has turned funerals, like that of Tonderai Ndira, in Harare, into political rallies.

There were rumors his name was on a hit list. For weeks he prudently hid out, but his wife, Plaxedess, desperately pleaded with him to come home for a night. He slipped back to his family on May 12. The five killers pushed through the door soon after dawn, as Mr. Ndira, 30, slept and his wife made porridge for their two children. He was wrenched from his bed, roughed up and stuffed into the back seat of a double-cab Toyota pickup. "They're going to kill me," he cried, Plaxedess said. As the children watched from the door, two men sat on his back, a gag was shoved in his mouth and his head was yanked upward, a technique of asphyxiation later presumed in a physician's post mortem to be the cause of death..............[/size][/quote]

[B][SIZE="4"][COLOR="Lime"]Killer Robert Mugabe anataka kuongoza vipofu na walioungua na moto ambao hawawezi kukaa chini.[/COLOR][/SIZE][/B]​
 
Bunge Backs Tough Stand On Zimbabwe






zimbabwe-torture-vi_681062c.jpg

A torture victim is given treatment for his burns in a hospital in Harare, Zimbabwe. He was set on fire by suspected Zanu PF militia



Assassins Aim at Zimbabwe Opposition

http://graphics8.nytimes.com/images/2008/06/22/world/22zimbabwe-span-600.jpg[/img[/CENTER]]



[B][SIZE="4"][COLOR="Lime"]Killer Robert Mugabe anataka kuongoza vipofu na walioungua na moto ambao hawawezi kukaa chini.[/COLOR][/SIZE][/B][/QUOTE]

Kama wakati wote suspect ndio mkosaji...pengine hatuna haja na mahakama!

I don't think if it is fair or reasonable to conclude every statement/action by Mugabe goverment is wrong and every statements by MDC and supporters is correct.... so far we know MDC is saying ZANU-PF is violently targeting its supporters and Mugabe goverment is saying MDC is behind the violence.

Mambo ya Kenya yalikua tofauti kidogo, lakini inasemekana watu zaidi ya 1,000 walikufa....lakini inashangaza kuona hakuna kilichofanyika kwa victims.
Pengine ilikua ni jinsi ya kujustify stakes and need for GNU without rerun.
Soma habari kwa undani:[url]http://www.talkzimbabwe.com/news/128/ARTICLE/2744/2008-06-20.html[/url]​
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

YAH: Iongoze Afrika kupinga utawala wa kidhalimu wa Robert Mugabe

Naomba husika na kichwa hicho cha habari;

Hivi hadi nini kitokee ndipo viongozi wetu wataona kuwa kinachoendelea Zimbabwe ni aibu ya bara letu, na udhalilishaji wa utu, hadhi, na tunu ya mwafrika? Ni mpaka nini kifanyike ndipo tutaweza kuchukua msimamo wa kupinga uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu, na kuchukua msimamo ulio dhahiri dhidi ya Robert Mugabe? Kwanini Tanzania nchi ambayo inadai katika Katiba yake kuwa "kila mtu anastahili haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake" ifumbie macho utu wa wana wa Zimbabwe ambao wanateswa katika mikono ya utawala wa kidhalimu wa Robert Mugabe?

Inakuwaje wanasiasa wetu na wabunge wetu wanashindwa kutoa msimamo wa kulaani kauli za kidikteta ambazo zimekuwa zikitolewa na utawala wa Robert Mugabe? Hivi kweli tunahitaji wazungu kutuonesha kuwa kinachotokea Zimbabwe hakina mfano wa haki za binadamu? HIvi kweli tunataka hadi Amnesty International na Human Rights Watch waje na kutuambia kuwa ya Mugabe ni uovu uliokithiri?

Je tumekuwa watii na wenye kuheshimu sura za watu kiasi hiki hadi tunaogopa kumwambia kuwa "tunashukuru kwa mchango wako lakini kwa hili tunakukana"? Je hakuna watu waliofanya mambo mazuri huko nyuma na katika maisha yao ya baadaye wakaharibu na historia zao zikatajwa na nyota pembeni?

