Barua ya Wazi kwa Rais Kikwete Kuhusu Zimbabwe

Ndugu yangu wembemkali,ardhi ya zimbabwe ilikuwa na faida kwa weusi chini ya milki ya wazungu kuliko ilivyo chini ya weusi wachache wateule wa Mugabe...Nafikiri ni wakati wa Mugabe kushitakiwa kwa uhalifu dhidi ya UBINADAMU,Kama ni uhuru hakupigania peke yake,na si kweli kwamba MDC ni chama kwa wale ambao hawakupigania Uhuru na si kweli kwamba wanachama wa MDC wote wamepewa fedha na wazungu ili wapige kura dhidi ya mugabe na si kweli kwamba kwamba taarifa ya POLISI ina ukweli kwa sababu kama mkuu wa majeshi anatoa amri ya kumpigia kura Mugabe kwa wanajeshi wote na kutishia ajira ya yule atekwenda kinyume itakuwaje Mkuu wa polisi athubutu kunena kwamba vurugu zinafanywa na wafuasi wa Raisi wake ? Muda umefika waafrika tuungane dhidi ya Dikteta Mugabe...tuwahurumie wazimbabwe tuwaondolee mugabe,kutokana na umri wake mugabe hana cha kupoteza hata kama nusu ya wazimbabwe watachomwa moto,tuache kudanganywa na hoja ya kwamba MDC ni kwa ajiri ya walionyang'anywa mashamba hata kama wanaiunga mkono ni kwa ajiri ya manifesto yake na si upendeleo ikiingia madarakani,propaganda za ZANU-PF zisitupumbaze tukapuuza mateso ya ndg zetu...
 
Mkuu...

Na suala la ardhi kwa weusi nalo si la kupuuzia ni haki yao kumiliki ardhi katika nchi yao!..fikiria uko katika nchi yako halafu robo tatu ya ardhi yenye rutuba inamilikiwa na wazungu!!! halafu kiongozi wenu akitaka kukugawieni ardhi yenu mliyonyag'anywa wakati wa ukoloni UK na Marekani inawawekea vikwazo.!!!!

-Wembe

Tuzungumzie swala la ardhi. Ni wazimbabwe wangapi wamegawiwa hiyo ardhi iliyorudishwa kutoka kwa hao wazungu? Mimi ningemuelewa mheshimiwa mwana mapinduzi kama baada ya kuwanyang'anya wazungu angewagawia wafanyakazi waliokuwa wakiyahudumia. La, hasha. mkuu kawapa cronies wake ambao hawajui lolote kuhusu kilimo! Heri ya hao wazungu waliokuwa angalau wanalima na kuajiri watu weusi kuliko hao cronies walioyaachia yadumae na kuwakosesha ajira wengi wa watu weusi wenzao. Muda wa visingizio umekwisha! Mtu dhalimu ni dhalimu tuu hata akiwa mweusi kama sisi.
 
Hon. Kikwete Umevaa Viatu Vilivyopata Kuvaliwa na 'Nyota ya Afrika'.

Wakuu bila ubishi Mwl. Nyerere ameacha 'standards' za hali ya juu ili viongozi watakaomfuatia wazifuate na pengine waweze kwenda mbali zaidi ya pale yeye alipofika.
Nasema pasi kuwa na shaka Mwl. alikuwa na mapungufu yake kama mwanadamu na kiongozi, lakini mzee yule alikuwa na visions na principles zake ambazo naamini kwa hili la Zimbabwe asingeliacha lipite kimyakimya.

Raisi Kikwete tunafahamu wewe kiumri na kiuzoefu pengine ni mchanga kwa BoB Mugabe, lakini ulipo sasa umevaa viatu vya hadhi ya juu kabisa ktk bara la Afrika. Umevivaa viatu vya muasisi wa Taifa la Tanzania, mwana wa Afrika, mwanamapinduzi asiyeyumbishwa Baba wa Taifa Mwl. Nyerere, na kwa muktadha huo basi unayo 'full-mandate' na authority kutoka kwa wale waliokutangulia hususan baba wa Taifa na viongozi wengine waliofanana nae ktk utumishi ulitukuka wa bara letu.

Kauli iliyotolewa hivi karibuni na Bob Mugabe kwamba hayuko tayari kuachia madaraka na ikiwezekana hata kwa kuanzisha vita, ni kauli za kuturudisha nyuma Waafrika.
Kudhani kwamba Morgan ni Kibaraka na yeye ni mteule mpakwa mafuta ni mawazo mufilisi maana huku ni kuogopa kivuli chake mwenyewe.

Mh. Kikwete wewe sasa ni Mwenyekiti wa AU, kofia hii inakupa nguvu zaidi ya kusimama 'tall' na unaweza kuitumia vyema kuwaletea 'raha' na matumaini mapya ndg. zetu wa Zimbabwe, ukwaondolea dhiki na udhalimu wanaokumbana nao wa makucha ya dikteta Mugabe.