Wale wanaolalamikia ukiukwaji wa haki za binadamu kule Palestine, Iraq na Afghanistani, walioandamana ujio wa Bush na ambao wakitetea haki za watu wa huko wako wapi leo hii wakati ndugu zetu wanaishi maisha ya wasiwasi na hofu kubwa chini ya mkono wenye kucha ndefu zichomazo wa Robert Mugabe?

Wakati umefika kwa viongozi wetu kuacha mazingaombwe ya diplomasia ya ukimya ambayo kimsingi ni ukimya wa kidiplomasia. Ni ukimya ambao unaendelea kutoa kibali kwa Utawala haramu wa Robert Mugabe kuendelea kutesa wananchi wa nchi hiyo. Je sisi Tanzania ambao tuliwahi kukiri katika imani zetu kuwa "binadamu wote ni sawa, na Afrika ni moja" leo hii tuko wapi?

Mch. Martin Luther King alipoandika barua yake kutoka Jela ya Alabama alisema wazi kuwa "udhalimu mahali fulani, ni udhalimu mahali pote" Je tunaweza vipi kukaa katika "kisiwa cha amani" wakati ndugu zetu wanateseka na kufanywa wakimbizi katika nchi yao wenyewe. Kwanini kina Morgan na wenzao waonekane si wananchi wa Zimbabwe kweli kwa sababu tu wanataka kuiokoa nchi yao?

Nini ambacho utawala wako unaogopa kusema na kufanya mbele ya Robert Mugabe? Hivi tukimtolea uvivu na kumuita kwa jina lake kuwa ni dikteta na kusema kuwa yanayofanyika Zimbabwe hayana nafasi katika bara la Afrika Mugabe atasema nini? Atatufanya nini? Hii heshima ya wazee ni heshima kweli wakati mzee anasimamia ubakaji na utesaji wa watu wake?

Naomba kutoa wito wa wazi, wa moja kwa moja na usio na utata kwako uwa Mhe. Kikwete kama Rais wa Tanzania, nchi ambayo imetoa na kulipa kwa damu ili nchi hizi za kusini mwa Afrika ziwe huru, asimame sasa na kusema "kama kutosha inatosha". Rais Kikwete ukiwakilisha mawazo ya kizazi kipya uungane na Botswana kwa kumwita Balozi wa Zimbabwe nchini na kuonesha kutokufurahishwa na yanayoendelea Zimbabwe.

Zaidi ya yote, Rais Kikwete akiwa ni Mwenyekiti wa AU aitishe mkutano wa haraka kati ya Morgan na Mugabe Jijini Dar (na si mtu mwingine nje yao) ili kujadiliana na kukubaliana jinsi uchaguzi wa marudio utakavyokuwa na kupata uhakika kuwa kila mmoja wao ataheshimu matokeo ya uchaguzi huo. Kikwete anaweza kufanya hivyo kwa kutumia kivuli cha NEPAD ambamo ndani yake kuna "African Peer Review Mechanism". Huu ni wakati wa kuonesha uongozi.

Na endapo Mugabe hatokuwa tayari kusikiliza ushauri wa rafiki, basi wakati umefika wa kuvunja uhusiano wetu wa kidiplomasia na Zimbabwe. Itauma, lakini inabidi.

Nikukumbushe maneno ya Rais Nyerere kwenye mkutano wa Jumuiya ya Madola mwanzoni mwa miaka ya sitini ambapo hoja ya kukubali kuiingiza Afrika ya Kusini katika jumuiya hiyo. Nyerere alisema wazi kuwa kwa kadiri ya kwamba siasa za kibaguzi zilikuwepo Afrika ya Kusini basi Afrika ya Kusini haiwezi kuwa mwanachama. Na akatamka yale maneno mashuhuri ya msimamo wa kiongozi mbele ya Malkia "Mkiwapigia kura kuwaingiza Afrika ya Kusini, mtakuwa mmepika kura kututoa sisi". Na hoja ya Mwalimu ikashinda.

Na ni Mwalimu huyo huyo ambaye alizungumzia suala la "uraia" baada ya Idi Amin kuanza kuhoji uraia wa waasia wa Uganda na kuanza sera zake za kibaguzi kule. Mwalimu alizungumza siku ile August 21, 1972 pale Chuo cha Ualimu Chang'ombe, Mwalimu alisema hivi "Afrika lazima ikatae kudhalilishwa, kunyonywa, na kusukumwa sukumwa. Na kwa moyo huo huo ni lazima tukatae kuwadhalilisha, kuwanyonya, na kuwasukuma sukuma wengine. Ni lazima tutende siyo maneno tu".

Mhe. Rais, Afrika inadhalilishwa na vitendo vya Mugabe na mashabiki wake. Afrika inafanywa duni kwa viongozi kama yeye. Ni kweli tuna matatizo yetu Tanzania, nafahamu tuna kashfa zetu za mambo ya fedha nchini na uongozi wa kishkaji; nafahamu wazi kabisa ndani ya CCM na serikali kuna kubebana na kulindana. Lakini ukweli ni wazi kuwa hatujafikia walipofikia Zimbabwe, hatujafikia mahali pa kufanyana vibaya kiasi cha Zimbabwe. Ni kweli tuna matatizo yetu lakini tukiyaweka ya Zimbabwe upande wa pili, ya kwetu yanaonekana ni kheri tupu!

Sisemi upuuzie matatizo yetu, sitoi ushauri kuwa ya kwetu kwa vile ni madogo basi usiyafuatilie. La hasha, ninachosema ni kuwa chukua msimamo kama kiongozi na kwa niaba ya wale waliotangulia mbele ya haki, kwa niaba ya wale waliomwaga damu yao kukomboa bara letu, usimame na kumwambia Mugabe inatosha na saa na wakati wake umepita aamue kujiuzulu na kustaafu kwani yeye kama wanadamu wengine, atakufa tu, na Zimbabwe itatawaliwa na mwingine. Mugabe hana ubavu wa kuzuia hatima ya nchi hiyo, na siku moja wengine watasimama mahali pake.

Akiamua kuachia ngazi sasa na kufanya mapatano ya kisiasa na wale walioumia chini yake, labda historia itamuonea huruma. Lakini Zimbabwe haiwezi kuendelea jinsi ilivyo, huku sisi rafiki zao na ndugu zao tukikaa nje kuangalia. Mhe. Rais, onesha msimamo sasa, na uliongoze Taifa letu kuchukua msimamo dhidi ya Mugabe ili tuwape nafasi ya ndugu zetu wa Zimbabwe ya kuishi katika nchi ya amani, utulivu, na mshikamano.

Sijaomba vingi, lakini hilo nakuomba kwa machozi.

Nimalizie kwa kukumbusha maneno haya ya baba wa Taifa tena alipozungumza mwaka 1959 kwenye mkutano ule uliofanyika Uingereza Juni 26 (karibu miaka 50 kamili iliyopita). Katika mkutano huo uliokuwa unazungumzia Afrika ya Kusini na utawala wa Makaburu Mwalimu alisema maneno haya "Serikali ya Afrika ya Kusini inapigana na historia, ni wao watakaoshindwa. Tunafahamu harakati za ukombozi zitafanikiwa katika Afrika ya Kusini. Kama tunajiamini tutashinda".

Mheshimiwa, Mugabe anashindana na historia na kwa hakika atashindwa; harakati za mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea yatafanikiwa, na kama sisi sote tunajiamini kwamba tuko sahihi basi tutashinda. Tuongoze katika hili kwani bwana mdogo kutoka Botswana ameshaonesha njia.

Wasalaam katika Kuliinua Bara letu

M. M. M.

Mkuu...

Na suala la ardhi kwa weusi nalo si la kupuuzia ni haki yao kumiliki ardhi katika nchi yao!..fikiria uko katika nchi yako halafu robo tatu ya ardhi yenye rutuba inamilikiwa na wazungu!!! halafu kiongozi wenu akitaka kukugawieni ardhi yenu mliyonyag'anywa wakati wa ukoloni UK na Marekani inawawekea vikwazo.!!!!

-Wembe
 
Back
Top Bottom