Ndio BoB alikuwa ni 'hero' wetu lakini sasa anaharibu, mashaka na wasiwasi yanayotawala Zimbabwe nadiriki kusema nchi ile inahitaji ukombozi mwingine zaidi ya ule wa kuwaondoa Wakoloni miaka ile ya ukombozi wa kusini mwa Afrika.

Nchi yetu ina heshima kubwa, kutokana na misimamo ya wazee wetu waliotangulia nawe Mh. Raisi Unasimama ktk nafasi ile leo hii.

Uliyoyaongoza na kuyasimamia visiwani 'Comoro' yameonyesha unavivaa vyema viatu vya waasisi wale, ingawa unateleza hapa na pale, tunakuombea Mungu akupe uthabiti na nguvu zaidi , ukisimamia haki na ukweli daima utashinda. Kuwa upande wa wanyonge na wanaodhulumiwa, maana Mungu hapendi dhuluma.

Lazima kuwe na 'plan B', vipi kama Bob Mugabe akishindwa na akakataa matokea na kuanzisha vita kama alivyosema, je tunafanya nini?
Mimi si mpenzi wa vita, maana madhara yake ni makubwa na wahenga walisema vita havina macho; Lakini kwa mashaka na madhila yale wanayoyapata Wazimbambwe chini ya Mugabe, Mission kama ile ya 'Comoro' hakuna atakaekulaumu, ingawa daima huwezi kuridhisaha watu wote.
Chukua hatua na wanyonge watakuunga mkono.

Mungu Ibariki Afrika
Mungu wabariki Wazimbabwe na Waafrika
 
SADC To Hold Emergency Summit On Zimbabwe - Tanzania



DAR ES SALAAM, Tanzania (AFP)--Southern African leaders will meet Wednesday in an emergency summit over the political crisis in Zimbabwe, the Tanzanian presidency said.

The Southern Africa Development Community (SADC) will meet in the Swaziland capital of Mbanane, it said in a statement.

"It will be attended by some SADC members as well as members of the bloc's security organ, namely Swaziland, Angola and Tanzania."

-Dow Jones Newswires, 201-938-5500


(END) Dow Jones Newswires
06-24-081329ET
 
Wednesday, 25 June 2008
Southern African Catholic Bishops extremely concerned at the situation in Zimbabwe.

The people of Zimbabwe have the right to choose their President in an election that is contested freely and fairly. The Southern African Catholic Bishops' Conference (SACBC) passionately supports this legitimate aspiration of the Zimbabwean people.

Sadly, the politically motivated violence, intimidation and torture have made a just and fair run-off presidential election virtually impossible. The electoral playing field is not level. Opposition candidates cannot present their views to the electorate, nor do they have equitable access to the media. Monitoring systems are not in place.
The violence has intensified in the last few weeks to the extent that the Movement for Democratic Change has made the difficult decision not to participate in what has degenerated into a sham. The choice by the MDC to try to protect the lives of supporters and others who have been targeted is understandable. The alternative would have been an undeclared civil war.

A consensus model of government that involves all Zimbabweans must be sought. The International Community must co-operate with the Southern African Development Community to bring about a just settlement. A ‘winner-takes-all' solution that rewards the ruling party for its atrocities and criminal mismanagement will only entrench the sufferings of the most vulnerable.

We, together with other organisations, warn that the atrocities and barbarism of Zanu-PF are being documented. Mr Mugabe's actions and those of his Generals, their wives, his thug supporters and the so-called ‘war veterans' are offensive in the eyes of God. Judgement awaits.
Everyone needs to keep asking the question as to who is benefiting from the current crisis in Zimbabwe.

We, the Catholic Bishops of Southern Africa, believe that the actions of the incumbent ruling elite deserve rigorous censure. They are blight on every African.
We call on the member States of the African Union to register their commitment to democracy in Zimbabwe by rejecting the legal fiction that this election has become and by not recognising Robert Mugabe and his party as the legitimate government.

We are deeply concerned at this situation and warn that unless there is a unified effort from the International Community with the leadership of Southern African Countries, the hopeless situation of violence, famine and uncertainty will result in a vast humanitarian crisis that will engulf the whole Southern African region.


Cardinal Wilfrid Napier OFM.
Archbishop of Durban.
Spokesperson of the Southern African Catholic Bishops' Conference.

Issued on behalf of Cardinal Napier by Fr Chris Townsend, Information Officer of the Southern African Catholic Bishops' Conference.
All Media enquiries to Fr Chris Townsend

Mobile: +27 82 7834729
Email: townsend@sacbc.org.za
 
Mwanakijiji,

So you want Bush and Cheney to label Mugabe a War criminal after the Iraqi fiasco? The same people who do not recognize the authority of the International criminal courts? Kaaaz kwel kwel.........
 
Naona OBAMA kafata ushauri hapa...Anasema SA wahusishwe!
Na kama kawa SA hawakubaliani na vita!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom